STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 17, 2014

TANZIA! Mnenguaji Aisha Madinda afariki Dar

image
Aisha Madinda enzi za uhai wake
TASNIA ya sanaa imezidi kupata majozi baada ya aliyekuwa mnenguaji wa bendi za African Stars 'Twanga Pepeta' na Extra Bongo, Aisha Mohammed Mbegu 'Aisha Madinda' amefariki dunia mchana huu akiwa ndani ya Bajaj wakati akiwahi hospitali ya Mwananyamala.
Taarifa ambazo MICHARAZO imezipata zinasema kuwa Aisha Madinda alikodisha Bajaj na wakiwa kwenye foleni alikumbwa na mauti na mwili wake kwa sasa upo hospitali ya Mwananyamala ukiwa umehifadhiwa.
Akiongea na EATV Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa na daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.
“Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea,” amesema Asha Baraka.
Hata hivyo taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa Madinda aliita dereva wa bajaj nma kuomba apelekwe Mwananyamala Hospitali na kukumbwa na mauti njiani bila dereva kujua mpaka akiwa hospitalini hapo.
Inaelezwa kuwa msiba wa marehemu Aisha uko Kigamboni na huenda akazikwa kesho huko huko.
MICHARAZO inaendelea kufuatilia na kitakachopatikana tutawafahamisha zaidi juu ya msiba huu ambao umekuja siku mooja tu baada ya Mkongwe Shem Ibrahim Karenga kufariki na kuzikwa jana jijini Dar.

Tuesday, December 16, 2014

Dirisha dogo lafungwa, 15 waombewa ITC

http://www.rockersports.co.tz/wp-content/uploads/2014/11/meshak.jpg
Meshack Abel alipokuwa Bandari Fc
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/11/wawa-2.jpg
Wawa
 
 USAJILI wa dirisha dogo msimu wa 2014/2015 umefungwa rasmi jana (Desemba 15 mwaka huu) huku wachezaji 15 kutoka nje wakiombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka nchi mbalimbali.
Wachezaji walioombewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam na Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara.
Wengine ni  Charles Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu Michael Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.
Pia wamo Dan Serunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil) kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na Juuko Murushid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba.
Wachezaji wengine ni Kpah Sean Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB (Kenya) kwenda Polisi Morogoro na Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United.
Pia wamo Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Serge Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Serunkuma kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kupitia usajili wa wachezaji wote walioombewa katika dirisha dogo wakiwemo wale wa mkopo.

Breaking News! Jaji Werema aachia ngazi

http://2.bp.blogspot.com/-HfIVzV9HEPE/Uq2Qh28re9I/AAAAAAAALfk/iZ76iAX0yLA/s640/1.png
jaji Werema aliyetangaza kuachia ngazi mwenyewe

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema ametangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo.
Habari hizo zinasema Jaji Werema mmoja wa vigogo wanaotuhumiwa kuhusika na sakata la uchotwaji wa fedha za Akaunti za Tegeta Escrow zipatazo zaidi ya Sh Mil 300.
Kwa mujibu wa taarifa hizo zinasema kuwa Jaji Werema ameamua kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake na kwamba Rais Jakaya Kikwete ameafikiana na maamuzi hayo na kumshukuru kwa ujtendaji wake na kumtakia kila la heri katika maisha yake mapya.
Hata hivyo taarifa hizo zinasema kuwa, maamuzi hayo yamekuja baada ya shinikizo kubwa ambalo limekuwa likitolewa kila pembe ya nchi kwa Rais JK kuwawajibisha wote waliotajwa kwenye mapendekezo nane ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusiana na sakata hilo ambalo limeitia doa Tanzania mbele ya nchi wahisani.
MICHARAZO itazidi kuwaletea habari zaidi.

Gwiji Shem Karenga afariki, kuzikwa leo Kisutu

Shem Ibrahim Karenga enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI mkongwe nchini aliyekuwa amejaliwa kipaji cha kuimba na kucharaza gitaa kiongozi la Solo, Shem Ibrahim Karenga amefariki dunia jana akiwa katika Hospitali ya Amana  jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa na anatarajiwa kuzikwa leo.
Marehemu Kalenga anayekumbukwa kupitia tungo zake mbalimbali zilizochangia kumpa umarufu, alizozifyatua akiwa na bendi mbalimbali kama vile ‘Tucheze Segere’, ‘Muna’, ‘Kila jambo’ na ‘Mbelaombe’, alifariki asubuhi ya jana wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4wpGMAyOuYjuumKhAvBULpmmVN7j8iYWt3pn5pydekJm6qKAiT67ntH80ZpBjtDt7c9s5ewZsTIyWO4J9KC5B1o4Ysw0YVAM2VwbCPtbXVXaa8jSxvRwJfjtiRK2dkhGi_ETYZuaP9pM/s1600/DSCN9027.JPG
Mzee Shem Karenga akiwa jukwaani enzi za uhai wake
Kwa mujibu wa Kiongozi wa bendi ya African Minofu, Joseph Matei, marehemu aliugua siku chache zilizopita kabla ya kukumbwa na mauti na kwamba anatarajiwa kuzikwa leo kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar. 
Gwiji hilo Shem Karenga alizaliwa mwaka 1950, Bangwe, Kigoma na kupata elimu ya msingi katika shule ya kimishionari ya Kihezya kuanzia mwaka 1957 hadi mwaka 1964.  
Mwaka 1964 alijiunga na bendi ya Lake Tanganyika Jazz ambayo maskani yake yalikuwa mjini Kigoma. Mwaka 1972, aliitwa kwenye bendi ya Tabora Jazz kama mwanamuziki mwenye kipaji cha utunzi, mwimbaji na mpigaji wa gitaa la Solo. 
Mwaka 1983 alijiengua kutoka Tabora Jazz na kusimama kabisa kujihusisha na muziki, ambako kilichofuatia ilikuwa ni kifo cha bendi hiyo. 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivfVcUbJ3EtZF8fu2-MOehiBeFARjSF0W4Bund8Mk9Yk8pE7YiR7QXlX-T5zL8HBGKVAWTiHGmYR_8WHcw-M_xFKwTjYZTAtr96hyO37PwP9VLqzVfNV2QuAe7U-QsKxqGDtsRQHvaCdA/s1600/PICTURE+07.jpg
Shem Karenga akicharaza gitaa na kuimba kiasi cha kumkuna Mayaula Mayoni (kulia)
Mwaka 1990 aliondoka Tabora na kutua jijini Dar es Salaam. Mwaka 1990 alijiunga na MK Beats. 
Mwaka 1995, MK Beats ilisambaratika, ambako mwaka uliofuata, yaani 1996 alianzisha bendi ya Tabora Jazz Star kwa kushirikiana na Ibrahim Didi. Mpaka mauti yanamfika, Shem Karenga Mkurugenzi Msaidizi katika Bendi ya Tabora Jazz Star ambapo Mkurugenzi Mkuu ni Ibrahim Didi. Moja ya vibao vyake viliwahi kunyakuliwa na kurejewa na kundi la Sokousou Stars kuonyesha alivyokuwa mkali.
MICHARAZO inatoa pole kwa ndugu, jamaa na familia ya marehemu pamoja na wanamuziki na wadau wote wa fani ya muziki nchini kwa msiba huo.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU Mahali PEMA PEPONI.

