STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 2, 2014

Blind atua Mashetani Wekundu mtazame katika uzi mpya

Daley Blind aliyekamilisha uhamisho United
KLABU ya Ajax imethibitisha kuwa Daley Blind amejiunga na  Manchester United.
Vilabu hivyo vimefikia makubaliano kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani wiki iliyopita ambapo United na Ajax walikubaliana ada ya uhamisho wake kufikia pauni milion £14.2 hii ikiwa ni baada ya mawindo ya muda mrefu ya mashitani wekundu.
Sasa imethibtishwa kua Blind atakuwa akiichezea United msimu huu baada ya kufanikiwa vipimo vya afya na kukubali maslahi ndani ya mshahara wake na kigogo hicho cha Premier League.
Blind ni mtoto wa nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi Danny, ambaye alikuwa ni msaidizi wa bosi wa United Louis van Gaal katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi katika michuano ya kombe la dunia na alianza kucheza soka kama mlinzi wa kushoto kabla ya kugeukia katika nafasi ya ulinzi wa kati katika klabu ya Ajax.

Miyeyusho kuyeyushana na Emilio Mkwakwani Nov 5

Miyeyusho na Emilio katika pozi
Wakitunishiana misuli
BONDIA machachari wa ngumi za kulipwa anayeshikilia mataji ya WBF na UBO, Francis Miyeyusho anatarajiwa kupanda ulingoni jijini Tanga kuzipiga na Mtanzania anayepigana nchini Kenyam Emilio Norfat.
Mabondia hao watapambana katika pigano la uzito wa Feather (kilo 57) siku ya Novemba 5 kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mratibu wa pambano hilo Anthony Rutta alisema maandalizi yameanza kwa kumalizana na mabondia hao wenye sifa zinazolingana kwa sasa katika medani ya ngumi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
"Mabondia Francis Miyeyusho na Emilio Norfat wanatarajiwa kupanda ulingoni kupigana kwa mara ya kwanza Novemba 5 na watasindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi siku hiyo," alisema Rutta.
Rutta alisema itakuwa mara ya kwanza kwa Miyeyusho kupanda ulingoni mkoani Tanga sawa na ilivyo kwa Emilio anayeshikilia nafasi ya pili nchini katika uzito huo wa Feather kati ya mabodia 60.
Emilio anashikilia kwa sasa taji la Afrika Mashariki na Kati la WPBC na rekodi zinaonyesha amecheza michezo 27 akishinda 23 na kupoteza minne, wakati Miyeyusho amecheza 51 ameshinda 38 na kupoteza 11 na kudroo miwili..
Pambano la mabondia hao litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) ambalo Rutta ndiye Katibu Mkuu wake.

Falcao katika uzi mpya baada ya kutambulishwa Old Trafford

Falcao akiwa katika uzi mpya wa Mashetani Wekundu
Akiteta na Kocha msaidizi, Ryan Giggs

KLABU ya Manchester United imemtambulisha mshambuliaji wake mpya kutoka Monaco, Ramadel Falcao, huku baadhi ya mashabiki wakipigwa na butwaa na kitendo cha kuongezwa mshambuliaji kikosini badala ya mabeki safu inayoonekana kupwaya baada ya kuondoka kwa visiki Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na patrci Evra.

Ndege yaanguka Serengeti na kuua abiria wote


Ndege iliyopotea mapema jana ikitokea Mwanza kuelekea Magadi nchini Kenya, imepatikana huko eneo la Serengeti Mara, na abiria wote watatu waliokuwa kwenye ndege hiyo imetaarifiwa wamekufa.

