STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 25, 2014

Diamond, Lady Jaydee watisha Kili Music Awards


'Sukari ya Warembo' Diamond Platnumz
Lady Jaydee 'Comando' a.k.a Anaconda
WANAMUZIKI nyota nchini, Nassib Abdul 'Diamond Platinum' na Judith Wambura Mbibo 'Lady jaydee' a.k.a Comando au Anaconda wameteuliwa mara nyingi kuwania tuzo za muziki za Kili Music zilizotangazwa leo.
Diamond ameingia katika vipengele 6 vya kinyan’ganyiro cha tuzo za muziki nchini, maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014, huku Binti Machozi akiteuliwa mara 7.
Wimbo bora wa mwaka;
1 Number one-Diamond,
2 Joto hasira-Lady Jaydee Ft Prof Jay,
3 I love u-Cassim Mganga,
4 Yahaya-Lady JayDee,
5 Kidela -Abdu Kiba Feat Ali Kiba 
6 Muziki gani-Ney ft Diamond.


Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya Kitanzania;
1 Kwejaga nyangisha-Batarokota,
2 Nalonji-Kumpeneka,
3 Bora Mchawi-Dar Bongo massive,
4 Tumbo lamsokota-Ashimba,
5 Aliponji –Wanakijiji 
6 Agwemwana-Cocodo African music band.

Wimbo bora wa kiswahili –Bendi;
1 Ushamba mzigo-Mashujaa Band,
2 Shamba la Bibi -Victoria Sound,
3 Chuki ya nini -FM Academia,
4 Yarabi nafsi -Mapacha Watatu
5 Kiapo mara 3 -Talent Band.

Wimbo bora wa Reggae;
1 Niwe na wewe-Dabo,
2 Hakuna Matata-Lonka,
3 Tell Me-Dj Aron ft Fidempha,
4 Bado nahitaji-Chikaka ft Bless p & Lazzy B
5 Bongo Reggae-Warriors from the east.

Wimbo bora wa Afrika Mashashariki;
1 Tubonge-Jose Chamelleone,
2 Nakupenda Pia-Waire Ft Allain,
3 Badilisha-Jose Chamelleone,
4 Kipepeo-Jaguar
5 Kiboko Changu-Aman FT Weizal and Radio.

Wimbo bora wa Afro pop;
1 Number one-Diamond,
2 Joto hasira-Jay Dee,
3 Kidela-abdul kiba ft Ali Kiba,
4 I love you-Kassim,
5 Tupogo-Ommy Dimpoz Ft J Martins
6 Roho yangu-Rich Mavoko.

Wimbo bora wa Taarab;
1 Wasi wasi wako-Mzee Yusuf,
2 Asiyekujua Hakuthamini-Isha Ramadhani & Saida Ramadhani,
3 Nipe stara -Rahma Machupa,
4 Sitaki shari-Leyla Rashid,
5 Fahari ya Mwanamke-Khadija Kopa,
6 Mambo bado-Khadija Yusuf
7 Kila muomba Mungu -Mwanahawa Ali.

Wimbo bora wa Hip hop;
1 Bei ya mkaa-Weusi,
2 Nje ya box-Nick wa pili ft Joh Makini na Gnako,
3 Siri ya mchezo-Fid q ft Nature,
4 2030-Roma
5 Pesa-Mr Blue Ft Becka Title.

Wimbo bora wa R&B;
1 Listen-Belle 9,
2 Closer -Vanessa Mdee,
3 So crazy-Maua ft Fa,
4 kama huwezi-rama dee ft jay dee
5 Wa ubani-Ben Pol ft. Alice

Wimbo bora wa kushirikisha/kushirikiana;
1 Music Gani-Ney Mitego ft Diamond,
2 Joto Hasira-Lady JayDee ft. Prof Jay,
3 Kidela -Abdul Kiba ft. Ali Kiba,
4 Bila Kukunja Goti-Mwana FA na AY ft. Jay Martins
5 Tupogo-Ommy Dimpoz ft. Jay Martins.

Wimbo bora wa Ragga/Dancehall;
1 Nishai-Chibwa Ft Juru,
2 Sex girl-Dr Jahson,
3 My sweet-Jettyman Dizano,
4 Feel Alright-Lucky Stone,
5 Wine-Princess Delyla.

Wimbo bora wa Zouk /Rhumba;
1 Yahaya-Lady Jaydee,
2 Yamoto-Mkubwa na wanawe,
3 Msaliti-Christian Bella,
4 Nakuhitaji-Malaika Band
5 Narudi kazini-Beka.

Mwimbaji bora wa kike -kizazi kipya;
1 Vanessa Mdee,
2 Lady Jaydee,
3 Linah na 4 Maua

Mwimbaji bora wa kiume -kizazi kipya
1 Ben Pol,
2 Rich Mavoko,
3 Diamond,
4 Ommy Dimpoz
5 Cassim Mganga.

Mwimbaji bora wa kike –Taarab;
1 Khadija Kopa,
2 Isha Ramadhani,
3 Khadija Yusuf,
4 Mwanahawa Ali
5 Leyla Rashid,

Mwimbaji bora wa kiume –Taarab wanashindana
1 Mzee Yusuf,
2 Hashimu Saidi
3 Mohamedi Ali aka Mtoto Pori.

Mwimbaji bora wa kiume –Bendi;
1 Jose Mara,
2 Kalala Junior,
3 Charz Baba,
4 Khalid Chokoraa
5 Christian Bella,

Mwimbaji bora wa kike -Bendi
1 Luiza Mbutu,
2 Catherine (Cindy) 
3 Ciana.

Msanii bora wa -Hip hop;
1 FID Q,
2 Stamina,
3 Young killer (Msodoki),
4 Nick wa pili,
5 Gnako.