Jennifer Mgendi 'aifumua' Shelina

Muimbaji na muigizaji filamu, Jennifer Mgendi
MUIMBAJI nyota wa muziki wa Injili nchini ambaye pia ni mtayarishaji na muigizaji wa filamu, Jennifer Mgendi amesema anaifanyia marekebisho filamu yake mpya ya 'Shelina' kuwa filamu fupi ya mfumo wa wimbo ili kuzidi kuwapa raha mashabiki wake.
Akizungumza na MICHARAZO, Jennifer alisema ameona ni vema kuibadilisha 'Shelina' kuwa katika mfumo mwingine ili kuwapa ladha tofauti mashabiki wake ambao wamemzoea katika kazi nyingine alizowahi kuzitoa nyuma.
Jennifer alisema atautumia wimbo wake uitwao 'Kaa Chonjo'.
"Nimeamua kufanyia marekebisho filamu yangu ya 'Shelina' na sasa naitengeneza kama filamu fupi ya mfumo wa wimbo, nikiutumia wimbo wa 'Kaa Chonjo," alisema Jennifer anayejiandaa kuachia albamu yake ya nane iitwayo 'Wema ni Akiba'.
Filamu hiyo ya 'Shelina' inakuja wakati akitamba na kazi yake iitwayo 'Mama Mkwe' ambayo inaendelea kusumbua sokoni.
Mbali na 'Mama Mkwe', Jennifer pia amewahi kutamba na filamu nyingine kama  'Chai ya Moto', 'Joto la Roho', 'Teke la Mama', na 'Pigo la Faraja'.

Salha wa Hammer avunja ukimya na Kishtobe cha Mtaa

MUIMBAJI nyota wa muziki wa taarab, Salha Abdallah amevunja ukimya baada ya kutoka kwenye likizo ya uzazi kwa kuibuka na wimbo uitwao 'Kishtobe cha Mtaa' uliopo kwenye albamu mpya ya kundi la Five Star Modern.
Akizungumza na MICHARAZO, Salha maarufu kama 'Salha wa Hammer' alisema wimbo huo ni miongoni mwa nyimbo tano zitakazokuwa katika albamu yao itakayozinduliwa Ijumaa wiki hii.
Salha alisema wimbo huo ni wa kwanza kwake tangu alipoenda likizo ya uzazi na kuwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye uzinduzi huo ili kupata uhondo toka kwake na wanamuziki wote wa Five Star.
"Baada ya likizo ya uzazi, hatimaye natarajia kuanza kazi na wimbo wa 'Kishtobe cha Mtaa' ambao nimekiimba mwanzo mwisho nikisaidiana na akina Mwape Kibwana na wengine kitakuwa kwenye albamu itakayozinduliwa Ijumaa," alisema Salha.
Mbali na wimbo huo wa Salha, albamu hiyo ya 'Kichambo Kinakuhusu' ina nyimbo za 'Big Up Dear', 'Ubaya Hauna Soko', 'Sina Gubu Nina Sababu' na 'Kichambo Kinakuhusu' wenyewe.

Everton yaiangamiza QPR, Redknapp maji ya shingo!

QPR striker Bobby Zamora scores against Everton
Bobby Zamora akimtungia Howard
Everton midfielder Ross Barkley
Barkley akifunga bao la kuongoza la Everton kwa shuti kali
KLABU ya Everton usiku wa kuamkia leo wamepata ushindi mwepesi nyumbani baada ya kuifumua QPr mabao 3-1 na kuzidi kukwea katika Ligi Kuu ya England inayozidi kushika kasi.
Ross Barkley alifunga kwa shuti kabla la mita 20 katika dakika ya 33, kabla ya Kevin Mirallas kufungwa kwa mpira wa adhabu ndogo katika dakika ya 43 na mpira wa kichwa wa Steven Naismith kwenye dakika ya 53 yalitosha kuwaangamiza QPR inayonolewa na kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur, Harry Redknapp.
QPR ambao kipigo hicho kilikuwa cha nane ugenini katika ligi ya msimu huu, ilipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 80 kupitia Bobby Zamora aliyeuwahi mpira uliotemwa na kipa Tim Howard.
Ushindi huo umeifanya Everton kuitambuka wapinzani wao wa jadi Liverpool wsanaolingana nao pointi 21 na kukaa nafasi ya 10 huku Reds wakiporomoka hadi nafasi ya 11. wakati QPR wamesalia katika nafasi ya tatu toka mkiani wakiwa na pointi 14, nne zaidi ya timu inayoshilikia mkia ya Leicester City.