WWF yatoa mafunzo kwa watumishi wa Manispaa ya Kinondoni

http://www.tic.co.tz/media/kinondoni.jpgSHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la WWF, limeendesha mafunzo kwa watumishi wa idara mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni , kuhusiana na ueneaji wa hewa ukaa na matumizi sahihi ya nishati jadidifu nchini.
Mafunzo hayo yametolewa na Mratibu kutoka WWF.  Teresia Olemako aliyesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha  watumishi wa umma wanakuwa na ufahamu juu ya kukabiliana na madhara ya hewa ukaa na umuhimu wa kutumia nishati jadilifu.
Alisema mafunzo hayo yanahusu watumishi kutoka mikoa mitatu ambayo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha ambao majiji na miji yao imeingia katika shindano la kimataifa la kukabiliana na utunzaji wa mazingira ambalo litafanyika mwakani kwa kushirikisha nchi 18 duniani, Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza.
Olemako alisema juhudi za WWF kwa kushirkiana na ICLEI ni kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya nishati jadilifu kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira ambao unachangia kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi kote duniani.
“WWF tumejipanga kushirikiana na watumishi wa mikoa hiyo niliyoitaja hapo juu kuhakikisha suala la kupunguza hewa ukaa na kuhimiza matumizi ya nishati jadilifu ni moja ya majukumu yao ambao watatumia mafunzo hayo kuwapatia wananchi elimu zaidi”, alisema.
Mratibu huyo wa Programu ya Nishati Jadilifu alisema mradi huo utakuwa ukitambaulika kwa kauli mbiu ya (Chakula, Nishati, Taka Ngumu na Maji) kutumika kama njia mbadala ya kukabiliana na uharibifu mazingira katika maeneo husika.
Alisema nishati jadilifu ikitumika ipasavyo itakuza uchumi wanchi pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na ukweli haina madhara na ipo kwa wakati wote hivyo ni vema kila mmoja kuwa balozi mzuri katika kuelimisha jamii.
Akizungumzia juu ya shindano hilo alisema ni vema kwa mikoa husika kufanya kila liwezekano ili kuweza kuleta ushindani wa kweli jambo ambalo linaweza kupelekea Tanzania kuibuka na ushindi ambao utakuwa kichochoe cha utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati jadilifu kuongezeka zaidi.
Aidha alisema kutokana na tathmin iliyofanywa na WWF inakadiriwa hadi mwaka 2025 jiji la Dar es salaam litakuwa na wakazi zaidi ya mil. 6.2 huku mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka mara mbili zaidi ya sasa jambo ambalo linahitaji kufanyika maandalizi mapema kabla hali haijawa mbaya.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Injinia Mussa Natty, alisema kila idadi ya watu inapoongezeka, miundombinu na mahitaji ya kibinadamu pia huongezeka hivyo kuifanya jamii kuboresha mahitaji muhimu.
Natty alisema kutokana na hali hiyo WWF inapaswa kuongeza juhudi zaidi za kutoa elimu na kusaidia utekelezaji wa miradi ambayo inaweza kuwa na tija kwa Taifa na wananchi wake kwa vizazi vijavyo kwani kutokufanya hivyo kunaweza kuwa sababu ya kuleta mitafaruku mijini.
Mkurugenzi huyo alisema miradi kama hiyo ikiwa endelevu ni wazi kuwa kila mwanajamii atakuwa balozi mzuri wa kuhitaji mbadilo chanya ambao hayatamuathiri yeye na kizazi chache.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza WWF Tanzania kwa kushirikina na WWW Sweden kwa kuja na mradi huu na manispaa yangu ikawa moja wapo naamini tutaufanyia kazi vizuri kwani sisi Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla tumeathirika sana na mabadiliko ya Tania nchi”, alisema.
“Pia kila mmoja wetu ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es salaam, anahitaji kuwajibika katika sehemu yake ili kuhakikisha mahitaji muhimu ya kibinadamu yanapatikana jirani na jamii ili kuiondoa jamii katika hali ya umasikini unaosababisha ukataji na uharibifu wa misitu”, alisema.
Naye Mwanasheria wa Jiji, Philip Mwakyusa aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe alisema jiji limeupokea mradi kwa mikono yote na watatoa ushirikiano kwa WWF ili iweze kutekeleza mradi huo kwa mafanikio makubwa na ya yenye tija kwa jiji.

Arsenal yamnyakua Welbeck wa Man Utd

http://articles.squarefootball.net/.a/6a00e5521030508834019104738508970c-pi 
KOCHA Arsene Wenger amefanya jambo la maana katika kutatua tatizo la safu yake ya ushambuliaji baada ya kukubali kumsaini kwa Pauni Milioni 16 mshambuliaji wa England, Danny Welbeck.
Kocha huyo wa Arsenal, alikuwa Italia kuthibitisha ahadi ya kucheza mechi hisani, ameonyesha hisani inaanzia nyumbani baada ya kuwapiga bao Spurs kwa kumsaini mshambuliaji huyo wa Manchester United.
Welbeck, anayeondoka Old Trafford baada ya kushindwa kumvutia kocha Louis van Gaal tangu Mholanzi huyo awasili msimu huu, awali alitolewa kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kwa Pauni Milioni 3.
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akalazimishwa kuuzwa moja kwa moja aka pate mwanzo mzuri mpya na kuisaidia Arsenal kuilazimisha United kupunguza bei kutoka Pauni Milioni 18 walizotaka awali kabla ya mchezaji huyo kusaini Mkataba wa miaka mitano.

Ajali yaua baba, mtoto akiwa hoi kwa majeraha

MTU mmoja aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili  T. 495 ALM aina ya Nissan Pick Up amefariki dunia katika ajali mbaya, huku mtoto wake akijeruhiwa vibaya maeneo ya Nane Nane  jijini Mbeya usiku wa kuamkia jana majira ya saa saba za usiku.
Dereva huyo aliyefariki dunia amefahamika kwa jina la Boniface Mwasoba alifariki dunia baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka katika maeneo hayo ya Nane Nane achali iliyopelekea pia kujeruhiwa kwa mtoto wake anayefahamika kwa jina la Willy Boniface Mwasoba mwenye miaka 7 na mwanafunzi wa shule ya msingi Mkapa na amelazwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.
Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika japokuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini, lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto kwa kuzingata sheria na alama za usalama wa barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Monday, September 1, 2014

