STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 21, 2014

Rais JK kukataje kiu ya watanzania kesho?

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLcBTaUn2K5EFfb-YZJkKO2h55foHxnikx-untCz65m2xFREdv72IRXmAU_a7FExuI-7Hw5MHx9rhneKpTihkeuDO10muvGq9ZF-2fuNkIHaiu6ZqaXXNF8BKaaQdnVef9igzFvd2t6Hs/s640/Rais+JK+2.jpgRAIS Jakaya Kikwete anasubiriwa kwa hamu na watanzania kukata kiu juu ya baadhi ya mambo yaliyojiri nchini ambayo yameliacha taifa kwenye sintifashamu.
Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow zipatazo bil. 306, na mvurugano uliojitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ni kati ya vinavyosubiriwa kusikia Rais atasema nini.
Juzi watanzania walidokezwa kuwa kungekuwa na fursa kwa Rais kuzungumza na wananchi kabla ya kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu kukanusha taarifa hizo na kudai Rais atazungumza na Watanzania kesho kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
Je mawaziri waliotajwa kuhusika kwa namna moja juu ya sakata ya Escrow na uchaguzi wa serikali za mitaa waenda na maji au watapeta kulingana na duru za kisiasa na kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaigana kwamba hatajiuzulu na pia yeye na Rais wametoka mbali?
Ngoja tusubiri tuone Rais atakata kiu ya watanzania kivipi hiyo kesho katika hotuba yake!

Liverpool, Arsenal hakuna mbabe

Borini akilimwa kadi kizembe
Olivier Giroud akiifungia Arsenal bao la pili
PAMBANO la kukata na shoka baina ya Liverpool na Arsenal limemalizika hivi punde kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2, huku wenyeji wakimaliza pungufu baada ya Fabio Borini kuonyesha kadi ya pili ya njano iliyoambatana na nyekundu na kutolewa nje ya uwanja wakati timu yake ikiwa nyuma ya ba02-1.
Borini aliyeingia toka benchi alipewa kadi hiyo, dakika ya 90 lakini vijana na Branden Rodgers walicharuka na kurejesha bao dakika za majeruhi kupitia Martin Skrtel.
Kabla ya hapo wageni walipata bao la pili dakika ya 64 kupitia kwa Olivier Giroud na kuonekana kama Arsenal wataibuka na ushindi kabla ya beki Skrtel akiwa amefungwa kichwani kutokana na kuumia kuryka juu kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Adam Lallana na kuipa afueni Liverpool iliyoiengua Everton na kukaa nafasi ya 10 kutoka ile ya 11 waliokuwa wakishikilia.
Arsenal kwa sare hiyo imeishusha Tottenham hotspur na kukalia nafasi ya sita licha ya zote kulingana pointi 27 kila moja baada ya timu zote kucheza mechi 17, ila zinatenganishwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Zaidi ya Uuaji! Mwenye VVU amnyonyesha mtoto wa jirani

MWANAMKE mmoja raia wa Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto wa jirani bila ruhusa anakabiliwa na kifungo cha karibu miaka miwili kwa kumwambukiza mtu HIV kwa kukusudia kwa kuwa yeye ni mwathirika.
Annie Mpariwa, 39, alifikishwa mbele ya mahakama ya Gaborone wiki iliyopita na kesi hiyo iliahirishwa hadi january 24 kuruhusu kipimo cha pili cha HIV kufanyiwa mtoto huyo.
Matokeo ya kwanza ya mtoto huyo yalionyesha hana virusi ilhali ya mama huyo yalikuwa na virusi. Mpariwa alikamatwa wiki jana kwa mashtaka ya usumbufu na iwapo mtoto huyo atapatikana na virusi, mashtaka hayo yatazidishwa hadi 'kumwambukiza mtu mwingine HIV kimakusudi.
Mama wa mtoto huyo wa miezi14, Nyasha Mironga,alisema kumwona mwanawe akinyonyeshwa na jirani wake lilikuwa ni jambo lililomshtua sana.
Kisa hicho kimetokea baada ya kupitishwa kwa sheria mpya ya HIV/Aids inayotoa adhabu kali zaidi kwa wale wanaowaambukiza.Je kama wewe ndio mwanao utachukua hatua gani?
ALWAYS POSITIVE ATTITUDE.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Kumekucha Anfield! sasa mapumziko 1-1

Mathieu Debuchy akiisawazishia Arsenal bao dakika za majeruhi kabla ya mapumziko
Coutinho (10) kulia akiifungia Liverpool bao la kuongoza uwanja wa Anfield.

PAMBANO la Liverpool na Arsenal limeenda mapumziko matokeo yakiwa bao 1-1 baada ya wababe hao kutumia sekunde chache kabla ya mapumziko kupata mabao yake, wenyeji Liverpool wakianza kupitia Phillipe Coutinho katika dakika ya 45.
Hata hivyo dakika mbili za nyongeza, Mathieu Debuchy aliisawazishia timu yake ya Arsenal na kufanya mambo yaendelee kuwa magumu tofauti na mechi kama hiyo msimu uliopita ambapo mpaka dakika ya 20 Liverpool walikuwa tayari wapo mbele kwa mabao 4-0.

Muhammad Ali akimbizwa hospitalini

http://media.washtimes.com/media/image/2012/09/13/people-muhammad-ali_lea.jpg
Bingwa wa zamani wa Dunia, Muhammad Ali
 BINGWA wa zamani wa Dunia wa Ngumi za Kulipwa Uzito wa Juu, Muhammad Ali, amekimbizwa hopitalini baada ya kubanwa na 'Vichomi' (Pneumonia)
Mwanamasumbwi hiuyo aliyenyakua ubingwa huo wa dunia mara tatu kwa mujibu wa msemaji wake Bob Gunnell, hali yake inaendelea vema.
Gunnell amesema kwamba familia ya bingwa huyo mwenye miaka 72 inahitaji faragha wakati akiendelea kupata matibabu dhidi ya maambukizi hayo ya mapafu.
Kwa muda mrefu bondia huyo wa zamani amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa 'Kutetemeka' (Parkinson) tangu alipostaafu ngumi mwaka 1984.

Sunderland yaizamisha Newcastle Utd nyumbani kwao

Sunderland's Adam Johnson
Adam Johnson akiwaliza wapinzani wao
http://news.bbcimg.co.uk/media/images/79876000/jpg/_79876229_newcastlevsunderland.jpgSunderland's Steven Fletcher and Newcastle's Steven TaylorBAO la dakika ya 90 lililofungwa na Adam Johnson limeiwezesha Sunderland kuwatambia wapinzani wao wa jadi Newcastle United wakiwa nyumbani kwao katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England.
Sunderland ambayo imekuwa ikipigana kuondoka maeneo ya mkiani, imeweza kufikisha jumla ya pointi 19 ns kuchupa hadi nafasi ya 14 ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Chelsea.
Kipigo hicho cha Newcastle ni cha pili mfululizo katika ligi hiyo baada ya awali kupata ushindi mfululizo na kusaliwa na pointi zake 23 ikiwa nafasi ya 9.
Ligi hiyo inaendelea usiku huu kwa pambano la kukata na shoka kati ya Arsenal waliowafuata Liverpool nyumbani kwao kwenye uwanja wa Anfield na mpaka sasa matokeo ni 0-0.