Manchester Utd yatabiriwa kutwaa ubingwa wa England

http://i.huffpost.com/gen/1226648/thumbs/o-PHIL-NEVILLE-570.jpg?6
Phil Neville enzi akiichezea Manchester United kabla ya kutimkia Everton
USHINDI wa mara sita mfululizo katika mechi zake za Ligi Kuu ya England iliyopata klabu ya Manchester United kumetajwa ni dalili za kurejea kwenye 'fomu' yake na kutabiriwa kutwaa ubingwa wa msimu huu.
Nyota na kocha msaidizi wa zamani wa klabu hiyo, Phil Neville, amenukuliwa akisema kwamba klabu hiyo ina nafasi kubwa ya kuwa mabingwa wa England baada ya kutulia kutoka kwenye misukosuko ya msimu msimu uliopita.
"Ndiyo wanaweza'' alisema Neville aliyenyakua mataji sita ya Ligi Kuu ya England akiwa kama mchezaji kabla ya kuangukia kuwa miongoni mwa makocha msaidizi chini ya David Moyes aliyetimuliwa.
 "Wachezaji wanaamini wanaweza kutwaa taji na hilo Louis Van Gaal anaweza kulifanya," alisema Neville.
Kauli ya Neville imekuja baada ya Manchester United kupata ushindi wa sita mfululizo kwa kuifumua Liverpool kwa mabao 3-0 katika pambano lililochezwa siku ya Jumapili.
Kabla ya hapo klabu hiyo ilionekana kuyumba kiasi cha mashabiki kuanza kupoteza imani kwa Van Gaal kabla ya kocha huyo kuwatuliza na kuanza kuwapa raha kwa kushinda mfululizo.
Mechi hizo sita za Manchester United iliyoshinda mfululizo ni hizo hapo chini:

8 November:  Crystal Palace 1-0 (nyumbani)
22 November: Arsenal 2-1 (ugenini)
29 November: Hull 3-0 (nyumbani)
2 December: Stoke 2-1 (nyumbani)
8 December: Southampton 2-1 (ugenini)
14 December: Liverpool 3-0 (nyumbani)

Nyota Manchester Utd katika 'kashfa' ya rushwa Hispania

http://www4.pictures.zimbio.com/gi/Manchester+United+v+Valencia+ODBuEmnisftx.jpg
Ander Herrera anayetuhumiwa kwa upangaji matokeo ya mechi ya La Liga 2011
http://www4.pictures.zimbio.com/gi/Jefferson+Montero+Exeter+City+v+Swansea+City+Rttkn623zmEl.jpg
Montero naye yumo katika mkumbo huo
http://static.goal.com/187500/187540_heroa.jpg
Nahodha Gabi,  naye anatuhumiwa
http://static.weltsport.net/picmon/e9/dVK_baa3z_l.jpg
Kocha Aguirre

KIUNGO nyota wa Manchester United, Ander Herrera na nahodha wa Atletico Madrid, Gabi ni miongoni mwa wachezaji wanaochunguzwa kwa kujihusisha na tuhuma za upangaji wa matokeo ya mechi ya kufungia msimu wa 2010-2011 wa Ligi Kuu ya Hispania.
Wengine waliohusishwa na kadhia hiyo ni Kocha wa zamani wa Real Zaragoza anayefundisha timu ya taifa ya Japan Javier Aguirre na mchezaji wa Swansea City, Jefferson Montero.
Kwa mujibu wa BBC, Mwendesha Mashtaka wa Idara ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Hispania Alejandro Luzon, ameiagiza Mahakama kumchunguza kocha wa zamani wa klabu ya Real Zaragoza na baadhi ya wachezaji kutokana na tuhuma za kudaiwa kuuza mchezo dhidi ya Levante.
Katika pambano hilo la kufungia msimu Zaragoza ilishinda mchezo huo kwa mabao 2-1 na kuepuka kushuka daraja, lakini sasa imebainika kuwa matokeo hayo yalipangwa baada ya kutembezwa mlungula.
Upande wa mashitaka uliowasilisha mashtaka yake katika Mahakama mjini Valencia jana Jumatatu, unadai kuwa watuhumiwa wanahusishwa na rushwa ya dola million mbili. 
Baadhi ya wachezaji wanaotuhumiwa katika kashfa hiyo ni Kiungo wa Manchester United aliyewahi kukipiga Zaragoza wakati wa mchezo huo kabla ya kuhamia Athletico Bilbao, Ander Herrera, anayeichezea Manchester United, nahodha wa Atletico Madrid, Gabi, Montero na Javier Aguirre.
Inadaiwa kuwa wachezaji wa Lavante walishikishwa fedha ili kupoteza pambano hilo na kuinusuru Zaragoza isishuke daraja katika pambano la Mei 21, 2011.
Jumla ya watu 41 wakiwamo wachezaji, makocha na wakurugezi wa timu hizo mbili wamehusishwa katika upangwaji huo wa matokeo ya pambano hilo.

Kumekucha! Maximo atupiwa virago kama Brandts, Pluijm arejeshwa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirHsHAOLesgeko6449ITJAGxd3GFzvxJ4YBsnuG54Z_IHmqZpPn0Rcn5HtpJ20BHmV_Xmm3ra1JRpa1YBgtVVw-KSoIGH0WZJvcJpteX_m9EYMWT_OK1dT-MVqydunhScqSyS6RsOndkH5/s1600/DSC_0306.JPG
Marcio Maximo na msaidizi wake Leonardo Neiva wakati wakiinoa Yanga

KAMA ilivyokuwa kwa kocha Ernie Brandts aliyetimuliwa baada ya Yanga kufungwa na Simba kwenye mchezo wa 'bonanza' wa Nani Mtani Jembe, hali hiyo imemkuta Marcio Maximo.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars kutoka Brazil ametimuliwa Yanga baada ya kipigo cha mabao 2-0 katika pambano la Nani Mtani Jembe-2.
Taarifa ambazo ni za uhakika toka ndani ya Yanga zinasema kuwa, kocha Maximo amepewa mkono wa kwaheri na nafasi yake inarudi kwa aliyekuwa kocgha wa timu hiyo  Hans Van Der Pluijm.
Mmoja wa viongozi wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga amesema, Maximo ataondoka nchini ndani ya siku tatu baada ya kukubaliana na uongozi.  
"Si kwamba amefukuzwa, lakini ni makubaliano kwamba anaondoka.  
"Ni kweli, lakini msitake kulikuza hili jambo ionekane kama tumemfukuza," aliuliza na alipotakiwa kujua mrithi ni nani, alikataa kusema.  
Hata hivyo ni kwamba Maximo amepewa mkono wa KWAHERI sambamba na kiungo aliyekuja naye toka kwao, Emerson Oliveira ambaye inaelezwa amekosa ITC japo ukweli ni kwamba ameonekana ni bomu.
Yanga ilimfurusha Brandt na wasaidizi wake, Fred Felix Minziro na Razack Ssiwa baada ya timu yao kulala mabao 3-1 na safari hii Maximo anaondoka na wasaidizi wake akiwamo Mbrazil mwenzake Leonardo Neiva ambaye alimleta baada ya kusaini mkataba.