Ebu angalia usajili kabla ya dirisha kufungwa usiku wa leo

http://static.goal.com/439600/439663.jpg
WAKATI dirisha la usajili kwa klabu barani Ulaya likifungwa usiku wa leo, chini ni baadhi ya wachezaji waliohama na kutua katika klabu zao mpya mpaka sasa tukielekea ukingoni.
  • Javier Hernendez 'Chicharito' ametua Real Madrid kwa mkopo akitokea Manchester United
  • Radamel Falcao ajiunga na Manchester United kwa mkopo wa msimu mzima
  • Arsenal inapigana kupata saini ya Matija Nastasic na Ron Vlaar
  • Lewis Holtby awasili Ujerumani Germany kwa mkopo wa kipindi chote cha msimu ambapo anajiunga na Hamburg
  • Tottenham inaongoza mbio za kumnasa Danny Welbeck ambapo Arsenal nao wanamtaka mshambuliaji huyo wa Manchester United
  • Mlinda mlango aliye na wakati mzuri katika klabu ya Chelsea Petr Cech anatakiwa na QPR
  • Arturo Vidal huenda akasalia Juventus baada ya Manchester United kushindwa mpango wa pauni milioni £30
  • Sandro anatgakiwa na QPR huku Tottenham wakihitaji pauni milioni £16
  • Victor Valdes yuko katika mazunguzmo ya kujiunga na Liverpool akiwa huru
  • Benjamin Stambouli amefanikiwa vipimo vya afya kabla ya kuelekea Tottenham
  • Neil Warnock anataka wachezaji wanne kujiunga na Crystal Palace 
  • Micah Richards beki wa Manchester City anaelekea kutua Fiorentina.
  •  Alvaro Morata ameondoka Real Madrid na kutua Juventus ya Italia kumpisha Chicharito
  • Dirisha la usajili linafungwa saa tano kamili usiku huu wa Jumatatu.

  • Dunga amrejesha Robinho kikosini

    KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Brazil, Dunga amemuita mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Real Madrid, Manchester City na AC Milan, Robinho kuziba pengo la majeruhi Hulk wa Zenith kwa ajili ya mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Colombia na Ecuador. 
    Dunga ambaye alitaja kikosi chake cha kwanza toka achukue mikoba kwa mara ya pili kutoka kwa Luiz Felipe Scolari baada ya Kombe la Dunia, amemchukua nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye ameichezea nchi hiyo mechi 92. 
    Robinho amerejea nyumbani Brazil kucheza katika klabu ya Santos ambayo ndio alianzia kucheza soka lake baada ya AC Milan kumuuza kwa mkopo wa mwaka mmoja. 
    Dunga aliyewahi kuinoa Brazil katika miochuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 kabla ya kutimuliwa sasa anaelekea katika mchezo dhidi ya Colombia utakaochezwa jijini Miami Ijumaa hii akiwa na wachezaji 10 pekee waliokuwepo katika kikosi cha Scolari. 
    Baada ya kukwaana na Colombia, Brazil itachuana na Ecuador huko East Rutherford jijini New Jersey Septemba 9 mwaka huu.

    Messi aanza na gundu, yathibishwa yu majeruhi

    http://www.barcapakistan.com/wp-content/uploads/2014/01/1388427761_extras_noticia_foton_7_3.jpgNYOTA wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi huenda  akawa nje ya dimba kwa kipindi kifupi baada ya kudaiwa kuumia paja jana wakati wa Ligi Kuu ya Hispania.
    Klabu ya Barcelona imetoa taarifa ikidai kuwa nyota wake huyo amepata majeraha ya paja katika mchezo waliopata ushindi mwembamba dhidi ya Villarreal jana. 
    Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, imedai Messi aliumia msuli wa nyuma ya paja katika mguu wake wa kulia lakini sio majeraha makubwa sana. 
    Pia ilithibitisha kuwa mshambuliaji wao mwingine Munir El Haddadi naye aliumia nyama na vipimo vya wote wawili vinatarajiwa kufanyika leo kujua ukubwa wa matatizo ya nyota wake hao. 
    Kuna hatari kubwa Messi akakosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Argentina na Ujerumani unaotarajiwa kuchezwa keshokuwa.

