STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, November 6, 2013

MAAFA! WATU SITA WAUWAWA, 35 WALAZWA MAPIGANO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA MVOMERO

http://www.herald.co.zw/wp-content/uploads/2013/08/knife-blood.jpg
WATU sita wamefariki baadhi watatu wakiwa wamechinjwa, huku watu wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya katika mapigano ya kugombea ardhi kati ya wafugaji na wakulima huko kijiji cha Lukindo wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
Taarifa zinasema kuwa, chanzo cha vita hivyo ambavyo vimeleta athari kubwa ikiwemo familia kuparaganyika kwa hofu ya mapigano hayo ni mifugo ya wafungaji kuingia katika shamba moja la mkulima na kula mazao.
Baada ya kitendo hicho kilichotokea jana kinaelezwa kuwa, mifugo ya wafungaji ikikamatwa na wakulima na kisha kutaka walipwe fidia ya Sh Milioni 3 na kushindwa kupatikana muafaka kabla ya Polisi kuja kuingilia kati.
Hata hivyo mbele ya polisi makundi hayo mawili yanadaiwa yalianza kupigana mawe na kufanya Polisi walienda kusuluhisha kutimka na ugomvi huo kuibuka upya mapema leo na kusababisha maafa hayo makubwa.
Inaelezwa watu sita wanne wakiwa ni wakulima wameuwawa wengine wakichinjwa kama kuku na wawili wakiwa ni wafungaji na watu 35 wamejeruhiwa vibaya katika miili yao kwa silaha za jadi na kulazwa hospitali ya Bwagala huko huko Mvomero kwa sasa.
Jeshi la Polisi linaelezwa limefanikiwa kutuliza mapigano hayo, lakini watu waliojeruhiwa wakiwa hoi baadhi wakijeruhiwa vibaya na kulazimisha kufanyiwa upasuaji kunusuru maisha yao, ingawa mashuhuda wanasema huenda idadi ya vifo vilivyotokana na mapigano hayo vikaongezeka.

Yanga, Azam, Mbeya City nani kukaa kileleni kesho


Wageni Mbeya City kuweka rekodi kesho kwa Azam?

Mabingwa watetezi watamaliza vipi kesho kwa Oljoro?
PAZIA la duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara linatarajiwa kufungwa rasmi kesho kwa mechi tatu, huku mechi mbili kati ya hizo zitakuwa zikitupiwa macho ili kujua ni timu hiyo kati ya zilizopo kwenye Tatu Bora, Azam, Mbeya City na mabingwa watetezi watakaomaliza kileleni kuuaga mwaka 2013?
Yanga itaikaribisha Oljoro JKT kutoka Arusha kwenye uwanja wa Taifa, huku Azam na Mbeya zilizopo juu ya Yanga zikiumana zenyewe kwa wenyewe katika pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Chamazi.
Vinara Azam watafanya nini kesho kwa Mbeya City?
Matokeo yoyote katika mechi hizo mbili yatatoa nafasi kwa timu hizo tatu moja wapo kukaa kileleni kutokana na kuwa na pointi zisizopishana sana.
Azam wanaongoza msimamo kwa tofauti na yamabo ya kufungwa na kufunga licha ya kulingana pointi na Mbeya City iliyoipanda daraja msimu huu zote zikiwa na pointi 26 kila moja, wakati Yanga wenyewe waliopo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 25.
Kutokana na hali hiyo iwapo Yanga itashinda na wapinzani wake kutoka sare watakalia kiti cha uongozi, lakini kama itashinda na Azam au Mbeya City ikashinda ina maana Yanga itashika nafasi ya pili na moja kati ya timu hizo mbili itaangukia katika nafasi ya tatu na nyingine kukalia kiti cha uongozi.
Tayari kumekuwa na tambo kwa timu za Azam na Mbeya City kuhusiana na pambano lao, lakini Yanga wenyewe wanaombea waendelee rekodi yao ya kutoa dozi kwa timu za maafande kwa kuikwanyua Oljoro JKT katika pambano lao huku wakiombea wapinzani wake kutoka sare.
Mechi nyingine kwa kesho itawakutanisha Rhino Rangers yua tabora itakayovaana na maafande wa Prisons ya Mbeya kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Je, ni Yanga, Azam au Mbeya City watauaga mwaka kileleni hadi mwaka 2014 au watauvuruga vipi msimamo wa ligi hiyo katika nafasi ya Tatu Bora? Tusubiri tuone hiyo kesho!

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014    
                                  P    W     D     L      F     A    GD  PTS
01.Azam                    12   07    05    00   20    07    13   26
02.Mbeya City           12   07    05    00   16    07    09   26
03.Yanga                    12   07    04    01   28    11    17   25
04.Simba                    13   06    06    01   26   13     13   24
05.Kagera Sugar         13   05    05    03   14   09     05   20
06.Mtibwa Sugar         13   05    05    03   19   17     02   20
07.Ruvu Shooting        13   04    05    04   15   15     00   17
08.Coastal Union         13   03    07    03   10  07     03    16
09.JKT Ruvu               13   05    00    08   10  16    -06   15
10.Rhino Rangers        12   02    04    06   09  16     -05   10
11.Oljoro                    12   02    04    06   09  16     -07   10
12.Ashanti                  13   02    04    07   12   24    -12    10
13.Prisons                  12   01    05    06    05  15    -10    08
14.Mgambo               13   01    03    09    03  23    -20    06
 
Wafungaji:

10- Tambwe Amisi (Simba)
9- Elias Maguri (Ruvu Shooting)
8- Hamis Kiiza (Yanga), Juma Luizio (Mtibwa Sugar)
7- Kipre Tchetche (Azam)
6- Themi Felix (Kagera Sugar)
5- Tumba Sued (Ashanti Utd), Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa (Yanga)
4- Peter Michael (Prisons), Jerry Santo (Coastal Union), Jerry Tegete (Yanga), Betram Mombeki (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu)
3- Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerry Santo (Coastal Union),  Mcha Khamis (Azam), Amir Omary (Oljoro), Ramadhani Singano (Simba)
2- Haruna Moshi, Crispian Odulla (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya, Jeremiah John, Peter Mapunda,(Mbeya City), Godfrey Wambura (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa (JKT Oljoro), Joseph Kimwaga (Azam), Shaaban Nditti, Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar), Said Dilunga (Ruvu Shooting)
1- Abdi Banda, Danny Lyanga (Coastal Union), Henry Joseph, Joseph Owino, Gilbert Kazze (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Frank Dumayo, Mbuyi Twitte, Oscar Joshua (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah, Abbas Mohammed (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah,  Aggrey Morris,  John Bocco, Faridi Maliki, Hamphrey Mieno, Salum Abubakar, Erasto Nyoni (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter, Deo Deus  (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader  (Ruvu Shooting), Masoud Ally, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Paul Maono(OG), Samir Luhava (OG), John Matei, Mwinyi Ally, Hussein Sued, Said Maulid (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Clement Douglas, Salum Kanoni (Kagera Sugar), Paul Malipesa, Expedito Kidulo, Nurdin Mohammed, Fikiri Mohammed (Oljoro JKT)

Matokeo yote ya mechi za Duru la KwanzaDURU LA KWANZA
Agosti 24, 2013
Yanga vs Ashanti United (5-1)
Mtibwa Sugar vs Azam (1-1)
Oljoro JKT vs Coastal Union (0-2)
Mgambo JKT vs JKT Ruvu (0-2)
Rhino Rangers vs Simba (2-2)
Mbeya City vs Kagera Sugar (0-0)
Ruvu Shooting vs Prisons (3-0)

Agosti 28, 2013
Mtibwa Sugar vs Kagera Sugar (1-0)
Rhino Rangers vs Azam (0-2)
JKT Ruvu  vs Prisons (3-0)
Mbeya City vs Ruvu Shooting (2-1)
Mgambo  vs Ashanti United (1-0)
Oljoro JKT vs Simba (0-1)
Yanga  vs Coastal Union (1-1)

Sept 14, 2013
Simba  vs Mtibwa (2-0)
Coastal Union  vs Prisons (0-0)
Ruvu Shooting va Mgambo JKT (1-0)
Oljoro JKT vs Rhino Rangers (1-1)
Mbeya City  vs Yanga (1-1)
Kagera Sugar vs Azam (1-1)
Ashanti United  vs JKT Ruvu (0-1)

Sept 18, 2013
Prisons vs Yanga (1-1)
Simba vs Mgambo JKT (6-0)
Kagera Sugar vs JKT Oljoro (2-1)
Azam  vs Ashanti United (1-1)
Coastal Union  vs Rhino Rangers (1-1)
Mtibwa Sugar  vs Mbeya City (0-0)
Ruvu Shooting vs  JKT Ruvu (1-0)

Sept 21, 2013
Mgambo JKT vs Rhino Rangers (1-1)
Prisons vs Mtibwa Sugar (1-1)
Simba vs Mbeya City (2-2)
Kagera Sugar vs Ashanti United (3-0)