Msanii bora chipukizi anayeibukia;
1 Young Killer(Msodoki),
2 Walter Chilambo,
3 Y Tony,
4 Snura
5 Meninah,

Rapa bora wa mwaka –Bendi kuna
1 Kitokololo,
2 Chokoraa,
3 Furguson,
4 Canal Top
5 Totoo ze Bingwa.

Mtumbuizaji bora wa kike wa Muziki.
1 Khadija Kopa,
2 Vanessa Mdee,
3 Isha Ramadhani,
4 Luiza Mbutu
5 Catherine (Cindy)

Mtumbuizaji bora wa kiume wa Muziki
1 Diamond,
2 Christian Bella,
3 Rich Mavoko,
4 Ommy Dimpoz
5 Abdu Kiba.

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka –Taarab;
1 Enrico,
2 Ababuu Mwana ZNZ
3 Bakunde

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka -Kizazi kipya
1 Marco chali-Mj Records,
2 Man Water-Combination Sound,
3 Mazoo-Mazoo Records,
4 Sheddy Clever-Burnz Records
5 Nahreel -Home Town Record.

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka –Bendi;
1 Allan Mapigo,
2 C9,
3 Enrico,
4 Amoroso
5 Ababuu Mwana ZNZ,

Mtunzi bora wa mwaka –Taarabu,
1 Mzee Yusuf,
2 El-Ahad Omary,
3 El-khatib Rajab,
4 Kapten Temba,
5 Sadiki Abdul
6 Nassoro Seif,

Mtunzi bora wa mwaka -kizazi kipya,
1 Belle 9,
2 Ben Pol,
3 Diamond,
4 Rama dee
5 Rich mavoko.

Mtunzi bora wa mwaka –Bendi
1 Christia Bella,
2 Jose Mara,
3 Chaz Baba,
4 Nyoshi Saadat
5 Kalala Junior

Mtunzi bora wa mwaka -Hip hop,
1 Nikki wa Pili,
2 Young Killer(Msodoki),
3 Roma,
4 FID Q
5 G- Nako.

Video bora ya muziki ya mwaka;
1 Number One-Diamond,
2 Yahaya-lady Jaydee,
3 Joto hasira-Lady Jaydee Ft Prof Jay,
4 Uswazi takeaway-Chege Ft Malaika,
5 Mama Yeyo-Gnako Ft Ben Pol.

Bendi bora ya mwaka;
1 FM Academia,
2 Mapacha Watatu,
3 African Stars ‘Twanga Pepeta’,
4 Akudo Impact,
5 Malaika Band,
6 Mashujaa Band,

Kikundi cha mwaka cha Taarab ni
1 Jahaz Modern Taarab,
2 Mashauzi Classic
3 Five Stars

Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya;
1 Makomandoo
2 Navy kenzo,
3 Weusi
4 Mkubwa na wanawe

(CHANZO: www.saluti5.com).

Easy Man kuweka Mashetani wake videoni

Easy Man  katika 'kichupa' chake cha Kasoro Wewe
MSANII anayetajwa kama 'mfalme' wa mchiriku nchini kwa sasa, Is'haka Salehe 'Easy Man',  anatarajiwa kurekodi video ya wimbo wake mpya uitwao 'Mashetani'.
Easy Man alisema wimbo huo ambao ni wa pili kwake baada ya kutesa na 'Kasoro Wewe', alisema kazi ya kurekodi video hiyo inatarajiwa kuanza keshokutwa chini ya kampuni moja iliyopo maeneo ya Temeke.
"Kuanzia Alhamisi natarajia kuanza kazi ya kurekodi video ya wimbo wangu wa 'Mashetani' na baada ya hapo nitaingia tena studio kwa ajili ya kurekodi wimbo mwingine ambao nitauachia kabla ya Mei mwaka huu," alisema Easy Man.
Msanii huyo alisema ana imani video ya wimbo wake wa 'Mashetani' unafunika kama ule wa 'Kasoro Wewe', huku akikatishwa tamaa baada ya kushindwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Tuzo za Muziki wa Kili Music alizokuwa akiziombea awemo safari hii.

Kamati ya Sheria TFF kukutana juu ya Katiba

Rais wa TFF, Jamal Malinzi
KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inatarajia kukutana mwishoni mwa wiki kupitia taarifa ya utekelezaji wa agizo la wanachama kurekebisha katiba zao. TFF ilitoa agizo kwa wanachama wetu kufanyia marekebisho katiba ikiwemo kuingiza Kamati ya Maadili. Mwisho wa utekelezaji wa agizo hilo ulikuwa Machi 20 mwaka huu. Hivyo, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapokea taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo kutoka kwa Sekretarieti, na baadaye kutoa mwongozo wa hatua inayofuata.

Japanese ataka wasanii wa kike kujifunza kupiga ala

Japanese (kulia) akiwa na wanamuziki wenzake wa Jambo Survivors
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgxe5Rtm0ti7byoMQu71Qu2RCeP9KEud2GUkrLmeGrxVLRPJp1gKactUXZTOHXJoo7jhXXQbSZTnLG8klbNhVehA7oIbPN1esGX21SAjpyExhcK1wLO_mtK85shSRI2zmvGELH-iAE88iw/s1600/FIL0.JPG
Marehemu Asia Daruwesh enzi za uhai wake akionyesha umahiri wake katika kinanda
MUIMBAJI nyota wa zamani wa African Revolution na Double M Sound, Amina Ngaluma 'Japanese' amewataka wasanii wenzake wa kike kujibidiisha kujifunza kupiga ala za muziki badala ya kuishia kuimba tu.
Japanese alisema wasanii wengi wa kike wamekuwa wakikwepa kujifunza kupiga ala au kujifunza vitu zaidi ya uuimbaji na kuwafanya waachwe nyuma na wasanii wa kiume.
Alisema imefika wakati wanawake wenzake kuacha uvivu na badala yake kukamilia ala mbalimbali ili wawe wanamuziki kamili na kuweza kusimama pamoja na wanamuziki wa kiume wanaoonekana kutawala anga la muziki nchini.
"Mimi natunga, napanga muziki, napiga gitaa na ala nyingine, kitu ambachio natamani wasanii wa kike wengine wafuate nyayo ili kuondoa dhana muziki ni wa wanaume tu na sisi kazi yetu kuimba tena wakati mwingine kuitikia tu," alisema.
Alisema pia angependa kuona idadi ya wiambaji wa kike nchini inaongezeka maradufu kama ilivyokuwa miaka ya 1980-2000 waimbaji wa kike walipokuwa wengi na wengine kama marehemu Asia Daruwesh akiwa mahiri katika kupapasa kinanda kwa ustadi mkubwa.