    Beki Manchester City Micah Richards atimkia Fiorentina

    http://www.ljsfoundation.org.uk/wp-content/uploads/2013/12/Micah-Richards_4.jpg
    Micah Richards
    BEKI wa klabu ya Manchester City, Micah Richards anatarajiwa kujiunga na klabu ya Fiorentina ya Italia baada ya kumaliza miaka 12 akiwa Etihad. 
    Richards, 26 tayari ameshawasili Italia na anatarajiwa kuwa Mwingereza wa 24 kuichezea klabu hiyo mara atakapokamilisha usajili wake. 
    Beki huyo alikuwa mchezaji muhimu ya kikosi cha City kilichonyakuwa taji la Ligi Kuu mwaka 2012 lakini amejikuta akikosa nafasi ya kucheza chini ya meneja Manuel Pellegrini aliyeibebesha ubingwa msimu uliopita. 
    City pia bado wanasiliza ofa kwa wachezaji wao Matija Nastastic, John Guidetti na Scott Sinclair ambao wanaonekana kutokuwepo katika mipango ya Pellegrini. 
    Richards ambaye ni mzaliwa wa Birmigham alifanikiwa kucheza mechi mbili pekee za Ligi Kuu msimu uliopita na alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.

    TFF ya Malinzi yaanza kumeguka, Mtawala abwaga Manyanga

    https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSQ7BeiDzxhk14-HL8gurpeyPz64Qn0tI8Gj2omoupD6K16O-zr_DKEXD68dKyPKFjspbnWu26oGUXv8rIqDr00euTQs8yEy_KCHcTtm_kVoj9G2e1gWXNpDmN1exK-AsWbAT_2YLhTlgN/s1600/DSC_0392.JPG
    Evodius Mtawala (kulia) akiwa na viongozi wenzake wa TFF kabla ya kubwanga manyang'a
    TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, aliyekuwaMkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya Kisheria katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Evodius Mtawala, ameachia ngazi katika nafasi hiyo.
    Inaelezwa kuwa
    Mtawala Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Simba,  alikuwa na hali ya kutokuelewana na uongozi wa shirikisho hilo na ndiyo chanzo cha kung'atuka TFF.
    Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, alithibitisha kuachia ngazi kwa Mtawala lakini akasema ni kutokana na sababu mbalimbali za taaluma yake ya uanasheria.
    “Ni kweli Mtawala hataendelea kufanya kazi TFF lakini ameamua kuchia ngazi mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali alizodai kwamba ni kujikita na taaluma yake zaidi kwa sasa, lakini mambo mengine juu ya hilo yatabaki kuwa siri baina yake na mwajiri wake.
    “Ila mpaka makubaliano ya mwisho yalieleza kuwa itakapofika mwisho wa mwezi wa nane (jana 31, Agosti) atakuwa tayari ameshakabidhi ofisi na kuendelea na masuala ambayo alidai anahitaji kujikita zaidi kulingana na taaluma yake,” alisema Mwesigwa.
    Mtawala amedumu kwenye wadhifa huo kwa miezi nane tu tangu alipoteuliwa Desemba 24, mwaka jana chini ya uongozi wa rais mpya, Jamal Malinzi. 

    Rasmi Chicharito mali ya Real Madrid

    Akiwa na jezi yake mpya ya Real Madrid na Rais wa klabu hiyo Perez
    Wakati akichukuliwa vipimo vya afya na kubainika yupo fiti
    Akiangunga saini ya kuichezea klabu hiyo bingwa ya Ulaya
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Mexico, Javier Harnendez Chicharito amefaulu vipimo vya kujiunga na klabu ya Real Madrid na amekabidhiwa jezi namba 14 kwa ajili ya kuichezea wababe hao wa Ulaya kwa mkopo akitokea klabu yake ya Manchester United.
    Chichirito ambaye hakuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu tangu alipotua akitokea kwao Mexico, amejiunga na Madrid akimpisha Ramadel Falcao aliyetokea Monaco aliyetua Old Trafford kwa mkopo vilevile.
    Mshambuliaji huyo alitua Ol Trafford mnamo mwaka 2010 na amenyakuliwa na Madrid ili kuchukua nafasi ya Alvaro Morata ambaye aliuzwa Juventus.

    Rais Kikwete atuma Salamu za rambirambi Mbeya

    http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/08/ajali-mbeya-298x295.jpg

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
    DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

    Telephone: 255-22-2114512, 2116898
    Website : www.ikulu.go.tz              

    Fax: 255-22-2113425



    PRESIDENT’S OFFICE,
          STATE HOUSE,
                  1 BARACK OBAMA ROAD,  
    11400 DAR ES SALAAM.
    Tanzania.
     

    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Abbas Kandoro kuomboleza vifo vya watu 10 vilivyotokea Mbalizi, Mkoani Mbeya tarehe 29 Agosti, 2014 baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace maarufu kama Daladala Na. T 237 BFB kugongana na lori aina ya Tata Na. T 158 CSV.   Katika ajali hiyo, watu saba wengine walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
    “Nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya watu 10 na wengine saba kujeruhiwa katika ajali hii iliyotokea siku chache baada ya ajali nyingine kutokea Mkoani Tabora iliyoua watu 19 na wengine 81 kujeruhiwa”, amesema Rais katika salamu zake.
    Rais Kikwete amesema mfululizo wa ajali hizi unaonyesha dhahiri kuendelea kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa umakini miongoni mwa madereva, hivyo jitihada zaidi zinatakiwa kufanywa kusimamia kikamilifu Sheria ya Usalama Barabarani na kufuatiliwa kwa karibu kwa mienendo ya wanaoendesha vyombo vya moto, ili ajali hizi ziweze kupunguzwa na hata kudhibitiwa kabisa katika barabara zetu.