Sept 22, 2013
JKT Ruvu vs Oljoro JKT (0-1)
Azam  vs Yanga (3-2)
Coastal Union v Ruvu Shooting (1-0)

Sept 25, 2013
Rhino Rangers vs Ashanti Utd (2-0)

Sept 28, 2013
Yanga vs Ruvu Shooting (1-0)
Rhino Rangers v Kagera Sugar (0-1)
Mbeya City vs Coastal Union (1-1)
Mgambo JKT vs Oljoro JKT (0-0)

Sept 29, 2013
Ashanti Utd vs Mtibwa Sugar (2-2)
JKT Ruvu vs Simba (0-2)
Prisons vs Azam (1-1)

Okt 05, 2013
Ruvu Shooting vs Simba (1-1)
JKT Ruvu vs Kagera Sugar (2-1)
Coastal Union vs Azam (0-0)
Oljoro JKT vs Mbeya City (1-2)

Okt 06, 2013
Mgambo JKT vs Prisons (0-1)
Yanga vs Mtibwa Sugar (2-0)

Okt 09, 2013
Rhino Rangers vs Mbeya City (1-3 )
Oljoro JKT vs Ruvu Shooting (2-2)
Azam vs Mgambo JKT (2-0)
Mtibwa Sugar vs JKT Ruvu (2-1)

Okt 12, 2013
Kagera Sugar vs Yanga (1-2)
Simba vs Prisons (1-0)
Ashanti Utd  vs  Coastal Union (2-1)

Okt 13, 2013
Ruvu Shooting vs Rhino Rangers (1-0)
Mgambo JKT vs Mbeya City (0-1)
Azam vs JKT Ruvu (3-0)
Mtibwa Sugar vs Oljoro JKT (5-2)

Okt 16, 2013
Ashanti Utd vs Prisons (2-1)

Okt 19, 2013
Kagera Sugar vs Coastal Union (1-0)
Oljoro JKT vs Azam (0-1)
Mtibwa Sugar vs Mgambo JKT (4-1)
Mbeya City vs JKT Ruvu (1-0)
Ashanti Utd vs Ruvu Shooting (2-2)

Okt 20, 2013
Simba vs Yanga (3-3)

Okt 23, 2013
Coastal Union vs Simba (0-0)
Prisons vs Kagera Sugar (0-0)
Yanga vs Rhino Rangers (3-0)

Okt 28, 2013
Simba vs Azam (1-2)
Ruvu Shooting vs Kagera Sugar (1-1)
Coastal Union vs Mtibwa Sugar (3-0)
Oljoro JKT vs Ashanti Utd (0-0)

Okt 29, 2013
Prisons vs Mbeya City (0-2)
Rhino Rangers vs JKT Ruvu (1-0)
Yanga vs Mgambo JKT (3-0)

Okt 31, 2013
Simba vs Kagera Sugar (1-1)

Nov 1, 2013
JKT Ruvu vs Yanga (0-4)

Nov 2, 2013
Mgambo JKT vs Coastal Union (0-0)
Azam vs Ruvu Shooting (3-0)
Mtibwa Sugar vs Rhino Rangers (1-0)
Mbeya City vs Ashanti Utd (1-0)

Nov 3, 2013
Prisons vs Oljoro JKT (0-1)

Nov 06, 2013
JKT Ruvu vs Coastal Union (1-0)
Ashanti Utd vs Simba (2-4)
Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar(2-2)
Kagera Sugar vs Mgambo JKT (2-0)

Nov 07, 2013
Azam vs Mbeya City (-)
Rhino Rangers vs Prisons (-)
Yanga vs Oljoro JKT (-)

Elias Maguri, Juma Luizio wazidi kukifukizia kiatu cha dhahabu Mtibwa, Ruvu zikitoka sare Mabatini


Juma Luizio 'Ndanda'
MABAO mawili ya mshambuliaji nyota wa Ruvu Shooting, Elias Maguri yaliyoisaidia timu yake kupata sare ya 2-2 na Mtibwa Suigar yamefanya mbio za kuwania kiatu cha dhahabu kuzidi kuwa ngumu baada ya mchezaji huyo kufikisha bao la tisa na kumjongelea Amissi Tambwe wa Simba anayeongoza orodha hiyo.
Maguri amefunga mabao hayo katika pambano la timu yake kufungia duru la kwanza kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi na kuonyesha dhamira yake ya kunyakua kiatu hicho cha dhahabu ambacho msimu uliopita kilichukuliwa na 'Pro' Kipre Tchetche.
Mabao ya wapinzani wao yaliwekwa kimiani na mshambuliaji anayezidi kuja juu nchini, Juma Luizio'Ndanda' ambaye alifikisha bao lake la nane msimu huu na kumfikia Hamis Kiiza huku akibakisha mawili kumkamata Tambwe.
Bao jingine la Mtibwa liliwekwa kimiani na kiungo mzoefu nchini, Shaaban Kisiga 'Marlon' na kuifanya timu yao ya Mtibwa kupata pointi moja na kufikisha pointi 20 na kushika nafasi ya sita ikiipisha Kagera kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

JKT Ruvu wazinduka waikwanyua Coastal, Kagera yaua 2-0

JKT Ruvu iliyozinduka leo Chamazi

Kagera iliyoikwanyua Mgmabo mabao 2-0
BAADA ya kupokea vipigo mfululizo maafande wa JKT Ruvu leo wamezinduka kwenye uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam baada ya kukwanyua Coastal Union kwa bao 1-0, huku Kagera Sugar wakiishikisha adabu MKatika pambano la Chamazi, bao pekee la maafande hao linalowafanya wafikishe pointi 15 liliwekwa kimiani na Bakar Kondo.
Nako Kaitaba mabao mawili ya Themi Felix na Seleman Kibuta yalitosha kuizima Mgambo JKT iliyosafiri hadi mjini Bukoba baada ya kuwanyuka mabao 2-0 katika pambano jingine la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa matokeo hayo Kagera imefikisha pointi 20 huku JKT Ruvu ikifikiosha pointi 15 na kusalia kwenye nafasi ya tisa katika msimamo  wa ligi hiyo. Huku bao la Themi anayewania Tuzo ya Mwanasoka Bora inayoendeshwa na gazeti la MWANASPOTI imemfanya afike jumla ya mabao sita, huku Bakar Kondo akifika bao lake la nne katika orodha ya wafungaji inayoongoza na Amissi Tambwe wa Simba mwenye mabao 10 na kufuatiwa na Elias Maguri wa ruvu Shooting kisha Hamis Kiiza 'Diego' mwenye mabao nane akiwa na nafasi ya kuongeza idadi kwa vile timu yake ya Yanga itashuka kesho dimbani kuvaana na Oljoro JKT.

MAKAMBA MGENI RASMI TUZO ZA MWANASOKA BORA


NAIBU Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa mwana soka bora wa mwaka katika ligi kuu ya Vodacom mwaka 2013, itakayofanyika katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 
Tuzo hiyo itashuhudia wachezaji walioingia hatua ya Tano bora, AMRI KIEMBA, HARUNA NIYONZIMA, SHOMARI KAPOMBE, THEMI FELIX, na KELVIN YONDANI wakichuana kuwania umwamba wa soka Tanzania,  Baada ya kupigiwa kura na mashabiki na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake Zamoyoni Mogela kuchambua majina hayo kulingana na kura walizopata.
 
Akizungumza juu ya hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Kelvin Twissa amesema, wanafurahi kuwa sehemu ya  maendeleo ya soka nchini na siku zote kampuni yake imekuwa msitari wa mbele katika kuunga mkono michezo nchini, hususani mchezo wa soka na kuhakikisha unakuwa moja ya ajira muhimu kwa watanzania.
 
“Vodacom tumeendelea kuwa wadau muhimu katika mapinduzi ya soka la Tanzania, sasa mpira umekuwa zaidi ya burudani kwa watanzania kutokana na chachu ambayo tumeiweka tangu tuanze kudhamini ligi kuu, ambayo sasa imekuwa na ushindani mkubwa na thamani yake inazididi kupanda siku hadi siku,” alisema Twissa.
 
Aidha Twissa amesema kampuni yake itaendelea kushirikiana na wadau wengine wote wanaopenda maendeleo ya soka bila kusita kutokana na namna ambavyo kampuni yake imejidhatiti katika kuinua michezo nchini.
 
“Mafanikio yanayopatikana katika soka letu sasa hayajapatikana hivivi ni kutokana na dhamira tuliyoiweka katika kuinua mchezo huu wa soka na uwekezaji mkubwa tulioufanya hadi sasa, watu ambao wanaleta mafanikio haya ni wachezaji ambao wamekuwa wanapambana kufa na kupona kutoa burudani kwa Watanzania, Ni lazima tuwaenzi wachezaji hawa kwa njia tofauti tofauti,” alisema Twissa.
 
Kwa upande wake Meneja Masoko wa MCL Bernad Mukasa amesema kuwa, wamefurahi kushirikiana na Naibu waziri Mh. Makamba katika utoaji wa tuzo hizi, ambazo zinatambua mchango wa wanasoka nchini.
 