Yanga, Azam vitani tena kesho VPL

Yanga SC
Azam Fc
KLABU za Azam na Yanga ambazo zinachuana kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, zinashuka tena viwanjani kesho (Machi 26 mwaka huu) kuwania pointi tatu. Azam yenye pointi 47 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Mgambo Shooting ipo katika nafasi ya kumi na moja kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 19.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Yanga na Tanzania Prisons kuanzia saa 10.30 jioni. Yanga ipo nyuma ya Azam kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 47. Hata hivyo, timu hiyo ina mchezo mmoja mkononi. Tanzania Prisons ambayo ipo chini ya Kocha David Mwamaja hivi sasa ina pointi 22 ikiwa katika nafasi ya kumi. Timu tatu za mwisho katika ligi hiyo itakayomalizika Aprili 19 mwaka huu zitashuka kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Ligi itaendelea tena Jumamosi (Machi 29 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ashanti United na Oljoro JKT itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Jumapili (Machi 30 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine), Kagera Sugar na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kaitaba), Mtibwa Sugar na Coastal Union (Uwanja wa Manungu), JKT Ruvu na Rhino Rangers (Uwanja wa Azam Complex), Azam na Simba (Uwanja wa Taifa) na Mgambo Shooting na Yanga (Uwanja wa Mkwakwani).

Mahakama yaagiza Yanga ikatwe kuwalipa akina Malashi

Steven Malashi na Wisdom Ndlovu wanaoidai Yanga
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) kukamata Sh. Milioni 106 za klabu ya Yanga kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake, Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.
Taarifa ya TFF imesema kwamba, tayari wameanza utekelezaji wa amri hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa Machi 22 mwaka huu mjini Tabora walizuia Sh. 9,221,250 ambazo ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika mchezo huo ulioingiza jumla ya sh. 38,655,000.
Wachezaji hao walifungua kesi kortini kupinga mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa haki zao za kimkataba. Malashi na Ndlovu walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo ya sh. milioni 106.
Tunawakumbusha wanachama wetu (klabu za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na vyama shiriki) kuzingatia mikataba wanayoingia na watendaji wao wakiwemo wachezaji, makocha na maofisa wengine.
“Iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka kufanya hivyo,”imesema taarifa ya TFF.

Monday, March 24, 2014

Golden Bush wachekelea kutoa mmoja timu ya taifa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjM_enMZwt885hVpN4DNDsO2xLFfCdYaoIdFadOJsGdS73hmKfaQ8fZuX-cFXsmqBpP2SFeiWDVZubmKg_2EXx1PnIG5r33elKJNzCuA8flTadNPHJ0fG59PkLm5lsMhDA0jRcfzbJs5CI/s640/Golden+Bush+FC+Logo.JPG
UONGOZI wa timu ya Golden Bush umesema umefurashwa na kitendo cha mmoja wa wachezaji wake wa timu ya vijana ya Golden Bush FC inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu Wilaya ya Kinondoni, Ayoub Lipati kuteuliwa kwenye timu ya Taifa ya Maboresho iliyotangazwa na TFF.
Lipati ambaye ni mashambuliaji ni mmoja wa wachezaji 36 walioteuliwa na jopo maalum la makocha 40 waliokuwa na kazi ya kusaka wachezaji kwa ajili ya kuboresha timu ya taifa, Taifa Stars katika kuelekea kwenye Fainali za Afrika 2015.
Mlezi wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' aliiambia MICHARAZO kuwa Golden Bush umejisikia faraja uteuzi wa Lipati kutokana na ukweli timu yao ndiyo kwanza ina miaka miwili tangu kuundwa kwake.
"Tumefurahia sana kufanikiwa kutoa mchezaji mmoja katika kikosi cha wachezaji 36 walioteuliwa na jopo maalum la kusaka vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars," alisema Ticotico.
Ticotico alisema imani yake Lipati atakuwa balozi mwema wa Golden Bush katika kikosi kinachotarajiwa kuingia kambini mjini Tukuyu Mbeya mapema mwezi ujao.

Yabainika asilimia 25 ya wanawake Bongo hurukwa 'Ukuta'

 
WAKATI kasi ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, imebainika kuwa asilimia 26.5 ya wanawake nchini Tanzania wanafanya mapenzi kinyume na maumbile. 
Mfumo wa uzazi unaharibika; Watafiti wanabainisha kuwa kitendo hicho licha ya ukweli hakifai kwa vile kinaharibu mfumo wa uzaz.
Pia kina athari kubwa mno kwa mwanadamu, mojawapo ni ikiwemo uwezekano mkubwa wa wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna vilainishi, hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya kuambukiza vijidudu hivyo.


 Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR) alitoa ripoti hiyo hivi karibuni hapa jijini Dar Es Salaam.

Mremi akiwa na jopo la watafiti kutoka NIMR anasema kuwa wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinachowapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi na Kuogopa kupata Mimba.