    “Naomba upokee  salamu zangu za rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na ajali hiyo, na kupitia kwako naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa wafiwa wote kwa kupotelewa ghafla na wapendwa wao”Ameongeza.

    Rais Kikwete amesema anatambua machungu waliyo nayo wanafamilia, ndugu na jamaa wa watu waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo, lakini anawaomba wote wawe wavumilivu na wenye subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.

    “Ninawaombea kwa Mola majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea katika hali zao za kawaida ili waweze  kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika salamu zake. 


    Imetolewa na;
    Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
    Ikulu – Dar es Salaam.
    31 Agosti,2014

    Manchester United yamnasa Falcao kilaini

    http://img.thesun.co.uk/aidemitlum/archive/01643/falcao_1643245a.jpg
    Add caption
     
    KLABU ya Manchester United imezipiga bao klabu za Arsenal na Manchester City zilizokuwa zikidaiwa kumnyemelea  mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao baada ya nyota huyo kutua kwao kwa mkopo akitokea Monaco ya Ufaransa. 
    Falcao, 28 amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka muda mrefu kiangazi hiki kutoka Monaco ambao walimsajili kwa paundi milioni 50 mwaka jana. 
    Toka ametua Monaco Falcao amefanikiwa kufunga mabao 11 katika mechi 20 huku akikaa nje nusu msimu kutokana na majeruhi ya goti yaliyomsababisha pia kuikosa michuano ya Kombe la Dunia. 
    Mahasimu wa United katika Ligi Kuu Manchester City walishindwa kumuwania nyota huyo kwa sababu hawakuweza kumhakikishia namba katika kikosi chao. 
    Falcao pia alikuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na Arsenal, mabingwa wa Italia Juventus na mabingwa wa Ulaya Real Madrid.

    Sunday, August 31, 2014

    Chelsea yazidi kujiimarisha, Kagawa arejea Dortmund

    KLABU ya Chelsea imezidi kujiimarisha baada ya kukamilisha uhamisho wa Loic Remy kwa dau la Pauni Milioni 8 kutokaq QPR, huku Mjapan Shinji Kagawa wa Manchester United akirejea klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund.
    Remy aliyekuwa anatakiwa pia na Arsenal, anakwenda kuziba nafasi ya Fernando Torres aliyehamia AC Milan kwa mkopo wa muda mrefu.
    Uhamisho huu ni faraja kwa Remy ambaye sasa anakwenda kujiunga na klabu inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kocha Mreno, Jose Mourinho alihitaji mshambuliaji baada ya kumtoa kwa mkopo Torres.
    Katika kuelekea mwisho wa kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, Shinji Kagawa ambaye hakuwa akipewa nafasi kubwa ndani ya Mashetani WEkundu amerejea Ujerumani kuichezea Dortmund.
    Kiungo huyo amerejea Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 6.3, miaka miwili tu tangu aondoke klabu hiyo ya Ujerumani.
    Kagawa atasaini Mkataba wa miaka minne na Dortmund, ambayo ilimuuza Mjapani huyo United mwaka 2012 kwa Pauni Milioni 12.
    Shinji Kagawa akikabidhiwa uzi wake mpya wa Dortmund baada ya kuondoka Manchester Utd

    Remy: 'When I heard Chelsea wanted me I said "let's go" because they are one of the best clubs in the world.'
    Remy akisaini mkataba wa kujiunga na Chelsea
    Akionyesha uzi mpya wa klabu yake ya Chelsea

    Arsenal bado haijatulia, Sanchez aendelea kufunga

    Alexis Sanchez scores his first Premier League goal for Arsenal
    Sanchez akifunga bao la Arsenal
    Jamie Vardy goes close to putting Leicester 2-1 in frontYaya SanogoARSENAL imeendelea kugawa pointi bada ya kulazimishwa sare ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Engaland dhidi ya timu ya Leicester City uwanja wa ugenini.
    Vijana wa Arsene Wenger walilazimisha sare ya 2-2 na Everton kabla ya leo kupata sare ya 1-1 kwa Leicester City waliotanguliwa kufungwa bao katika dakika ya 20.
    Bao hilo liliwekwa kimiani na Alexis Sanchez kabla ya Leonardo Ulloa kulirejesha dakika mbili baadaye.
    Kwa matokeo hayo Arsenal wameongeza kibindoni pointi moja na kufanya wafikishe tano baada ya mechi tatu na itarejea nyumbani kuisubiri mabingwa watetezi Manchester city katika mechi ya ligi hiyo wiki mbili zijazo yaani Septemba 13.
    Bao la Sanchez ni la pili katika mashindano baada ya katikati ya wiki kufunga bao pekee lililoivusha Arsenal hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