“Tuzo hizi zinatambulika rasmi kwa jina la zitaitwa MWANASPOTI BORA WA SOKA WA VODACOM 2013. Ni za kipekee na za kwanza kabisa nchini kwa wigo wa wachezaji wanaohusishwa, ushirikishwaji wa uteuzi wa mshindi, na vigezo husika.” alisema Mukasa na kuongeza.
 
“Kwa mwaka huu, licha ya kumpata Mwanaspoti Bora wa soka wa mwaka , pia tutatoa Tuzo kwa “categories” zaidi ya 10 ikiwemo kocha bora, mwamuzi bora, mchezaji bora wa kike, mchezaji bora chipukizi, “1st eleven”, goli bora, mchezaji bora wa kigeni, Mchezi bora wa kulipwa anayecheza nje, na Kipengele kingine kitajulikana siku ya ijumaa,” alisema Mukasa.
 
Mukasa alihitimisha kwa kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwapigia kura wachezaji hao  kwa  kuandika ujumbe mfupi unaoanza na neno KURA kisha jina la mchezaji anayemchagua kati ya hao waliotajwa na kisha kutuma kwenda namba 15678.

Simba yamaliza hasira zake kwa Ashanti, Tambwe, Mombeki nouma

Mombeki akitafuta njia ya kumtoka beki wa Ashanti huku, Haruna Shamte akiwa tayari kwa msaada (picha: Lenzi ya Michezo)

KAMA walivyoanza ndivyo walivyomaliza duru la kwanza, Ashanti United 'Wana wa Jiji' wameshindwa kuhimili hasira za 'mnyama' baada ya jioni hii kukubali kipigo cha aibu cha mabao 4-2 kutoka kwa Simba.
Ashanti Utd iliyorejea Ligi Kuu msimu huu, ilikumbana na kipigo hicho kwenye uwanja wa Taifa ikiwa ni miezi karibu mitatu tangu walipolala kwa mabao 5-1 na Yanga katika mechi ya kufunga dimba la ligi hiyo.
Mabao mawili ya Betram Mombeki na mengine ya Ramadhani Singano 'Messi' na Amissi Tambwe yalitosha kuiangamiza Ashanti Utd ambayo kabla ya pambano hilo waliapa kutoa kisago kwa wapinzani wao hao.
Messi, ndiye aliyeanza kufungua karamu ya mabao ya Simba katika dakika ya 8 kabla ya Ashanti kusawazisha kwenye dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza kupitia kwa Hussein Sued.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kucharuka kwa kupata mabao ya harakaharaka kupitia Tambwe aliyefunga dakika ya kwanza tu ya kipindi hicho na kufikisha jumla ya mabao 10 katika orodha ya ufungaji bora.
Dakika ya nne baadaye Mombeki alifunga bao la tatu kabla ya kuongeza jingine dakika ya 15, wakati huo Ashanti ikiwa imerejesha bao jingine na la pili kwao kupitia mkongwe Said Maulid 'SMG' aliyevurumusha kombora lililomshinda kipa Abuu Hashim.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha jumla ya pointi 24 na kumaliza mechi zake za duru la kwanza, Ashanti ikisaliwa na pointi 10, huku pia ikijikuta ikimaliza pambano hilo bila kipa wake, Amani Simba kuwepo uwanjani kwa kulimwa kadi nyekundu na mwamuzi Andrew Shamba.
Kipa huyo alipewa kadi hiyo baada ya kuudaka mpira nje ya eneo lake akizuia kupigwa kanzu na nyota wa mchezo wa leo, Ramadhani Singano Messi.

NEWZ ALERT: MFANYAKAZI TBC APIGWA RISASI NA KUFARIKI

No comments

MFANYAKAZI  wa Shirika la Utangazaji Nchini  TBC, pichani, RAMADHAN GIZE ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosaidiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo katika eneo la UBUNGO Maziwa Jijini DSM.

Tukio hilo limetokea baada ya watu hao kuvamia duka moja katika eneo hilo la UBUNGO MAZIWA kwa lengo la kupora, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MWARAMI RAJABU amejeruhiwa na watu hao wanasadikiwa kuwa ni majambazi.
Chanzo:MICHUZI

Msiba! DJ RANKEEM RAMADHANI HATUNAYE DUNIANI


KWA mujibu wa taarifa zilizopatikana jioni ya leo, zinaeleza kuwa mmoja wa Ma Dj Maarufu sana hapa jijini Dar na Tanzania kwa ujumla ,Dj Rankeem Ramadhani amefariki mchana huu.
Inaelezwa kuwa DJ Rankeem aliyewahi kufanya kazi Radio One Stereo na vituo vingine mbalimbali alifariki kwenye hospitali ya Mwananyamala baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na tatizo la kidole utumbo.
Mwili wa mkali huyo katika kupangilia muziki aliyetingisha kwa miaka kadhaa, umehifadhiwa kwenye hospitalini hiyo ikifanywa mipango ya mazishi yake.
Taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaletwa kwenu kadri tukavyopata kwa undani zaidi ikiwemo kujua atazikwa lini na wapi, ingawa inaelezwa huenda akazikwa kesho jijini Dar es Salaam.
MICHARAZO inatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na wadau wote wa habari na muziki kwa msiba wa gwiji hilo, na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu kwa kukumbuka kuwa Sote tu wa Allah (SW) na Kwake Tutarejea.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-AMEN

Manchester City yaweka rekodi Ulaya, Juve, Man Utd wabanwa

Aguero akishangulia moja ya mabao yake ya jana kwa CSKA
Bale akiwatungua Juve walipopata sare ya 2-2
 KLABU ya Manchester City kwa mara ya kwanza katika michuano uya Ligi ya Mabingwa Ulaya imevuka salama hatua ya makundi na kuweka rekodi kwao baada ya kuwadungua 'wabaguzi wa rangi' CSKA ya Urusi kwa mabao 5-2 katika pambano kali ya michuano hiyo ya Ulaya.
Mabao mawili ya Sergio 'kun' Aguero na hat trick ya Alvaro Negredo yalitosha kuwavusha wakali hao wa EPL mbele ya Warusi hao.
Bapa la kwanza la Aguero lilitokana na mkwaju wa penati baada ya David Silva kuchezwa vibaya kisha kuongeza jingine kabla ya Negredo kufunga mabao mengine, huku yale ya wageni yote mawili yakifungwa na Doumbia.
Katika mechi nyingine za kundi hilo, Mabingwa watetezi Bayern Munich ilipata ushindi kiduchu wa bao 1-0 na kuendeleza rekodi ya kushindwa kwa asilimia 100 mbele ya Victoria, Juventus ya Italia ikiwa nyumbani ilijitutumua na kuibana Real Madrid na kutoka nao sare ya 2-2, japo walishindwa kuwazuia Cristiano Ronaldo na Bgareth Bale kuwatungua kwani wote wawili walifunga mabao ya wahispania hao.
Manchester United ikiwa ugenini ililazimishwa suluhu na Real Sociedad, huku Shakhtar Doneksk na Bayer Leverkusen nao wakitoka suluhu na mabinhwa wa Ufaransa PSG na Anderletch zikitoka pia sare ya 1-1.
Benfica ikiwa ugenini ililala kwa bao 1-0 kwa Olympiakos na Galatasaray ilikubali kichapo cha ugenini cha bao 1-0 toka kwa Kobenhavn.
Ligi hiyo itaendeela tena usiku wa leo kwa michezo minane baadhi ikiwakutanisha Arsenal itakayokuwa ugenini dhidi ya Borussia Dotmund, Barcelona dhidi ya Ac Milan na Ajax itaikaribisha Celtic.
Mechi nyingine ni kati ya Chelsea dhidi ya Schalke 04, Napoli watakaoumana na Olympique Marseille, Zenit na Porto na Atletico Madrid itakayoumana na Viena.