Vilevile alizitaja sababu nyingine za wanawake kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.

Sampuli za utafiti Utafiti huo ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Tanga, Makete na Siha. Mremi anasema “Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo.

Imani potofu kwa wanaume Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maaambukizi ya VVU, kitu ambacho ni uongo, kwani huko ndiko kwenye kuchangia ukimwi kwa haraka zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote.
Credit:E.Shiratu

Hizi ndizo mechi za lala salama za VPL


MACHI 26, 2014
Yanga v/s Tanzania Prisons- Taifa, Dar
Mgambo Shooting v/s Azam Fc- Mkwakwani, Tanga

MACHI 29, 2014
Ashant United v/s JKT Oljoro- Chamazi, Dar

MACHI 30, 2014
Mbeya City v/s Tanzania Prisons- Sokoine, Mbeya
Kagera Sugar v/s Ruvu Shooting- Kaitaba, Bukoba
Mtibwa Sugar v/s Coastal Union- Manungu, Morogoro
JKT Ruvu v/s Rhino Rangers- Chamazi, Dar
Azam Fc v/s Simba- Taifa, Dar
Mgambo v/s Yanga- Mkwakwani, Tanga

APRILI 5, 2014
Kagera Sugar v/s Simba- Kaitaba, Bukoba
Ashanti United v/s Mbeya City- Chamazi, Dar

APRILI 6, 2014
Coastal Union v/s Mgambo Shooting-Mkwakwani, Tanga
JKT Oljoro v/s Tanzania Prisons- Sheikh Amri Abeid, Arusha
Rhino Rangers v/s Mtibwa Sugar- Ali Hassan Mwinyi, Tabora
Ruvu Shooting v/s Azam Fc- Mabatini, Pwani
Yanga v/s JKT Ruvu- Taifa, Dar

APRILI 9, 2014
Yanga v/s Kagera Sugar- Taifa, Dar

APRILI 12, 2014
Mtibwa Sugar v/s Ruvu Shooting- Manungu, Morogoro
Coastal Union v/s JKT Ruvu- Mkwakwani, Tanga
Tanzania Prisons v/s Rhino Rangera- Sokoine, Mbeya

APRILI 13, 2014
Mgambo Shooting v/s Kagera Sugar- Mkwakwani, Tanga
Simba v/s Ashant United- Taifa, Dar
Mbeya City v/s Azam Fc- Sokoine, Mbeya
JKT Oljoro v/s Yanga- Sheikh Amri Abeid, Arusha

APRILI 19, 2014
Rhino Rangers v/s Ruvu Shooting- Ali Hassan Mwinyi, Tabora
Mbeya City v/s Mgambo Shooting- Sokoine, Mbeya
Tanzania Prisons v/s Ashant United- Jamhuri, Morogoro
JKT Ruvu v/s Azam Fc- Chamazi, Dar
JKT Oljoro v/s Mtibwa Sugar- Sheikh Amri Abeid, Arusha
Coastal Union v/s Kagera Sugar- Mkwakwani, Tanga
Yanga v/s Simba- Taifa, Dar

Tevez azidi kuipaisha Juve Italia, Milan yadroo

http://e2.365dm.com/14/03/660x350/Catania-v-Juventus-Carlos-Tevez-L-vies-with-C_3106513.jpg?20140323214233
Tevez akichuana na mchezaji wa Catania usiku wa jana kwenye Seria A
http://sport.bt.com/images/juve-grind-out-catania-win-136388712671108302?v=140323221505
Akishangilia bao lao

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Italia, Juventus imeendelea kutakata kwa kupata ushindi mwembamba ugenini dhidi ya Catania shukrani za pekee ziende kwa Carlos Teves aliyefunga bao hilo la pekee katika dakika ya 59.
Ushindi huo wa Juve umewafanya wafikishe jumla ya pointi 78 baada ya kucheza mechi 29 wakiiacha mbali Roma inayoshuka dimbani  kesho kuumana na Torino ikiwa na pointi zake 64.
Bao alilofunga Tevez nytota wa zamani wa Aston Villa, Manchester Utd na Manchester City, limemfanya afikishe jumla ya mabao 16 katika ligi hiyo na kulingana na nyota wa Torino, Ciro Immobile.
Katika mechi nyingine zilizochezwa usiku wa jana Napoli ilikubali kipigo kwenye uwanja wake wa nyumbani toka kwa Fiorentina, nazo timu za Lazio na AC Milan zikitoshana nguvu kwa kufunga bao 1-1, wanyeji wakijifunga kabla ya kusawazisha katika kipindi cha pili.
Kipute cha pili kinatarajiwa kuendea tena kesho kwa pambano la Roma itakayoikaribisha Torino, kabla ya keshokutwa Chievo kuumana na Bologna, Cagliari dhidi ya Hellas Verona, huku Genoa itaikaribisha Lazio na  Atalanta itaumana na Livorno.
Siku hiyo ya Jumatano pia kutakuw ana mechi nyingine ya kukata na shoka kati ya Fiorentina itakayoikaribisha Ac Milan, huku  Catania itaumana na Napoli, wakati  Juventus watakuwa nyumbani kuwakaribisha Parma na Sassuolo itakuwa mwenyeji wa Sampdoria.
Alhamis kutakuwa na pambano moja tu litakalowakutanisha Inter Milan ambayo jana ilichezea kichapo itakayoumana na Udinese.