Southampton yazinduka, Spurs kanyaga twende England

Southampton
Southampton wakiangika moja ya mabao yao
Graziano Pelle
Pelle akimtungua Tim Howard
Erik Lamela, Tottenham
Spurs wakiangilia moja ya mabao yao mawili walipoizamisha Burnley
BAADA ya kufungwa mechi tano mfululizo zikiwamo nne za Ligi Kuu na moja ya Kombe la Ligi, hatimaye Southampton wikiendi hii imezinduka baada ya kuinyoa Everton mabao 3-0 na kuendelea kusalia kwenye nafasi ya tano katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Chelsea.
Bao la penati la Romeo Lukaku katika dakika ya 38 na mengine mawili ya kipindi cha pili kupitia kwaGraziano Pelle katika dakika ya 65 na lile la Maya Yoshida dakika nane kabla ya kumalizika kwa pambano kuliwafanya Southampton kuonja ushindi ikiwa nyumbani na kufikisha pointi 29.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Mashetani Wekundu wakiwa ugenini walishindwa kuitambia Aston Villa waliokuwa pungufu kw akutoka sare ya 1-1, Mabingwa watetezi, Manchester City wakipata ushindi wa nyumbani wa mabao 3-0 dhidi ya Crystal Palace na Tottenham Hotspur ikiwa nyumbani White Hartlane waliishinda timu ya Burnley mabao 2-2 na kuwaengua Arsenal waliokuwa juu yao.
Pia timu ya QPR ikiwa nyumbani iliwaduwaza wageni wao West Bromwich kwa kuwalaza mabao 3-2, Hull City ikakubali kipigo cha nyumbani cha bao 1-0 dhidi ya Swansea City na West Ham United ikatamba nyumbani dhidi ya Leicester City kwa kuilaza mabaio 2-0.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa michezo miwili, Liverpool itaialika Arsenal uwanja wa Anfield na wapinzani wajadi Newcastle United itaonyeshana kazi na Sunderland katika mchezo mwingine kabla ya kesho kushuhudiwa vinara Chelsea wakikwaruzana na Stoke City ugenini.

Mkutano Mkuu wa TFF kufanyika mkoani Singida


Kamati ya Utendaji imejadili rasimu ya Kanuni za Leseni za Klabu (Club Licensing Regulations), na kuagiza Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ifanye marekebisho ya mwisho, kabla ya kanuni hizo kusainiwa na kuanza kutumika.
UANZISHAJI MFUKO WA MAENDELEO YA MPIRA WA MIGUU (FDF)Kamati ya Utendaji imepokea taarifa ya maendeleo ya mchakato wa uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (Football Development Fund- FDF).
Imeipongeza Kamati ya Mfuko huo inayoongozwa na Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Tenga, na kuitaka fanye jitihada za kukamilisha rasimu ya kanuni za uendeshaji mfuko huo.
Mbali ya Tenga, wajumbe wengine wa mfuko huo ni Ayoub Chamshama, Ephraim Mafuru, Frederick Mwakalebela, Tarimba Abbas na Zarina Madabida. Sekretarieti ya mfuko huo inaundwa na Henry Tandau ambaye ni Katibu, Wakili Emmanuel Muga na Boniface Wambura.
FDF ambao ni mfuko utakaokuwa unajitegemea utakuwa unashughulika na maendeleo ya mpira wa miguu kwa vijana, na nyanja nyingine za maendeleo kwa mchezo huo.
MKUTANO MKUU KUFANYIKA SINGIDA MACHI 14
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepanga Mkutano Mkuu wa Kawaida wa mwaka ufanyike Machi 14 na 15 mwakani mjini Singida.
MGOGORO NDANI YA ZFA
Kamati ya Utendaji imepokea kwa masikitiko taarifa za masuala ya mpira wa miguu Zanzibar kupelekwa mahakamani.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za uendeshaji mpira wa miguu ambazo zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa katika mahakama za kawaida.
Kamati ya Utendaji inatoa rai kwa pande zote mbili zinazohusika na mgogoro huo kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao.
Kamati ya Utendaji imejitolea kutuma ujumbe wake Zanzibar ili ukutane na pande zinazohusika katika mgogoro huo.
Ni muhimu usuluhisho upatikane haraka ili tuweze kujua hatma ya washiriki wetu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Raheem Sterling atwaa tuzo akiisubiri kwa hamu Arsenal leo

http://assets.lfcimages.com/uploads/9559__1458__sterling560_512X287.jpg
Raheem Sterling akiwa na tuzo yake
http://i1.liverpoolecho.co.uk/incoming/article8287825.ece/alternates/s1023/JS52985656.jpg
Sterling akiwajibika uwanjani

WAKATI leo akitarajiwa kuiongoza klabu yake ya Liverpool watakapoikaribisha Arsenal, Raheem Sterling amefanikiwa kushinda tuzo ya Golden Boy kwa mwaka huu na kuwa Mwingereza wa kwanza kushinda tuzo hiyo toka Wayne Rooney aliposhinda mwaka 2004. Msghambuliaji huyo nyota wa Liverpool ametwaa tuzo hiyo kwa umahiri wake uliomfanya kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Liverpool huku akiwa amejihakikishia namba katika kikosi cha timu ya taifa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, amewashinda chipukizi wenzake akiwemo Adnan Januzaj wa Manchester United na Hakan Calhanoglu wa Bayer Leverkusen pamoja an wachezaji wenzake wa Liverpool Lazar Markovic na Divock Origi. 
Akihojiwa Sterling aliuambia mtandao wa Liverpool kuwa ni mafanikio makubwa kushinda tuzo kama hiyo na ni jambo la furaha kwake na familia yake. Wachezaji wengine wlaiowahi kushinda tuzo hiyo ni pamoja na Lionel Messi, Cesc Fabregas na Sergio Aguero.
Mshambuliaji huyo leo anatarajiwa kuingoza timu yake kuikaribisha Arsenal kwenye uwanja wa Anfield katika mechi ya Ligi Kuu ya England linalosubiriwa kwa hamu.
Katika mechi kama hiyo katika msimu uliopita, Raheem akisaidiana na nyota wenzake Martin Skrtel na Daniel Sturridge waliiangamiza Arsenal kwa mabao 5-1.
Raheem katika mchezo huo alifunga mabao mawili sawa na Skrtel na jingine liliwekwa kimiani na Sturridge ambaye bahati mbaya leo hatakuwepo dimbani kutokana na kuwa majeruhi.
Pia mchezaji aliyechangia ushindi huo Luis Suarez hayupo kikosini kwa vile amehamia Barcelona hali na kwa mwenendo iliyonayo timu hiyo msimu huu inaleta mashaka kama wanaweza kurudia ilichofanya msimu uliopita.

