STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 15, 2015

Azam wazidi kunoa makali Zanzibar

11846696_1009621735744849_7161429854397873130_n
Kikosi cha Azam kilipopelekea Kombe lao la Kagame Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete
BAADA ya kuikong'ota KMKM ya Zanzibar katika pambano lao la kirafiki, mabingwa wa Kombe la Kagame, Azam jioni ya leo inatarajiwa kushuka Uwanja wa Amaan kucheza mchezo wake wa pili visiwani humo wakiwa wamepiga kambi kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga wikiendi ijayo.
Azam chini ya kocha Stewart Hall imejichimbia humo ikiwa na kikosi chake chote isipokuwa Allan Wanga aliyepo Kenya alipoenda kwa matatizo, huku Mganda Brian Majwega akiwa ametemwa rasmi kikosini.
Mabingwa hao wanajaribu kusaka ushindi kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya Ngao ya Hisani kwani tangu mwaka 2012 haijawahi kushinda mbele ya Simba na Yanga waliowatungua mara mbili mfululizo ikiwamo mwaka 2013 walipowafunga bao 1-0 na mwaka jana kuwafumua mabao 3-0.
Azam inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam Jumanne baada ya kuwepo kwa taarifa ya ziara ya TP Mazembe kufutwa rasmi, na kabla ya kutimka visiwani inaelezwa kuwa huenda ikaiita URA ambayo leo inashuka Uwanja wa Taifa kucheza na Simba katika pambano la kirafiki la kimataifa, ili angalau kuwapa makali ya kuikabili Yanga ambayo ina hasira ya kung'olewa kwenye Kombe la Kagame kwa matuta.

Ratiba ya Ligi Kuu ya England wikiendi hii ipo hivi

optimized-premier-league-2015-2016-700x400

BAADA ya Mashetani Wekundu, Manchester United jana kupata ushindi na kukwea kileleni mwa Msimamo, Ligi ya England itaendelea leo na kesho kwa michezo kadhaa na ratiba kamili tunakuwekea kama ifuatavyo:

Jumamosi Agosti 15
14:45 Southampton vs Everton
17:00 Sunderland vs Norwich
17:00 Swansea vs Newcastle
17:00 Tottenham vs Stoke
17:00 Watford vs West Brom
17:00 West Ham vs Leicester
Jumapili Agosti 16
15:30 Crystal Palace vs Arsenal
18:00 Man City vs Chelsea

Jumatatu Agosti 17
22:00 Liverpool vs Bournemouth
 

Huku Simba, kule Yanga Utamu Ulioje!

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2015/08/KIKOSI.jpg
Kikosi cha timu ya Simba
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgBANjTf-2fkrx3RLm5RPaUrUbyBwYcFEdzPN7vo1to9_q2hUECoRKM5sjZMEd6wKlYjM72Itb9JeMgpbevjrJZAmBeXrbFiVN2ohR7iP20AWcyQ7rwfR__s4p6_Gx2dc7gmy0Ivy3BZ6R/s640/DSC_6726.JPG
Mabingwa wa Tanzania Yanga
WAKATI kocha Dylan Kerr akiwa na mtihani mwingine mgumu wa kutaka kuwathibitishia mashabiki wa Simba kwamba kikosi chake kimeiva wakati jioni ya leo Jumamosi watakabiliana na URA ya Uganda, watani zao Yanga wenyewe wataendeleza libeneke lao jijini Mbeya kesho kuwa kuumana na Mbeya City.
Mechi hizo za kirafiki ni maalum kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu, ambapo Simba yenyewe baada ya kuweka kambi ya mwezi mmoja na ushei katika wilaya ya Lusohoto, Tanga na Zanzibar imerudi jijini Dar es Salaam ikijifua Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini na leo itaumana na URA Uwanja wa Taifa.
Mechi hiyo ni ya sita kwa Kerr tangu apewe jukumu la kuinoa timu hiyo akimpokea Goran Kopunovic, akiwa na rekodi ya kushinda mechi zote, zikiwemo tano na timu za visiwani Zanzibar na moja ya kimataifa walipoumana na SC Villa ya Uganda kwenye tamasha la Simba Day Jumamosi iliyopita.
Simba inatarajiwa kuwatumia nyota wake wale wale iliyowatumia katika mchezo wao na Villa, huku ikiwa imeshamalizana na nyota wao wa kimataifa, Vincent Agban na Justice Majabvi.
Yanga wenyewe ambao wamekimbilia Tukuyu Mbeya baada ya kutolewa Kombe la Kagame, kesho Jumapili itaumana na Mbeya City katika mechi yao ya tatu jijini humo, awali ilianza kwa mkwara kwa kuitandika Kimondo Fc ya Mbozi kwa mabao 4-1 kabla ya bkuizabua Prisons Mbeya kwa mabao 2-0 na baada ya mchezo hio wa kesho itawasubiri Zesco ya Zambia na Bata Bullets ya Malawi kumaliza kazi kabla ya kurudi Dar kuisubiri Azam kwenye pambano la Ngao ya Hisani litakalochezwa Jumamosi ijayo.
Mechi hiyo ya Ngao ya Hisani itakayopigwa Uwanja wa Taifa ni maalum katika kuzindua msimu mpoya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara amabyo itaanza kutimua vumbi lake, Septemba 22.