    Falcao akana taarifa za kuitamani Real Madrid

    http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/002/646/272/hi-res-174611730-radamel-falcao-of-monaco-looks-on-during-the-the-pre_crop_north.jpg?w=630&h=420&q=75MSHAMBULIAJI Ramadel Falcao amekanusha taarifa kwamba anaitamani Real Madrid na kudai taarifa iliyoandikwa kwenye akaunti ya Twitter haikuandikwa na yeye ndiyo maana ilikuwa hewani kabla ya kufutwa.
    Mchezaji huyo toka Colombia anayeichezea Monaco amesema bado yupo Monaco na hajui chochote kuhusu kutaka kujiunga Real Madrid.
    Awali mitandao mbalimbali vilidokeza kiu ya Falcao kutaka kwenda Bernabeu Santiago na kuiacha kwenye mataa Manchester City iliyokuwa ikitajwa kumnyemelea.
    Done deal? Colombian international tweeted about his move to the Bernabeu before the message was deleted

    Yanga wamrejesha Bin Kleb, Mayay Jangwani

    https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigmMCsDvsvatO7Ks4FTRpYb65iIPD0Xa862O2e8CK7v0EhDcHssDgIXyv_bJwPuDmW59cl7Zc-Nh5AD4uAMSCAvfWlJKxXtEXn9UELzVdH7lBM-WosGhcclfjP5-3dbz961KZuVxvLyn8/s1600/MAYAI+NA+MOSHA.jpg
    Mayay
    https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgA5YySWRcd9L8IvN54wEhFTqZ-Q07h1s-mM2-pigTTJdzAF3bAu_Zf0UTublQc5qMflINX5-w3hdCTK0dKYtUDTLYbf9PsyRB8Ft_Z2Ity3wXAqyYXfsTiJVPtVvc2Az0TPm-D4GQdEPw/s1600/kleb.jpg
    Bin Kleb (kushoto)
    KLABU ya Yanga imeendelea kutangaza kamati zake ambapo safari hii katika uundwaji wa kamati hizo imewarejesha kundini Abdallah Bin Kleb na Ally Mayay.
    Ebu zisome mwenyewe hapo chini;
    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
    WAJUMBE Wenza wa Kamati ya Utendaji ya YANGA (Maendeleo ya Michezo), Ndugu Seif Ahmed na Engineer Isaac Chanji, wanapenda kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kwa wanaYANGA, wameunda Kamati ndogo chini ya Kamati ya Utendaji ya YANGA zifuatazo:

       1) KAMATI YA UFUNDI Wajumbe:
     1)  Duduma, Nassoro
     2)  Lamlembe, Roger
     3)  Malulu, Pascal
     4)  Msolla, Peter
     5)  Zangira, Steve

    2) KAMATI YA SOKA YA VIJANA NA WANAWAKE Wajumbe:
    1) Katwila, Shaban
    2) Kabisa, Jessica (Advocate)
    3) Mazwile, Isack  
    4) Mwita, George
    5) Tembele, Ally Mayay
    3) KAMATI YA MASHINDANO   
    Wajumbe:  
    1)  Cheyo, Magembe      
    2)  Didi, Ibrahim                  
    3)  Hussein, Ndama Risasi      
    4)  Katabalo, Moses             
    5)  Katunzi, Mudhamiri        
    6)  Kihanga, Pascal   
    7)  Kingo, Ray Shauri
    8)  Kleb, Abdallah Bin
    9)  Luhago, David  
    10) Lukumay, Samwel  
    11) Macha, Innocent   
    12) Maige, Jackson   
    13) Mahende, Mugaya   
    14) Makay, Sule       
    15) Malebo, Michael    
    16) Malume, Paul   
    17) Matata   
    18) Mbise, Anandumi Timothy   
    19) Mlangwa, David   
    20)  Mogha, John  
    21) Mutaboyerwa, Joseph John
    22) Ntimizi, Said  
    23) Nyambaya, Lameck
    24) Nyika, Hussein  
    25) Nyumbamkaly,
    26) Ramadhan, Fulgence 
    27) Rashid, Ahmed    
    28) Suleman, Majid    
    29) Tenga, Frank    
    30) Tindwa, Beda  
    31) Zakaria, Dr.    
       