M

Real Madrid bingwa wa Dunia, Aucland City waitoa nishai Cruz Azul

Bale akilibuzu kombe la Klabu Bingwa la Dunia baada ya jana kuiwezesha Real Madird kulitwaa kwa kuinyuka San Lorenzo
Wachezaji wa Real madrir wakiwa na taji la Klabu Bingwa la Dunia
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia taji lao
Real Madrid star Cristiano Ronaldo kisses the Club World Cup trophy after their triumph
Ronaldo akilibusu taji
MABINGWA wa Ulaya, Real madrid wameliwekwa kibindoni taji la kwanza la Klabu Bingwa ya Dunia na kuwa taji la nne katika mwaka 2014 baada ya kuinyuka San Lorenzo ya Amerika Kusini kwa mabao 2-0.
Madrid iliinyoa Mabingwa hao wa Amerika Kusini katika panbano la fainali ya michuano hiyo ya Klabu Bingwa Duniani lililochezwa usiku wa jana mjini Marrakech, Morocco ikiwa ni baada ya miaka 12 tangu klabu hiyo iliposhiriki michuano hiyo.
Mabao ya beki Sergio Ramos katika dakika ya 37 na jingine na winga na mchezaji ghali duniani, Gareth Bale katika dakika ya 51 yalitosha kuwapa Real Madrid taji hilo la kwanza kwao na kuendeleza reklodi ya kucheza mechi 22 bila kupoteza msimu huu.
Katika mechi nyingine ya kusaka mshindi wa tatu wa michuano hiyo timu ya Aucland City ya New Zealand ilifanikiwa kutwaa ushindi wa tatu baada ya kuinyuka Cruz Azul ya Mexico kwa mikwaju ya penati 4-2.
Awali timu hizo zilizomaliza muda wa kawaida wa dakika 90 na ule wa nyongeza wa 120 kwa kufungana bao 1-1, Wamexico wakilazimika kusawazisha baada ya kutanguliwa na wapinzani wao ambao waliong'olewa hatua ya Nusu fainali za San LOrenzo.

Friday, December 19, 2014

Wananchi King'ongo kuandamana kupinga matokeo ya Uchaguzi

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRYGNK4P0cFIyKRqOFynOrQq3EIcCP4FHCqYF9HopGj2yWE0li5U95QShB5g6C5tyfVNd6rQZix8eewbtSTxRe5-c3My82W5tXZIy2_4U5Ugq8tTUcyyGuAgGc9nDbHRECNaAQ2qXPtLU/s1600/Waalimu.JPG
Mwenyekiti anayedaiwa kutangazwa kinyemela, Mapesi katika mija ya mikutano yake kama kiongozi wa mtaa wa King'ongo
KUFUATIWA kukerwa na kitendo cha kupokwa kwa ushindi kwa mtu waliyemchagua katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika siku ya Jumapili, wakati wa Mtaa wa King'ongo uliopo Kata ya Saranga, wilaya ya Kinondoni wamepanga kufanya maandamano sambamba na kuifunga ofisi ya Uongozi wa mtaa huyo mpaka mtu waliyemchagulia atakapopewa ushindi wake.
Wakizungumza na MICHARAZO wakazi hao wengi wakiwa na hasira, wamedai kuwa wamechukizwa na uhuni waliofanyiwa na wasimamizi wa Uchaguzi wa Mtaa wao kwa kumtangaza kinyemela aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa huo, Demetrius Mapesi wakati mshindi halali waliyemchagua akiwa ni aliyekuwa Mgombea wa UKAWA kupitia chama cha CUF, Aboubakar Nyamuguma.
Wananchi hao walisema wapo katika kujiorodhesha majina kwa ajili ya kuandaa maandamano kwenye ofisi za Manispaa ya Kinondoni kulalamikia waliouita uhuni wa wasimamizi kutumia askari wa jeshi la Polisi kuwatawanya kwa mabomu kisha kutangaza mshindi ambao aliangushwa kwa kura walizopiga.
"Walichelewesha kutangaza majina baada ya kutokea sintofahamu, walipoona tumeamua kuwakomalia wamtangaze mtu tuliyemchagua usiku wa saa 4 wakaita Polisi wakaja kutupiga mabomu kisha wakamtangaza Mapesi kuwa kashinda bila wagombea kusaini fomu wala kubandika mpaka sasa matokeo hayo ubaoni kama inavyotakiwa, huu ni nini kama sio uhuni," alihoji mmoja wa wakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la Baba Ramadhani.
Alisema pamoja na hila wanazofanya CCM za kutaka kulazimisha matokeo ili Mapesi aendelee kuwa kiongozi wa eneo lao wameapa hawatakubali na ikiwezekana wataifunga ofisi kwa makufuri mpaka Nyamuguma apewe ushindi wake kwa sababu ndiye waliyemchagua.
Mgombea anayedaiwa kuporwa ushindi, Aboubakar Nyamuguma alisema kuwa mpaka sasa hajui kitu gani kilichotokea baada ya awali kukubaliana na msimamizi kuziondoa kura zilizoonekana zimeongezeka kuliko idadi ya waliojiandikisha na kupiga kura.
"Ilionekana kura 32 zilizidi zaidi ya waliojiandikisha na kupiga kura ambao walikuwa 930, baadaye tukakubaliana zilizozidi ziondolewe kama taratibu zinavyotaka kisha zihesabiwe zinazopaswa na matokeo yalionyesha nimepata kura 461 dhidi ya 431 za mpinzani wangu," alisema.
"Cha ajabu baada ya kuona nimembwaga Mapesi Msimamizi na wasaidizi wake ambao wengi ni walimu wanaofundisha Shule ya King'ongo ambayo mpinzani wangu ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule waligoma kutangaza matokeo na kusababisha wananchi kucharuka kabla ya kuita Polisi na kuwapiga watu mabomu na kuwatawanya na kumtangaza Mapesi kuwa mshindi kwa kumpa kura 32 zilizoondolewa na hivyo kumfanya afikishe kura 463 dhidi ya zangu," alisema Nyamuguma.
Alisema kitu cha ajabu msimamizi alitangaza matokeo bila hata wagombea kusaini fomu kama inavyotakiwa na pia kutobandikwa ubaoni na kutokomea zake.
Aliongeza kuwa kwa kutambua kuwa amepokwa haki yake ameandika barua ya pingamizi dhidi ya kitendo hicho kwa Mratibu wa Uchaguzi Mkuu Kinondoni na nakala kutuma katika ofisi zote zinazohusika ikiwamo kwa viongozi wake wa UKAWA kuhakikisha haki inapatikana.
Alipoulizwa kama ni kweli wapo watu wanaotaka kufanya maandamano alisema, hana taarifa ila kama ni kweli ni uthibitisho kuwa wananchi hata wenyewe wanasbabu ya kufanya hivyo kwani walimchagua ili awaongoze baada ya kutoridhishwa na uongozi wa kiongozi aliyekuwapo awali.
Mapesi mwenyewe hakuweza kupatikana kueleza juu ya mtarafuku huo na anaelezaje wananchi wanavyotaka kufanya maandamano kumpinga kuonyesha hakubaliki katika mtaa huo, ila MICHARAZO inaendelea na juhudi hizo.