Tuesday, November 5, 2013

Mneguaji wa zamani wa Twanga afariki

BREAKING NEWS
MCHEZA SHOO MAARUFU NCHINI ALIYEKUWA NA BENDI ZA AFRCAN STARS TWANGA PEPETA NA EXTRA BONGO MWATUMU ATHUMANI (KUSHOTO) PICHANI AMEFARIKI DUNIA LEO JUMANNE SAA 10 ALASIRI KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA ALIKOKUWA AMELAZWA. MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWAO MANZESE JIJINI DAR ES SALAAM. MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMIN
MCHEZA SHOO MAARUFU NCHINI ALIYEKUWA NA BENDI ZA AFRICAN STARS 'TWANGA PEPETA' NA EXTRA BONGO 'WANA KIZIGO' MWATUMU ATHUMANI (KUSHOTO) PICHANI AMEFARIKI DUNIA LEO JUMANNE SAA 10 ALASIRI KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA ALIKOKUWA AMELAZWA. MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWAO MANZESE JIJINI DAR ES SALAAM. MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI. AMEEEN

Rage anusuru pambano la Simba vs Ashanti

Ismail Aden Rage
 MWENYEKITI wa klabu ya soka ya Simba, Ismail Aden Rage amefanikiwa kunusuru pambano la timu yake na Ashanti United lililopangwa kufanyika kesho kuchezwa kama kawaida, baada ya awali kutakiwa kulipa kwanza Sh Milioni 25 kama fidia ya uvunjwaji wa viti kwenye uwanja wa Taifa.
Serikali ilitoa adhabu hiyo kwa klabu hiyo kufikiaviti vilivyovunjwa na mashabiki wao wakati wa pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara kati yao na Kagera Sugar lililoisha kwa sare ya 1-1.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana hivi punde na kuthibitishwa na Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ni kwamba Rage alilazimika kuwasiliana na serikali na kuahidi kulipwa kwa fedha hizo mradi waruhusu pambano hilo lichezwe kesho na kufuatiwa na kikao cha pamoja baina ya serikali, Simba na TFF.
Awali TFF ilitumiwa barua toka serikali ikiwataka izuie pambano hilo la Simba na Ashanti United mpaka kwasa Simba walipe fidia hiyo ambayo ilifanywa na mashabiki wao kwa kile kilichoelezwa kukerwa na penati iliyopewa wapinzani wao dakika za lala salama.
"Mechi itachezwa kesho kama kawaida baada ya Mwenyekiti wetu kuweza kuzungumza na serikali kwa ajili ya kukaa chini kujadiliana kuhusu barua hiyo ya kutaka fidia hiyo ilipwe kabla ya kuchezwa kwa mchezo huo." Kamwaga alinukuliwa hivi punde.