Manchester United yafanya kweli Ligi Kuu ya England

Luke Shaw grabs Januzaj after his opening goal put Manchester United on course for their second consecutive victory
Januzaj akishangilia bao lake la wachezaji wenzake wa Man United
MASHETANI Wekundu, Manchester United usiku wa jana walifanikiwa kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kushinda baoa 1-0 ugenini dhidi ya Aston Villa.
Baoa pekee la dakika ya 29 lililofungwa na Adnan Januzaj limewawezesha vijana wa Louis Van Gaal kushinda mechi ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya England na kukaa kileleni ikiwa na pointi 6.
Pambano hilo lililochezwa Uwanja wa Villa Park, liliwahishwa kuchezwa kutokana na muingiliano wa masuala ya kijamii karibu na mji huo na Mashetani WEkundu wakaona wafanye yao mapema kabla ya kuelekea kwenye pambano lao la mchujo la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Warusi.
Januzaj alifunga bao hilo akimalizia pasi murua ya Juan Mata. Ligi hiyo itaendelea leo kwa michezo kadhaa, lakini kivumbi kitakuwa kesho kati ya Manchester City dhidi ya mabingwa watetezi Chelsea kwenye Uwanja wa Etihad, mjini Manchester. Tayari makocha wa timu hizo wametoa tambo zaom lakini Manuel Pellegrin amesisitiza ni lazima safari hii ampe mkono Jose Mourinho.

Hapana! Hii ni Barcelona kweli? Yapigwa 4-0 na Bilbao

Athletic Bilbao's defender Mikel San Jose points to the heavens after scoring an incredible goal to put the underdogs ahead
Wachezaji wa Bilbao wakishangilia mabao yao dhidi ya Barcelona
Gorka Iraizoz comes out to deny Luis Suarez as the former Liverpool man tries to round the home keeper and bring his side level
Suarez akijitahidi kuipiugania Barcelona, lakini wapi walilala 4-0
Mikel Balenziaga ushers the ball away from Messi as the home defence looked to minimise the impact of Barcelona's best player
Messi hakufurukuta kabisa
SIKU chache baada ya kufanikiwa kushinda UEFA Super Cup kwa mbinde kwa kushinda mabao 5-4 dhidi ya Sevilla, mabingwa wa Hispania, Barcelona imetoa ishara mbaya ya kwamba msimu huu huenda ikawa urojo baada ya usiku wa jana kupigwa 4-0.
Barca wamekumbana na kipigo hicho kwenye pambano la Super Cup la Hispania kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa La Liga na klabu ya Athletico Bilbao waliokuwa uwanja wa nyumbani.
Mabao matatu ya Aritz Aduriz na jingine la Mikel San Jose kwenye Uwnaja wa wa San Mames Barria, yalitosha kuizima Barcelona licha ya kuwa na nyota wake kadhaa akiwamo Messi na Luis Suarez.
San Jose alianza kumtungua kipa Marc-Andre ter Stegen dakika ya 13 kabla ya Aduriz kufunga mabao mawili ya haraka haraka dakika za 53 na 62.
Aduriz akakamilisha hat-trick yake kwa bao la mkwaju wa penalti, baada ya beki Dani Alves kumchezea rafu. 

Bayern Munich yatoa onyo mapema Bundesliga

Benatia (left) races away to celebrate following his 27th opener at the Allianz Arena
Wachezaji wa Bayern Munich wakipongezana baada ya kufunga moja ya mabao yao jana katika Bundesliga
Bayern striker Robert Lewandowski jumps for joy after the Poland striker made it 2-0 after the break
Robert Lewandowski akishangilia bao alililoifungia Bavarian usiku wa jana
MTAISOMA namba! Hivyo ndivyo Bayern Munich ilivyojitambulisha baada ya usiku wa jana kuanza vema Ligi Kuu ya Ujerumani wao kama mabingwa watetezi kwa kuikandika Hamberger kwa mabao 5-0.
Bavarians hao walipata ushindi huo kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo katika Uwanja was nyumabi wa Allianz Arena kwa mabao ya Robert Lewandowski, Mehdi Benatia, Thomas Muller aliyefunga mawili na Douglas Costa.

