STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 16, 2013

Hivi ndivyo Kigogo wa CCM alivyokumbwa na mauti Mwanza

 Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kushambuliwa 
Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa Bugando.
Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina enzi za uhai wake
---
MWENYEKITI wa zamani wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza Clement Mabina, ambaye pia ni diwani wa kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza ameuawa na wananchi wenye hasira katika ugomvi wa mashamba.

Tukio la kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa Ccm Mkoa wa Mwanza ambaye alishindwa katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mwanza mwaka jana na Waziri wa zamani na Mbunge wa zamani wa Ilemela Dk Antony Diallo lilitokea jana  katika eneo la kijiji cha Kanyama wilayani Magu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa polisi wa wilaya(OCD) ya Magu ODC Mkapa pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga zimeeleza kuwa tukio limetokea majira ya saa mbili asubuhi.

ODC Mkapa alikiri kutokea kwa tukio la kupigwa na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm Mkoa na Mwenyekiti wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu baada ya kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi wa eneo la kijiji cha Kanyama alikokuwa na shamba lake alikokuwa amekwenda kupanda miti.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga alisema kuwa amepokea taarifa za kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kutokana na ugomvi wa mashamba na kuelezwa kuwa amesikitishwa sana na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu.

Taarifa zaidi toka eneo la tukio la Kanyama kulikotokea mauaji hayo zimeeleza kuwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa CCM alifika katika eneo hilo majira ya asubuhi kwa ajili ya kupanda miti katika eneo la milima ya Kanyama ambalo analimiliki ambavyo hata hivyo linadaiwa kuwa na mgogoro baina yake na wananchi.

Baada ya kufika katika eneo hilo,wananchi nao walifika katika eneo hilo na kumhoji sababu za kupanda miti katika eneo hilo ambalo bado lina mgogoro wa umiliki na kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi.

Baada ya majibishano ya muda mrefu na kuona wananchi wameanza kumzingira Mabina aliamua kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao ambapo kwa bahati mbaya mojawapo ya risasi hizo zilimpiga mtoto aliyekuwa katika eneo hilo na kupoteza maisha.

Taarifa hizo toka katika eneo hilo la tukio zimeeleza kuwa kutokana na tukio hilo wananchi walimzingira Mabina na kuanza kumpiga kwa silaha mbalimbali za jadi kama vile mapanga, fimbo, mawe, mikuki na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kabla ya kurejea chama cha mapinduzi (CCM) na kufanikiwa kuwa diwani wa Kata ya Kisesa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mabina aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi na aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo mwaka 1995 na kushindwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Malaki Lupondije.

Saturday, December 14, 2013

Yanga yaipigisha kwata KMKM uwanja wa Taifa












Kikosi cha Yanga kilichoisulubu KMKM jioni ya leo
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imeipigisha kwata maafande wa KMKM ya visiwani Zanzibar kwa kuicharaza mabao 3-2 katika pambano la kirafiki lililoichezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo dhidi ya KMKM ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya Nani Mtani Jembe kati yao na Simba litakalochezwa kwenye uwanja huo wa Taifa Jumamosi ijayo.
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts alimuanzisha langoni mlinda mlango Juma Kaseja katika mchezo huo ikiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na Yanga katika kipindi cha usajili dirisha dogo, huku msomi Reliants Lusajo akianza katika nafasi ya dimba kubwa.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa timu zote kucheza taratibu huku zikisomana na Yanga ndo ilikuwa ya kwanza kufanya mashambulizi langoni mwa KMKM lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake kulipelekea kupoteza nafasi hizo.
Dakika ya 43 mshambuliaji Jerson Tegete aliipatia Yanga bao la kwanza na kuifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele kwa bao moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga wakisaka mabao ya haraka haraka, Nahodha Nadir Haroub "Cannavaro" aliipatia Yanga bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira uliorushwa na mlinzi wa kati Mbuyu Twite.
Mabadiliko yaliyofanywa na Brandts ya kuwatoa Nadir Haroub, Reliants Lusajo, Oscar Joshua, Jerson Tegete, Didier Kavumbagu, Nizar Khalfan yaliwapelekea KMKM kupata mabao mawili ya haraka haraka kufuatia uzembe wa walinzi na kufanya matokeo kuwa 2-2.
Dakika ya 84 ya mchezo kiungo Hamis Thabit aliipatia Yanga bao la tatu na la ushindi kwa shuti kali nje ya eneo la hatari ambapo mlinda mlango wa KMKM aliruka bila mafanikio.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3-2 KMKM.
Mara baada ya mechi ya leo kocha mkuu wa Yanga Ernie Brandts amesema vijana wake walipunguza umakini katika mchezo hasa kipindi cha pili hali iliyopelekea KMKM kupata mabao mawili lakini kikubwa nashukuru waliweza kupigana na kupata ushindi.
Mabingwa hao wa visiwani Zanzibar, KMKM kesho itashuka tena dimbani kupepetana na Simba katika mchezo mwingine wa kirafiki katika ziara yake ya jijini Dar es Salaam.

Andy Cole nyota wa zamani wa Man Utd atua Tanzania

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimkaribisha Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) mara tu baada ya kuwasili nchini kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kati kati ni Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole akikabidhiwa maua mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania .
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kushoto) akimuongoza Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (katikati) kuelekea sehemu ya VIP kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)mara tu baada ya kuwasili nchini jana usiku.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) pamoja na Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (kulia) wakikamilisha taratibu zakupata hati ya kuingia nchini kwenye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania .
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimuelekeza jambo Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (katika) mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kushoto ni Picha na Mpiga picha wetu. Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (mbele) akitoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwelekea hotelini alipofikia mara bada ya kuwasili nchini jana usiku. Nyuma yake ni mwenyeji waka ambaye ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando . 
Picha kwa hisani ya AIRTEL TANZANIA

Chelsea yaipumulia Arsenal kileleni, Everton yaua

Fernando Torres and Willian
Torres akipongezwa baada ya kuifungia Chelsea
Leon Osman
Everton wakiwatungua Fulham

VIJANA Jose Morinho, Chelsea muda mfupi uliopita imepata ushindi muhimu wa mabao 2-1 ikiwa uwanja wa Stanford Bridge kwa kuicharaza Crystal Palace.
Bao la kwanza la Chelsea kutumbukiwa wavuni na Fernando Torres katika dakika ya 16 kabla ya Marouane Chamakh kuisawazishia wageni dakika ya 29.
Katika dakika ya 35 Ramires aliiongezea Chelsea bao la pili na kudumu hadi wakati wa mapumziko na hata kipindi cha pili kilipoanza matokeo yalibaki hivyo na wenyeji kuvuna pointi tatu na kukamata nafasi ya pili nyuma ya Arsenal waliopigwa mchana wa leo.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Everton walikwea hadi nafasi ya nne baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 wakiwa nyumbani dhidi ya Fulham,  huku Newcastle United ilibanwa nyumbani na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Southampton.
West Ham United nayo ikiwa nyumbani ililazimishwa suhulu ya bila kufungana dhidi ya Sunderland, ilihali Cardiff City ilipata ushindi wa kushtukiza wakiwa nyumbani kwa kuilaza West Brom kwa bao 1-0.
Hull City muda mchache uliopita imeanza pambano lake dhidi ya wageni wao Stoke City katika pambano jingine la kufungia dimba siku la leo kabla ya kesho kushuhudiwa kivumbi cha mechi nyingine tatu.