Monday, December 15, 2014

Ratiba ya Ligi ya Mabingwa hii hapa


KLABU ya Manchester City imepangwa kucheza na Barcelona katika hatua ya mtoano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika ratiba iliyopangwa leo jijini Nyon, Ufaransa. 
Timu hizo zilikutana pia katika hatua hiyo msimu uliopita ambapo Barcelona waliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4-1 na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. 
Timu zingine ambazo zilikutana msimu uliopita katika hatua hiyo ni pamoja na Paris Saint-Germain ambao watakwaana tena na Chelsea msimu huu. 
Wengine ni mabingwa watetezi Real Madrid ambao watakwaana na Schalke wakati mshindi wa pili msimu uliopita Atletico Madrid wao wataivaa Bayer Leverkusen. 
Mabingwa wa Serie A Juventus wao watawakaribisha Borussia Dortmund huku mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakicheza na Shakhtar Donetski, Arsenal wenyewe watacheza na Monaco na Porto watakwaana na FC Basel. 
Timu ambazo zilimaliza katika nafasi ya pili katika hatua ya makundi zitacheza mechi zao za kwanza nyumbani kati ya Februari 17/18 na 24/25 huku zile za marudiano zikitarajiwa kuchezwa kati ya Machi 10/11 na 17/18.

Liverpool wapewa Waturuki, Ligi Ndogo ya Ulaya

http://www1.pictures.zimbio.com/gi/Andre+Wisdom+BSC+Young+Boys+v+Liverpool+FC+DEcmweK_E8Sl.jpg 
KLABU ya Liverpool ambayo ilichemsha katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepewa timu ya  Besiktas ya Uturuki katika hatua ya timu 32 bora ya michuano hiyo kwenye ratiba iliyopangwa leo. 
Timu zingine zilizoondoshwa katika michuano hiyo ni pamoja na Ajax Amsterdam ambao wamepangiwa kucheza na Legia Warsaw, Anderlecht wao wakipangwa na Dinamo Moscow huku Sporting Lisbon wao wakiwa wenyeji wa Wolfsburg. 
Katika mechi zingine zitazikutanisha timu za AS Roma dhidi ya Feyenoord, Inter Milan wao watacheza na Celtic, Tottenham Hotspurs dhidi ya Fiorentina wakati Athletic Bilbao wao watakuwa wenyeji wa Torino. 
Mechi za mkondo wa kwanza za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa Februari 19 huku zile za marudian zikitarajiw akuchezwa Februari 26.

Breaking News! Amissi Tambwe atua Yanga

tambwe yanga
HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa dakika chache zilizopita ni kwamba klabu ya Yanga imemsajili mshambuliaji wa Simba aliyeachwa Amisi Tambwe .
Yanga imemsajili Tambwe dakika chache zilizopita ambapo anakuja kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Emerson Oliveira wa Brazil aliyetemwa kwa kukosa ITC.
Tambwe ametua Yanga ikiwa ni siku chache baada ya Mganda Hamis Kiiza kuachwa na klabu hiyo na kukimbilia URA ya Uganda baada ya Kpeh Seen Sherman wa Liberia kupewa kandarasi ya kuichezea timu hiyo.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe amesajiliwa na Yanga baada ya kuachwa na Simba.
Tambwe alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita ambapo alifunga mabao 19 kwenye ligi lakini alishindwa kuwika msimu huu baada ya kutopewa nafasi ya kutosha chini ya Patrick Phiri.
Simba imemuacha Tambwe baada ya kumsajili Danny Serunkuma toka Gor Mahia ya nchini Kenya .
Yanga imekamilisha usajili huu saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa leo na TFF.

Sunday, December 14, 2014

Spurs yaitambia Swansea City kwao, yachupa EPL

Harry Kane clinches his first in celebration after putting Tottenham Hotspur 1-0 ahead against Swansea City at the Liberty Stadium
Harry Kane akifunga bao la lkuongoza la Spurs
Harry Kane
Eriksen akishangilia bao lililowapa Spurs ushindi wa 2-1 nyumbani kwa Swansea City
BAO la dakika za jioni lililofungwa na Christian Eriksen lilitosha kuwapa ushindi muhimu Tottenham Hotspur katika mfululizo wsa Ligi Kuu ya England.
Eriksen aliyehusika pia katika kutengeneza bao la kuongoza la Spurs lililowekwa kimiani kwa kichwa na Harry Kane katika dakika ya nne tu ya mchezo huo, alilifunga katika dakika ya 89 na kuifanya timu yake kuendeleza ubabe kwa Swansea City waliokuwa nyumbani kwao.
Pambano hilo lilionekana kama lingeisha kwa sare ya 1-1 baada ya wenyeji kufunga bao la kusawazisha dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kupitia Winfried Bony.
Hata hivyo vijana wa Maurico Pochettino walicharuka na kusaka bao hilo muhimu lililofungwa na Eriksen na kuifanya Spurs kuchuopa hadi nafasi ya saba kwa kufikisha pointi 24 wakiporomosha Newcastle United ambayo jana ilinyukwa mabao 4-1 na Arsenal.
Ligi hiyo ya England inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo mmoja tu kati ya Everton itakayoikaribisha QPR kwenye uwanja wa Goodson Park.