Neymar amwagiwa sifa lukuki na Carlos

http://img.crunchsports.com/crunchsports/NewsImages/160422581.jpg
Neymar
http://img01.mundodeportivo.com/2013/03/08/Roberto-Carlos-Neymar-tiene-un_54368194317_54115221213_490_300.jpg
Roberto Carlos (kushoto) akifurahia jambo na Neymar (kati) na Ronaldo de Lima
MSHAMBULIAJI nyota wa Brazil anayekipiga Barcelona, Neymar amemwagiwa sifa akidai kuwa kiwango chake kinachuana na nyota wengine wa dunia, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Beki wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Roberto Carlos ndiye aliyemmwagia misifa nahodha huyo wa sasa wa Brazil akisisitiza kuwa sasa anashindana na Lionel Messi na Ronaldo akiwa kama mchezaji bora duniani. Neymar,22 alipewa unahodha wa timu ya taifa ya Brazil na kocha mpya Dunga ambapo tayari ameshaingoza timu hiyo kushinda mechi sita mfululizo toka baada ya Kombe la Dunia huku akifunga mabao saba. 
Neymar alikuwa mchezaji pekee wa Brazil kuwepo katika orodha ya wachezaji 23 waliotajwa kugombea tuzo ya Ballon d’Or na Carlos anaamini mshambuliaji huyo wa Barcelona ni mchezaji bora wa tatu kumuona msimu huu. 
Carlos amesema Neymar ni mchezaji wa aina yake kwani amezoea soka la Ulaya haraka tatizo kubwa ni kwamba Messi na Ronaldo wanaimarika kila siku hivyo kila Neymar akijaribu kuwakaribia wanamuacha tena.

FIFA yakubali kuchapisha taarifa ya rushwa hadharani

http://www.playlouisianasoccer.org/assets/946/15/FIFA%20Logo.jpg 
MAOFISA wakuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA wamekubaliana kutoa ripoti yote kuhusu uchunguzi wa madai ya ufisadi uliotokea wakati wa kutolewa kwa uenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 na Qatar mwaka 2022.
Maofisa hao wamekubali kutoa kurasa 430 za uchunguzi wa Michael Garcia baada ya kufanya mkutano kufuatia pendekezo la rais wa FIFA Sepp Blatter.
Hatua hiyo ya kuichapisha ripoti hiyo inaonyesha mabadiliko ya sera baada ya FIFA kukataa shinikizo kutoka kwa Garcia mwenyewe na wengine kutoa ripoti hiyo. 
Garcia alijiuzulu siku ya Jumatano baada ya ombi lake la kupinga ripoti fupi ya uchunguzi wake iliotolewa na mwenyekiti wa kamati ya maadili katika shirikisho hilo Hans-Joachim Eckert kukataliwa.

Huyu ndiye Katibu Mkuu wa Yanga

https://24tanzania.com/wp-content/uploads/2013/06/a753Jerry-Muro.jpg
Jerry Muro Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga
KLABU ya Yanga imetangaza watendaji wake wapya wa kuajiriwa na kuweka hadharani taarifa za kumtema rasmi kocha Marcio Maximo na msaidizi wake Leornado Nieva.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, klabu yao imemuajiri Dk Daktari Jonas Tiboroha kuwa Katibu Mkuu kuchukua nafasi ya Beno Njovu.

Njovu ameondoka Yanga baada ya mkataba wake kwisha na amekuwa akiendelea na shughuli zake mbalimbali kwa kuwa alihitaji muda zaidi.
Mbali na DK Tiboroha ambaye ni mhadhiri katika vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya Tanzania, aliyewahi  kufanya kazi Norway na Sweden, pia wengine waliolamba shavu Jangwani ni Muro mwenyewe aliyekuwa mtangazaji wa zamani wa ITV na TBC.
Wengine ni Omar Kaya anayekuwa Mkuu wa Idara ya Masoko , Frank Chacha-Idara ya Sheria na Baraka Deusdedit anayekuwa Mkuu wa Idara ya Fedha.
Pia imefahamika wazi kuwa kocha Maximo na msaidizi wake wametimuliwa klabu hapo na nafasi zao kushikwa na 'Babu' Hans van der Pluijm na Charles Boniface Mkwasa 'Master'.
Makocha hao awali waliwahi kuinoa Yanga kwa nusu msimu uliopita kabla ya kupata kazi Umangani na kutimkia huko na sasa wanarudi kuendeleza libeneke.

Breaking News! Ikulu yakana Rais Kikwete kulihutubia taifa leo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPAd2mufOSWsRJT4w_lKEdDQCc1IMqTtswgJ123OH67pmpaEbvH90ACdbz_jNqCAh11YC_eof9AM6zPZoZgsExCqU_ZVKJgruZgtjgQH4OmVApzg_PkjzbOI4bNY_a3RfrKVq4BwgdyKE/s1600/RAIS+KIKWETE+1.JPG
Rais Jakaya Kikwete atakayelihutubia taifa siku ya Jumatatu na siyo leo kama ilivyodokezwa awali na vyombo vya habari
WAKATI masikio ya watanzania yakiwa yamejiandaa kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba huenda angelihutubia taifa leo na kufichua mambo mbalimbali yaliyolighubika taifa, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imekanusha taarifa hizo.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo MICHARAZO imezipata muda mfupi uliopita zinasema kuwa kilichokuwa kimeandikwa kwenye  mitandao ya kijamii na katika gazetini kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete siyo kweli.
Kurugenzi hiyo ya Mawasiliano imesema kuwa ukweli wa taarifa ni kwamba Rais atalihutubia taifa siku ya Jumatatu, Desemba 22 mwaka huu muda utakaopangwa.
Watanzania wana hamu kubwa ya kusikia kauli ya Rais kutokana na Sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow pamoja na vurugu zilizofanywa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika Jumapili na kushuhudia madudu yaliyosababisha wakurugenzi 17 wa Halmashauri na miji kukubwa na 'rungu' toka kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia.