Edin Dzeko atua AS Roma toka Etihad

www.bukobasports.com
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester City Edin Dzeko amejiunga na klabu ya ligi ya Seria A Roma kwa mkopo.
Roma imetoa kitita cha pauni milioni 2.9, na nyingine pauni 7.9 zikitarajiwa kulipwa iwapo uhamisho huo utabadilika na kuwa wa kudumu.
''Nimekuja hapa kushinda mataji'',alisema Dzeko.
''Ninaweza kuahidi kitu kimoja kwamba nitajitahidi vilivyo katika kilabu hii''.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na kilabu ya Etihad kutoka Wolfsburg mnamo mwaka 2011 kwa pauni milioni 27.
Alikuwa ameweka sahihi ya kandarasi ya miaka minne katika uwanja wa Etihad msimu uliopita.
Hatahivyo,meneja manuel Pelegrini hivi majuzi alikiri kwamba Dzeko alikuwa na uwezo mkubwa kuondoka katika Etihad kufutia usajili wa Raheem Sterling kutoka Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 49.

Mtaipendaje Simba? Baada ya Agban kusaini sasa zamu ya Mzenji

Simba Day
Simba wakishangilia ushidni wa mechi yao na SC Villa ya Uganda siku ya Tamasha la Simba Day
KLABU ya Simba kwa hakika imepania msimu huu, kwani baada ya kumlambisha mkataba wa miaka miwili kiungo wake wa Kizimbabwe, Justice Majabvi, iliona haitoshi, ikamsainisha tena kipa Muivory Coast, Vincent Agban. Sasa kama  ulidhani walishamaliza kazi, umekosea kwa sasa klabu hiyo imemuita jijini kipa wa JKU-Zanzibar, Mohammed Abdulrahman ili kumalizana naye.
Kipa huyu ndiye waliyewahi kumtangaza mapema kwamba imemnasa kisha ikabainika kuwa bado ana mkataba mrefu na klabu yake kama ilivyokuwa pia kwa straika wa Vital'O, Laudit Mavugo.
Baada ya kutafakari kwa kina na hasa kutokana na kipa Ivo Mapunda kuwadengulia tangu wampe Sh. Milioni 10 za kusaini mkataba mpya, Simba ilipiga hesabu kumleta kipa Mbrazili, Ricardo Andrade, lakini ikamshtukia ana umri mkubwa mno, hivyo wakaachana naye.
Ndipo wakaamua kurudi kwa Abdulrahaman ambaye leo hii atatua jijini Dar es Salaam kumalizana na viongozi wa Simba tayari kuidakia timu hiyo katika michuano ya Ligi Kuu msimu wa 2015-2016.
Viongozi wa Simba wamekuwa wasiri katika suala la kipa huyo, lakini MICHARAZO inafahamu kuwa Abdulrahaman jana alikuwa Bububu na leo Jumamosi atapata boti kuitikia wito wa viongozi wa Simba ambao wiki sasa wamekuwa wakifanya mazungumzo naye na klabu yake ya JKU itakayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani,
Simba tayari imeshamshainisha kipa Agban aliyewahi kufanya majaribio timu ya vijana ya Chelsea na kuonekana kijeba na mwezi mmoja uliopita alikuwa akijifua na Azam kusaka nafasi ya kusajiliwa kabla ya kocha Stewart Hall kumpotezea kwa kuamini kazi nzuri ya Aisha Manula na Mwadini Ali.

Tuesday, August 11, 2015

Yaya Toure aibeba Man City, ikishinda ugenini

Yaya Toure akifunga moja ya mabao yake usiku wa jana kuisaidia Manchester City kushinda ugenini mabao 3-0
http://img.bleacherreport.net/img/images/photos/003/494/423/hi-res-b27d356a2da129aaa8e144db5c571976_crop_north.jpg?w=630&h=420&q=75
Vincent Kompany akishangilia bao lake lililokuwa la tatu kwa Man City
Ivorian midfielder Toure wheels away in celebration as Fernandinho congratulates his team-mate for the early strike
Oyooo Oyoooo! Man City wakishangilia mabao yao jana usiku
MANCHESTER City imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya West Bromwich.
City ilipata ushindi huo usiku wa kuamkia leo, huku Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure akifunga mabao mawili na kuipeleka timu yake kileleni mwa msimamo baada ya raundi ya kwanza.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure aliyefunga alianza kuifungia Manchester City dakika ya tisa baada ya shuti lake la umbali wa mita 20 lililombambatiza Boaz Myhill na kutinga nyavuni, kabla ya kufunga la pili dakika ya 24.