Simba yazidi kusajili wapya, Tambwe byebye!


seru
Simon Sserunkuma akisaini fomu za Simba
KLABU ya Simba imekatisha mkataba na wachezaji wake wawili wa kimataifa wote raia wa Burundi, ambao ni Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania, Mshambuliaji Amissi Tambwe na Kiungo Pierre Kwizera, siku moja tangu Simba kuifunga Yanga 2-0 katika pambano la Nani Mtani Jembe.
musheed
Mursheed akisaini mkataba wake leo
Simba, imevunja mkataba na wachezaji hao ili ipate nafasi ya kuwasajili nyota wa Kiganda, mshambuliaji Simon Sserunkuma na beki Juuko Murushid, ambao wamesanishwa mikataba yao leo.
Simon maarufu kama Sam Sserunkuma na Juuko Murushid, waliichezea Simba dhidi ya Yanga jana katika uwanja wa Taifa Jijini Dar-es-salaam, na wote walionesha uwezo mkubwa na kuisaidia Simba kupata ushindi huo wa mabao mawili dhidi ya Yanga.
Baada ya usajili huu sasa wachezaji wa kigeni kutoka Uganda wanafikia watano katika klabu hiyo, wakiongozwa na beki Joseph Owino, mshambuliaji Emanuel Okwi, Dan Sserunkuma, Simon Sserunkuma na Juuko Murushid.

Hata hivyo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Simba, Zakaria HansPoppe kuwa Dan amepewa nafasi ya kupunguza kilo alizonazo.

Iran kuja kukipiga na Taifa Stars

http://www.igrooveradio.com/wp-content/uploads/2014/06/iran-national-football-team-inter-263366.jpg
Kikosi cha timu ya taifa yua Iran inayokuja kucheza na Tanzania
SHIRIKISHO la Soka la Iran, limetangaza kuwa timu ya taifa ya nchi hiyo itaweka kambi yake nchi Afrika Kusini huku wakicheza mechi tatu za kirafiki ili kujiandaa na michuano ya Kombe la Asia mwezi ujao. Kocha wa timu hiyo Carlos Queiroz ambaye aliivusha katika mzunguko wa pili katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil amechukua jumla ya wachezaji 21 katika safari yake hiyo. 
Katika kambi hiyo ya wiki mbili, Iran inatarajia kucheza mechi za kirafiki na Afrika Kusini wenyewe, Guatemala na Tanzania kabla ya kurejea Iran na kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Palestina Desemba 28 mwaka huu. 
Michuano ya Kombe la Asia inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 9 mwakani huku Iran ikipangwa kucheza na Bahrain, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE katika hatua za makundi.
Hata hivyo Shirikisho la Soka Tanzania, TFF bado haijaweka bayana juu ya kuwepo kwa pambano hilo ambalo la kirafiki la kimataifa.

Arsene Wenger awashukuru mashabiki

http://www.kooxaha.com/wp-content/uploads/2014/10/weng-kooxaha1.jpgKOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amewashukuru mashabiki waliokuwa wakiimba jina lake wakati timu hiyo iliporejesha makali yake ya ushindi katika Ligi Kuu.
Wenger, 65 alishambuliwa kwa kuzomewa na kutukanwa na mashabiki wa timu hiyo baada ya kipigo cha mabao 3-2 kutoka Stoke City wiki iliyopita.
Lakini katika mchezo dhidi ya Newcastle United uliochezwa jana na Arsenal walishinda mabao 4-1, mashabiki hao walisikika wakiimba nyimbo za kumsifu kocha huyo.
Akihojiwa na waandishi wa habar, Wenger amesema kazi yao ni kuhakikisha wanashinda mechi za soka na pindi wasipofanya hivyo huwa anawaelewa kwani hawafurahishwi.
Arsenal bado wako nyuma ya vinara Chelsea kwa alama 13 lakini ushindi wa jana ukichanganya na ule wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray kidogo umepandisha morali ya timu baada ya kipigo dhidi ya Stoke.
Pia huenda ikatuliza munkari ya mashabiki hao waliokerwa na kauli ya kocha huyo kwamba huenda asingefanya usajili wowote katika usajili wa mwezi Januari.

Ruvu yanyakua mwingine, kukipiga na Friends Rangers kesho

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/11/MWOMBEKI.png
Betram Mwombeki aliyekuwa akiichezea Simba msimu uliopita ni mmoja ya walionyakuliwa na Ruvu Shooting
KLABU ya Ruvu Shooting ambaye kesho inatarajiwa kushuka uwanja wa Shule ya Mwalimu Nyerere (Makurumla) katika mechi ya kirafiki, imefanikiwa kusajili wachezaji wengine wawili akiwamo nyota wa zamani wa Chemlin na Sony Sugar, Mwita Semlonge John aliyetokea Toto Africans.
Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire alisema kuwa mchezaji huyo wa safu ya ushambuliaji ni wa tatu baada ya Betram Mwombeki na Yahya Tumbo.
Bwire aliongeza kuwa pia wamempandisha mchezaji mmoja toka timu ya vijana U20, Ally Yusuph kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao ambacho kesho kitawapima vifaa hivyo kwa kuumana na Friends Rangers katika pambano la kirafiki.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa kali kutokana na ukweli Friends imefanya usajili wa kuvutia katika dirisha dogo kwa kuwanyakua Haruna Moshi 'Boban', Amir Maftah na wengine kitu kinachofanya mtanange huo usio wa kitoto.

Mashetani Wekundu waifumua Liverpool 3-0

Wayne Rooney, Man Utd
Rooney akifunga bao la kuongoza la Manchester United
Robin van Persie, Man Utd
Weweeeee! van Persie akishangalia bao lake na wachezaji wenzake
Mario Balotelli, Liverpool
Mario Balotelli akionyeshwa kadi ya njano, mshambuliaji huyo aliyekuwa majeruhi alichangamsha pambano hilo baada ya kuingia akitoka benchi, ingawa aliendelea kukosa mabao ya wazi mbele ya De Gea
JAHAZI la Liverpool limezidi kwenda mrama baada ya kutandikwa mabao 3-0 na Manchester United katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England.
Ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford, Mashetani Wekundu walianza kuiadhibu Liverpool iliyopo chini ya kocha Branden Rodgers katika dakika ya 12 wakati nahodha Wayne Rooney kuandika bao akimalizia kazi ya Valencia.
Dakika nne kabla ya mapumziko Manchester iliongeza bao la pili baada ya Juan Mata kumalizia kazi nzuri ya Robin van Persie.
Bao lililowanyong'onyesha 'vijogoo' vya Anfield, liliwekwa kimiani na van Persie akimalizia pasi murua kutoka kwa Juan Mata.na kuifanya Mashetani Wekundu kufikisha pointi 31 na kung'ang'ania nafasi ya tatu nyuma ya Chelsea inayoongoza kwa pointi 39 na Manchester City yenye pointi 36.
Hivi sasa dimbani Swansesa Cit inaumana na Tottenham Hotspur na wageni Spurs wako mbele kwa bao 1-0.