Arsenal nyang'anyang'a kwa Manchester City

Yaya Toure akiwajibika uwanjani kuisaidia City kuiua Arsenal mabao 6-3

Kun Aguero akishangilia bao lake lililofungua kapu la mabao kwa Arsenal leo
MASHABIKI wa klabu ya Arsenal, vinara wa Ligi Kuu ya England leo watalala wakiota njozi mbaya baada ya timu yao kupokea kipigo cha aibu cha mabao 6-3 toka kwa Mancherster City katika mfululizo wa Ligi hiyo.
Wakicheza ugenini huku wakiwa wanaugulia kipigo cha mabao 2-0 walichopewa na Napoli ya Italia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya,  vijana wa kocha Arsenal Wenger walishindwa kufurukuta kwa City waliokuwa uwanja wao wa Itihad.
Goli la mapema la Sergio 'kun' Aguero katika dakika ya 14 lilionyesha dalili mbaya kwa wageni japo winga aliyerejea tena dimbani, Tim Walcot alisawazisha bao hilo dakika ya 31 kwa pasi ya Mesut Ozil kabla ya Negredo kuongeza bao la pili dakika nane baadaye na kufanya hadi mapumziko matokeo kuwa 2-1.
Fernandinho aliiongezea City bao la tatu dakika tano baada ya kipindi cha pili  kabla ya Walcot kurejea tena nyavuni kwa kuifunga Arsenal bao la pili dakika ya 63 akimalizia kazi ya Aaron Ramsey.
Hata hivyo jahazi la Gunners liliendelea kuzama ugenini kwa mara ya pili mfululizo baada ya David Silva kufunga bao la nne dakika tatu baadaye kwa pasi ya Juses Navas na Fernandinho kuongeza bao jingine dakika mbili kabla ya mchezo huo kuisha akimalizia pasi ya Samir Nasir.
Beki Pet M Mertesacker aliifungia Arsenal bao dakika ya nne ya nyongeza ya pambano hilo kabla ya Yaya Toure kupigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao kwa mkwaju wa penati dakika mbili baadaye katika muda huo wa nyongeza na kufanya mechi kuisha kwa mabao 6-3, Arsena ikiwa hoi.
Mechi nyingine zinaendelea hivi sasa katika ligi hiyo na MICHARAZO itaendelea kuwaleta.

Hatari! Ajali nyingine tena yaua wawili

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhx_WAjq_EmxNFNzmr5N_sdMyYNC6gHIbtlxBMjcrq-xftKzqgCZGe5YveNwrsZgN1zt03CdNE5FljeJzc5rJlQe-YDM3eDdlGPMS5dMtP3cLfnR-J_wcYBaeSyZE5ZLiv54gLEnsFGYNo/s1600/bunda+express+accident-kuninews+blog.jpg
Hii kati ya ajali ambazo zimekuwa zikitokea kila mara Tanzania
WATU wawili wamekufa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya basi 
waliolokuwa wakisafiria la Simiyu Express kupinduka katika eneo la 
Ihumwa nje kidogo ya manispaa ya Dodoma.

Basi hilo lenye namba za usajili T 717 ANL aina ya scania basi lilikuwa
likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Mramba Issa (31).

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Kamanda wa Polisi
mkoani hapa Susan Kaganda, alisema kuwa basi hilo lilikuwa linatokea
Bariadi kwenda Dar es salaam likiwa na abiria 60 liliacha njia na 
kupinduka kutokana na mwendo kasi .
Kamanda alisema kwamba ajali hiyo ilitokea leo alfajiri majira ya saa tisa
usiku katika barabara ya Dodoma-Dar es salaam  eneo la Elshadai .
Kamanda Kaganda aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni 
pamoja na dereva wa basi hilo Mramba Issa mkazi wa Magomeni 
Dar es salaam na Frola Erenest(21) Mwali wa shule ya msingi Mwamoto 
kolokolo, Bariadi.
Aidha kamanda akizungumzia zaidi ajali hiyo alisema kwamba basi hilo
lilikuwa likiwakwepa askari wa barabarani kwa kupita njia za panya.
Alifafanua kuwa kwa basi hilo kusafiri usiku huo ni kukwepa askari .
Aliwataka pia wamiliki wa magari kuweka madereva wawili kwa 
magari ya masafa marefu na pia wazingatie sheria za barabarani. 
HABARI LEO 

Mabinti wengine wanaswa na 'unga' uwanja wa JKN

 http://api.ning.com/files/NWvFMlVPFcx5SxCYa4RDXr0NMMnq6gRcpSfjyInB*mxa*WWMz0x1MendQbi7EkT588mJKfgz3DjGsbaCvcR6Q0AgTJ03rTXA/Pipi.jpg Biashara ya dawa za kuelvya ni hatari, lakini hivi sasa imevamiwa hata na wanawake.