Nahodha wa Man City, Vincent Kompany akakamilisha ushindi mnono katika mchezo wa kwanza wa timu yake kwa kufunga bao la tatu dakika ya kwa kichwa 59.  

Mchezaji mpya, Raheem Sterling aliyesajiliwa kutoka Liverpool, alicheza vizuri katika kikosi cha City jana, lakini akapoteza nafasi nzuri na ya wazi ya kufunga.

Arsene Wenger awashushua wapambe nuksi

http://xmedia-nguoiduatin.cdn.vccloud.vn/149/2014/8/12/Arsene%20Wenger.jpg
BAADA ya kuanza Ligi Kuu ya England kwa kipigo cha nyumbani cha mabao 2-0 kutoka kwa West Ham United, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amewashushua wanaolazimisha afanye usajili ili kuimarisha kikosi chake kwa kusema huwa hakurupuki.
Wenger amesema kuwa hatakurupuka kukimbilia sokoni kutafuta wachezaji wapya kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa kiangazi baada ya kipigo cha kushtusha walichopewa.
Kipa Petr Cech ndio sura mpya pekee iliyotua Emirates katika kipindi hiki cha usajili na ameonekana kuanza vibaya kibarua chake hicho toka atoke Chelsea.
Kuna tetesi kuwa Wenger ameshatenga fungu kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema.
Lakini meneja huyo amesema hatakurupuka kusajili kwasababu ya kupoteza mchezo wao kwanza katika ligi kwani jambo la msingi ni kuangalia walipokosea na kurekebisha.

Depay ajiapiza kuhusu jezi No. 7

http://images.thepeoplesperson.com.s3-eu-west-1.amazonaws.com/wp-content/uploads/2015/06/12150615/memphis.jpg
Depay
UKISIKIA kujishtukia ndiko huku, Mshambuliaji Mpya wa Manchester United, Memphis Depay amesem ana uhakika kuwa ataweza kuitendea haki jezi namba namba aliyopewa na klabu hiyo kama nyota wengine waliowahi kuivaa.
Depay alipewa namba hiyo mashuhuri baada ya Angel Di Maria kuondoka kwenda PSG na kufuatia nyayo za nyota wengine waliowahi kuvaa jezi kama Cristiano Ronaldo, David Beckham, Eric Cantona na George Best.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi amesema yuko tayari kuitendea haki jezi hiyo kama ilivyokuwa kwa nyota wengine na kutamba kuwa atafanikiwa akiwa Old Trafford.
Depay aliendelea kudai kuwa anafahamu changamoto yake na historia lakini ana uhakika ataendelea kuimarika zaidi na kupata mafanikio kama ilivyokuwa kwa wengine.
Manchester ilianza Ligi Kuu ya England kwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur kwa bao la kujifunga la beki wa Spurs Kyer Walker.

Monday, August 3, 2015

Uchafu waikwaza Rio de Jeneiro Olimpiki 2016

Maeneo ya Fukwe za Rio De Jeneiro yatakayofanyika mashindano ya Olimpiki ya mwakani

Rais wa Kamati Kuu ya Kimataifa ya Olimpiki (OIC), Thomas Bach, amesema kuwa uchafuzi wa bahari ni moja ya kikwazo kwa jiji la Rio de Janeiro, Brazili katika maandalizi ya michuano ya hapo mwakani.
Hata hivyo kutokana na hali hiyo waandaji wa mashindano hayo ya riadha wamesema kuwa watafanya kila linalowezekana kwa afya ya wanariadha wakati wa Olympiki.
Takribani asilimia 70 ya maji taka yanamwagika Rio de Janeiro katika fukwe za Guanabara,eneo ambalo wapiga mbizi watafanyia mashindano yao.
Katika hali inayoonyesha ni hatari kwa afya wanariadha walioko kwenye mafunzo katika pwani hiyo wameona mizoga ya wanyama na uchafu ukiwa ukingoni mwa eneo hilo ambalo mashindano hayo yatafanyika.