    Ifahamike kwamba, kutakuwa na nyongeza ya uteuzi wa Wajumbe wengine wa Kamati za YANGA zilizotajwa hapo juu.
    Ndugu Seif Ahmed na Engineer Isaac Chanji Wajumbe Wenza wa Kamati ya Utendaji ya YANGA (Maendelo ya Michezo) watakuwa Wenyekiti Wenza wa Kamati zilizotajwa hapo juu.
    Kamati ya Utendaji ya YANGA, ina karibisha Wajumbe waliotajwa katika Kamati zilizotajwa hapo juu kwa dhamira njema kuwa watasaidia kujenga YANGA bora, na wanaomba ushirikiano kutoka kwa wanaYanga wote ili Wajumbe walioteuliwa waweze ketenda kazi zao vyema kwa manufaa ya YANGA.
    (YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO)
     (BENO NJOVU)  
    KATIBU MKUU WA YANGA

    Balotelli aiongoza Liverpool kuisambaratisha Spurs kwao, Villa yaua



    Liverpool beat Tottenham
    Nahodha Steven Gerrard akifunga bao la pili la Liverpool kwa mkwaju wa penati
    Gabby Agbonlahor
    Mshambuliaji wa Aston Villa akishangilia bao la kwanza jioni hii
    MSHAMBULIAJI mtukutu kutoka Italia, Mario Balotelli ameanza na mguu mzuri katika klabu ya Liverpool baada ya kuiongoza kupata ushindi mnono ugenini jioni hii dhidi ya Tottenham.
    Liverpool ilitoka kuangushiwa kisago na mabingwa watetezi waliishindili Spur kwa mabao 3-0 na kutibua rekodi ya wenyeji kushinda mfululizo katika Ligi Kuu ya England.
    Mabao ya Raheem Sterling katika dakika ya nane akimalizia kazi ya Hernandez na mengine ya kipindi cha pili toka kwa Nahodha Steven Gerrard dakika ya 49 na Alberto Moreno la dakika ya 60 yaliwapa ahueni vijogoo wa Anfield kw kuvuna pointi tatu muhimu.
    Mara baada ya kuhakikisha mabao matatu yametinga katika nyavu za wenyeji, kocha Branden Rodgers alimpumzisha Balotelli kuonyesha kuridhika na kazi aliyofanya uwanjani akishirikiana na wenzake.
    Katika mechi nyingine Aston Villa ikiwa nyumbani iliisasambua Hull City kwa mabao 2-1 na kuvuna pointi tatu na kuipeleka hadi katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 7 ikiporomosha Spurs iliyopigwa na Liverpool zenye pointi sita kila mmoja.
    Punde timu iliyorejea ligi kuu, Leicester City itaikaribisha Wapiga Mitutu wa London, Arsenal katika mechi ya mwisho kwa siku ya leo.

    Jaydee afunguka tuhuma za kutoka dogodogo

    https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgL_DpQDx_nAdT5tOkF7w7CRqf4ZEqOhdfaungIvQQOm2-kejqZl4c_br2e4pdFO3ujVgpDsYRF7zWn42K6xuC1tnZKuhadKif6fA33VmJ0W9jQZcd_ctk8bqBGb8J9xnF3QbvS1mtdQGo_/s400/DSC05503.JPGNYOTA wa muziki na mmoja wa wasanii wenye mafanikio makubwa nchini lakini asiye na makeke, Judith Wambura Mbibo 'Lady Jaydee' a.k.a Anaconda ameamua kujibu habari iliyoandikwa katika gazeti moja la udaku kuhusu kuwa na uhusiano na aliyewahi kuwa mtuma salamu maarufu kwenye redio, Meddy Ahmed aka ‘Mtoto wa Vitoto’.
    Kwenye habari hiyo, gazeti hilo linalotoka mara mbili kwa wiki lilidai kuwa Jaydee ambaye anadaiwa kuachana na mume wake Gadner G Habash ameonekana mara kadhaa na Mtoto wa Vitoto na kwamba amewahi kuonekana akiwa na gari lake.
    Kupitia Instagram, Jaydee ameandika:
    "Kuna habari za kuniudhi Ila hii imenichekesha. Kwahiyo mtoto wa vitoto ndio bwana angu???? Basi sawa nashukuru naona mmenianzia tena sasa picha za February Na nilizi post mwenyewe humu insta leo ndio mmeziona? Ukweli mnaujua mmeamua tu kuzingua ,,, wangapi wameshapiga picha na hiyo Range? Duuuh! !!!!! Shkamoooni Moyo wangu chuma. Pigeni mawe mpk mchoke Kama ambavyo mmekuwa mkifanya miaka yote na bado nipo hapa hapa.

    Huyu ndiye Shishiiii, Shilole achaaaa!



    KWA jina maarufu kama Shilole a.k.a Shishhhii Baby....wazazi wake walimpa jina la Zuwena Mohammed hapa ni katika mtokolezeo wake kupitia mtandao wa Instagram ni Hatareeeeeeee







    Hali ya Hewa yatahadharisha upepo mkali

    Manchester Utd yakaribia kumnasa Blind

    http://completesportsnigeria.com/wp-content/uploads/2014/07/Daley-Blind.jpg
    Delay Blind
    KLABU ya Manchester United imekubaliana na Ajax Amsterdam ya Uholanzi kutoa kitita cha pauni millioni 13.8 kumnunua mlinzi wa timu hiyo Daley Blind.
    Blind ambaye ana umri wa miaka 24 alikuwa katika kikosi cha Kombe la dunia cha Uholanzi chini ya mkufunzi Louis Van Gaal na inaelezwa amesalia kidogo kutua mikononi mwa kocha huyo anayeinoa kwa sasa Mashetani Wekundu ambao bado 'hawajatulia' katika Ligi Kuu ya England.
    Blind anaweza kucheza kama beki wa kushoto na pia beki ya kati na iwapo makubaliano hayo yatatiwa sahihi, huyo atakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na klabu hiyo.
    Manchester imeshatumia zaidi ya pauni millioni 130 katika msimu huu pamoja na kuvunja rekodi ya England kwa kusajili Angel Di Maria kwa kitita cha pauni 59.7 kutoa Real Madrid, pia  memnunua beki wa kushoto Luke Shaw, Marco Rojo na kiungo matata Ander Herrera.