 POLISI imewakamata wasichana wawili wa Kitanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, wakiwa na zaidi ya pipi 187 walizokuwa wamezimeza za madawa ya kulevya kwa ajili ya kusafirisha nchini China.
Aidha, polisi imemtia mbaroni, raia wa China Guoyn Shen (44), kwa kukutwa na madini aina ya quates kilo 19 aliyokuwa akiyasafirisha kwa njia ya ndege kuelekea China.
Wasichana waliokamatwa Jumatano ya wiki hii saa 11:00 jioni. uwanjani hapo walikuwa kwenye harakati za kupanda ndege ya kampuni ya ndege ya Qatar kuelekea China kupitia Hong Kong.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha kupambana na dawa za kulevya, nchini Kamanda Godfrey Nzoa, wasichana hao ni Mariam Makuhani (29) mkazi wa Tabata Kimanga  na Khadija Shomari (30), mkazi wa Magomeni Mapipa ambao hadi jana asubuhi walikuwa wanaendelea kuzitoa pipi hizo kwa njia ya haja kubwa.
Alisema Mariam kwa wakati huo (saa 5:00) alikuwa ametoa pipi 65  wakati Khadija alifanikiwa kutoa pipi 122 ambazo zitapelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kubaini ni za aina gani na thamani yake.
Alisema wasichana hao bado wapo chini ya uangalizi ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo wataandaliwa mashitaka yao na kufikishwa mahakamani kujibu makosa yanayowakabili.
Kaimu wa Viwanja vya Ndege nchini, Mratibu wa polisi, Renatus Chalya, alisema awali baada ya wasichana hao kukamatwa, Mariam alikiri kumeza pipi 72 huku Khadija akidai alimsindikiza Mariam.
Akizungumzia changamoto za kupambana na madawa ya kulevya, Kamanda Nzoa alisema wasafirishaji wamekuwa wakiibuka na mbinu tofauti na wengine wakisafirisha viatilifu vya kutengenezea dawa hizo badala ya dawa zenyewe.
Alisema mbinu hizo zimekuwa zikifanywa kwa msimu na kutaja njia ambazo hutumiwa kuwa ni majini, viwanja vya ndege na nchi kavu.
Kufuatia changamoto hiyo, Tanzania na nchi nyingine duniani zilishiriki mikutano mbalimbali ambapo wa mwisho ulifanyika mwezi Oktoba mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Alisema katika mkutano huo washiriki pamoja na mambo mengine walipata fursa ya kueleza changamoto wanazokabiliana nazo kwenye mapambano dhidi ya dawa hizo ambapo lililojitokeza ni usafirishaji wa viatilifu.
"Tuliliongelea kwa upana wake suala hili na kuafikiana kuwepo kwa sheria kali kwa kuwa tunayoitumia kwa mfano Tanzania haiwabani sana," alisema na kuongeza:
Alisema nchi zilizoshiriki mkutano huo zilibaini hiyo ni moja ya changamoto hivyo wakakubaliana kutungwe sheria itakayokuwa na makali zaidi.
Kamanda Nzoa aliwataja Watanzania wawili waliokamatwa kwa nyakati tofauti na viatilifu Agnes Masogange, Afrika Kusini na mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Sada  aliyekamatwa Tanzania ambao kutokana na sheria hiyo walilipa faini ndogo na kuachiwa huru.
Alisema sheria iliyopo inatoa nguvu kwa mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambapo mtu akikamatwa na viatilifu hivyo bila kibali atachukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda Nzoa alisema kuanzia mwezi Machi hadi Julai mwaka huu, wamefanikiwa kukamata kilo 1482 ambazo tayari zilishaharibiwa.
Alisema dawa hizo zilikamatwa kwa nyakati tofauti kwenye meli ambapo moja ilikutwa na kilo 500, nyingine kilo 300.
"Ipo iliyokutwa na kilo 200 meli nyingine ilikutwa na kilo 182 ambapo hata hivyo kutokana na eneo walilokutwa walishindwa kuwafikisha mahakamani badala yake waliharibu mzigo huo," alisema.
Kwa upande wa njia ya anga, alisema kwa mwaka huu wamefanikiwa kukamata kilo 50 bila kuzijumlisha zinazoendelea kutolewa na wasichana hao wawili waliokamatwa Jumatano.
"Ipo kesi ambayo ukija hapa ofisi kwangu nitakuonyesha mlolongo mzima, huwezi amini tulikamata watu tena wakazitoa dawa hizo kwa njia ya haja kubwa lakini mahakama iliwaachilia, kama nilivyosema tunapoenda mahakamani tunatakiwa kuthibitisha pasipo kuacha shaka," alisema.
Kamanda Nzoa alisema kutokana na changamoto hizo, tayari wameshawapeleka vijana wao nchi mbalimbali na kutaja baadhi kuwa ni Afrika Kusini, Ghana, India, Iran, Ivory Cost  kwa ajili ya mafunzo maalum.
Kuhusu Mchina aliyekamatwana madini alisema kuwa Shen alikamatwa Jumatano wiki hii uwanjani hapo akiwa kwenye harakati za kusafirisha mzigo huo kuelekea nchini humo.
Alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akisafiri na ndege ya kampuni ya ndege ya Ethiopia iliyokuwa iondoke jioni ya siku hiyo.
Alisema mtuhumiwa huyo alipokamatwa alipotakiwa kutoa kibali cha kusafirisha mzigo huo hakuwa nacho na alipoulizwa ameyapata wapi alidai ameyanunua kwa wananchi.
Alitaja namba za hati ya kusafiria ya mtuhumiwa huyo kuwa ni 00609687.
Alisema upelelezi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kubaini thamani ya madini hayo.

Bango kutoka TFF

FA MIKOA YAPATA MIPIRA TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa mipira kumi kwa kila chama cha mpira wa miguu cha mkoa ili isaidie kuendesha ligi za mikoa husika.

Mipira hiyo 250 yenye thamani ya sh. 16,250,000 tayari imeanza kutumwa kwa makatibu wa vyama vya mikoa husika. Mpira mmoja una thamani y ash. 65,000.

Ni maratajio ya TFF kuwa mipira hiyo itakuwa chachu kwa vyama vya mikoa katika uendeshaji wa ligi hizo.

MITIHANI YA WAAMUZI KUFANYIKA JUMAPILI
Robo ya mwisho ya mitihani ya waamuzi (Cooper Test) na utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa mwaka 2013 kwa waamuzi inafanyika Jumapili (Desemba 15 mwaka huu).

Mitihani hiyo inayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam inashirikisha waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) na wale wa kundi la waamuzi (elite) ambao wanaweza kupendekezwa kupewa beji za FIFA.

Wakufunzi wa mitihani hiyo ya waamuzi ni Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.

Waamuzi wa FIFA watakaofanya mitihani hiyo ni Ferdinand Chacha, Hamis Chang’walu, Israel Mujuni, Jesse Erasmus, John Kanyenye, Josephat Bulali, Mgaza Kinduli, Oden Mbaga, Ramadhan Ibada, Samwel Mpenzu na Waziri Sheha.

Washiriki kutoka kundi la elite ni Charles Simon, Dalali Jaffari, Hellen Mduma, Issa Bulali, Issa Vuai, Janeth Balama, Jonesia Rukyaa, Judith Gamba, Lulu Mushi, Martin Saanya, Mfaume Nassoro na Mohamed Mkono.

KILIMANJARO STARS YAREJEA DAR
Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) iliyoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika jana jijini Nairobi, Kenya inarejea jijini Dar es Salaam leo.

Kilimanjaro Stars iliyomaliza michuano hiyo katika nafasi ya nne inatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 kamili jilioni kwa ndege ya RwandAir.

Wenyeji Kenya (Harambee Stars) ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Sudan mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa jana Uwanja wa Nyayo.

Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Friday, December 13, 2013

Offside Trick sasa watoa Talaka hadharani

Mmoja wa wanaounda kundi la Offside Trick, Hammer Q
KUNDI maarufu la miondoko nya mduara, Offside Trick la visiwani Zanzibar, limeachia wimbo mpya uitwao 'Talaka' ikiwa ni siku chache tangu waachie video ya wimbo wao wa 'Nipe Nikupe waliomshirikisha Mzee Yusuf.
Mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Hussein Mohammed 'Hammer Q', aliiambia MICHARAZO kuwa wameamua kutoa wimbo huo mpya kama zawadi kwa mashabiki wao katika kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014.
Hammer Q alisema wimbo huo kama zilivyo nyimbo zao nyingine zipo katika miondoko hiyo ya mduara na wanafanya mipango kurekodi video yake.
"Baada ya kuachia video ya 'Nipe NIkupe' tuliyoimba na Mzee Yusuf, tumeachia wimbo mwingine mpya uitwao 'Talaka' ambao tumeimba sisi wenyewe Offsiede Trick bila kumshirikisha mtu wakati tukijipanga kufanya video yake," alisema Hammer.
Kundi hilo la Offside Trick linaundwa na wasanii wawili Said Amdani 'Lil Ghetto' na Hammer Q aliyeziba nafasi ya Mudi Chriss aliyepo masomoni.

CECAFA aibu tupu Kenya, kisa...!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgrmP5BiHFglkwvnrMibnq4AQ_aSqD4vOZa3Us2aK3qsPI4i33h2ONpSixBBlFDMyvtVKIpZsLStp8DY33gYJkFK8qd8JKjm28hh3ukFyeOJ0v8FWAKq7CwnbInY-pMsB65SxD_huGIrnRp/s1600/CECAFA+Cup+2013+b.jpg
Na Somoe Ng'itu, Nairobi
SHIRIKISHO la Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na la Kenya (FKF) yamechafuka baada ya kushindwa kulipia malazi kwa wakati timu zinazoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji huku pia wakikumbwa na kashfa ya kutoa hundi 'feki'.
Licha ya mbwembwe za Kombe kupelekwa uwanjani kwa helikopta,
Timu ya Taifa ya Sudan ilichelewa kufika uwajani kutokana na uongozi wa Hoteli ya Milele kuwazuia wakitaka kulipwa kwanza fedha zao kutoka FKF.
Waamuzi waliochezesha mechi kati ya Kilimanjaro Stars na Zambia (Chipolopolo), pia uongozi wa Hoteli ya Mvuli House uliwazuia kwa muda kutoka ukidai kulipwa kwanza kwa gharama zao za malazi.
Wachezaji wa timu ya soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) jana walizuiwa na uongozi wa Hoteli ya The Strands iliyoko Nairobi West, kuondoka kutokana na deni la Sh.milioni 5.5 za Kenya.
Uongozi wa hoteli hiyo kwa kutumia askari wake iliwazuia wachezaji wa Zanzibar Heroes kuondoka hotelini hapo hadi watakapolipwa fedha wanazoidai FKF.
Wachezaji hao ambao timu yao ilitolewa katika hatua ya makundi ya mashindano ya Kombe la Chalenji tangu Desemba 5, mwaka huu walishindwa kurejea kwao kutokana na kukosa tiketi za kurudia pamoja na kuzuiwa na wamiliki wa hoteli mpaka deni lao watakapolipwa na FKF.
Kutokana na vurugu zilizokuwa zinafanywa na wachezaji wa Zanzibar Heroes wakisisitiza  kuondoka iliwalazimu wamiliki wa hoteli hiyo kuwaita askari wengine wa Jeshi la Polisi la Kenya kwa ajili ya kuhakikisha amani inakuweao kwenye eneo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, nahodha wa Zanzibar Heroes, Awadh Juma, alisema kwamba walipigiwa simu na Mwenyekiti wa FKF, Sam Nyamweya, jana saa 10:00 alfajiri akiwataka wajiandae ili waondoke na ndege ya saa tatu.
Juma alisema baada ya kujiandaa na kubeba mabegi yao saa 12 asubuhi jana, walikuta askari wamejaa kwenye geti wakiwaeleza hawaruhusiwi kuondoka mpaka FKF watakapolipa deni wanalowadai.
Habari kutoka ndani ya hoteli hiyo zilieleza kuwa FKF ilikuwa inadaiwa zaidi ya Sh. milioni 20 za Kenya ambazo ni gharama za kuihudumia timu hiyo pamoja na kikosi cha Nigeria (Super Eagles) kilichokaa hapo wakati kimekuja nchini hapa kuikabili Harambee Stars mapema mwaka huu.
Hata hivyo, FKF ililipa nusu ya deni hilo na ilidaiwa pia kutoa hundi feki ya Sh. milioni 5.5  za Kenya jambo ambalo liliwaudhi wamiliki wa hoteli hiyo.
Saa 3: 20 asubuhi Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, alifika katika hoteli hiyo ili kuanza mazungumzo na wamiliki wa hoteli hiyo lakini hakufanikiwa mpaka pale alipoamua kumuita Nyamweya.
Saa 4:44 Nyamweya alifika katika eneo la tukio kuendelea na mazungumzo lakini kilichoafikiwa ni uongozi wa hoteli kuhitaji fedha zao ndiyo iwaruhusu wachezaji wa Zanzibar Heroes waondoke.
Hata hivyo, wachezaji wa Zanzibar Heroes waligoma kumruhusu Nyamweya kuondoka kwenye hoteli hiyo na kulazimisha waruhusiwe kuondoka na ikiwezekana wakalale hata uwanja wa ndege na si kubaki hotelini hapo.
Kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes, Salum Bausi, alilazimika kufanya maamuzi magumu ya kuwataka wachezaji wake wawe wavumilivu na kumruhusu Nyamweya aondoke na kuongozana na mwakilishi wa hoteli kwenda kulipwa fedha wanazodai.
Saa  6:12 mchana Nyamweya na wenzake pamoja na Musonye waliondoka hotelini hapo na kuelekea benki ili kukamilisha zoezi hilo na kuwaeleza wachezaji kwamba wataondoka leo kurejea Tanzania.
Mbali na Zanzibar Heroes, pia wachezaji wengine wa timu ya Sudan Kusini ambao nao walitolewa kwenye hatua ya makundi walilazimika kujilipia wenyewe tiketi za kurudi nyumbani.
NIPASHE