Barca yaizima Rea kwao, Messi apiga hat trick

Matchwinner: Messi points to the Barcelona support as Gerard Pique (centre) and Alexis Sanchez catch up
Messi akishangilia moja ya mabao yake matatu alipoiangamiza Real Madrid
Flying high: Sergio Ramos celebrates Madrid's third with Ronaldo (left) while the Madrid star jumps for joy (right)
Real Madrid wakishangilia moja ya mabao yao

KLABU ya Real Madrid usiku wa kuamkia leo imechezea kichapo cha mabao 4-3 toka kwa wapinzani wa jadi Barcelona na kutoa baraka kwa mahasimu wao wa jiji la Madrid, Atletico Madrid kukikalia jumla kiti cha uongozi wa Ligi Kuu ya Hispania.
Mshambuliaji nyota wa Argentina, Lionel Messi alidhihirisha yeye ni bora baada ya kufunga hat trick kwenye pambano hilo lililochezwa uwanja wa Santiago Bernabeu, mjini Madrid.
Wageni walianza kuandika bao dakika ya saba kupitia kwa Andres Iniesta kabla ya Mfaransa,  Karim Benzema kusawazisha bao hilo dakika ya 20 na kuongeza jingine la pili dakika ya 24.
Dakika tatu kabla ya mapumziko Messi aliisawazishia bao na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimefungana mabao 2-2.
Kipindi kilipoanza iliwachukua wenyeji dakika 10 kuandika bao la tatu kupitia kwa Cristiano Ronaldo aliyefunga kwa mkwaju wa penati.
Hata hivyo Lionel Messi alisawazisha hilo dakika ya 65 kwa mkwaju wa penati pia kabla ya kuongeza jingine dakika tano kabla ya pambano hilo kumalizika na kukamilisha hat trick yake na kuipa ushindi wa mabao 4-3 timu yake ya Barcelona.
Ushindi huo umeifanya Barcelona imeendelea kubakia nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 69, moja zaidi ya wapinzani wao Real Madrid na Atletico Madrid waliopo kileleni kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na matokeo baina yao wawili hao waliopo juu.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho Jumanne hadi Ijumaa kwa mechi ambazo zitaendelea kutoa taswira ya ubingwa wa nchi hiyi.
Jumanne;
Almería vs Real Sociedad
Málaga  vs  Espanyol
Jumatano:
Elche vs Athletic Club
Barcelona vs Celta de Vigo
Rayo Vallecano vs Osasuna
Alhamis:
Atlético Madrid vs Granada
Sevilla vs Real Madrid
Getafe vs  Villarreal
Real Sociedad  vs Real Valladolid
Ijumaa:
Levante vs Real Betis
Almería vs Valencia

TP Mazembe yafa ugenini, Mbwana kama kawa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPcbztEZEpnlosWiXEocIS2HDtp7-xxKd2CpOOqJ8ABEqV2R8cXTFSuU-hmbUwOF98KNrE9G8OypEoBHSUDZNvM0YjXWj3qCdILvnjXJ4_j6v_JPdXGMb684Ib7QY1MeKmWxl8feSypeC_/s1600/Samata-Bwana58021.jpgMABINGWA wa zamani wa Afrika, TP Mazembe jana wamekumbana na kipigo cha mabao 2-1 katika pambano lao la mkondo wa kwanza wa hatia ya 16 Bora dhidi ya we nyeji wao, Sewe ya Ivory Coast.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta aliifungia timu yake bao la kufitia machozi baada ya wenyeji kujipatia mabao yake kupitia kwa Roger Assale  katika dakika ya 38 kaba la kuongeza jingine kwa mkwaju wa penati  dakika ya 82 kupitia  Christian Kouame.
Hata hivyo wenyeji wakiamini wameisulubu Tp Mazembe kwa mabao mawili kavu, mtokea benchi Mbwana Samatta aliifunga bao la kufutia machozi ambalo linaweza kuwa msaada kwa vijana hao wa Lubumbashi kwa mechi ya mkondo wa pili wikiendi hii.
Samatta tegemeo la Taifa Stars na Mchezaji Bora wa Mazembe kwa msimu uliopita alifunga bao hilo dakika mbili kabla ya kumalizika kwa pambano hilo.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo ya Mabingwa Afrika, Horoya AC ya Guine ilikubali kichapo cha bao 1-0 kwa CS Sfaxien ya Tunisia, huku Cotonsport ya Cameroon ikidonyolewa kidude kimoja na ES Sétif ya Algeria wakiwa ugenini mjini Algers.
Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, CS Constatine ya Algeria imeizabua ASEC Memosa ya Ivory Coast kwa bao 1-0.

Sunday, March 23, 2014

Atletico yaibutua Betis, yaiengua Real kileleni kwa muda

Atletico Madrid
Atletico Madrid wakishangilia moja ya mabao yao
IKIWA imesalia kama saa moja na ushei kabla ya mahasimu wa Ligi Kuu ya Hispania, Real Madrid na  Barcelona kupepetana katika pambano lao la El Clasico, Atletico Madrid imekalia uongozi kwa muda baada ya hivi punde kutoka kuifua Real Betis ikiwa kwao kwa mabao 2-0 na kuiengua Real.
Atletico imefikisha pointi 70 sawa na Real Madrid lakini imekwea kileleni kwa uwiano wa mechi baina yao huku uwiano wa mabao Real wakiwa zaidi ya wapinzani wao hao wa jiji moja la Madrid.
Mabvao yaliyozidi kuwapa tumaini la kuwa mabingwa kwa vijana hao wa Diego Simon yaliwekwa kimiani na Gabi katika dakika 58 kwa pasi ya Turan kabla ya Diego Costa kuongeza la pili dakika sita baadaye akimalizia kazi ya Koke.
Katika mchezo huo wenyeji walijikuta wakicheza pungufu baada ya mchezaji wake mmoja Rodriguez kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kufuatiwa na nyekundu katika kipindi cha kwanza.
Hivi sasa uwanjani zipo timu za  Valencia inayoikaribisha Villarreal kabla ya Real Madrid na Barca kuonyesha kazi uwanja wa Santiago Bernabeu ambapo taswira ya ubingwa kwa timu hizo mbili kubwa itafahamika.