Hawa ndiyo waliofungwa nje ya nchi kwa dawa za kulevya


Haya ni maelezo binafsi ya Mheshimiwa Ester Amos Bulaya bungeni Dodoma November 4 2013 kuitaka serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya dawa za kulevya na kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia wahalifu wa dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 28(8) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2013, napenda kutoa maelezo binafsi ya juu ya tatizo sugu la uagizaji, uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya linaloongezeka kwa kasi kubwa nchini, lengo likiwa ni kuitaka serikali ifanye mabadiliko/marekebisho ya sheria ya Dawa za kulevya na kuanzisha Mahakama Maalum kushughulikia wahalifu wanaojihusisha na usafirishaji na biashara ya dawa za kulevya.
Mheshimiwa Spika,
Nimeona ni wakati muafaka kutoa maelezo haya, ili Bunge lako tukufu na Serikali ipate fursa ya kuona uzito wa tatizo hili kutokana na ukweli kwamba katika miaka ya karibuni tatizo la dawa za kulevya katika nchi yetu limeongezeka kwa kasi ya ajabu hali inayopelekea athari kubwa za kiuchumi, kijamii na kiafya. Na mbaya zaidi kundi kubwa linaloathirika ni kundi la vijana, ambao ndio nguvu kazi ya Taifa letu. Na mbaya zaidi sasa hivi, wafanya biashara hawa wa dawa hizi haramu wameanza kuwatumia watoto wa shule za msingi chini ya falsafa yao mpya “wapate wakiwa wadogo…wafanye watumwa wa dawa za kulevya… na kupata uhakika wa soko la baadae pale ambapo watakuwa wameajiriwa au wamejiajiri”.
Mheshimiwa Spika,
Tafiti za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba kuna ongezeko kubwa na la kutisha katika matumizi ya dawa za kulevya aina ya heroin na kwa njia ya kujidunga katika nchi za Kenya, Libya, Mauritius, Shelisheli na Tanzania. Halikadhalika, Ripoti ya mpya ya hivi karibuni ya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na mihadarati na uhalifu (UNODC) imetamka bayana kwamba Tanzania ni kinara wa kupitisha dawa za kulevya katika nchi za Afrika Mashariki, na Mkoa wa Tanga ukitajwa kama mkoa hatari zaidi!
Mheshimiwa Spika,
Ripoti hiyo inasema jumla ya Tani 64 za dawa za kulevya aina ya Heroin ilisafirishwa bila kukamatwa kwenda au kupitia Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania kati ya 2010 na 2013. Na kwa Mkoa wa Tanga, ambao umetajwa wazi kama eneo hatari zaidi Afrika Mashariki wastani wa ukamataji wa shehena za dawa za kulevya eneo hilo umefikia KG 1,011 mwaka 2013 toka KG 145 mwaka 2010. Na kwamba Dola za Kimarekani takriban milioni 160 zinatumiwa na Watanzania na wakenya kila mwaka kwa utumiaji na usafirishaji kwa mwaka!Hili sio jambo la kufumbia macho, lazima tuchukue hatua sasa.
Mheshimiwa Spika,
Lazima tuchukue hatua sasa, kwa sababu kama nilivyoainisha hapo juu kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu tu (2010-2013), wakati Tani 64 za dawa za kulevya zilipita bila kukamatwa…zikiwa mtaani zikiharibu vijana na watoto wetu katika kipindi hicho hicho, kiasi kilichoweza kukamatwa ni tani 1.6 tu! Takwimu hizo za kutisha zinatoa picha kwamba sehemu kubwa ya shehena za dawa za kulevya hupitishwa bila kugundulika au kukamatwa na vyombo vya dola!
TASWIRA YA NCHI KATIKA JUMUIYA YA KIMATAIFA
Mheshimiwa Spika,
Maelfu ya watanzania wanatumikia vifungo mbali mbali ikiwamo vifungo vya maisha nje ya nchi, wengine wengi wamepoteza maisha kwa kunyongwa. Nitatoa mifano michache; China peke yake inasemekana kuna wafungwa 176 (99% – dawa za kulevya) , Brazil kuna wafungwa zaidi ya 103 na Hong Kong kuna zaidi ya watanzania 200 wenye kesi za dawa za kulevya, ambapo 130 zimeshakwisha hukumiwa na kesi 70 zikiwa zinaendelea!
Mheshimiwa Spika,
Aibu ya hivi karibuni, ambayo hatuwezi kuikwepa ni meli iliyosajiliwa Tanzania (upande wa Zanzibar- MV Gold Star ) iliyoripotiwa kukamatwa nchini Italia ikiwa imesheheni tani 30 za dawa za kulevya zenye thamani ya pauni milioni 50 ( sawa na bilioni 123 za Kitanzania). Mheshimiwa Spika, uhalifu huu, unaofanywa na mtandao huu wa watu wachache, lakini wenye nguvu umewafanya watanzania wanaokwenda nje ya nchi kudhalilika kutokana na upekuzi unaofanywa dhidi yao kwa hofu kwamba yawezekana na wao wamebeba dawa hizo haramu.
HALI YA DAWA ZA KULEVYA
Mheshimiwa Spika,
Changamoto ya dawa za kulevya sio tatizo letu peke yetu ni tatizo ambalo hata Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikipambana nalo kwa kipindi kirefu kwani tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 5 ya idadi ya watu wazima duniani (watu takribani milioni 230) wanakadiriwa kutumia dawa za kulevya.
Mheshimiwa Spika,
Tukiwa sehemu ya Jumuiya hii ya Kimataifa, Waheshimiwa Wabunge mtakumbuka kuwa tarehe 19 Desember, 1988 Jumuia ya Kimataifa ilipitisha Mkataba wa kupambana na dawa za kulevya yaani United Nations Convention Against Illicit Traffic in Narcotic Drugs and Psychotropic Substances. Tanzania ni sehemu ya Mkataba huo na hili limewekwa wazi hata kwenye kifungu cha 55 cha Sheria ya kuzuia dawa za kulevya [sura 95 ya sheria zetu kama zilivyorekebishwa mwaka 2002]. Mkataba wa mwaka 1988 ulikuwa unakazia zaidi Mkataba wa mwaka 1961 (Single Convention on Narcotic Drugs, 1961), Itifaki (Protocol) za 1972 zilizofanyia marekebisho Mkataba wa mwaka 1971 (Convention on Psychotropic Substances, 1971). Licha ya juhudi zote, tatizo la uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya, limezidi kuwa kubwa.
HALI YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI NA MADHARA KWA AFYA YA BINADAMU
Mheshimiwa Spika,
Mwaka 1995 tulitunga Sheria ya kuzuia biashara ya dawa za kulevya ambayo ilianza kufanya kazi mwaka 1996 kupitia GN.No.10/1996. Sheria hiyo inatumika Bara na Zanzibar. Kabla ya Sheria hiyo tulikuwa tuna Sheria iitwayo the Dangerous Drugs Ordinance (Cap.95). Pamoja na kutungwa kwa Sheria mpya, tatizo la dawa za kulevya limeendelea kuwa kubwa zaidi hapa nchini. Ukamataji wa dawa za kulevya kwa miaka ya nyuma ilikuwa kidogo na idadi ya walioathirika (mateja) ilikuwa ni ndogo kulinganisha na sasa hivi.
Mheshimiwa Spika,
Ni kwa bahati mbaya sana, licha ya ukubwa wa tatizo, pamoja na athari zake kwa jamii ya Watanzania, hakuna tafiti zinazoonyesha ukubwa wa tatizo kwa Nchi nzima, tafiti nyingi zilizofanywa zimejikita katika maeneo machache yaliyoathirika zaidi na dawa za kulevya . Tafiti zinaonyesha kwamba Dawa zinazotumika kwa wingi ni bangi, mirungi, heroine, mihadarati, vidonge na cocaine.Tafiti iliyofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya UNODC (United Nations Office on Drugs and Crime) zinaonyesha kwamba 0.2% ya Watanzania, ambao ni karibia watu milioni 1.2 wameshawahi kutumia dawa za kulevya aina ya heroine.
Mheshimiwa Spika,
Halikadhalika Shirika la afya duniani (World Health Organisation -WHO) inaripoti kuwa takribani 0.2% ya Watanzania wameathirika na Ugonjwa wa TB na takwimu za kitaifa katika program ya Kifua Kikuu na Ukoma Tanzania zinaonyesha maambukizi ya TB ni 0.4% wakati tafiti katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili inaonyesha kwamba maambukizi ya TB kwa wanaotumia dawa za kulevya ni 11% ambayo ni mara 44 zaidi ya kiwango cha maambukizi kwa watu ambao hawatumii dawa za kulevya.
Mheshimiwa Spika,
Kwa upande wa maambukizi ya UKIMWI takwimu za mwaka 2011/2012 za TACAIDS zinaonyesha kwamba 5.1% ya Watanzania wameathirika na virusi vya UKIMWI wakati tafiti ndogondogo zinaonyesha maambukizi ya virusi ya ukimwi kwa watu wanaotumia dawa za kulevya ni mara 10 zaidi ya maambukizi ya kawaida. Kwa mfano 51.9% ya wanaotumia dawa za kulevya kwa njia kujidunga sindano, 37% wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kuvuta na kufanya biashara ya ngono na 22.6% kwa wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kuvuta.
Mheshimiwa Spika,
Madhara ya kiafya kwa utumiaji wa dawa za kulevya sio tu katika magonjwa ya TB na maambukizi ya virusi vya ukimwi, bali pia katika homa ya ini. Japokuwa hakuna tafiti za kitaifa zilizofanyika kuhusiana na mchango wa matumizi ya dawa katika homa ya ini, tafiti ndogondogo za mwaka 2012 zinaonyesha kati ya 65% mpaka 75.6% ya watumiaji wa dawa za kulevya wameathirika kwa homa ya Ini, hasa homa ya ini aina ya Hepatitis. Homa ya ini ni hatari sana katika kupata magonjwa sugu ya ini ikiwepo kansa ya ini na ini kushindwa kufanya kazi.
UKUBWA WA TATIZO NA UTENDAJI WA VYOMBO VYA DOLA
Kesi kubwa ya kwanza inayohusu dawa za kulevya ni ile ya mfanyabiashara NURDIN AKASHA @HABAB V.R [1995] TLR. 227 (CAT) ambaye tarehe 20/7/1993 alikamatwa nyumbani kwake Msasani village akiwa na paketi 105 za menthaqualone (mandrax) alizo ziingiza nchini kutoka Mombasa akitumia malori yake. Sasa hivi tunaongelea uingizaji wa kilo kadhaa za dawa za kulevya na siyo paketi tena. Mwezi Machi, 2010 kilo 92 za dawa za kulevya aina ya Heroine zilikamatwa maeneo ya Kabuku Mkoani Tanga na tayari washitakiwa 5 wanatumikia kifungo. Tarehe 19/12/2010 kilo 50 za dawa za kulevya aina ya Heroini zilikamatwa tena wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. Mwezi Septemba, 2011 kilo 179 za dawa za kulevya aina ya Heroini zilikamatwa Dar es salaam, tarehe 14/6/2011 Kilo 35 za dawa za kulevya aina ya Heroine zilikamatwa mkoani Mbeya na tarehe Januari kilo 211 za dawa za kulevya zilikamatwa mkoani Lindi.
UTENDAJI WA OFISI YA DPP
Natambua jitihada zinazofanywa na baadhi ya watendaji wa Serikali ya awamu ya nne katika vyombo vya dola kwa kufanikisha jitihada za kuwakamata watuhumiwa wanaojihusisha na dawa za kulevya. Kutokana na jitihada hizo, kuanzia mwaka 2008 mpaka mwaka huu wa 2013 watuhumiwa wa dawa za kulevya ni kama ifutavyo:-
i) Cocaine kilo 395 zilikamatwa na washitakiwa waliokamatwa ni 1074
ii) Heroini kilo 768.8 na washitakiwa waliokamatwa ni 1130,
iii) Mirungi kilo 56,562 na washitakiwa waliokamatwa ni 3,712,
iv) Bangi kilo 487,472 sawa na tani 487 na washitakiwa waliokamatwa ni 20,255
v) Mandrax kilo 5 na gramu 9 na washitakiwa waliokamatwa ni 20.
Licha ya juhudi za baadhi ya watendaji waaminifu kuwakamata watu walioko katika mtandao huu hatari kumekuwa na hujuma za dhahiri dhidi ya wanaopambana na dawa za kulevya. Moja kati ya ofisi inayoshutumiwa kuwa na maafisa wanaoshirikiana na wanamtandao, ni ofisi ya DPP
MTANDAO KATIKA OFISI YA DPP NA MAHAKAMA