KMKM kutua leo jioni kuivaa Yanga na Simba Taifa wikiendi hii

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi59R0MYcrxWHLeSNnC_vM50rvpo6pW4S079-xz073BM1qMzHu78BZ3M2A6-Rcffg0AKuCNlGJTx77XuEspNUQTYpSZxeIwClivBXmTswWbLyuGBKDZoXuu3mnXKpUwrCIZ62qjbxpxVhkw/s640/4.jpg
Kikosi cha KMKM kitakachotua leo Dar kuumana na Simba na Yanga mwishoni mwa wiki
TIMU ya KMKM ya Zanzibar inatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam jioni ya leo  ikitokea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki na Yanga na Simba, ambapo katika mechi ya kesho dhidi ya Yanga kiingilio cha chini kabisa ni sh.5,000.
Kwa mujibu wa mratibu wa mechi hiyo George Wakuganda alisema, timu hiyo itawasili jioni kwa Boti ya kwenda Kasi ikiwa na kikosi kamili na mechi ya kwanza ni kati ya Yanga na KMKM Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam, huku Simba wakicheza keshokutwa katika uwanja huo huo.
Alisema vingilio kwa VIP A ni sh.20,000, VIP B sh.15,000, VIP C sh.10,000, orange sh.7,000 , bluu na kijani viingilio ni sh.5,000.
"Tunaamini kwa kipindi hiki kirefu ambacho timu zilikuwa mapumzikoni, wachezaji watarudi na kitu kipya uwanjani ikiwa na makocha kuwatambulisha wachezaji wao wapya," alisema Wakuganda
Kwa upande wa kocha wa Yanga Ernest Brandts alisema anaimani kabisa mechi hiyo itampa mwanga kuelekea mechi hiyo na wapinzani wao Simba, hivyo anazidi kuwanoa wachezaji wake ili wawe fiti zaidi.
"Naamini KMKM sio timu mbaya hasa kipindi hiki ambacho timu yangu inajiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo kwa kiasi kikubwa itanisaidia kujenga kikosi changu," alisema kocha huyo.
Alisema pia mechi hiyo atawatumia wachezaji wake wapya kipa Juma Kaseja na kiungo Hassan Dilunga ambao wamesajiliwa kipindi hiki cha dirisha dogo kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chake.
Kocha huyo alisema wachezaji wake wote wapo fiti ukiondoa wale ambao wapo kwenye timu zao za Taifa, waliomo kwenye michuano ya Kombe la Challenji ambayo inamalizika leo nchini Kenya.
Alisema mechi hiyo imekuja kipindi kizuri kwa kuwa wachezaji wake walikuwa mapumziko, hivyo hata wakivaana na Simba atakuwa amejua wapi kuna mapungufu katika kikosi chake kabla ya mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.
Hata hivyo kocha huyo alisema wachezaji waliomo kwenye timu za Taifa, hana uhakika kama watacheza mechi hiyo kwa kuwa siku ya mechi ndio wanatua nchini wakitokea Nairobi, Kenya.

Golden Bush Veterani kuzivaa Kilwa Veterani, Mwana United Dar


BAADA ya kufanikiwa kuwasambaratisha KMKM Vetereani nyumbani visiwani Zanzibar, wakali wa soka la wazee jijini Dar es Salaam wikiendi hii wanatarajia kushuka tena dimbani kuvaana na mateverani wenzao wa Kilwa na Mwanza United katika mechi za kuelekea pambano lao na watani zao Wahenga Fc.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mlezi wa klabu hiyo inayoundwa na wanasoka nyota wa zamani na wale wanaoendelea kukipiga katika timu za Ligi mbalimbali nchini, Onesmo Waziri 'Ticotico', mechi hizo zitachezwa Jumamosi na Jumapili kwenye viwanja tofauti.
Ticotico alisema mechi ya kwanza itachezwa jioni kwenye uwanja wa TP Afrika uliopo Sinza, dhidi ya Kilwa Veterani na mechi itakayofuata itakuwa ya Jumapili kwa kiuwakabili Mwanza United.
 Taarifa yake kamili inasomeka kama ifuatavyo:
 
Wadau,
 
Wale Mabingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watakuwa uwanjani tena weekend hii kama ifuatavyo:
 
Siku
Muda
Uwanja
Mechi
Jumamosi
1630hrs
TP
Golden Bush Veterans VS Kilwa Viterens
Jumapili
0800hrs
St James' Park
Golden Bush Veterans VS Mwanza United
 
Karibuni njooni muangalie soka la hali ya juu sana likitandazwa na Mabingwa wenu ikiwa ni sehemu mahususi kabisa ya maandalizi ya mechi yetu na Wahenga ambayo iko karibu sana.
 
Kwa kuzingatia hilo mechi zote zinazofuata sasa tutalazimika kutowatumia wachezaji wanaochezea Wahenga kwasababu tuko kwenye maandalizi ya mwisho mwisho kuandaa kikosi cha maangamizi siku ya kufunga mwaka.
 
Karibuni sana.
 
Onesmo Waziri

Ajali hii imetokea asubuhi hii Kimara-Korogwe

Bodaboda ikiwa chini ya Fusso lenye namba T961 BZF baada ya kugongwa eneo la Kimara asubuhi ya leo

Bodaboda ikiwa chini ya Fusso lenye namba T961 BZF baada ya kugongwa eneo la Kimara asubuhi ya leo

Bodaboda ikiwa chini ya Fusso lenye namba T961 BZF baada ya kugongwa eneo la Kimara asubuhi ya leo

Bodaboda ikiwa chini ya Fusso lenye namba T961 BZF baada ya kugongwa eneo la Kimara asubuhi ya leo
MATUKIO ya ajali zinazohusu Pikipiki maarufu kama bodaboda yanaendelea kukithiri ambapo asubuhi ya leo eneo la Kimara mwendesha chombo hicho alijikuta akibamizwa na kuaachwa hoi yeye na abiria wake eneo la Kimara Korogwe.
Dereva huyo ambaye hakufahamika jina lake anadaiwa alikuwa akimpeleka abiria wake Ubungo kutokana na kero ya foleni katika barabara ya Morogoro na kujikuta wakiishia Hospitali baada ya kujeruhiwa huku pikipiki yake ikiwa imeharibika baada ya kugongwa na Fusso hilo lililokuwa likitokea mkoani kuja jijini Dar.
Pia katika ajali hiyo ilihusisha basi la wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo lilibamizwa kwa nyuma upande wa kulia na Fusso hilo na kuharibika huku ikielezwa baadhi ya abiria wa basi hilo dogo aina ya Toyota Coaster kujeruhiwa kidogo.