Aston Villa yafa nyumbani yagongwa 4-1 kwa Stoke City

Peter Crouch
Peter Crouch akifunga bao lake dhidi ya Aston Villa
Peter Odemwingie
Peter Odemwingie
TIMU ya soka ya Aston Villa imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kufumuliwa mabao 4-1 na Stoke City katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika hivi punde.
Villa ikiyoiduwaza Chelsea wiki iliyopita kwa kuilaza bao 1-0, ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya tano tu ya mchezo kupitia kwa Christian Benteke akimalizia kazi ya Delph.
Hata hivyo wageni walirejesha bao hilo katika dakika ya 22 kupitia Peter Odemwingie aliyemaliza kazi ya mshambuliaji ngongoti, Peter Crouch, ambaye dakika nne baadaye aliipatia Stoke bao la tatu na dakika atatu kabla ya mapumziko N'Zonzi alifunga bao la nne.
Stoke iliongeza bao la nne lililoifanya iiporomoshe Villa katika nafasi ya 10 na kuikalia wao wakibadilishana na wapinzani wao hao wanaowapokea nafasi ya 11 kutokana na kufikisha pointi 37, lilifungwa dakika ya  90 na Cameron.

AS Vita yaifyatua Kaizer Chiefs 3-0

http://www.michezoafrika.com/NewsImages/VIta-club-of-Congo.jpg
KLABU YA AS Vita ya DR Congo imeifumua Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa mabao 3-0 katika mechi za 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, huku AC Leopards ya Kongo ikilazimishwa sare nyumbani na Al Hilal ya Sudan.
mabao yote ya Vita katika pambano hilo yalifungwa na Firmin Ndombe Mubele na kuiweka katika nafasi nzuri timu yake ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo iwapo itakomaa kwenye mechi ya marudiano wiki ijayo nchini Afrika Kusini.
Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Zesco ya Zambia ikiwa ugenini nchini Ghana imechezea kichapo cha mabao 2-0 toka kwa wenyeji wao Medeama, huku Ismailia ya Misri na Petro du Luanda ya Angola zikishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu.
Nayo timu ya Warri Woriors ya Nigeria imelazimishwa sare tasa na Bizertin ya Tunisia katika pambano jingine la mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho.
Mechi nyingine za ratiba ya mkondo wa kwanza zinaendelea kuchezwa kwa sasa ukiwamo pambano la TP Mazembe dhidi ya wenyeji wao Sewe Sports ya Ivory Coast.

Inter Milan yapigwa nyumbani, Sampdoria yaua Italia

 http://www.iberita.com/wp-content/uploads/2013/04/inter.jpg
MABINGWA wa zamani wa Ulaya, Inter Milan licha ya kucheza nyumbani, imejikuta ikikong'otwa na Atalanta kwa mabao 2-1katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Seria A.
Milan watakuwa wanamuota Giacomo Bonaventura, aliyefunga mabao yote katika kila kipindi na kuipa ushindi timu yake ugenini.
Bonaventura alianza kuwashutua wenyeji kwa kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 35 kabla ya Inter Milan kuchomoa dakika moja baadaye kupiyia kwa Mauro Icardi na kwenda mapumziko wakiwa nguvu sawa.
Kipindi cha pili timu zote zilishambuliana kwa zamu na hasa baada ya kufanya mabadiliko ya wachezaji na wageni wakajiandikia bao lao la pili katika dakika ya 90 lililofungwa tena na Bonaventura.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Parma ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 na Genoa, Bologna ikaifumua Cagliari kwenye uwanja wao wa nyumbani na Sampdoria  ikautumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kuisambaratisha Hellas Verona kwa mabao 5-0 na Udinese ikiwa nyumbani ikapata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sassuolo.
Baadaye watetezi Juventus watakuwa ugenini kuumana na Catania, Napoli itapepetana na Fiorentina na Lazio wataumana na AC Milan ambao msimu huu wamekuwa wakipepesuka katika ligi hiyo.

Jahazi la Ashanti Utd lazidi kuzama, yapigwa 2-0

* Mgambo JKT yakomaa Mkwakwani
Ashanti waliyonyukwa 2-0 na Ruvu Shooting

Mgambo waliokomaa Mkwakwani na kutoka sare ya Mtibwa Sugar
Ruvu Shooting walioinyoa Ashanti Utd
TIMU ya soka ya Ruvu Shooting imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuifumua Ashanti Utd kwa mabao 2-0 katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Mgambo JKT ikibanwa nyumbani na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Mkwakwani-Tanga.
Elias Maguli ambaye alikuwa hajafunga bao lolote tangu duru la pili lianze alifunga bao la kwanza katika dakika ya sita na kuongeza jingine katika dakika ya 63.
Hata hivyo Ruvu iliyokuwa kwenye uwanja wa Mabatini-Mlandizi walijikuta wakicheza pungufu baada ya mchezaji wao Ali Kani kutolewa kwa kadi nyekundu.
Ushindi huo umeifanya Ruvu kufikisha jumla ya pointi 31 na kushika nafasi ya sita pointi moja dhidi ya Kagera Sugar wanaokamata nafasi ya tano.
Katika mechi ya Mkwakwani, Mgambo na Mtibwa zilitoka sare ya 1-1 katika pambano linalodaiwa lilikuwa kali.
Wenyeji walitanguliwa kufungwa bao na Vincent Barnabas kabla ya kuchomoa baadaye kupitia kwa Peter Malianzi na kufanya mchezo huo kuisha kwa sare ya 1-1 na timu zote kuambulia pointi moja kila moja.
Katika pambano hilo mshambuliaji nyota wa Mgambo, Fully Maganga aliwaweka roho juu mabeki wa Mtibwa kwa muda mrefu wa pambano hilo licha ya kwamba hakufanikiwa kufunga bao kwa kukosa bahati siku ya leo.