News Alert! Wanusurika kufa baada ya lori kuvamia nyumba yao

 
WATU zaidi ya 8 wamenusurika kifo wakati wakiwa wamelala nyumbani mwao  mtaa wa Heri manispaa ya Tabora, baada ya gari la mizigo aina ISUZU kuparamia nyumba yao, lilipomshinda dereva alipokuwa akikata kona, ambapo mama mjamzito aliyenusurika amekimbizwa hospitalini akiwa na hali mbaya kutokan a na mshituko na hali yake ya ujauzito.

Mashuhuda wa ajali hiyo walioharibiwa thamani zao mbali mbali wamesema kuwa, umefika wakati serikali kubadili adhabu za madreva wazembe ambao wanaendesha vyombo vya usafiri bila kuzingatia sheria zilizowekwa na serikali huku wakipoteza maisha ya wananchi na mali zao.
 
 Akizungumza juu ya ajali hiyo na kubaini uzembe wa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili t 396 AGS, ambaye hakupatikana mara moja, kamanda wa polisi mkoani tabora kamishina msaidizi Suzani Kaganda aliyefika eneo la ajali hiyo amesema kuwa, mwendesha gari hilo atatafutwa na hatua  stahiki zitachukuliwa dhidi yake.
 
Aidha mmiliki wa nyumba hiyo bw.Ramadhani Musa Kaswezi, anayeishi kijijini ilolangulu hakusema lolote akidai kikao cha familia kitatoa maamuzi ili  kuelezea hatua atakazochukua kutokana na wapangaji wake wawili kubolewa nyumba.

Karatu Marathoni kufanyika kesho, Rais wa RT mgeni rasmi

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgK66HOqLkGYeaTGTYAgjwfe_JwlnAJFPRjjPltK_Ny_Q6cU__cyttsAmd-UlL1HIV_pf_tNsOVei2FQkPNRBXmCi1k75PdHfuV57QV3Typ-RbwjqvZnzSGrhBEUXZ0BrqBBIi5Ry0AzNo/s1600/NGOR+10a.jpg
Kesho Mambo yatakuwa kama haya kwa wanaridha mbalimbali kuchuana Karatu Marathon
RAIS wa Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka leo Jumamosi atakuwa mgeni rasmi katika mbio za 13 za kilometa 10 za Karatu zitakazofanyika mjini Karatu.
Mratibu wa tamasha hilo ambalo mbali na riadha, ambao ndio mchezo mkuu, michezo mingine inayoshindaniwa ni pamoja na soka, mpira wa wavu na mbio za baiskeli, Meta Petro alisema kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa na msisimko wa aina yake.
Akizungumzia mbio za kilometa 10 na zile za kilometa tano na 2.5 kwa wanaume, wanawake na watoto, Petro alisema kuwa mwaka huu msisimko ni mkubwa sana kwa washiriki na ushindani utakuwa wa aina yake.
Alisema tayari zaidi ya  wanariadha 200 hadi juzi walikuwa wamejiandikisha kushiriki mbio hizo za wanaume na wanawake, huku watoto wa shule wenyewe wakitarajia kujisajili mapema leo asubuhi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mbio hizo.
Alisema kuwa mbio za baiskeli zitakuwa za kilometa 60 kwa wanawake na wanaume huku, fainali za soka na mpira wa wavu zilitarajiwa kufanyika jana na washindi wake kuzawadiwa leo na mgeni rasmi, ambapo zawadi za fedha taslimu, jezi na mipira hutolewa kwa washindi.
Meta alisema kuwa mingoni mwa wanariadha nyota waliothibitisha kushiriki mbio hizo ni bingwa wa Uhuru Marathoni Fabiano Joseph aliyeng’atwa kidole gumba na mshiriki mwenzake baada ya kumaliza mbio hizo.
Alizitaja klabu za riadha zitakazoshiriki mbio hizo ni pamoja na Magereza, Jambo, Winning Spirit, Arusha Sports Training Centre (ASTC), Ambassador, Hakika na Polisi Kilimanjaro.
Wakati klabu zingine ni pamoja na Magereza na Mukojope zote za Zanzibar, CCP Moshi, TPC Moshi, Guwangw ya Mbulu na Manyara Athletics Club ya Babati.
Meta aliongeza kuwa pia watakuwepo wanariadha wengi  binafsi kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha, Singida na kwingineko.
Mbio za Karatu zimekuwa zikiandaliwa na Filber Bayi foundation (FBF) na kudhamiwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kupitia Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC).

Hawa ndiyo walioingia na kutoka katika dirisha dogo la usajili Bara

http://darcitycenter.com/wp-content/uploads/2014/12/IMG_0173.jpg
Kpeh Sean Sherman aliyetua Yanga
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/11/54.png
Pascal Wawa aliyetua Azam

http://static.goal.com/227600/227665_heroa.jpg
Dan Sserunkuma aliyetua Simba
http://api.ning.com/files/xMCtlOLhuRdvIKJ4IqlKQo5swrvUDSiogHOrPOVEYWIequGvkbAoW7Wk7MyessH-3CcKu48nulnsNIcpKw9FPSciLbck8jnD/SIMBANAYANGA4.jpg
Tambwe katemwa Simba na kuibukia Yanga
DIRISHA Dogo la Usajili nchini Tanzania, lilifungwa rasmi siku ya Jumatatu baada ya pilikapilika ya klabu za soka kupigana vikumbo kuingia hapa na kutoka kule kusaka wachezaji wa kuimarisha vikosi vyao.
Kwa sasa mashabiki wanasubiri kusikia nani na nani waliopitishwa katika klabu zao, baada ya majina kuwasilishwa kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania, TFF.
Katika heka heka hizo za usajili kuna mambo ya kushangaza yaliyojitokeza ikiwamo kwa aliyekuwa Mchezaji Bora wa mwezi (Septemba), Antony Matogolo, kiungo mkali wa Mbeya City kupelekwa kwa mkopo katika timu ya Daraja la Kwanza ya Panone ya Kilimanjaro ili tu kuongeza kiwango chake, huku Deo Julius alivunjia mkataba baada ya dirisha la usajili kufungwa.
Kama hiyo haitoshi, Mbeya City pia iliamua kumtoa Mfungaji Bora wa FDL 2012/13 Saad Kipanga waliyemsajili katika dirisha dogo la msimu uliopita kutoka Rhino Rangers kwend kukuza kiwango chake Polisi Tabora ya Daraja la Kwanza. Kipanga aliyeifungia mabao 12 katika mechi 14 Rhino na kuipandisha Ligi Kuu, alikuwa akiwaniwa kwa udi na uvumba na Simba SC msimu huu lakini dili lake lilikwama.
Cha kushangaza kingine ni Yanga kumtema mkali wao wa mabao Hamis Kiiza 'Diego' na kumsajili mchezaji toka Liberia ambaye hakuna mwenye hakika kama ataibeba timu hiyo kama ilivyokuwa kwa Mganda huyo, huku watani zao wakitoa kali ya mwaka kwa kumtema Mfungaji Bora wa msimu uliopita, Mrundi Amissi Tambwe.
MICHARAZO inakudondolea baadhi ya walioingia na kutoka katika dirisha hilo dogo la usajili kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, pia majina ya walioombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) baada ya dirisha dogo la usajili msimu wa 2014/2015 kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF kama alivyoweka bayana Mkurugenzi wa Mashindano wa shirikisho hilo, Boniface Wambura.
Wambura alidokeza kuwa wachezaji 15 kutoka nje wameombewa ITC kutoka nchi mbalimbali na kufafanua kuwa, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF itakutana muda wowote kupitia usajili wa dirisha dogo ili kuweka mambo hadharani nani karuhusiwa kucheza wapi kutoka wapi na yupi amekwama.
Walioombwewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam FC, Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara, Charles Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu Michael Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.
Dan Sserunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil) kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na Juuko Murshid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba.
Kpah Sean Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB (Kenya) kwenda Polisi Morogoro, Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Serge Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Sserunkuma kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.
Orodha kamili ya waliosajiliwa katika dirisha dogo lipo kama ifuatavyo;