Natambua kazi nzuri na jitihada zinazofanywa na baadhi ya watumishi wazalendo kwa upande kwa Ofisi ya Muendesha Mashtaka, Majaji na Mahakimu waaminifu. Lakini katika ofisi hizo za umma, kumekuwa na baadhi ya watumishi ambao wamekuwa wakihujumu kesi za dawa za kulevya kwa kushirikiana na watuhumiwa katika kupanga jinsi ya kuwasaidia washinde kesi kwa kuwapatia taarifa za siri zinazohusiana na ushaidi na jinsi ya kuharibu ushahidi nzima.
Mheshimiwa Spika,
Kutokana na kupanuka kwa mtandao huu wa kuhujumu, licha ya kushirikiana na washitakiwa, mtandao uliopo katika Ofisi hiyo ya DPP umekuwa ukituhumiwa kufanya njama za kushirikiana na baadhi ya watumishi wa mahakama hasa Majaji kuhamisha kesi kupeleka kwa Majaji ambao wanadaiwa kuhusika na mtandao huu (sihitaji kutaja majina ya Majaji hapa, baadhi yao wanafamika na wengine wametajwa mara kadhaa na vyombo vya habari).
Mheshimiwa Spika,
Kwa kutumia mtandao huo, baadhi ya Majaji wamekuwa wanatafsiri sheria kwa jinsi wanavyotaka na kuwapa dhamana watuhumiwa wa kesi za dawa za kulevya ambazo hazina dhamana. Mfano mzuri ni kesi Na.6/2011, Jamhuri dhidi ya Fred William Chonde na wenzake ambao walikutwa na kilo 179 za Heroine yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.5. Washitakiwa hawa wanashitakiwa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 148(5)(a)(ii) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai pamoja na kifungu cha 27(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia usafirishaji wa dawa za kulevya halina dhamana. Kwa tafasiri yoyote ile aliyokuwa nayo mheshimiwa Jaji, bado asingewapa dhamana kwani kifungu cha 148(5)(a)(iii) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na kifungu cha 27(1)(b) cha Sheria ya Kuzuia usafirishaji wa dawa za kulevya kinazuia dhamana kwa kosa ambalo thamani ya dawa za kulevya inazidi shilingi milioni kumi.
Mheshimiwa Spika,
Kutokana na Mahakama kutoa dhamana, washitakiwa wawili raia ya Pakistani wametoroka na hawapo tena nchini. Aidha, katika kesi ya R. v. Mwinyi Rashid Ismail @Mkoko, (KLR /IR 4143/2011), mshitakiwa aliomba dhamana Mahakama Kuu wakati kesi ilikuwa bado ipo Mahakama ya Kisutu ndipo wakili wa Serikali akamwambia jaji kuwa anaomba kuifuta.
Mheshimiwa Jaji huku akifahamu kuwa kesi hiyo imefika mbele yake kwa ajili ya kusikiliza maombi ya dhamana tu, na kuwa ilikuwa haijafikishwa Mahakama Kuu kwa taratibu wa sheria, aliamua kumfutia kesi mshitakiwa na kuamuru kuwa yuko huru. Sambamba na hilo, katika kesi No. 794/2011 katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Mheshimiwa Hakimu aliwafunga kifungo cha nje kwa miezi kumi na tano washikiwa Abdurahman Shaban Sindanema, said Nassoro Khamis na Abdurahim Haroub Said waliokiri kosa la kuuza na kusambaza dawa za kulevya aina ya Heroini.
Mheshimiwa Spika,
Adhabu iliyotolewa na Hakimu huyu, haipo kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya kuzuia dawa za kulevya, adhabu iliyowekwa kwa wauzaji au wasambazaji wa dawa za kulevya ni kifungo cha maisha na si chini ya miaka ishirini (20) jela kwa kipindi hicho. Kesi nyingine ni Na. 274/2005 Jamhuri dhidi ya Yusuph Hashim Nyose aliyekamatwa na kilo 1.3 za dawa za kulevya aina ya Heroine alizokuwa amemeza na kisha kuzitoa kupitia njia ya haja kubwa baada ya kukamatwa na zilikuwa na thamani ya shilingi milioni kumi na mbili na laki sita (12,600,000/=). Pamoja na ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi sita(6) wa upande wa Jamhuri ikiwa ni pamoja na mkemia aliyethibitisha kuwa ni dawa za kulevya na mashahidi walioshuhudia mshitakiwa akizitoa kwa njia ya haja kubwa, Hakimu alimuachilia huru.
Mheshimiwa Spika
Katika hukumu yake Hakimu alisema kuwa ameridhika kuwa hizo ni dawa za kulevya na zina madhara kwa binadamu na kuwa hana ubishi kuwa mshitakiwa alikutwa nazo. Hata hivyo alimuachilia huru kwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuelezea mbinu walizotumia kumgundua mshitakiwa kuwa alikuwa amebeba dawa za kulevya kabla ya kumkamata. Mfano mwingine ni hukumu iliyotolewa tarehe 4/5/2007 inayoihusisha Jamhuri dhidi ya Chriswell Simon Mobini (561/2007) ambapo mtuhumiwa alikamatwa tarehe 9/4/2007 katika uwanja wa JKNA akiwa na pipi 93 aina ya heroine yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30 za kitanzania. Baada ya kufikishwa Mahakama ya Kisutu na kufunguliwa mashtaka chini ya kifungu 16 (1) (b) (i) cha dawa za kulevya.
Mheshimiwa Spika,
Katika shauri hili, Hakimu alimwachia huru baada ya mshtakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 1 za kitanzania kwa maelezo kwamba kwa kumtazama tu mtuhumiwa, anaonekana ni mgonjwa wa vidonda vya tumbo na hivyo hawezi kupata huduma nzuri iwapo atapelekwa rumande! Hii ni mifano michache tu kati ya mingi iliyopo!
KESI ZILIZOKO MAHAKAMANI
Mheshimiwa Spika,
Kama nilivyoainisha hapo juu, na ili kuonyesha msisitizo naomba nirejee takwimu husika kama ifuatavyo, kwamba kati ya watuhumiwa 26,191 waliokamatwa mpaka sasa kuna jumla ya kesi 89 tu zinazosubiri kusikilizwa Mahakamani. Katika vikao vya Mahakama Kuu vilivyokaa kuanzia mwezi Augosti hadi Octoba, 2013 hakuna kesi hata moja ya dawa za kulevya iliyosikilizwa na kutolewa hukumu, japo zilikuwa zimepangwa.
DHANA YA UHURU WA MAHAKAMA
Mheshimiwa Spika,
Natambua kuwa Mahakama ni muhimili unaojitegemea katika kutenda shughuli zake na iko huru. Natambua pia kuwa Bunge haliwezi kuingilia shughuli za Serikali au Mahakama. Lakini pamoja na uhuru huo, Bunge hili limekuwa linakosoa Serikali pale linapoona imekosea. Kwa ujumla lazima kuwe na checks and balance. Pamoja na mapungufu niliyoelezea hapo juu kuhusiana na mwendendo wa Mahakama katika kusikiliza kesi za dawa za kulevya, Mahakama imekuwa inafanya kazi zake bila kukosolewa na chombo kingine na ndiyo maana baadhi wamekuwa wakitumia dhana ya uhuru wa Mahakama vibaya.
Mheshimiwa Spika,
Kutokana na matumizi mabaya ya uhuru wa Mahakama kwa baadhi ya watumishi wa Mahakama, ni mapendekezo yangu kwamba Serikali iunde tume maalumu ya kiuchunguzi kuchunguza mwenendo wa kesi hizi za dawa za kulevya ili watakao bainika kuwa wametumia nafasi /wadhifa/ madaraka yao vibaya wachukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuvuliwa madaraka waliyonayo. Kwa kufanya hivyo, itaonyesha kuwa hakuna aliye juu ya sheria. Na itakuwa ni fundisho kwa wengine. Na taarifa ya Tume iletwe katika Bunge lako tukufu kwa hatua zaidi.
KESI KUSIKILIZWA NA MAHAKIMU WASIO NA MAMLAKA
Mheshimiwa Spika,
Kwa ujumla watuhumiwa wote wanaokamatwa wakisafirisha dawa za kulevya hutakiwa kufunguliwa mashtaka chini ya kifungu 16(1)(b)(i) cha sheria ya dawa ya kulevya. Kosa hili halina dhamana na husikilizwa na Mahakama Kuu peke yake. Hata hivyo baadhi ya Mahakimu wamekuwa wakilisikiliza kesi hizo na wengine kushirikiana na waendesha mashtaka hubadilisha hati ya mashtaka na kufanya wawe na mamlaka ya kusikiliza kesi hizo. Mfano ni shauri la Jamhuri dhidi ya Shirima (CC 433/2009).
Mheshimiwa Spika,
Katika shauri hili Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 02/05/2009 katika Bandari ya Dar es salaam akiwa na kilo 1 ya heroine yenye thamani ya Tshs. 18,000,000/=….Tarehe 05/05/2009 alifikishwa Mahakamani na kufunguliwa mashtaka chini ya kifungu cha 16(1)(b)(i) cha sheria ya dawa ya kulevya, tarehe 9/05/2009 hati ya mashtaka ilibadilishwa na mashtaka kuwa chini ya kifungu 12(d) ya sheria ya dawa za kulevya . Tarehe 14/7/2009 aliamriwa kulipa faini ya Tshs. 4, 000,000. Ubadilishwaji wa vifungu vya sheria katika hati ya mashtaka hulenga kuwasaidia watuhumiwa washtakiwe na makosa madogo badala ya yale makubwa yenye adhabu kubwa kisheria.
Mheshimiwa Spika,
Kifungu cha 16(1)(b)(i) cha sheria ya dawa za kulevya kinataja kosa la dawa za kulevya kuwa kosa ambalo halina dhamana. Hivyo waendesha mashtaka kwa kushirikiana na watuhumiwa hupendelea kuwafungulia mashtaka madogo chini ya kifungu cha 12(d) cha sheria ya dawa za kulevya. Katika kesi ambazo watuhumiwa walifunguliwa mashtaka chini ya vifungu ambavyo haviendani na makosa yao halisi , Mahakama zimekuwa zikitoa adhabu ndogo ya faini na kuwaachia huru! tena katika mazingira mengine kutoa hukumu ndogo kuliko ambayo imeainishwa katika sheria.
MAPUNGUFU YA SHERIA
Mheshimiwa Spika,
Sheria ya kuzuia dawa za kulevya haina adhabu kwa mtu anayesafirisha au anayekutwa na kemikali bashirifu (Chemical precursors). Kemikali hizi ni muhimu sana katika kutengeza dawa za kulevya aina ya Heroin na Cocaini, crystal-methamphetamine. Muathirika wa dawa crystal-methamphetamine hawezi kutibika maishani mwake (Permanent Brain Damage). Kwa sasa hivi kuna wimbi kubwa la uingizaji wa kemikali hizo zinazoenda kuangamiza nguvu kazi ya Taifa letu.
Mheshimiwa Spika,
Miongoni mwa matukio ya uingizaji na usafirishaji wa kemikali hizo ni kesi ya Saada Ally Kilongo aliyekamatwa uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere akiwa na 10 kilo za Ephedrine. Nyingine ni kesi ya Agnes Gerald Delwaya (Masogange) na mwenzake waliokamatwa Afrika Kusini wakiwa na kilo 150 za Ephedrine. Aidha, Rumishaeli Mamkuu Shoo na mwenzake wamekamatwa kwenye Kiwanda cha kutengeza Ephedrine nchini Kenya na tayari alikuwa na kilo hamsini (50) za kemikali hizo. Hawa watu licha ya madhara makubwa waliolitelea Taifa, wako mtaani wanapeta na kujipongeza!
Mheshimiwa Spika,
Kama hatutarekebisha sheria mapema iwezekanavyo, tutajikuta tunakuwa na kiwanda au viwanda vya kutengeneza dawa za kulevya hapa nchini. Hivyo, wauzaji badala ya kuagiza dawa hizo nje ya nchi, wataanza kutengeneza hapa na kuna taarifa kwamba pindi dawa za kulevya zinapokosekana wafanyabiashara huuza kemikali hizo na watumiaji wanatengeza wenyewe na kutumia.
Mheshimiwa Spika,
Kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kama hoja yangu ilivyoeleza, naomba Serikali ifanye mambo yafuatayo:-
1: Iunde Mahakama Maalumu, haraka iwezekanavyo itakayokuwa na jukumu la kushughulikia kesi za dawa za kulevya tu kama ilivyo Mahakama ya Biashara na iliyokuwa Mahakama ya Ardhi.
2: Ifanye marekebisho ya sheria ya dawa za kulevya kwa kuongeza makosa ya kusafirisha, kuuza au kukutwa na kemikali bashirifu
3: Iundwe Tume ya kuchunguza baadhi ya watendaji wa Mahakama na Serikali ambao kwa makusudi wamekuwa wakihujumu kesi za dawa za kulevya pamoja na jitihada za Serikali katika kupambana na biashara hii haramu na kuleta taarifa katika Bunge hili tukufu
4: Kiundwe haraka chombo huru chenye nguvu na mamlaka kamili kitakachokuwa na dhamana ya kupambana na dawa za kulevya nchini.
Mheshimiwa Spika,
Naomba kuwasilisha.