Shule ya Joyland wahimiza amani Uchaguzi Mkuu 2015

Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Wanafunzi  shule Darasa la nne Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Wanafunzi  wa Darasa la awali  Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo  wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Capt 5
Wanafunzi waDarasa pili Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakicheza ngoma ya utamaduni (Ndolela) wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, Fedrick Otieno akiwasaidia watoto wa darasa la awali kupanda juu ya jukwaa kuimba wimbo maalum wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Skauti wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiruka sarakasi  wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mhitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, Colin Christopher akisoma hotuba wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Mkaguzi Mkuu wa Elimu Kanda, Shani Kanungira akitoa hotupa ya awali kabla ya mgeni rasmi wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam

Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Frank Makingi akizungumza Tuangoma Kigamboni Dar es Salaam wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo
Na Tariq Badru
UONGOZI wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, umewaomba kuwa kuwakumbusha watanzania na hasa viongozi na wanasiasa kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu unakuwa wa amani na utulivu.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Fredrick Otieno alisema vurugu za aina yoyote kutokana na ushindani wa kisiasa unaweza kuiweka Tanzania pabaya na kuvuruga kila kitu na kuwapa wakati mgumu watoto na watu wengine wasiojiweka ambao wanahitaji utulivu na amani kufanya mambo yao.
Otieno aliyasema hayo wakati wa hotuba yake katika mafahari ya wanafunzi wa masomo ya awali wa shule hiyo ya Joyland yaliyonyika mwishoni mwa wiki Tuangoma Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
"Leo wanafunzi na watoto wanafurahi na sisi wazazi na walezi tunajumuika pamoja shuleni kuwapongeza wahitimu wetu, kama kunakuwa na vurugu hili haliwezi kufanyika na watoto hawatapata haki yao ya kusoma au kufurahia maisha yao duniani," alisema Otieno.
Aliongeza ni vema wanasiasa, viongozi na wananchi kwa ujumla kushiriki uchaguzi uliopo mbele yetu kwa amani na utulivu kwa hizo ni neema ambazo kwa mataifa mengine wanatafuta kwa vile nchi zao zimevurugwa kwa sababu na mambo hayo na mengine yaliyokimiza amani na utulivu.
Aidha aliwakumbusha wazazi nchini kote kujenga utamaduni wa kuwalipa ada watoto wao na kufuatilia nyendo za watoto wao wanapokuwa likizo na hata shuleni ili kurahisisha kazi kwa walimu katika kuwapa elimu itakayojenga misingi imara ya maisha yao ya baadaye. Alisema kwa mfano shuleni kwake wazazi na walezi wamekuwa wazito wa kulipa ada kiasi kwamba shule inadai zaidi ya Sh milioni 100, lakini wanashindwa kuwafukuza watoto kwa vile wanaamini hawana makosa yoyote na ndiyo maana wanataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao katika suala la elimu za watoto wao.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa hakuna hazina bora kama mtoto kupewa elimu ambayo huja kumsaidia ukubwani kwa kuzingatia kuwa dunia ya sasa inaendeshwa kisasa na bila elimu bora na ya kutosha ni vigumu kijana kusimama na kukabiliana na changamoto hizo.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Elimu Kanda, Shani Kanungira aliwasisitiza wazazi kutumia kujitolea na kutimiza wajibu wao kuwasomesha watoto badala ya kutumia fedha nyingi kwa mambo yasiyo na tija kwa watoto na familia zao kwa ujumla.
Shani alitoa nasaha yake kabla ya kumpisha Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Temeke, Frank Makingi aliyesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kujenga utamaduni wa ushirikiano dhidi ya walimu wa shule wanazosoma watoto wao.
Makingi alisema siyo kila jambo la wanafunzi kuachwa mikononi mwa walimu tu, kadhalika alikumbusha kuwasaidia watoto katika kuwalea katika maadili mema ili kulifanya taifa kuwa na raia wema na viongozi wazuri na waadilifu wa baadaye.