AZAM;
Walioingia: Serge Pascal Wawa, Bryan Majwega na Amri Kiemba.
Waliotoka: Ismail Diara raia wa Mali (katemwa) na Mhaiti Lionel Saint-Preux (katemwa).

COASTAL UNION;
Walioingia: Humud na Geofrey Wambura (huru), Bakari Thabit (Friends Rangers).
Walioondoka: Razak Khalfan (mkopo Mwadui FC), Peter Heri (katemwa).

JKT RUVU: hakuna aliyeingia waka kutoka safari hii.

KAGERA SUGAR; hakuna aliyeingia wala kutoka.

MBEYA CITY;
Walioingia: Kalyesubula Hannington (huru), Juma Issa ‘Nyoso’ (huru), Idrisa Rashid, Fredy Cosmas, Soneka Peter (U20) na Selemani Hassan (U20).
Walioondoka: Anthony Matogolo (mkopo Panone FC), Saad Kipanga (mkopo Polisi Tabora), Ramadhani Abdu (mkopo Majimaji FC), Medson Mwakatundu – U20 (mkopo Rhino Rangers), Ramadhani Kapela – U20 (mkopo Coca Cola Mbeya), Majid Shabani – U20 (mkopo Coca-Cola Mbeya), Abdalah Said – U20 (mkopo Coca-Cola Mbeya) na Waziri Ramadhani – U20 (mkopo Burkinafaso FC) na Deo Julius (Aliyesitishiwa mkataba).

MGAMBO JKT; hakuna aliyeingia wala kutoka.

MTIBWA SUGAR;

Walioingia: Henry Joseph (huru) na Miraj (mkopo Simba) na Ibrahim Jeba (huru).
Walioondoka: Hassan Kessy (Simba).

NDANDA;
Walioingia: Omega (Yanga), Kiggi Makasi (huru), Stamili Mbonde (Villa Squad), Raymond Zabron (Villa Squad), Issa Said (huru), Mohamed Masoud 'Chile' (huru) na Zuberi Ubwa (huru).
Walioondoka: Amri Msumi (mkopo Kurugenzi Iringa) na Hamis Saleh (huru).

POLISI MORO;
Walioingia: Said Bahanunzi (Yanga), Zahoro Pazi (huru), Meshack Abel (KCB, Kenya) na Iman Mapunda (huru). Walioondoka: Danny Mrwanda (Simba), Makungu Siame (mkopo Malindi, Unguja), Emilian Mgeta (mkopo Villa Squad) na Mosses Mtitu (Majimaji FC).

PRISONS-MBEYA; hakuna aliyeingia wala kutoka.

RUVU SHOOTING;
Walioingia: Mwita Kimaronge (Toto Africans), Betram Mwombeki (huru), Yahya Tumbo (Mtendeni FC, Zanzibar) na Ally Yusuph (Ruvu Shooting B).

STAND UNITED;

Walioingia: Hamis Thabit (Yanga), Chanongo (Simba), Nduwimana (Burundi), Shaban Kondo, Chinedu, Hamis Shengo na Misheto (Ujerumani).
Walioondoka: Nelson Kimath na Omar Mtaki (wote Geita FC), Hussein Chepe na Lucas Charles (wote Polisi Tabora), Robert Magadula na Patrick Mrope (wamevunja mikataba).

SIMBA;
Walioingia: Dan Sserunkuma, Simon Sserunkuma, Murshid na Hassan Kessy (Mtibwa Sugar).
Walioondoka: Kiemba (Azam), Miraj Adam (mkopo Mtibwa Sugar), Haroun Chanongo (mkopo Stand United), Joram Mgeveke (mkopo Mwadui FC) na Uhuru Seleman (Mwadui FC – Uhuru kavunja mkataba Simba).

YANGA;
Walioingia: Sherman, Amissi Tambwe, Danny Mrwanda, Athuman Majogo (Friends Rangers) na Emerson (amesajiliwa na kutemwa).
Walioondoka: Hamis Kiiza (katemwa), Omega Seme (mkopo Ndanda FC), Hamis Thabit (mkopo Stand United), Geilson Santos Santana ‘Jaja’ (ametemwa) na Said Bahanunzi (mkopo Polisi Morogoro).

Diamond nouma! Alipa nusu mshahara wa Boban ili akipigie Friends

Diamond Platnumz aliyejitolea kulipa mshahara wa Boban katika klabu ya Friends Rangers
Boban anayemtia wazimu Diamond kwa umahiri wake uwanjani
MSHINDI wa tuzo saba za Kili Music-2014 na tatu za CHAOMVA-2014, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ameonyesha namna gani yeye ni mtu wa kujichanganya ndani ya jamii baada ya kudaiwa kukubali kulipa nusu ya mshahara anaolipwa kiungo mshambuliaji anayemhusudu, Haruna Moshi 'Boban' aliyetua Friends Rangers.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu hiyo ni kwamba Diamond amekubali kutoa fedha hizo ili tu Boban mchezaji anayemzimia kupita maelezo akipige timu hiyo iliyopo Ligi Daraja la Kwanza na ambayo ipo katika nafasi nzuri katika kinmyang'anyiro cha kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015-2016.
"Diamond amekubali kulipa nusu ya mshahara wa Boban, na mwingine katoka theluthi ya mshahara huyo na kilichobaki kitalipwa na uongozi wa klabu ya Friends ambayo inapiga kupanda Ligi kuu," mtoa habari huyo aliidokeza MICHARAZO.
Kiwango cha mshahara cha mchezaji huyo ndani ya klabu hiyo
MICHARAZO inayo, ila kwa kuwa ni suala la mtu binafsi imeamua kuuweka kapuni, na kiwango atakapochotoa Diamond pia inafahamu na kile kingine cha mdau wa klabu hiyo ni Sh. 300,000 na huku uongozi ukiwa na jukumu jepesi la kumaliza mzigo kamili.
Nyota huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars aliyekuwa hana timu tangu alipoachwa na Coastal Union mwsihoni mwa msimu uliopita amejiunga na timu hiyo sambamba na wakali wengine kama Amir Maftaha kuonyesha namna gani klabu hiyo imepania kucheza ligi kuu msimu ujao.