Bahati Bukuku apatwa msiba mzito, ampoteza baba yake

http://strictlygospel.files.wordpress.com/2008/04/bahati2.jpg
Pole Bahati Bukuku kwa kumpoteza baba
MUIMBAJI wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku amefiwa baba yake mzazi Mzee Paul Bukuku baada kuugua kwa muda mrefu. 
Marehemu amefia katika Hospitali ya Kardinali iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam na msiba upo nyumbani kwa Bahati maeneo ya Tabata, jijini Dar es Salaam.
MICHARAZO inatoa pole kwa Bahati Bukuku na familia yake kwa ujumla kwa msiba huo na kumtakiwa kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu kwa kutambua kuwa 'Kila Nafsi Itaonja Mauti, Mzee Paul Bukuku ametangulia na sisi tu nyuma yake.

Golden Bush kupongezana Dar kwa kupanda daraja


Kikosi cha Golden Bush Fc walipokuwa wakijiandaa na Ligi daraja la Nne Kinondoni
KLABU ya soka ya Golden Bush inatarajiwa kuwapongezana baada ya vijana wao, kufanikiwa kutwaa ubingwa wa wilaya ya Kinondoni na kupada Ligi Daraja la Tatu.
Golden Bush Fc inayonolewa na nyota wa zamani Madaraka Seleman 'mzee wa Kiminyio', Shija Katina na Wazir Mahadhi 'Mandieta', ikishiriki kwa msimu wake wa kwanza tangu isajiliwe ilifanikiwa kufunika Ligi Daraja la Nne na kupanda daraja.
Kutokana na kitendo hicho, uongozi wa klabu hicho chini ya melzi wao, Onesmo Waziri 'Ticotico' wameamua kuandaa hafla maalum ya chakula cha jioni siku ya Ijumaa kuwapongeza vijana wao.
Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi huo, shughuli hiyo itafanyika katika hoteli moja ya jijini Dar es Salaam, ingawa bado hawajaiweka bayana.
"Naomba nitoe taarifa kwamba ule mpango wa kuwa na dinner ya pamoja kama sehemu ya kuwapongeza vijana wetu kwa mafanikio madogo waliyoyapata katika ligi iliyomalizika hivi karibuni, utafanyika siku ya ijumaa tarehe 8 November 2013 hapahapa Dar es Salaam. Bado hujajua sehemu ambayo tutakutana lakini tutaendelea kupeana taarifa juu ya venue ambako event hii itafanyika."
Sehemu ya taarifa hiyo ya uongozi wa klabu hiyo ya Golden Bush maarufu kama Wakali wa soka jijini Dar kwa maveterani inasomeka hivyo. 
 

The Tanzanite kwenda Msumbiji kesho

KIKOSI cha timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) kinaagwa kesho (Novemba 6 mwaka huu) saa chache kabla ya kuanza safari ya kwenda Maputo, Msumbiji.
 
Hafla fupi ya kuikabidhi bendera Tanzanite itafanyika kesho saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF wakati kikosi hicho kinatarajiwa kupaa saa 11 jioni kwa ndege ya LAM na kuwasili Maputo saa 3.45 usiku.
 
Msafara wa Tanzanite ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 10-0 karibu wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Kidao Wilfred.
 
Mechi hiyo ya marudiano itachezwa Novemba 9 mwaka huu Uwanja wa Taifa wa Zimpeto, na timu itarejea nyumbani Novemba 10 mwaka huu saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.

TFF yataka orodha ya waliotolewa 'lupango' kwa msamaha wa Malinzi

Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliyewatoa kifungoni waliokuwa wamefungiwa katika soka
 SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma waraka kwa vyama vya mpira wa miguu vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuvitaka kuwasilisha orodha ya wote waliofaidika na msamaha wa Oktoba 28 mwaka huu.
 
Oktoba 28 mwaka huu wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu baada ya uchaguzi, Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote waliofungiwa kwa sababu mbalimbali.
 
Hata hivyo, msamaha huo hauwahusu waliofungiwa kutokana na makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya klabu.
 
Vyama vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha waraka huo unafika kwa wanachama wao (vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF inataka orodha ya wote waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake (records).

Ashanti Utd kumaliza vipi duru la kwanza kwa Simba?

Ashanti United
Simba
ASHANTI United iliyorejea Ligi Kuu Tanzania Bara ya kushuka mwaka 2007 iliianza ligi hiyo kwa aibu kwa kulala mabao 5-1 mbele ya Yanga na kesho itashuka dimbani kufungua mechi za duru la kwanza kwa kuumana na Simba.
Mashabiki wa kandanda wanapenda kujua klabu hiyo maarufu kama Wana wa Jiji watamaliza vipi kwa Simba, moja ya vigogo viwili vya soka Tanzania.
Walipoavaana na Yanga ilikuwa chini ya Hassani Banyai na kesho wakiivaa Simba ipo chini ya kocha mwingine Nico Kiondo, ambaye ameweza kuitoa timu hiyo katika unyonge iliyokuwa nao hapo awali, ingawa bado ipo katika ukanda wa hatari.
Simba wenyewe kwa sasa hawapo vyema baada ya kuporomoka toka kileleni mwa msimamo hadi nafasi ya nne ambapo hata kesho ikiifunga Ashanti haiwezi kutoka katika nafasi hiyo kwa vile timu zilizoitangulia zimevuka pointi ambazo itaweza kufikisha.
Simba kwa sasa ina pointi 21 na kama ikishinda itafikisha pointi 24, wakati Yanga, Mbeya City na Azam wenyewe wana zaidi ya pointi hizo.
Pambano hilo mojawapo kati ya manne yatakayochezwa kesho kuanza kufungia duru la kwanza litachezeshwa na mwamuzi Andrew Shamba kutoka Pwani na viingilio vyao vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. 
Waamuzi wasaidizi ni Abdallah Mkomwa na Rashid Abdallah wote kutoka Pwani wakati mezani atakuwa Hamisi Chang’walu.
Mbali na mechi hiyo, mapambano mengine ya kesho ni; JKT Ruvu Stars na Coastal Union (Uwanja wa Chamazi), Kagera Sugar na Mgambo Shooting (Uwanja wa Kaitaba, Bukoba) na Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Keshokutwa (Novemba 7 mwaka huu) raundi ya 13 kumaliza mzunguko wa kwanza itakamilika kwa mechi kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Rhino Rangers na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.

Kinyambe: Mvunja mbavu aliyegeukia muziki wa Injili

Kinyambe katika pozi zake za kisanii
MWENYEWE anasema baada ya kuwatumikia wanadamu kwa muda mrefu  kupitia fani ya uchekeshaji na muziki wa kizazi kipya, sasa ni wakati wake kuanza kumtumikia Mungu wake.
Mohammed Abdallah au James maarufu kama Kinyambe anasema anaamini ni vyema kukitumia kipaji alichojaliwa kumtumikia na kumtukuza Mungu kupitia muziki wa Injili.
Kinyambe anayesifika kwa kuigiza kama 'jitu zoba' huku akichezesha na kugeuza macho yake kama kinyonga, anasema anaamini njia ya kumshukuru Mungu kwa kipaji alichompa ni kuimba nyimbo za kumtukuza yeye.
"Wazo hili la kuimba muziki wa injili nilikuwa nalo kitambo kirefu, lakini nilibanwa na mambo ya dunia na kujikita zaidi katika kuchekesha na kuimba muziki wa kizazi kipya, ila kwa sasa naona nina nafasi ya kufanya hivyo."
Kinyambe anayetamba kwenye kipindi cha 'Vituko Show' na filamu mbalimbali za komedi anasema kwa kuanza kumtumikia Mungu amefyatua wimbo wa Injili unaoitwa 'Acha ya Dunia' aliomshirikisha muimbaji wa kwaya ya KKKT Makongolosi Chuya mkoani Mbeya, Mederick Sanga.
Mchekeshaji huyo anasema kibao hicho ni mwanzo wa safari yake katika miondoko hiyo, akipanga kutoa wimbo mmoja baada ya mwingine mpaka kukamilisha albamu hapo baadaye.
"Huu ni mwanzo tu, japo nitaendelea kuchekesha na kupiga muziki wa kizazi kipya," anasema.
Msanii huyo anadokeza kuwa, kuimba kwake miondoko ya Injili hakuna maana kwamba ameokoka bali anataka mashabiki wake kupata ladha tofauti.
Kinyambe aliyekuwa amepanga kufunga ndoa Julai mwaka huu kabla ya mipango yake kutibuka baada ya kutemana na mchumba wake, anafichua mchanganyiko wa majina yake kwa maana ya Mohammed na James inatokana na kuzaliwa na wazazi wenye dini mbili tofauti.
"Baba yangu mimi ni muislam na mama yangu ni mkristo. ndiyo maana unaona ninayo majina mawili, ila mie najiona niko kotekote tu kwa sababu ninayemuabudu ni Mungu tu," anasema.
Kinyambe (kushoto) akiwa na mchekeshaji mwenzake, Matumaini