Monday, July 20, 2015

Michael Olunga aipeleka Gor Mahia robo fainali Kagame Cup

http://www.standardmedia.co.ke/images/saturday/stdrclwhqpq.jpg
Michael Olunga
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKxRDIwrjKq6PNP8GUEXC5s6MqT9DpyWecXpY324qzrHOoXoIVRN1JTFo2JKNATy2Jsgaq2axLJ8TZAjWy9G7sdYv_QZSQK4XJBmlJA8gqO93Qfu2HMbmhFDE2Tvc2HSUBSkRfgJDIcrg/s1600/IMG_3285.JPG
Olunga (kulia) alipoikimbiza Yanga katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Kagame ambapo alifunga moja kuisaidia Gor Mahia kushinda 2-1
MSHAMBULIAJI nyota wa Gor Mahia, Michael Olunga ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kunyakua kiatu cha dhahabu katika michuano ya Kombe la Kagame baada ya jioni hii kutupia mabao mawili kambani wakati timu yake ikiizamisha KMKM kwa mabao 3-1.
Olunga alifunga mabao hayo katika kipindi cha pili na kuiwezesha Gor Mahia kuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza robo fainali ikitokea Kundi A kwa kukusanya pointi sita na mabao matano baada ya mechi yao ya awali kuitoa nishai Yanga kwa mabao 2-1.
Katika mechi huo wa kwanaa Olunga anayewindwa na Simba, ingawa ni ngumu kumpata kwani ana mkataba wa miaka miwili, alifunga bao moja.
Kwa kufunga mabao hayo mawili jana, imemfanya kuongoza orodha ya wafungaji wa michuano hiyo akiwa na magoli matatu akimzidi kete Sallah Bilal wa Al Khartoum ambaye alikuwa akiongoza kwa mabao mawili baada ya mchana wa leo kuingoza timu yake kuilaza Telecom kwa mabao 5-0.
Mara baada ya mechi yake ya Yanga, Olunga alinukuliwa akisema kuwa amekuja Tanzania akiwa na nia moja ya kuwa Mfungaji Bora wa michuano hiyo, kitu kinachoonyesha ni kweli baada ya kufanikiwa kufunga mabao hayo mawili.
Kabla ya Olonga kufunga mabao hayo, Meddie Kagere mkali mwingine wa Gor Mahia aliifungia timu hiyo bao la mapema akimalizia pande la Olunga kabla ya KMKM kusawazisha na kwenda mapumziki timu zikiwa sare ya 1-1 mpaka kwenye dakika ya 65 Olunga alipoanza kufanya yake na kuwazamisha Wazanzibar.

FIFA yatangaza tarehe ya uchaguzi wake mpya

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/04/Sepp-Blatter.jpg
Rais wa Fifa, Sep Blatter aliyetangaza kujiuzulu mrithi wake atapatika February
SHIRIKISHO  la Soka Duniani, FIFA limetangaza kwamba uchaguzi mkuu wa Rais utafanyika Februari 26 mwakani.
Maamuzi haya yamefanyika leo katika kikao cha kamati ya utendaji ya Shirikisho hilo kilichofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Sepp Blatter aliyejiuzulu siku nne baada ya kuchaguliwa amethibitisha kuwa ataendelea kukaa madarakani mpaka uchaguzi mkuu utapofanyika kupata mrithi wake.
Wakati huo, kundi la watu wanaoshinikiza  kufanyika kwa mageuzi wamekutana leo mjini humo wakimuomba katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan kuongoza mapinduzi hayo.
Kundi hilo limesema Annan ni mtu makini ambaye anapaswa kuongoza tume ya mageuzi wakati  huu Dunia ikielekea kupata mrithi wa Sepp Blatter aliyejiuzulu Urais kutokana na kashfa nzito ya rushwa iliyokumba FIFA.
Shirika la Ujasusi la Marekani, FBI liliwatia mbaroni Maafisa saba wa ngazi za juu wa FIFA kwa tuhuma za rushwa.

Stewart afungka mbinu walizoizamisha KCCA

Stewart Hall akiteta na Migi
KOCHA Stewart Hall ni mjanja sana, baada ya kufichua siri ya kuwaanzisha viungo wengi na kucheza soka la kujihami na kushambulia kwa kutumia mipira mirefu. Akizungumzia mbinu zake, Hall alisema alilazimika kutumia mbinu hiyo kwa sababu wachezaji wake wengi bado hawapo fiti. “Tupo katika kipindi cha maandalizi ya mwanzo wa msimu, wachezaji wangu Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu na Ramadhani Singano bado hawajawa fiti kwa asilimia mia, lakini naamini tutafika fainali.” alisema Hall Hall aliongeza kuwa timu inayomtisha zaidi ni Gor Mahia kwa sababu wamekuja wakati ligi ya Kenya inaendelea hivyo wachezaji wao wapo fiti.