438,960 wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wasome hapa!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsA3WpuEiX5vgwlBeYwyweMxrRst1WhE1EBR9om6MzVWSAtwVet0MqxiJ2KITd92xBvuKloWWP9h5wMJ_7v8SNjmR5yKyRM-8oxfPUsROsLNefXsdD0WMm5onXGNHnWxKRsqP406tMVF4c/s1600/c3.jpg
Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Kassim Majaliwa.
JUMLA ya wanafunzi 438,960 kati ya 451,392 ya waliofanya mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza.
Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe. Kassim Majaliwa  ametoa taarifa ya serikali kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015.
Akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa ofisi za  TAMISEMI, jijini Dar, Majaliwa alisema;

“Wanafunzi 438, 960 kati ya 451,392 waliofaulu mtihani wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika  shule za serikali katika awamu ya kwanza.”
Akaongeza: “Idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliofaulu mtihani na kwa matokeo hayo yanayonesha kuwa na alama ya juu kabisa kwa wavulana ilikuwa 243 na kwa wasichana 240 kati ya alama 250.”
Aidha, naibu huyo amewaagiza wazazi, walezi, wadau wa elimu na halmashauri zote kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2015.

Shilole ana Malele, akipika filamu mpya

http://vibe.co.tz/wp-content/uploads/2014/09/shilole.jpgMUIMBAJI nyota nchini aliye pia muigizaji filamu, Zuwena Mohamed 'Shilole' ameachia kazi yake mpya iitwayo 'Malele' wakati akijiandaa kutengeneza filamu iitwayo 'Shilole In Dar'.
Shilole  a.k.a Shishii Beibii' aliyekuwa akisumbua na 'ngoma' yake iitwayo 'Namchukua' ameiachia kazi hiyo mpya majuzi na tayari imeanza kusumbua hewani.
Msanii huyo alidokeza kuwa wimbo huo ameandikiwa na mkali kutoka Nyumba ya Vipaji (THT) Barnaba Boy na umetengenezwa katika studio za mtayarishaji Nahreel.
"Baada ya kutamba na nyimbo kadhaa nyuma, safari hii nakuja na Malele, pia nilitaka kuwadokeza mashabiki wangu pamoja na kuwa kimya katika masuala ya filamu, lakini kuna kazi natarajia kuanza kuirekodi itafahamika kama 'Shilole In Dar'," alisema Shilole.
Shilole alisema filamu hiyo itarekodiwa Igunga mjini Tabora na jijini Dar es Salaam ikirejea simulizi juu maisha yake kutoka kwao Tabora mpaka kuja kutikisa jijini Dar.
Msanii huyo ni mmoja ya waimbaji wa kike wanaofanya vizuri nchini baada ya kufaishwa na nyimbo kama 'Lawama', 'Dume Dada', 'Paka wa Baa', 'Chuna Buzi', 'Nakomaa na Jiji' na 'Namchukua'.

Zola D King sasa kuja na kipindi cha runinga

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7q5SJ6OOxchU55rwY3vDndEaHcOnbUOFr39NqBXqkID26wQDFrz9-ALJq1nF84wlrE7ikUfF8CBUSSztJ9iU-jbHvzB2MaIa1ewh5SeXh2jnVFik3CQJSYaNPJEz7e2kT2MH0n6wenu8/s1600/Zola+D2.JPG
Zola D King katika pozi

Zola D KIng baada ya kupiga tizi
MWANAHIPHOP  David Michael 'Zola D King' anajiandaa kurusha kipindi maalum cha mazoezi kitakachokuwa kikirushwa na kituo kimoja cha runinga nchini, kikiwa na lengo la kutaka kuwahamaisha watu kufanya mazoezi hata bila kwenda kwenye vituo vya mazoezi (gym).
Akizungumza na MICHARAZO, Zola D aliyeachia wimbo wake mpya wa 'I Don't Care' alisema kipindi hicho kwa matangazo ya awali tayari kimeshatengenezwa na kitakuwa kikirekodiwa kila siku ili kuwapa watazamaji mbinu mpya za kujenga mwili na kuuweka vema kiafya bila kupiga nondo (kunyanyua chuma).
"Katika harakati za kuisaidia jamii kujenga utamaduni wa kupenda kufanya mazoezi kwa afya zao, Zola D kupitia kampuni yake ya Under Films inatarajia kuanza kurusha hewani kipindi maalum cha mazoezi, hiki ni tofauti na vile vilivyozoeleka," alisema.
Alisema kipindi hicho kitawarahisishia watazamaji na watu wengine wanaopenda kufanya mazoezi kujifanyia kokote walipo bila kusubiri kwenda 'gym' au maeneo maalum la kufanyia mazoezi na kwa gharama rahisi.
"Nadhani kabla ya mwisho wa mwezi huu kitaanza kuruka hewani," alisema mkali huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kama 'Moto wa Tipper', 'Jana Sio Leo' na 'Msela Sana'.