Timu ya Babi yafufuka Malaysia yashinda 1-0

BAADA ya kupoteza mechi tatu mfululizo hatimaye timu anayoichezea kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'babi' ya UiTM imeona mwezi baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya 'vibonde' wa Ligi Kuu ya Malaysia, PBAPP.
Ushindi huo uliopatikana kwenye uwanja wa Bandaraya katika mji wa Penang, umeifanya UiTM kufikisha pointi saba baada ya kucheza mechi saba, ikishinda mechi mbili na kutoka sare moja na kupoteza mechi nyingine tatu na kushika nafasi ya 10 kati ya timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo.
UiTM iliyoingia mkataba wa mwaka mmoja na nyota huyo wa zamani wa Yanga, Mtibwa Sugar, Azam, KMKM na Taifa Stars, itashuka tena dimbani kesho Jumatatu kwa kuumana na Felda United itakayoialika kwenye uwanja wao wa Mini UiTM uliopo mji wa Shah Alam.

Spurs yaizamisha Southampton yaipumulia Arsenal

Christian Eriksen scores Tottenham's second goal
Eriksen akitupia bao lake la pili kimiani dhidi ya Southampton leo
Christian Eriksen
Eriksen akishangilia baada ya kufunga
MSHAMBULIAJI Christian Eriksen leo ameibuka kuwa shujaa wa Tottenham Hotspur baada ya kuhusika na mabao matatu yaliyoizamisha Southampton katika pambano la Ligi Kuu ya England lililochezwa jioni hii.
Mdenish huyo alifunga mabao mawili katika kila kipindi na kutengeneza jingine lililopachikwa wavuni na katika dakika za 'jioni' na Gylfi Sigurdsson na kuipa ushindi murua wa mabao 3-2 Spurs ikiwa kwenye uwnaja wake wa nyumbani.
Eriksen alifunga bao la kwanza katika dakika ya 31 kabla ya kuongeza jingine dakika moja baada ya kuanza kipindi cha pili.
Hata hivyo wageni ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 16 lililofungwa na Jay Rodriguez kabla ya Adam Lallana kuongeza la pili dakika ya 28 na kuwapa wasiwasi wenyeji kwamba huenda wakalala tena nyumbani kama mechi zao kadhaa zilizopita.
Hata hivyo Eriksen alifufua matumaini kwa bao la dakika 31 na kuifanya Spurs kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-1.
Kwa ushindi huo Spurs imerejea kwenye nafasi ya tano iliyokuwa imeteremshwa na Everton iliyoishinda Swansea City jana kwa mabao 3-2 kwa kufikisha pointi 56, sita pungufu na ilizonazo mahasimu wao Arsenal waliopo nafasi ya tanoi baada ya jana kukumbana na kipigo cha paka mwizi mbele ya Chelsea.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea muda mfupi baadaye kwa pambano kati ya Astin Villa dhidi ya Stoke City na Jumanne kushuhudia michezoi mingine ukiwamo wa Manchester City dhidi na Manchester United.

Simba yapigwa kidude na Coastal, Azam haishikiki

Mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Singano 'Messi' akijaribu kumtoka mchezaji wa Coastal katika mechi yao ya leoi (Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba wamejikuta wakiangukia pua mbele ya 'ndugu' zao kutoka Tanga, Coastal Union kwa kudunguliwa bao 1-0 na kuwafanya wapoteze matumaini ya kuendelea kuwepo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Simba, inayonolewa na kocha Zdrakov Logarusic, ilikumbana na kipigo hicho cha kushtukiza kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la mchezo ambao Coastal waliamua kuchezesha wachezaji wengi vijana badala ya wazoefu waliozoeleka, liliwekwa kimiani na beki Hamad Juma katika dakika ya 45 kwa shuti lililomshinda kipa Ivo Mapunda aliyerejea baada ya kuwa nje baada ya kupatwa na msiba wa baba yake mzazi.
Simba pamoja na kucharuka ili kutaka kurejesha bao hilo ilijikuta ikishindwa kumtungia kipa Fikirini Suleiman, aliyekuwa makini kwa dakika zote 90.
Ushindi huo wa Coastal Union umekuja baada ya 'Wazee hao wa Oman'  kutoka kupokea kipigo cha aibu cha mabao 4-0 toka kwa Azam na kujengeka hisia kwamba kuna hujuma iliyofanywa ndani ya kikosi hicho na ndicho kinachoelezwa kimemfanya kocha Yusuph Chipo kufanya mabadiliko katika kikosi chake kilichoivaa Simba.
Katika mechi nyingine, Azam imeendelea kuonyesha dhamira yao ya kutwaa ubingwa msimu baada ya kuinyuka Oljoro JKT kwa bao 1-0, bao lililofungwa na John Bocco 'Adebayor' katika dakika ya 71.
Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kuifanya Azam kufikisha pointi 47 nne zaidi na ilizonazo Yanga ambayo haya hivyo ina mchezo mmoja mkononi.
Kwa kuinyuka Simba, mabingwa hao wa Tanzania wamefikisha pointi 29, huku Simba wakisaliwa na pointi 36 wakisalia nafasi ya nne.