Neymar achekelea kuweka heshima Ulaya mapema zaidi

http://bostonherald.com/sites/default/files/styles/full/public/media/ap/d7a9ff3209aa48e190d014ef0569a8cf.jpg?c=612f6677417bc1fda3fcf6c08e08968f
Neymar akishangilia moja ya mabao yake matatu yaliyoizamisha Celtic juzi
BARCELONA, Hispania
NEYMAR amesema ameweka heshima Ulaya baada 'hat-trick' yake aliyofunga kuisaidia Barcelona kushinda 6-1 dhidi ya Celtic.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alifunga magoli matatu ndani ya dakika 13 wakati Bara walipomaliza hatua ya makundi kwa ushindi mnono, huku Gerard Pique, Pedro na Cristian Tello wakifunga mabao mengine.
Barca waliingia katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Nou Camp wakiwa wamepoteza mechi mbili katika ya tatu zilizopita na Neymar alifarijika kwamba kikosi cha kocha Gerardo Martino kimerejea kushinda tena.
"Nina furaha - siyo tu kwa kufunga magoli matatu kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ila pia kwa timu kushinda," alikaririwa na gazeti la Marca akisema.
"Sikuwa katika presha, lakini nilitaka kuweka heshima. Jambo muhimu ni kwamba tumeweza kuzipiku mechi zile mbili tulizopoteza na sasa ni lazima tubadili mitazamo yetu na kufikiria La Liga. "
Alipoulizwa kama anapenda kucheza katikati kuliko pembeni, alikataa kutoa maoni yake katika hilo, akisema anachohitaji ni kucheza tu.
"Napemda kucheza, sijali ni katikati ama pembeni," Neymar aliongeza.
Mechi ijayo ya Barca itakuwa ni ugenini dhidi ya timu ngumu ya Villarreal kesho baada ya kumaliza wakiwa vinara wa Kundi H la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Na tofauti ya mabao katika kipigo cha kwenye Uwanja wa Nou Camp imeifikia rekodi ya kufungwa 5-0 dhidi ya Artmedia Bratislava katika iliyokuwa mechi ya kwanza madarakani kwa kocha wa zamai Gordon Strachan mwaka 2005.
Celtic waliingia katika mechi hiyo wakiwa wamefunga jumla ya magoli 12 na hawajaruhusu hata moja katika mechi zao mbili za ligi zilizopita, wakati Barcelona walikuwa wamekula vipigo kutoka kwa Ajax na Athletic Bilbao.
Lakini Barca waliokuwa katika kiwango chao cha juu waliishushia Celtic kipigo chao cha 25 katika mechi 27 za ugenini za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Hatimaye Ivo Mapunda akata mzizi wa fitina

Ivo Mapunda akiweka dole gumba katika mkataba wake na Simba mbele ya Katibu Mkuu wa Simba, Evodias Mtawala. (Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry)
HATIMAYE mzizi wa fitina juu ya kipa Ivo Mapunda kutua Simba au kuendelea kuidakia Gor Mahia umekatwa baada ya kipa huyo wa Kili Stars, kuamua kusaini mkataba wa miaka miwili usiku wa jana jijini Nairobi.
Ivo ambaye amekuwa gumzo nchini Kenya kwa umahiri wake wa kudaka na hasa kunyaka mikwaju ya penati, alisaini mkataba huo mbele ya Katibu Mkuu wa Simba, Evodias Mtawala na kukamilisha tetesi zilizokuwa zimezagaa za Mnyama kumnyakua kipa huiyo wa zamani wa Yanga na Prisons na African Lyon.
Mbali na Ivo, Simba imenyakua pia beki wa Gor Mahia, Donald Musoti ikiwa ni katika kujiimarisha kwa duru la pili la Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza Januari 25.
Simba pia imenyakua kipa Yew Berko aliyekuwa akiidakika Yanga baada ya kutoridhishwa na kiwango cha kipa Abel Dhaira kutoka aUganda waliomsajili msimu huu.

Waliokufa ajali ya Burdan hawa hapa, majeruhi wengine hali tete

MAJINA ya abiria waliopoteza uhai katika ajali ya Basi la Burdan iliyotokea jana Kijiji cha Taula Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga yameanza kutajwa.
Ajali hiyo iliyotokana na basi hilo linalodaiwa kuwa katika mwendo kasi  na kupinduka mara kadhaa na kuacha na kujeruhi watu zaidi ya 70.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe walipopoteza maisha katika ajali hiyo wametambuliwa kuwa ni Dareva wa basi hilo, Luta Kundaeli Kimaro, Mama Ally mkazi wa eneo la Kwasamangube Korogwe, Joyce Mokiwa (36) mkazi wa NHC Korogwe na Rehema Mandondo ambaye ni mkazi wa kambi ya Maziwa.
Wengine waliokufa ni Msoke Mosha ambaye ni mwalimu wa Mgombezi Korogwe, Bashiri Shafii wa Kilole Korogwe, Bryton wa eneo la Lutheran Korogwe, Rehema Nassoro (23) mkazi wa Bagamoyo Kilole Korogwe, Agnes Linus mkazi wa Mandera na Mariamu Juma.

Thursday, December 12, 2013

Shaa aweka kiporo Sifa Ujinga akisaka madansa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEifTHyk2hW154PLhd-dO1ue1WNz2zW9kYykXLpBOfVnvl-fh6nXZJnuBAEdNktOq7o4NuUd03vtCRr8FauFMTCc7LAqrHGWcVnPG3LyYEb0IhQ070nKLFUBTlr2J0J4OiFyDTfdTKDGnKLE/s1600/SHAA.jpg
Shaa katika pozi

MCHAKATO wa kusaka madansa watakapamba jukwaa la msanii Sarah Kais 'Shaa' umeanza ukiendeshwa na mabosi wa msanii huyo, kituo cha Mkubwa na Wanae.
Mkurugenzi wa kituo hicho na meneja wa Shaa, Said Fella alisema tayari wameanza kupokea wasanii wanaotaka kuwa miongoni mwa madansa hao wanne kabla ya kuanza kuwafanyia usaili kisha wale watakaokithi viwango kushindanishwa kusaka madansa wanne wa kuunda kundi la Shaa.
Fella alisema mchakato wa kuwashindanisha madansa huo utafanyika kwa utaratibu maalum katika kundi zitakazotangazwa ndani ya wilaya ya Temeke kabla ya fainali ya mwisho kufanyika katika ukumbi mmoja maarufu hapa jijini Dar.
'Tumeshaanza kupokea madansa wanaotaka kuwania kuwa miongoni mwa madansa wanne wa Shaa, tutawachuja kisha wale watakapita watashindanishwa ili kusaka wanne wa mwisho watakaoambatana na Shaa katika maonyesho yake," alisema.
Aidha Fella alisema wimbo mpya na wa pili wa Shaa uitwao 'Sifa Ujinga' umeshakamilishwa na sasa unaandaliwa video yake ndipo vtyote viachiwe hadharani.
Pia alisema wameona isingekuwa vyema kuutoa wimbo huo mpya wakati wimbo wa 'Sugua Gaga' ulioachiwa hivi karibuni ukiendelea kutesa katika vituo vya redio na runinga.

Rais Kikwete awalilia waliokufa ajali ya Burdan

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2013/06/Jakaya-Kikwete-na.jpg
Rais Jakaya Kikwete
          THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Lt(Mst) Chiku Galawa kufuatia vifo vya watu 12 na wengine 71 kujeruhiwa baada ya basi Na. T610 ATR la Kampuni ya Burudani lililokuwa likitokea Korogwe kwenda Dar es Salaam kupinduka katika Kijiji cha Taula mapema asubuhi ya tarehe 12 Desemba, 2013.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu 12 vilivyotokea tarehe 12 Desemba, 2013 huku wengine 71 wakijeruhiwa, baada ya basi la Kampuni ya Burudani walilokuwa wakisafiria kutoka Korogwe kuelekea Dar es Salaam kupinduka katika Kijiji cha Taula”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.

