| Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam |
| Wanafunzi shule Darasa la nne Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam |
| Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam |
| Wanafunzi wa Darasa la awali Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam Capt 5 |
| Wanafunzi waDarasa pili Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakicheza ngoma ya utamaduni (Ndolela) wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam |
| Skauti wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiruka sarakasi wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam |
| Mhitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, Colin Christopher akisoma hotuba wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam |
| Mkaguzi Mkuu wa Elimu Kanda, Shani Kanungira akitoa hotupa ya awali kabla ya mgeni rasmi wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam |
| Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Frank Makingi akizungumza Tuangoma Kigamboni Dar es Salaam wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo |
UONGOZI wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, umewaomba kuwa kuwakumbusha watanzania na hasa viongozi na wanasiasa kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu unakuwa wa amani na utulivu.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Fredrick Otieno alisema vurugu za aina yoyote kutokana na ushindani wa kisiasa unaweza kuiweka Tanzania pabaya na kuvuruga kila kitu na kuwapa wakati mgumu watoto na watu wengine wasiojiweka ambao wanahitaji utulivu na amani kufanya mambo yao.
Otieno aliyasema hayo wakati wa hotuba yake katika mafahari ya wanafunzi wa masomo ya awali wa shule hiyo ya Joyland yaliyonyika mwishoni mwa wiki Tuangoma Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
"Leo wanafunzi na watoto wanafurahi na sisi wazazi na walezi tunajumuika pamoja shuleni kuwapongeza wahitimu wetu, kama kunakuwa na vurugu hili haliwezi kufanyika na watoto hawatapata haki yao ya kusoma au kufurahia maisha yao duniani," alisema Otieno.
Aliongeza ni vema wanasiasa, viongozi na wananchi kwa ujumla kushiriki uchaguzi uliopo mbele yetu kwa amani na utulivu kwa hizo ni neema ambazo kwa mataifa mengine wanatafuta kwa vile nchi zao zimevurugwa kwa sababu na mambo hayo na mengine yaliyokimiza amani na utulivu.
Aidha aliwakumbusha wazazi nchini kote kujenga utamaduni wa kuwalipa ada watoto wao na kufuatilia nyendo za watoto wao wanapokuwa likizo na hata shuleni ili kurahisisha kazi kwa walimu katika kuwapa elimu itakayojenga misingi imara ya maisha yao ya baadaye. Alisema kwa mfano shuleni kwake wazazi na walezi wamekuwa wazito wa kulipa ada kiasi kwamba shule inadai zaidi ya Sh milioni 100, lakini wanashindwa kuwafukuza watoto kwa vile wanaamini hawana makosa yoyote na ndiyo maana wanataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao katika suala la elimu za watoto wao.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa hakuna hazina bora kama mtoto kupewa elimu ambayo huja kumsaidia ukubwani kwa kuzingatia kuwa dunia ya sasa inaendeshwa kisasa na bila elimu bora na ya kutosha ni vigumu kijana kusimama na kukabiliana na changamoto hizo.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Elimu Kanda, Shani Kanungira aliwasisitiza wazazi kutumia kujitolea na kutimiza wajibu wao kuwasomesha watoto badala ya kutumia fedha nyingi kwa mambo yasiyo na tija kwa watoto na familia zao kwa ujumla.
Shani alitoa nasaha yake kabla ya kumpisha Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Frank Makingi aliyesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kujenga utamaduni wa ushirikiano dhidi ya walimu wa shule wanazosoma watoto wao.
Makingi alisema siyo kila jambo la wanafunzi kuachwa mikononi mwa walimu tu, kadhalika alikumbusha kuwasaidia watoto katika kuwalea katika maadili mema ili kulifanya taifa kuwa na raia wema na viongozi wazuri na waadilifu wa baadaye.










Meneja
wa Manchester United Louis van Gaal Leo huko Old Trafford Jijini
Manchester alimtambulisha rasmi Mchezaji mpya Memphis Depay mbele ya
Wanahabari katika Mkutano maalum na pia kuthibitisha Mchezaji wa
Kimataifa wa Italy Matteo Darmian anaelekea England kukamilisha Uhamisho
wake kutoka Torino.
Nae Memphis Depay, mwenye Miaka 21 na
alienunuliwa Mwezi uliopita kutoka PSV Eindhoven ya Holland Klabu
aliyoisaidia kuwa Mabingwa Msimu uliopita huku yeye akiwa ndie Mfungaji
Bora wa Ligi, alisisitiza amejiunga na Manchester United ili kutwaa
Vikombe vyote vinavyowezekana na yeye atajituma hadi mwisho. 
KIUNGO wa kimataifa wa Uturuki, Arda Turan amekamilisha usajili wake katika klabu ya Barcelona baada ya kutia saini katika mkataba wa miaka mitano leo.
BAADA ya kuelekea kumpoteza mshambuliaji wake matata, Robin van Persie, klabu ya Manchester United imepanga kutoa kitika cha pauni Milioni 60 ili kumnasa mshambuliaji wa Kijerumani Thomas Muller.

STRAIKA Donald Ngoma wa FC Platinum ya Zimbabwe alitarajiwa kutua nchini jioni ya leo na ilitarajiwa jioni ya kesho angeishuhudia Yanga inayotaka kumsajili ikitambulisha nyota wake wapya katika pambano dhidi ya Sc Villa ya Uganda.
UNYAMA dhidi ya wanadamu umeendelea tena baa da ya Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye pwani ya Tunisia na kuwauwa watu 27.






KOCHA Mkuu Mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ameanza mambo yake baada ya kutangaza kikosi cha wachezaji 26 akimjumuisha kipa wa Yanga Ally Mustafa 'Barthez'.