UTAMU WA KOMBE LA KAGAME WAZIDI KUNOGA DAR

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AKh2imIAABZpVaY5ZwsQCBMD2%2BU&midoffset=2_0_0_1_4350124&partid=2&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000http://rushyashya.net/IMG/jpg/apr_fc_team_-_rwanda_-_kigalitoday-2-2.jpg
APR Rwanda
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/07/Yanga-leo-14.jpg
Yanga na Gor Mahia
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgU-pwUoReK1Inoqwa-tv9F7B4FsQQHzQW9GaG7wzubvb9SCAbF6zgGuLW0T-HTTo2ede7ls9zqJuGTrYNNSoghMV8GO4-5kfnAbuNX1yjWmHghK_qRzBu2MQ1YkUVYSo-N7z6p23PgLzs/s640/426464_358635040821389_1508036080_n.jpg
Al Shend
http://kabumbu.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/kikosi-azam-fc.jpg
Azam ya Tanznaia Bara
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYr-ePKerYIvN49hCZ9IJI-ICEdPieA86ey85RJHvQ131iGA6GEbCXWWbDogjLkjX3y6u7CQrhi07Wnmkj3cDy2Drr-O8hj23no_e0NxN6qDxt_0KSgzSb0084QpabXSEI7dIMJoRXD4bc/s1600/1385637_526389100785782_1638137288_n.jpg
Telecom ya Djibout
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg3v7qvqTyHyaPiHb4iJPQ2UjF7MIw0nVpNbqWGraZLfn3zrJ6t9J4bGJ0Ok268cn_goKj9RqzWVvhzIbNvWOTsBfGmrrJGfaTXfZfAcFez2kVA97hfblC6PDlqUiHoUIKjm5SeoML2U9q_/s1600/IMG_9898.JPG
KMKM ya Zanzibar
http://entebbenews.com/wp-content/uploads/2014/09/KCCA-Mulindwa-9.jpg
KCCA ya Uganda
Kikosi cha Yanga

Kikosi cha Gor-Mahia

Mchezaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwa chini huku wachezaji Collins Okoth (kulia) na Harun Shakava (kushoto) wa Gor Mahia ya Kenya wakiwania mpira wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Kagame uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imefungwa mabao 2-1.
Mashabiki wa Yanga

MICHUANO ya Kombe la Kagame imezidi kushika kasi ikiwa inaingia siku yake ya tatu leo tangu yalipofunguliwa rasmi siku ya Jumamosi, huku Al Khartoum ya Sudan ikitoa onyo kwa kuopata ushindi wa kishindi mchana huu dhidi ya Telecom ya Djibout.
Wawakilishi hao wa Sudan waliokuwa sambamba na Al Shandy kuchukua nafasi za mabingwa watetezi Al Merreikh na Al Hilal waliitandika bila huruma Telecom kwa mabao 5-0 na kukwea kileleni mwa Kundi A, ingawa kwa sasa Gor Mahia inayokamata nafasi ya pili na KMKM waliopo nafasi ya tatu wakiendelea kutifuana kwenye Uwanja wa Taifa.
KMKM ambayo ilichukuliwa poa katika kundi hilo, inaendelea kuonyesha kuwa haisindikizi mtu kwani ilitanguliwa kufungwa bao la kwanza na Gor Mahia iliyowazamisha Yanga kwa mabao 2-1 katika pambano la ufunguzi juzi, lakini ikakomaa na kulirejesha dakika tisa baadaye.
Wakenya walipata bao la mapema dakika ya tatu kupitia Meddie Kagere aliyemaliza pande tamu la Michael Olunga ambao ulimbabatiza beki mmoja wa KMKM na kumpoteza kipa wao, lakini Simon Mateo alifunga bao dakika ya 12 tu ya mchezo na muda huu wametoka kukosa bao la wazi.
Mpaka sasa wakati karibu timu zote zikiwa zimeshacheza mechi moja moja, Yanga na Telecom ndio wanaoburuza mkia katika kundi A zikiwa hazina pointi, ingawa Yanga wanakamata nafasi ya nne.
Katika Kundi B, APR ya Rwanda inaongoza msimamo baada ya kuishinda Al Shandy kwa bao 1-0 katioka mchezo wa kwanza, huku timu za Heggan ya Somalia na LLB AFC ya Burundi zinafuatia baada ya jana kutoka suluhu ya kutofungana.
Malakia ya Sudan Kusini inaongoza kundi C ikiwa na pointi tatu sawa na Azam iliyoitambia KCCA ya Uganda jana, lakini wanatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa. Malakia iliitambia Adama City ya Ethiopia kwa bao 2-1, wakati Azam yenyewe iliishinda KCCA bao 1-0.
Mpaka muda huu unaosoma blogu hii jumla ya mabao 18 yameshatinga wavuni kwa mechi 8 zilizokwisha kucheza mpaka sasa baada ya jioni hii Gor Mahia kuitambia KMKM kwa mabao 3-1.


Utamu wa michuano hiyo upo hivi kwa mwaka huu wa 2015
MAKUNDI:

KundiA: Yanga-Tanzania, Gor Mahia-Kenya, Khartoum-Sudan, Telecom-Djibout, KMKM-Zanzibar
Kundi B: APR-Rwanda, Al Shandy-Sudan, LLB-Burundi, Heegan-Somalia,
Kundi C: Azam-Tanzania, Malakia-Sudan Kusini,  KCCA- Uganda, Adama City- Ethiopia.