Rais Kikwete amesema vifo vya watu hao ni pigo kubwa siyo tu kwa familia za watu waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo, bali pia Taifa letu kwa ujumla ambalo limepoteza nguvu kazi muhimu iliyokuwa bado inahitajika kwa ujenzi wa Taifa.

“Kutokana na msiba huo mkubwa uliotokea katika eneo la Mkoa wako, ninakutumia Salamu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu wewe Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Lt. (Mst) Chiku Galawa kwa kupoteza watu wengi kwa mara moja katika ajali hiyo.  Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Mahala Pema Peponi Roho za Marehemu wote, Amina”.

Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga kumfikishia Salamu zake za Rambirambi na pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa waliopotelewa na wapendwa wao katika ajali hiyo, lakini amewahakikishia kwamba yuko pamoja nao katika kipindi hiki cha maombolezo.  Amewaomba wawe na moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia wakiomboleza vifo vya ndugu zao.

Aidha Rais Kikwete amesema anawaombea kwa Mwenyezi Mungu majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea katika hali zao za kawaida, ili waungane tena na ndugu na jamaa zao na kuendelea na maisha yao kama ilivyokuwa kabla ya kutokea kwa ajali.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12 Desemba, 2013

Hii ndiyo taarifa rasmi ya ajali ya basi la Burudan



WATU 12 wamekufa papo hapo huku wengine 71 kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali basi la abiria la Kampuni ya Burdan kupinduka katika kona ya Kwaluguru kata ya Kabuku wilayani Handeni Mkoani Tanga leo asubuhi.

Basi hilo ambalo linafanya safari zake kati ya Korogwe Dar es Salaam lilipata ajali majira ya ya asubuhi kutokana na mwendo kasi uliopelekea dereva kushindwa kumudu gari hilo na kuacha njia.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga,Costantine Massawe amethibitishwa kutokea kwa ajali hiyo,na kusema majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Wilaya Magunga kwa ajili ya matibabu.

Kamanda Massawe alitaja namba za gari hilo kuwa ni T.610 ATR aina ya Nisani lilikuwa likitokea Korogwe likielekea Dar es Salaam lililokuwa likiendeshwa na Luta Mpenda ambaye alipoteza maisha papo hapo.

Mwendo kasi unatajwa kuwa chanzo kikubwa cha ajali ambayo majeruhi imeitaka serikali kusimami kikamilifu na kuchukua hatua kwa madereva wanao kikuka sheria.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akaiomba serikali kuboresha huduma za afya kwenye hosptali hiyo ili kuondokana na changamoto iliyojitokeza ya ukosefu wa damu.

Majeruhi wengine 19 wamepelekwa katika kospitali ya KCMC Moshi na Moi Dar es Salaam kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi.

BARAZA lafungia shindano la Miss Utalii Tanzania, kisa...!

BARAZA  la Sanaa la Taifa (BASATA) limeyafungia mashindano ya urembo ya Utalii 'Miss Tourism Tanzania' kutokana na kukiuka taratibu na maagizo ya baraza hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari Mkuu wa baraza hilo, Agness Kimwaga inaelezwa kuwa Miss Utalii imefungiwa kwa sababu kuu mbili;
taarifa hiyo ya BASATA inasomeka kama ifuatavyo;

Baraza la sanaa Taifa limefungia mashindano hayo kutokana na sababu kuu mbili,kwamza mashindano Miss Tourism Tanzania 2013 kushindwa kufanya tathmini ya mashindano ya miss Tourism 2012/2013 kwa muda uliokubalika baada ya maonyesho hayo kufanyika,na sababu nyingine kwamba Miss Tourism Tanzania kukiuka masharti,kanuni,miongozo na taratibu za uendesheaji wa mashindano ya urembo kama zilivyowekwa na serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa kwa hiyo hizo ndo sababu zilizofanya sisi kulifungia shindano hili kwa muda usiojulikana"
"Tukiwa na ushahidi uliokamilika kutoka kwa warembo wenyewe waliohusika hatuwezi kufungia kitu pasipo ushahidi,kumbuka mashindano haya yanapokuwa yanaendelea serikali hatukai kwenye zile kambi kwa muda wote wanaokaa kwa kuwa mara nyingi tunapokwenda kutembelea warembo wakiwa kwenye zile kambi tunawaambia popote panapokua na tatizo kunakiukwa taratibu tunawapa taratibu tunazotaka zifuatwe zinapokiukwa wao watupe taarifa,tusipopata taarifa sisi hatuwezi kumfungia mtu pasipo kuwa na taarifa tumekua na taarifa za uhakika toka kwa warembo wenyewe ndo maana tumechukua hatua".
"Tunasema kwamba tunapoendesha shughuli yoyote ya sanaa usifanye vitu ambavyo vinaweza kumdharirisha mtazamaji au mhusika anaefanya kitu kile kwa hiyo kuna vitu ukifanya vinaweza kumdharirisha mtu kwa njia moja au nyingine umekiuka kanuni na taratibu kumnyanyasa mfano kijinsia,kwanza kabla ya kukufungia tunakupa pre ya muda na tunakwambia umekosea nini na tunakupa muda kurekebisha yale makosa yaliyofanyika,kama unakumbuka zamani Miss Tanzania watu walikua wanapanda na yale mavazi ya ufukweni yakiwa tupu bila kufunga jukwaani lakini taratibu tumewaambia hairuhusiwi kupanda hivyo,kwa sababu ni lazma wakaguliwe wakiwa vile hakuna watazamaji wanaokuwepo kwa muda huo,lakini kabla hatujakufungia tunakupa barua kwamba umekosea A,B,C,D na ufanye marekebisho kwenye hatua hiyo vinginevyo tunakufungia,sasa kama umetuma barua na hakuna kilichorekebishwa pia inakua ni kinyume na utaratibu kwamba tunafika lakini si kila siku sisi huwa tunafika tunawapa wale warembo semina lakini si siku zote wanazokaa kambini sisi tunafika,siwezi kuwa na taarifa bila kuniambia mtu aliekuepo hapo.


Kenya ndiye bingwa mpya wa Chalenji 2013

http://www.standardmedia.co.ke/images/sunday/Harambee-09082013.jpg
Harambee Stars

WENYEJI wa michuano ya Kombe la Chalenji, Kenya Harambee Stars imefanikiwa kutawazwa mabingwa wapya wa michuano hiyo baada ya kuinyuka Sudan kwa mabao 2-0 katika pambano lililochezwa jioni hii jijini Nairobi.
Harambee iliyowaondoa patupu Tanzania katika mechi ya nusu fainali, ilipata mabao yake yaliyoizima Sudan kupitia kwa Alain Mwanga na kunyakua taji lake la sita la michuano hiyo na mara ya kwanza kwa taifa hilo kutwaa taji hilo katika ardhi yake tangu ilipofanya hivyo mwaka  1983.
Mara ya mwisho kwa Kenya kunyakua taji hilo ilikuwa mwaka 2002 walipoitungua Tanzania Bara waliokuwa wenyeji wa michuano hiyo kwa mabao 3-2. Katika fainali za mwaka jana, Kenya inayosherehekea miaka 50 ya Uhuru wa taifa hilo ilifika fainali dhidi ya Uganda na kufungwa, lakini safari hii wamekomaa na kunyakua taji hilo.
Michuano hiyo ilishuhudia Salah Ibrahim kunyakua tuzo la Mfungaji Bora akifunga mabao matano.
Hongera Kenya, Hongera Harambee Stars kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru na Taji la Chalenji katika ardhi yenu baada ya miaka 30 iliyopita.