UBUNIFU
Kinyambe anasema aliamua kubuni staili ya kuzungumza kama 'zuzu' na kuchezesha macho katika namna ya ajabu kama njia ya kutaka kusaka  mashabiki na kujitofautisha na wachekeshaji wengine.
"Niliamini bila ubunifu ni vigumu kuhimili ushindani, hivyo nikaibuka na staili hiyo, nashukuru nimepokelewa vema kiasi cha kujivunia," anasema.
Kinyambe anadai pamoja kujifanyisha makengeza na kuyageuza macho kila mara kama kinyonga, ukweli haumii wala kupata tabu kwa sababu ni jambo alilolizoea kulifanya kitambo kirefu.
"Sipati tatizo lolote kuyachezesha au kuyazungusha macho kama kinyonga hii ni kwa sababu nimeshazoea kwani nilianza kitambo kufanya hivyo tangu nikiwa shuleni," anasema.
Kinyambe aliyevutiwa kisanii na N!xau Toma 'Bushman', muigizaji nyota wa Namibia aliyecheza filamu za 'Gods Must Be Crazy', anasema kipaji cha sanaa ni cha kuzaliwa nacho kwani alianza kuvunja mbavu watu tangu akiwa kinda.
"Nilipokuwa mdogo, hasa shuleni nilikuwa kipenzi cha wanafunzi wenzangu kutokana  na tabia ya kuwachekesha, pia nilijishughulisha na sanaa ya uimbaji na uchoraji fani ninazoendelea nazo hata sasa," anasema.

MAFANIKIO
Kinyambe anayependa kula ugali kwa dagaa na kunywa maji na juisi tu, anasema jina lake la Kinyambe lina maana ya mkoba kwa lugha yao ya asili ya kabila la Kiwanji lililopo mkoani Mbeya.
"Niliamua kujiita hivi kama njia ya kumuenzi babu yangu kipenzi aliyekuwa na mkoba (kinyambe) aliokuwa akiutumia kuwekea vitu vyake hivyo nilipojitosa kwenye sanaa mwaka 2000, nilijipachika," anasema.
Kinyambe anasema tangu atumbukie kwenye sanaa hana mafanikio makubwa ya kujivunia, ingawa anashukuru fani imemwezesha kulamba ajira katika kampuni ya Al Riyamy Production na kupata umaarufu mkubwa unaomrahisishia mambo yake.
"Japo sina cha kujivunia, lakini nashukuru sanaa imenipatia ajira na pia kunikutanisha na wasanii wakubwa wenye majina kama akina Mzee Magari, Steven Kanumba, Jacklyne Wolper na wengine," anasema.
Msanii huyo mwenye matarajio ya kufika mbali kisanii pamoja na kimaisha, ili aje kuitunza vema familia yake na kwa sasa amekamilisha filamu zake nne anazotarajiwa kuzitoa moja moja. Filamu hizo ni Nyumba, Chumba cha Maiti, Polisi Feki, Fundi Kinyambe na Fumbafu Thana.
Kinyambe akiwa na msanii mwenzake Masai Nyota Mbofu
MUZIKI
Katika muziki msanii huyo aliyezaliwa mwaka 1985 Uyole mjini Mbeya akiwa mtoto wa pekee wa kiume na wa tatu kati ya watoto saba wa familia yao anatamba na nyimbo kama 'Maumivu' alioimba na Baguje, 'Maimuna' alioimba na Leila Tot na Erick Ivyoivyo na 'Kiduku Mpapaso' aliomshirikisha  Kesse.
Anasema lengo lake ni kufyatua albamu kamili itakayokuwa na nyimbo nane na kusisitiza kuwa, hajabahatisha kuingia kwenye muziki kwani ni fani anayoijua nje ndani kwa muda mrefu.
Tofauti na vijana wengi, Kinyambe anayemzimikia mkali wa zamani wa Daz Nundaz, Ferooz, hana mzuka kabisa na mambo ya soka, akidai hana timu yoyote anayeshabikia wala kufuatilia mchezo huo.
Kinyambe aliyesoma Shule ya Msingi Uyole pia ni mchoraji mahiri kazi aliyoifanya kabla ya kuingia kwenye sanaa miaka 13 iliyopita akipitia makundi mbalimbali, anawataka wasanii wenzake kutokata tamaa na hali nya vikwazo anavyokutana navyo akidai tukio la furaha maishani mwake ni siku alipokubaliwa kujiunga Al Riyamy.
"Kwa upande wa matukio ya huzuni ni vifo vya babu na mjomba wangu niliokuwa naiva  nao na kunisaidia mno," anasema.
Kinyambe akiwa studio akirekidi kazi zake
Baadhi ya makundi aliyopitia msanii huyo ni Ufunguo Sanaa, Greenwood na Mbeya Films na filamu alizocheza awali alipoingia kwenye fani hiyo ni 'Msitu wa Maajabu','Kiapo Changu', 'God is Great', 'Leathal Weapon, iliyomkutanisha na marehemu Steven Kanumba, ndipo akaonwa na Al  Riyamy alikojipatia umaarufu mkubwa.
Kinyambe anayelia na wezi wa kazi za wasanii na kuiomba serikali iwasaidie pamoja na  kuiwekea miundo mbinu itakayowawezesha wasanii kunufaika na kazi zao, anasema fani  ya filamu Bongo imepiga hatua kubwa kwa sasa tofauti na siku za nyuma.
Kinyambe anayependa kutumia muda wake kusikiliza muziki na kuangalia 'muvi', amewamwagia shukrani wazazi wake, bosi wake Khalfan Abdallah, Shery Madhira, Mzee Shebby na wasanii wenzake anaoshirikiana nao Al Riyamy kwa jinsi  walivyomsaidia kwa hali na mali kufika hapo alipo.

Mridu Ally aanzisha kundi la Taarab ni Bombastic Modern 'Wana B Kubwa'

Mridu Ally 'TX'
BAADA ya kuyatumikia makundi ya wenzake kwa muda mrefu, hatimaye mtunzi na mcharaza gitaa maarufu wa muziki wa taarab nchini, Mridu Ally 'Tx' ameanzisha kundi lake la miondoko hiyo liitwalo Bombastic Modern Taarab ' Wana B Kubwa'.
Akizungumza na MICHARAZO asubuhi hii, Mridu alisema kundi lake linaundwa na wasanii wasiozidi 10 baadhi wakiwa ni chipukizi na kutamba kama alivyoweza kuwainua chipukizi wengine waliokuja kutamba nchini ndivyo atakavyofanya kwa wasanii hao wapya.
Mrudi alisema kundi hilo linatarajia kuanza rasmi leo kwa kujitambulisha maeneo ya Tabata kabla ya kuendelea katika maonyesho yao ya mwishoni mwa wiki.
"Katika kuhangaika kwangu, nimejianzishi kundi langu binafsi linaliofahamika kwa jina la 'Bombastic Modern Taarab na linaundwa na wasanii kama nane hivyo wengi wao wakiwa ni chipukizi hasa kwa waimbaji, lengo nao kuwainua kama nilivyofanya kwa akina Tizo Mgunda, Salha Abdallah, Sikudhani Ally, Mauji na wengineo," alisema Mridu.
Mridu aliyewahi kulipigia kundi la Mlimani Park 'Sikinde' na kupitia makundi kama Babloom Modern na Dar Modern, alitaja kikosi kizima cha Bombatic kuwa ni yeye (Mridu) kama mpiga solo, gitaa la besi linangurumishwa na Mudi Dirima, na mpapasa kinanda ni Ally Juma 'Za Mkwezi'.
Safu ya uimbaji ina wasanii Mwafatu Mohammed, Nuru Njama, Mwajabu Mtinginya, Fatuma Jafari na Cheka Dadi.
"Tayari tumeshakamilisha baadhi ya nyimbo ambazo trutazitambulisha katika maonyesho yetu ya Jumatano na Ijumaa maeneo ya Tabata kavbla ya Jumamosi na Jumapili kuwepo Mwananyamala na Buguruni," alisema Mridu.
Mridu ndiye mtunzi wa nyimbo zilizowahi kutamba nchini kama 'Acha Shobo' wa Babloom, Pembe la Ng'ombe, Kitu Mapenzi na Malavidavi.