Azam yaanza vibaya Uganda, yanyakua kifaa kipya


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania, Azam imeanza vibaya ziara yao nchini Uganda baada ya kufumuliwa mabao 3-2 na SC Villa.
Kwa mujibu wa Meneja wa Azam, Jemedari Said akihojiwa na kituo kimoja cha redio kutoka Kampala, alisema kuwa katika mechi hiyo Azam walienda mapumziko wakiwa sare ya bao 1-1.
Jemedari alisema walianza kufunga wao bao dakika za mapema kupitia Mrundi Didier kavumbagu kabla ya wenyeji kusawazisha na kipindi cha pili waliporejea Azam waliongeza bao la pili dakika hya 65.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Khamis Mcha 'Vialli' kabla ya wenyeji kutumia dakika 10 za mwisho za pambano hilo kurejesha bao la pili na kuongeza bao la ushindi katika dakika za 81 na 83.
Meneja huyo alisema kuwa Azam itashuka tena dimbani siku ya Jumatano kwa kuumana na URA, pambano likichezwa kwenye uwanja wa KCC, mjini Kampala.
Katika hatua nyingine klabu hiyo imemsajili winga machachari wa KCCA,  Brian Majwega mkataba wa miaka miwili baada ya kocha Joseph Omog kuvutiwa naye.
Majwega anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Azam FC katika dirisha dogo baada ya beki Serge Wawa Pascal kutoka Ivory Coast, aliyekuwa anacheza El Merreikh ya Sudan na Amri Kiemba aliyekuwa Simba SC, ambaye amesainiwa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.    

Huyu ndiye Awadh Juma 'Maniche' aliyewaliza Yanga mara mbili NMJ

Awadh Juma (kushoto) akipambana katika NMJ-2 jana ambapo Simba ilishinda mabao 2-0, moja likifungwa naye
Awadh Juma alivyokuwa akishughulika jana wakati wa pambano la NMJ-2
http://api.ning.com/files/7TcBzbi1eXpJR97d5lfhSWcQtc2ahMajCip36ZbbxLxyrWWQt56ydgr6kDAFSd9mG53EzvsTkDVjWGcWBg7FRE4MWF0UPSdm/KASEJA7.JPG
Awadh Juma alivyomtesha Kaseja katika NMJ-1
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRQqeYRvyVSRUl8NThI45bfeCdna0GQhYraS22s2Mv2wz_j1xTJP7fN1ykK1XpqT4AB_HWD3931ii_3f5SSeyFHMTACxuGpUXbmV-tGmhApgYS9FzJiAM_5FKW82v4BIc3Wfs_giBhRmTT/s1600/DSC00998.JPG
Awadh Juma akiwa na Jonas Mkude
KATIKA pambano la Nani Mtani Jembe lililochezwa mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa, alikuwa mmoja wa wafungaji wa mabo matatu yaliyoizamisha Yanga mbele ya Simba akiwa ndiyo kwanza ametoka kusajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar.Mara baada ya pambano hilo ambalo Yanga walilala mabao 3-1, Awadh Juma maarufu kama 'Maniche' alizungumza na MICHARAZO katika mahojiano maalum na kudai kuwa alijisikia furaha kubwa kucheza mechi yake ya kwanza kubwa inayohusisha watani wa jadi wa soka nchini, Simba na Yanga na kufunga bao.
Maniche alisema lililomsisimua zaidi ni kitendo cha kumzidi ujanja kipa bora nchini na Afrika Mashariki, Juma Kaseja.
Kiungo mshambuliaji huyo alifunga bao la tatu lililo gumzo kwa sasa na lililomletea kizaazaa kipa Kaseja akisakamwa akidaiwa 'aliiuza' Yanga kwa klabu yake ya zamani.
wakati mashabiki wakiamini labda alibahatisha tu kwenye mchezo huo, Maniche kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa ana bahati ya michuano hiyo ya Nani Mtani Jembe baada ya jana kufunga bao la kuongoza la Simba lililoisaidia kupata ushindi wa pili mfululizo dhidi ya Yanga.
Mchezaji huyo alifunga bao la kwanza katika dakika ya 31 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa kizembe na kipa Deogratius Munishi 'Dida' na yeye kuukwamisha kulia mwa lango ya Yanga lililokuwa likimdokolea macho.
Bao hilo lilitokana na mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa kiufundi na Mganda Emmanuel Okwi na kuchangia kummsha hamasa ya vijana wa Msimbazi walioandika bao la pili dakika chache kabla ya mapumziko kupitia kwa Elias Maguli aliyeuwahi mpira wake wa kichwa uliogonga besela na kurudi kwake.
Maniche aliyemtetea Kaseja baada ya kumtungua mwaka jana, alisema amefurahi sana kufunga tena kwenye michuano hiyo na kusaidia Simba kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Alisema kuwa kujiamini na kuwa katika kikosi bora chini ya kocha Patrick Phiri ndiyo siri ya ushindi wa timu yao na sababu ya yeye kuendeleza kuwaliza Yanga.
Mchezaji huyo anadai alichofanya katika mechi hiyo ya Nani Mtani Jembe, ni sehemu tu ya ujuzi alionao katika soka na kuwaahidi wadau wa Simba kusubiri kupata mambo makubwa wakati ngwe Ligi Kuu Tanzania Bara itakapoendelea tena kuanzia Desemba 26.
Kiungo huyo aliyezaliwa miaka 22 visiwani Zanzibar akiwa mtoto wa pili kati ya saba wa familia yao anasema angependa kufanya makubwa katika ligi ili aweze kupata nafasi ya kujitangaza katika soka la kimataifa kupitia Simba.
Nyota huyo wa zamani wa klabu za Jang'ombe, New National, Leba, Tanzania Soccer Academy (TSA) kabla ya kutua Mtibwa Sugar miaka mitatu iliyopita, anasema anatamani kucheza soka la kulipwa Ulaya.
Maniche anayependa kula ndizi kwa nyama na juisi halisi ni shabiki mkubwa wa klabu za Barcelona na Manchester United.
Juu ya pambano analokumbuka kichwani mwake ni lile la Zanzibar Heroes dhidi ya Sudan katika michuano ya Chalenji ya mwaka 2009.
"Naikumbuka mechi hiyo kwa vile ilikuwa ya kwanza kwa michuano ya Kombe la Chalenji," anasema.
Mchezaji huyo anayetaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kurekebisha mfumo wa ligi na kuongeza mashindano mengi ili kuwapa nafasi wachezaji kukuza viwango vyao.
"Kuwepo kwa michuano mingi kama ile ya Super8  itawasaidia wachezaji, pia mfumo wa ligi ubadilishwe kwani unafanya wachezaji wawe mapumziko muda mrefu bila sababu," anasema.
Maniche aliyevutiwa na kiungo nyota wa zamani wa Tanzania, Shekhan Rashid, japo kwa sasa anamzimia kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima, anasema  kubadilishwa mfumo wa soka nchini ni 'muarobaini' wa mafanikio ya Taifa Stars.
Anasema Stars inaangushwa na mambo madogo ambayo yakirekebishwa  huenda ikaifanya timu hiyo ikatamba kama mataifa mengine, huku akiwataka wachezaji wenzake kujituma na kuzingatia nidhamu na miiko ya soka.
Juu ya tukio la furaha Awadh anasema ni kitendo cha kusajiliwa na Simba na anahuzunishwa na tukio la ajabu lililowahi kumpata wakati akiwa uwanja wa Ndege kuelekea Thailand kucheza soka la kulipwa bada ya pasi yake ya kusafiria kushindwa kusoma kwenye mitando na kukwama kuondoka.
"Yaani ni kama miujiza, nilifaulu majaribio yangu ya soka la kulipwa Thailand, nikarejea kusubiri kutumiwa tiketi nikaanze kuitumikia, siku ikawadiwa tiketi ikaja sasa nikiwa uwanja wa ndege amini usiamini pasipoti yangu iligoma kusoma na kukwama safari," anasema.
"Mpaka leo nashindwa kujua ilitokana na nini, ila sijakata tamaa Mungu atanisaidia nitatimiza ndoto za kucheza soka la kulipwa," anaongeza.
Awadh Juma Issa, alianza kucheza soka la chandimu tangu akisoma Shule ya Msingi Jang'ombe na kuendelea wakati akiwa Sekondari ya Mtakuja aliposoma hadi kidato cha pili na kuhamia Makongo baada ya kumvutia Kanali Mstaafu Idd Kipingu kupitia michuano ya shule visiwani Zanzibar.
Kabla ya kuja Makongo alishaanza kung'ara katika soka kupitia Jang'ombe, New National na Leba Fc, na alipokuwa Makongo alichaguliwa TSA kabla ya Mtibwa kumchukua na hivi karibuni kutua Simba.