Kili Stars bado gonjwa Chalenji 2013

 
KILIMANJARO Stars bado haijapata dawa ya kufanya vyema kwenye mechi zake za kuwania ushindi wa tatu baada ya jioni hii kupoteza mchezo kwa Zambia.
Kili Stars inashiriki mechi ya kusaka mshindi wa tatu kwa mara ya tatu mfululizo toka mwaka 2011 na mara zote imekuwa ikiambulia vipigo kama ilivyokuwa jioni hii kwa Chipolopolo walioshinda kwa mikwaju ya penati.
Timu hizo mbili zilimaliza dakika 90 zikiwa zimefungana bao 1-1 na kuingia hatua ya kupigiana penati na Kili Stars kunyukwa kwa mikwaju 6-5. 
Kipa Ivo Mapunda aliendelea kuonyesha ushujaa kwa kupangua penati mbili, lakini hiyo haikusaidia kwa vile wachezaji wa Tanzania walikosa penati tatu.
Katika muda wa kawaida, Zambia ilianza kupata bao kupitia kwa Ronald Kampamba katika dakika ya 51 kabla ya Kili Stars kusawazisha kupitia nyota wa pambano hilo, Mbwana Samatta dakika ya 65. Kwenye penati Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhan Singano 'Messi' walipata penati zao, huku Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani wenyewe walikosa na kumaliza wakishika nafasi ya nne kwa mara ya tatu.

Nani bingwa mpya wa Chalenji 2013, Kili Stars kama kawa....!


MICHUANO ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kufikia tamati leo ambapo bingwa mpya atajulikana wakati wenyeji Kenya, Harambee Stars itakapovaana na Sudan 'Falcons' katika pambano la fainali.
Watanzania waliotumbukiwa nyongo na michuano hiyo baada ya timu zao kushindwa kufurukuta watasubiri kuona kama Kili Stars itakayoumana na Zambia itaambulia nini katika mchezo wa mshindi wa tatu.
Hiyo ni mara ya tatu mfululizo kwa Tanzania Bara kucheza hatua hiyo na mara zote imeambulia patupu mbele ya wapinzani wao.
Kili Stars iliyokuwa imewapa matumaini makubwa mashabiki wa kurejea na taji baada ya kulitwaa mara ya mwisho mwaka 2010 michuano ikifanyika Tanzania, licha ya kuivua taji Uganda, ilikwama kwa Kenya hatua ya nusu fainali.
Hivyo mchana wa leo itavaana na Chipolopolo kabla ya kupisha pambano la Kenya na Sudan ili kuandikisha bingwa mpya baada ya The Cranes kulitema taji lake.
Mechi zote za leo zitachezwa kwenye uwanja wa Nyayo na pambano la awali litachezwa kuanzia saa 8 mchana kabla ya fainali kupigwa jioni, huku Kenya wakijiamini watalinyakua taji hilo baada ya kulikosa tangu ilipotwaa mara ya mwisho mwaka 2002 nchini Tanzania.
Kabla ya mechi hizo kutakuwa na pambano la kukata na shoka la kukumbushia vipaji halisi vya Afrika Mashariki wakati timu ya wazee ya Tanzania itakapovaana na wenzao wa Kenya.
Hata hivyo pambano hilo litachezwa uwanja wa City, Nairobi majira ya saa 7 mchana na kisha shughuli zote kuhamia Nyayo Stadium kuhitimisha michuano hiyo.

Arsenal yafa ikifuzu 16 Bora, Neymar apiga hat trick ya kwanza Barca ikiua

Pilikapilika za Arsenal dhidi ya wenyeji wao Napoli

Neymar akitupia bao kambani

Demba Ba akifunga bao lake lililoipa Chelsea ushindi
VINARA wa Ligi Kuu ya Engalnd Arsenal imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 Bora lakini wakiangukia pua kwa kunyukwa mabao 2-0 na Napoli ambayo hata hivyo itacheza sasa Europa League licha ya ushindi huo wakiwa nyumbani.
Arsenal iliyokuwa kinara wa kundi lake kabla ya mechi ya usiku wa jana ilikumbana na kipigo hicho kilichowafanya washike nafasi ya pili na kuungana na Borussia Dotmund kucheza hatua ya mtoano kwa uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa.
Mabao ya Napoli yamefungwa na Gonzalo Higuain dakika ya 73 Callejon dakika ya 90, na kuifanya timu hiyo nayo kufikisha pointi 12 lakini ikiwa na uwiano mdogo wa mabao na kukamata mafasi ya tatu na kuangukia ligi ya Ulaya ndogo na timu nyingine ikiwamo Juventus waliolala bao 1-0 mbele ya Galatasaray mapema jana.
Katika michezo mingine ya ligi hiyo kuhitimisha hatua ya makundi, Barcelona licha ya kuwakosa Andres Iniesta, Leo Messi na Cesc Fabregas iliichapa Celtic kwa mabao 6-1.
Hat trick ya kwanza ya nyota wao mpya toka Brazil, Neymar na mengine ya  Gerrard Pique, Pedro na Tello yalitosha kuifanya vinara hao wa La Liga kukalia uongozi wa kundi hilo ikiwa ilishatangulia 16 Bora mapema.
Nao Chelsea ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya  Steaua Bucharest shukrani ikienda kwa Demba Ba aliyefunga dakika ya 11 ya mchezo huo uliochezwa darajani.
Marseille ya Ufaransa ilimaliza mechi zake za makundi bila ushindi wowote baada ya jana kukubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Wanafainali wa mwaka uliopita Borussia Dortmund waliokuwa ugenini, huku Atletico Madrid weakishinda mabao 2-0 dhidi ya Porto.
Timu ya Schalke 04 ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Basel, huku Austria Vien iliisasambua Zenith kwa mabao 4-1 na AC Milan ikiwakomboa Waitalia kwa kufuzu hatua ya 16 Bora baada ya sare isiyo na mabao dhidi ya Ajax.
Orodha kamili ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bota katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kama ifuatavyo;
Manchester  Utd, Bayer Leverkusen, Real Madrid, Galatasaray, PSG, Olympikaous,
Bayern Munich, Manchester City, Chelsea, Schalke 04, Borussia Dotmund, Arsenal, Atletico Madrid, Zenith, Barcelona na Ac Milan.