    Hashim Lundenga, Mudhihir waula YANGA

    https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj4yNL9q6uZ3_Y7ChyphenhyphenVWuLmfwNb_d9RBKB_R_ZJnFvooPtDi93j6iUaRjWGU2KbL1T0QHStuRuv55PC-NQS7W9GWal5a-IpWotn8XCCqvjGpiP-fpjxlwrdvp_ecOr902eAsio1uJr8hTc/s400/7.JPG
    Hashim Lundenga
    https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUIOuKG1gEFHQ75A4FWOuoi7qU0z6y2quohlAWohSDzFhA8e-ufICebVNT3caSrlB2lYCCcrBM8VwFlCtgfA4IVuX0p0X07lmMtZRw2vAJpi6Enbb9ds0M-OgEGGwnI-WnclsNl_p27LM/s1600/9.jpg
    Mudhihir M Mudhihir (kulia)
    KLABU ya Yanga imetanga majina ya Kamati zake mbalimbali ambapo Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga na Mbunge wa zamani wa Mchinga na mmiliki wa bendi ya Mchinga Sound, Mudhihir M Mudhihir ni baadji ya waliokula 'shavu' Jangwani.
    Soma mwenyewe majina ya wanachama waliotangazwa na uongozi wa wababe hao wa soka nchini;
     
    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
    Mwanasheria Sam Mapande, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya YANGA –(Utawala Bora) anapenda kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kwa wana YANGA,ameunda Kamati ndogo chini ya Kamati ya Utendaji wa YANGA zifuatazo:

    1) KAMATI YA MAADILI
    Wajumbe:
     
    1) Fimbo, Mgongo Prof. (Advocate)
    2) Kabudi, Mpalamaganda Prof. (Advocate) 
    3) Njaa, Salehe Ramadhani (Advocate)
    4) Rashidi, Tausi Abdallah (Advocate)
    5) Tenga, Cathbert (Advocate)
     
    2) KAMATI YA NIDHAMU
    Wajumbe:
     
    1) Karua, Tedy 
    2) Lamlembe, Roger
    3) Kihanga, Pascal 
    4) Mahenge, Burton Yesaya
    5) Mudhihir, Mudhihir (Advocate)

    3) KAMATI YA SHERIA NA KATIBA 
    Wajumbe:
     
    1) Fimbo, Mgongo Prof. (Advocate)
    2) Gikas, Farija (Advocate)
    3) Kabisa, Jessica (Advocate)
    4) Kabudi, Mpalamaganda Prof. (Advocate) 
    5) Kambamwene, January (Advocate)
    6) Lupogo, Herman (Advocate)
    7) Madibi, Richard (Advocate)
    8) Mahenge, Burton Yesaya
    9) Mgongolwa, Alex (Advocate)
    10) Mkucha, Elisha (Advocate)
    11) Mudhihir, Mudhihir (Advocate)
    12) Njaa, Salehe Ramadhani (Advocate)
    13) Rashidi, Tausi Abdallah (Advocate)
    14) Tenga, Cathbert (Advocate)
    15) Tenga, Ringo Dr. (Advocate)
    16) Vedasto, Audax (Advocate

    4) KAMATI YA UCHAGUZI
    Wajumbe:
     
     1)  Kajole, Mustafa
     2)  Lundenga, Hashim Ibrahim
     3)  Makele, Bakili
     4)  Mlelwa, Daniel 
      5) Ngongolwa, Alex (Advocate)

    Ifahamike kwamba, kutakuwa na nyongeza ya uteuzi wa Wajumbe wengine wa Kamati za YANGA zilizotajwa hapo juu.

    Mwanasheria Sam Mapande, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya YANGA – (Utawala Bora) atakuwa Mwenyekiti wa Kamati zilizotajwa hapo juu.

    Kamati ya Utendaji ya YANGA, ina karibisha Wajumbe waliotajwa katika Kamati zilizotajwa hapo juu kwa dhamira njema kuwa watasaidia kujenga YANGA bora, na wanaomba ushirikiano kutoka kwa wanaYanga wote ili Wajumbe walioteuliwa waweze kutenda kazi zao vyema kwa manufaa ya YANGA.

    (YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO)

    (BENO NJOVU)
    KATIBU MKUU WA YANGA