Viwanja:
Taifa- Temeke
Karume-Ilala


MATOKEO:

APR              1-0  Al Shandy
KMKM           1-0  Telecom
Yanga           1-2  Gor Mahia
Adama City   1-2  Al Malakia
LLB              0-0   Heegan
Azam           1-0   KCCA
Telecom        0-5  Al Khartoum
Gor Mahia     3-1  KMKM
 

MSIMAMO:
Kundi A:
                      P  W  D  L   F  A PtsGor Mahia       2   2   0  0   5  2  6Al Khartoum    1   1   0  0   5  0  3
KMKM             2   1   0  1   2  3  3
Yanga             1   0   0  1   1  2  0
Telecom          2   0   0  2   0  6  0

Kundi B:
                     P  W D  L  F  A Pts
APR               1   1  0  0  1  0  3
LLB AFC         1   0  1  0  0  0  1
Heegan          1   0  1  0  0  0  1
Al Shandy      1   0  0  1   0  1  0

Kundi C:

                     P  W D  L  F  A  Pts
Al Malakia       1  1 0  0  2  1   3
Azam              1  1 0  0  1  0   3
Adama City     1  0  0  1  1  2  0
KCCA              1  0  0  1  0  1  0

Wafungaji:

3-Michael Olunga         (Gor Mahia)

2- Salah Bilal               (Al Kahrtoum)
1- Ousmaila Baba         (Al Khartoum)
    Haruna Shakava       (Gor Mahia)
    Michael Olunga         (Gor Mahia)
    Kirkir Glay (og)         (Gor Mahia)
    John Bocco               (Azam)
    Bizimana Djihad        (APR)
    Takele Elemayehu     (Malakia)
    Samuel Ssekamatte  (Malakia)
    Jafar Delil                 (Adama City)
    Juma Mbwana           (KMKM)
    Wagdi Abdallah         (Al Khartoum)
    Murwan Abdallah      (Al Khartoum)
    Meddie Kagere          (Gor Mahia)
    Simon Mateo            (KMKM)
    Meddie Kagere          (Gor Mahia)
RATIBA
KESHO Jumanne

Saa 8 Mchana  Al Shandy vs LLB-Karume
Saa 10 Jioni     Heggan vs APR-Karume
Saa 10 Jioni     Malakia vs Azam-Taifa

Jumatano

Saa 10 Jioni     Khartoum vs KMKM-Karume
Saa 8 Mchana  KCCA vs Adama City-Taifa
Saa 10 Jioni     Telecom vs Yanga-Taifa

Julai 23

Saa 8 Mchana  Hegaan vs Al Shandy-Taifa
Saa 10 Jioni     APR vs LLB-Taifa

Julai 24

Saa 8 Mchana  Khartoum vs Gor Mahia-Taifa
Saa 10 Jioni     KMKM vs Yanga-Taifa

Julai 25

Saa 8 Mchana  KCCA vs Malakia-Taifa
Saa 10 Jioni     Adama City vs Azam-Taifa

Julai 26

Saa 8 Mchana  Gor mahia vs Telecom-Taifa
Saa 10 Jioni     Yanga vs Khartoum-Taifa

Julai 27 Mapumziko
Julai 28-Robo fainali
B1 vs A3
A1 vs Best Looser

Julai 29
B2 vs C2
Ca vs A2

Julai 30-Mapumziko

Julai 31-Nusu Fainali
Winner B2/C2 vs C1/A2
    ""      B1/A3 vs A1/Best Looser
Agosti 01-Mapumziko

Agosti 02-Fainali

Saturday, July 11, 2015

DK SLAA NDIYE MGOMBEA URAIS WA UKAWA

WAKATI CCM ikiendelea na mchakato wake wa kumteua mgombea mmoja wa Urais miongoni mwa wagombea watano waliopitishwa na Kamati Kuu ya chama hicho, Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA) wamemaliza udhia kwa kumteua Mgombea wao wa Urais kwa Uchaguzi wa 2015.
.

Baada ya jina la katibu Mkuu wa Chadema Dk Wibroad Slaa likiwa limeteuliwa na UKAWA kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.
Dakika chache zilizopita kwenye ukurasa  wa @twitter wa Dr Slaa kathibitisha kuteuliwa na UKAWA.
.

Nashukuru UKAWA kwa imani kubwa. Kazi ya mabadiliko iliyoanza 1992 kwa vyama vingi imebakiza miezi michache kushinda. Kura yako ni ukombozi –  @willibrordslaa
Nashukuru UKAWA kwa imani kubwa. Kazi ya mabadiliko iliyoanza 1992 kwa vyama vingi imebakiza miezi michache kushinda. Kura yako ni ukombozi.