Droo ya 16 Bora kesho, Arsenal roho juu!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJm6uGPnfQYuZOYeIc6TREJk992xYdYmz-I1iHvSBEMs3xq5IGc3xOP-kQuRWo5qBaC0NBAsixBOpvEcmcMhO-kwjhkK2I3QiWKHcqNck2Wsbas89EOkdxrxStVgX2ThqFHg5pkmFznNXU/s1600/UEFA-Champions-League-Draw-Group-Stages.jpgRATIBA ya Mtoano wa hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kupangwa kesho ambapo itafahamika klabu gani itakutana na nani katika hatua hiyo, huku presha kubwa ikiwa kwa klabu ya Arsenal ambayo ilimaliza nafasi ya pili katika kundi D nyuma ya Borussia Dortmund.
Kwa mujibu wa upangwaji wa hatua hiyo timu zilizoongoza hatua ya makundi zitatangulia kwenye vyungu kisha kutafutwa timu za kucheza nazo miongoni mwa timu nane zilizomaliza nafasi ya pili, huku kukiwa na hatari kwa Arsenal kuangukia tena mikononi mwa kigogo kati ya Real Madrid, Barcelona au Bayern Munich ambao zimekuwa zikimnyima raha kocha Arsene Wenger kiasi cha kulaumu sare ya 3-3 iliyopata kwa Dortmund na kumweka katika karinyekarinye hiyo.
Jumla ya timu 16 zimefaulu hatua hiyo baada ya mie4zi kadhaa ya kuchuana hatua ya awali na makundi, Real Madrid wakiendeleza rekodi ya kushinda mechi zake kwa mwaka wa pili mfululizo kwa asilimia 100 na kuongoza kundi B.
Mabingwa watetezi hao , Atletico Madrid, Fc Barcelona, Monaco, Chelsea, Bayern Munich, Porto na Dortmund ndiyo walioibuka kinara wa makundi yao, wakati timu za  Manchester City, Arsenal , Bayer Liverkursen, Shalke 04, Shakhtar Donetski, PSG, Juventus  na Basel wakimaliza nafasi ya pili.
Timu zilizomaliza kwenye nafasi ya tatu zenyewe zimeangukia kwenye michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya ambayo pia droo yake inatarajiwa kupangwa kesho.
Timu zilizoangukia huko kutoka Ligi ya Mabingwa ni pamoja na Olympiakos Pirates, Liverpool, Zenit Petersburg, AS Roma, Anderlecht, Ajax Amsterdam, Sporting Lisbon na Athletic Bilbao.
Unadhani unaweza kutabiri nani na nani watakaokutana katika hatua hiyo ya 16 Bora ya Mabingwa Ulaya kabla ya kuja kushuhudia Fainali baadaye Juni 6, 2015?

HATARI! Watu 6 wafa kwa kuchinjwa kama Kuku Bukoba

Kanisani alipouawa mwalimu Ng"wandu
KWA kipindi cha miezi miwili tu, kuanzia Octoba 9 hadi Desemba 4 mwaka huu, ambapo jumla ya vijana  6 wameuawa katika mazingira ya kutatanisha,  watatu wamechinjwa katika kata ya Kitendaguro, 1 katika kata ya Rwamishenye, huku wawili wakichinjwa katika kata ya Kibeta ndani ya manispaa, huku wananchi wakishangaa ukimya wa mamlaka bila kuchukua hatua.