Dk Kigwangwala anusurika kufa kwa risasi

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMJ3fLswzaKUo6eqARrqJxMzsNHNfa_QPWD1r0XSqRf34b7bj_H_QzUI5jdehMkX4aqDfR7yG-Aja-glnt3OeTXRAuVFdW6qAsZAUF-dtcPyeHJE03T-ZENkh2tsKVh5ZDcQPK4Vd_8LX_/s640/317924_417505948326261_1390417981_n.jpgkupitia ukurasa wake wa Facebook Hamisi kaandika "Nimenusurika kuuawa muda si mrefu. Mungu mkubwa. Askari kwenye gari ananiambia na bahati yako nimekukosa, nililenga kichwa....kijana mmoja alikaa mbele yangu amepigwa risasi kwenye paji la uso, sijui kama amenusurika! Vijana wamenilinda kwa ujasiri bila hofu. Leo askari wamenikamata kwa staha. Siwezi kukubali kamwe dhulma ya mabepari dhidi ya wanyonge! Niliwaahidi na niliapa kuwatetea..."




Mourinho adai PSG wna furaha kukutana nao

 http://www.mwebantu.com/wp-content/uploads/2012/12/Jose-Mourinho-Wallpaper-HD-2.jpg
KOCHA asiyeisha vituko na anayependa kucheza na akili za wapinzani wake, Jose Mourinho wa Chelsea amedai anaamini PSG wana furaha kubwa ya kupangiwa kukutana nao kwenye mechi ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mabingwa hao wa Ligue 1 nchini Ufaransa, ilipangwa Ijumaa kukutana na Chelsea katika mechi ya mkondo huo wa 8 Bora na itaanzia nyumbani April 2 kabla ya kuwafuata 'the Blues' kwenye uwanja wao wa Stanford Bridge siku sita baadaye.
Akizungumza mara baada ya pambano lao la jana la Ligi Kuu ya England dhidi ya Arsenal na kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 6-0, Mourinho alisema wapinzani wao hao wa Ufaransa ni wazuri na imani mechi yao itakuwa ngumu wakikutana mwezi ujao.

Kocha Man City atabiri nne zitakazotwaa taji EPL

 http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/05/15/article-2325090-19C218DE000005DC-373_634x413.jpg
MENEJA wa klabu ya Manchester City,  Manuel Pellegrini amesema ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa sasa unaweza kunyakuliwa na timu nne za ligi hiyo.
Pellegrini amesema ukiondoa timu yake na Chelsea inayoongoza msimamo wa ligi hiyo  nyingine zenye nafasi ya kutwaa taji hilo ni Liverpool na Arsenal ambayo jana ilichezea kipigo cha aibu toka kwa Chelsea.
Kocha huyo anayekabiliwa na pambano dhidi ya mahasimu wao wa Manchester, Mashetani Wekundi siku ya Jumanne alisema kwa mwenendo wa Liverpool na hata Arsenal bado zina nafasi licha ya wengi kuzipa nafasi Manchester City au Chelsea kubeba taji hilo msimu huu.
Chelsea inaoongoza msimamo ikiwa na pointi 69 wakati Liverpool inafuatia ikiwa na pointi 65 kisha City yenye pointi sita pungufu dhidi ya vinara hao, ingaw aina michezo mitatu mkononi ikiwa imecheza mechi 28 na Chelsea 3-1.

Thomas Mourice arudi nyumbani kujipanga upya kimataifa

Thomas Mourice (wa pili toka kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wa Bandari Kenya enzi akiichezea klabu hiyo
MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Moro Utd na Yanga, Thomas Mourice amerejea nyumbani baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Bandari-Kenya, huku akisema anafanya mipango ya kuondoka tena kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Akizungumza na MICHARAZO, Mourice aliyewahi kucheza pia katika Ligi Kuu ya Zanzibar, alisema badala ya kuongeza mkataba na klabu yake ya Bandari inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya ameona ni bora aje nyumbani kupumzika kabla ya kujipanga tena kutoka nje ya nchi.
"Nimerejea hivi karfibuni baada ya kumaliza mkataba na Bandari-Kenya, napumzika kidogo kabla ya kuondoka tena kwenda kucheza soka la kulipwa," alisema Mourice.
Mfumania nyavu huyo mahiri, alisema bado hajawa na uhakika ataelekea wapi safari katika mipango yake ya kucheza soka la kulipwa, lakini alidokeza huenda akaibukia Arabuni au barani Ulaya.
"Mimi kokote naweza kwenda kucheza, lakini katika mipango yangu huenda nikaenda Arabuni au Ulaya kulingana na wakala wangu anayeendelea kunisakia timu wakati napumziko hapa nyumbani," alisema.
Mshambuliaji huyo alijiunga na Bandari misimi mitatu iliyopita pamoja na wachezaji wenzake wa Kitanzania akiwamo Mohammed Banka aliyerejea na kujiunga Asdhanti Utd, Meshack Abel na David Naftal wanaoendelea kucheza mpaka sasa na kuisaidia kumaliza nafasi ya 6 msimu uliopita katika ligi ya nchi hiyo ambayo bingwa wake alikuwa Gor Mahia.

Wawili wauwawa Kanisani

mombasa 
VITENDO vinavyoonyesha binadamu hana ujanja mbele ya shetani vimeendelea baada ya leo jumapili tarehe 23/3 watu kadhaa ambao wanasadikika kuwa ni magaidi wamevamia kanisa moja linalojulikana kwa jina la Joy Jesus Church huko Mombasa na kuanza kupiga risasi kanisani hapo.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema baada ya watu hao kutekeleza tukio hilo walikimbia kwa miguu kuelekea pasipo julikana.
Afisa wa polisi wa eneo hilo amesema hadi sasa wamefariki watu wawili na wengine kumi wamepata majeraha ya risasi nakukimbizwa hospitali.
Kikundi cha Al Shabaab kiliwahi kuhusishwa na tukio kama hili huko Nairobi lakini hivi sasa limetokea Mombasa.
Maafisa wa polisi wamesema wanaendelea kufanya uchunguzi wa kuwakamata watu hao japokuwa hadi sasa bado hawajapata tetesi yoyote juu ya watuhumiwa hao