Tarehe 09 Oktoba, aliyeuawa mwalimu DIONIZ NGW’ANDU wa shule ya sekondari Kagemu, alipokuwa katika kanisa la PAGT, baada ya kukatwa kichwa na kitu chenye ncha kali, huku jamaa yake aliyekuwa mlinzi katika kanisa hilo siku hiyo akijulikana kwa jina mojala THEMISTOCRES akisalia na ulemavu wa maisha, kama alivyoeleza  mchungaji wa kanisa hilo FAUSTINE JOSEPH. 

Siku kati ya 5 au saba badaye, mwili wa kijana ambaye hakutambuliwa majina wala sura, ulikutwa umeharibiwa kwa kunyofolewa macho, huku ukitupwa kando mwa shamba la mmoja wa wakazi wa Kitendaguro, ambapo Anakret Laurent Kyaishozi miaka 30 alikuwa shuuda, aliueleza mtandao huu kuwa mwilihuoulichukuliwa na polisi mpaka sasa hawajajua ninikiliendelea.

Kando na hayo, familia ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka 37 Erick Kashaga akiacha mjane Sofia Mozes miaka 32 na watoto saba, imesalia katika mvutano mkubwa,na familia ya bwana Levocatus , ambaye mpaka sasa yuko mikononi mwa jeshi la polisi, huku jamaa zake wakielezwa kuwa uchunguzi unaendelea.
Kaburi la Mozes Kashaga
 Levocatusi ni kijana  mwenye umri wa miaka 33 huku akiwa na watoto watatu wawili wakizaliwa na mke wake wa Katoma walieachana, na mmoja akizaliwa na mke anayeishi naye Kitendaguro, Bi Ajat au Betrida mwenye umri wa miaka 32, alikamatwa baada ya kutajwa kuwa alitambuliwa na kijana aliyekuwa na marehemu wakatiwa tukio .
Mzee Rumumba akionesha eneo alipochinjwa Mozes
Mzee SILIDION RUMUMBA mwenye umri wa miaka 73,  ndiye mmiliki wa kilabu cha pombe, ambacho dakika za mwisho marehemu aliondoka hapo muda wa saa tano usiku, akiwa na jamaa zake wawili.

Ndani ya dk kama mbili baadaye, liyetajwa kwa jina moja tu la Eriki alirudi nyumbani kwa mzee SILIDION RUMUMBA akiwaeleza kuwa wamevamiwa na mtu ambaye alimtaja jina, huku akisema kuwa hana hakika kama watamkuta hai Kashaga, ilhali akitoa taarifa hizo kimyakimya, pasi na kupiga kelele wakati wa tukio,jambo ambalo linawashangaza wengi, kwasababu marehemu ameuawa karibu kabisa na makaazi ya watu.
Mama mzazi wa Mozes
Kando na maelezo hayo, nimetaka kusikiliza ushuuda wa Erick aliyethibitisha kuwa alishuudia mauaji hayo, lakini nyumbani kwaojamaa zakewalisema kuwa huwezi kumwona sababau wamemficha sehemu baada ya kutishiwa na mkewa mtuhumiwa.

Hayo yamesalia katika familia hizo ndani ya kata ya Kitendaguro, huku katika kata ya kibeta, lawama kubwa zikiangushwa kwa mamlaka, kuwa hawajaonesha juhudi zozote  baada ya kuuawa kijana GOODRUCK FRANCIS aliyekuwa na umri wa miaka 38, ambapo  taarifa za awali zinaonesha kuwa aliuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana, ikiwa ni kando kando mwa barabara ya mtaa wa Kibeta Amjuju.
Bi Stella Lenatus amesema amekata tama kwasababu tangu ahojiwe, ameenda kituoni kujua taarifa za mdodgo wake na kuambiwa asubiri walikuwa bize na kazi nyingine muhimu.
Hapo kustoto pichani ndipo aliuawa Gudrack eneo la Kibeta Anyama.
Sambamba na wanaouawa pasipo kutambulika majina na makwao ndani ya manispaa ya Bukoba, Ernest Kato ni kijana aliyeuawa mwezi novemba akiwa na miaka32,katika mtaa wa Bugezi kata Rwamishenye, majira ya usiku, na kutambulika asubuhi ya tarehe iliofuata kwa kukutwa amechinjwa, huku akiacha mjane na mtoto mmoja, ambaye hatahivyo  amekimbia kwa kuhofia naye kuawa.

Mmoja kati ya wanafamilia wa marehemu Ernest, ameomba jina lake lihifadhiwe, pamoja na kusema kuwa wanaishi kwa hofu kubwa kiasi cha kujipangia muda wa kurudi nyumbani mapema nyakati za usiku, na shughuli zimesimama.

Mauaji ya  mwisho hadi ninakamilisha makala haya, ni alivyouawa Joran Rutulaniisa, mkaazi wa Kibeta magoti, nilifika eneo la tukio muda mfupi tu baada ya polisi kuubeba mwili wake lakini taarifa za ndugu ambao hatahivyo wanahofu ya maisha yao, ni kuwa nduguyao  ameuawa kwa aina ile ile ya vifo vya kukatwa koromeo.
Marehemu Rutu enzi za uhai wake
Tetesi ambazo bado sijazithibisha, wananchi wanaofanya biashara ya senene, wamelazimika kuanza kujifunga vitu vigumu na tauro shingoni, kama taadhali watakapovamiwa.
Shangazi na mama mdogo wa marehemu kwenye kaburi la Rutu

Baba wa marehemu Rutulanisa
Mauaji nikitendo kisichokubalika kwa mwenyezi Mungu, jambo linalompa shekh mkuu wa mkoa wa Kagera Aruna Kichwabuta,kukemea hali hiyo katika mamlaka na wananchi.
Shekh mkuu wa mkoa, Haruna KICHWABUTA
Makala maalumu sehemu ya kwanza kuhusu mauaji hayo inaruka marudio leo saa moja jioni kupitia 88.5 Kasibante fm Bukoba.

 
Na Mwanaharakati