Rais Aveva kuteta Dar leo, 'mnyama' kurejea tena Zenji

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhQw0Q6Z99EoVWkyx9Yf4-SQu6v6ms0PaPb_sKenOOroi-QKbRnmecjHWsCkMjBGp9Gme9kVSLBI6loRiDVMNpxjyOidGhsx9k3uN8L4NzFcmC9SUT8cQrLUnJwL2a4pbDoK4TypzmK_ig/s1600/_HMB7014.JPG
Kikosi cha Simba a.k.a Mnyama
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhoLvuP581ivo5DmoJ7-fjAO0L4lb832uSRgANZSCM9_mFYRFWzQmWqVniwANO2gdM-86rgwsOYXQxAvV5u5_m6fMTYiqOws2QA1aEx564aOTK2BSbxy44UouXVynVHdAKqwBMwyFVc2ho/s1600/1.jpg
Rais wa Simba, Evance Aveva anayetatarajiwa kuzungumza na wanahabari leo
Wachezaji Simba wakishangilia ushindi wao dhidi ya Yanga katika Nani Mtani Jembe
RAIS wa klabu ya Simba, Evans Aveva leo anatarajuiwa kukutana na waandishi wa habari jijini ili kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu klabu hiyo ya Msimbazi.
Aveva anayetoka Kundi la Matajiri wa Simba (FoS), aliahidi kuzungumza na waandishi wa habari kwa kina juu ya suala linalotajwa la Simba Ukawa wanaohusishwa na matokeoa mabaya ya timu hiyo iliyoifunga Yanga SC Jumamosi.
Hamphrey Nyasio, Msemaji wa Simba SC, amesema Aveva atavunja ukimya juu ya Simba Ukawa na masuala mengine mengi yanayoihusu klabu hiyo.
Simba imekuwa na mwanzo mbaya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu ikitoka sare katika michezo sita ya awali kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi yao ya raundi ya saba.
Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Simba SC, Aveva alikuwa na sera ya vidole vitatu kila mkono akimaanisha kila mechi pointi tatu na magoli matatu lakini sera hiyo inaonekana kufeli katika mechi zote zilizopita tangu aingie madarakani kwani Simba haijawahi kuonja ushindi huo
katika hatua nyingine baada ya kuacha kilio Jangwani, kikosi cha Simba kinaingia kambini jijini Dar es Salaam leo kabla ya keshokutwa kwenda Zanzibar kujiandaa kwa mechi ya ufunguzi wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar.
Simba, iliyoichapa Yanga mabao 2-0 katika mechi ya 'NanI Mtani Jembe 2' iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Jumamosi na kumfukuzisha kazi kocha Mbrazil Márcio Máximo, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya kikosi cha Kagera Sugar katika mechi ya raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Desemba 26.
Kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri alisema jijini kuwa kikosi chake kinaingia kambini leo kwenye Hoteli ya Ndege Beach kabla na baadaye Jumapili kitarejea visiwani Zanzibar kuandaa dozi kwa ajili ya kukiua kikosi cha kocha Mganda Jackson Mayanja cha Kagera Sugar kilichoifunga Yanga bao 1-0 katika mechi ya raundi ya sita ya VPL msimu huu.
Simba iko nafasi ya saba katika msimamo wa VPL ikiwa na pointi tisa, moja nyuma ya Kagera Sugar wanaokamata nafasi ya tano.

Mtanzania aliyeua kikatili watoto wake Australia lamkuta


Mtanzania Albert Mihayo aliyehukumiwa kifungo cha maisha kwa kuwauwa watoto wake wawili kikatili
Mama wa watoto na mke wa zamani wa Mihayo
Watoto waliouwawa kikatili na baba yao, Indianna na Savannah enzi za uhai wao
 MTANZANIA anayeishi nchini Austaralia, Charles Mihayo ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kuwaua kikatili watoto wake mwnyewe ili kumkomoa mkewe aliyekuwa ameachana naye amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Mihayo mwenye miaka 36, alifanya ukatili huo kwa wanae Savannah (4) na Indianna (3) Aprili 20, 2014 nyumbani kwake huko Melbourne na amehukumiwa leo kifungo hicho.
Inadaiwa kuwa baada ya kuachwa na mke wake, hasira zilimfanya bwana Mihayo kuamua kufanya ukatili wa kukatisha uhai wa watoto wake mwenyewe Savannah (4) na Indianna (3), ili tu kumuumiza mke wake kama njia ya kumlipizia kisasi. Inadaiwa kuwa aliwauwa kwa kuwakandamiza na mto baada ya kucheza nao.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa siku mauaji hayo yalipofanyika, mama wa watoto hao aliwapeleka kwa baba yao bwana Mihayo. Baada ya kuwafikisha baba yao aliwafanyia shopping ya nguo na viatu vipya.
Kabla ya kutenda ukatili huo kwa damu yake mwenyewe, Mihayo aliwarekodi video wakicheza muziki huku akicheza nao. Na katika video ambayo polisi baadae waliiona, alisikika akiwaambia binti zake wamuoneshe mama yao nguo mpya alizowanunulia, na walifanya hivyo na kisha mwanaume huyo akakaa mbele ya camera na kusema “tutamuonesha mama kitu kingine dakika kumi zijazo”, na kuendelea kucheza nao hadi alipowakandamiza na mto (pillow) hadi kufa.
Baada ya kufanya mauaji Mihayo mwenyewe aliwapigia simu polisi ambao baada ya kufika nyumbani kwake wakiwa mlangoni aliwaambia , “Tayari, nimewaua. Nimewaua watoto wangu. Inabidi mumuulize huyu [mama yao] sababu.”
Polisi waliwakuta watoto hao wakiwa tayari wamefariki huku wakiwa wamevalishwa nguo na viatu vipya ambavyo walinunuliwa na baba yao siku hiyo.
Licha ya kuhukumiwa kifungu cha maisha, Charles Mihayo anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 31 kabla ya kupata haki ya kupewa msamaha.

Tanzania yapaa FIFA, Rwanda yaibwaga Uganda

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjUHpNy81p7tcuxaJLyJCA9ZibNm3tAoA6pY781As8t680d4_sWd7w0iWXTLjwsDUtWBnixs1raBOVO_m8uhh6oLry-_osjtD8R_mM7zj9kaDURYoEBpPI8lIrAkIVvJtFGnjiSWRYtKkQ/s400/IMG_2184.jpgNCHI ya Tanzania imepanda kwa nafasi saba kwenye viwango vya Shirikisho la Soka duniani, FIFA, vilivyotangazwa huku Rwanda ikiwa nchi iliyopanda kwa nafasi nyingi zaidi mwezi huu ikiibwaga Uganda waliokuwa wakiongoza katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa muda mrefu iliyoporomoka.
Katika Ukanda wa Cecafa, Rwanda ndiyo inayoongoza kutokana na kupanda kwa nafasi 22 hivyo kushika nafasi ya 68 Fifa wakati Tanzania ikishika nafasi ya 105 kwa sasa.
Uganda inashika nafasi ya pili Cecafa baada ya kupanda kwa nafasi mbili huku kwa upande wa Fifa ikiwa ni ya 76, wakati Sudan ni ya 110, Kenya (111), Ethiopia (116), Burundi (116), Sudan Kusini (189), Eritrea (202), Somalia (1204) na Djibouti ni ya 206.
Algeria ndiyo inayoongoza katika 10 bora kwa upande wa Afrika huku kidunia ikishika nafasi ya 18, ikifuatiwa na Tunisia ambayo ni 22, Ivory Coast (28), Senegal (35), Ghana (37), Guinea (39), Cape Verde (40), Cameroon (42), Nigeria (43) na Zambia ikiwa ya 46.
Hakuna mabadiliko yoyote kwa timu zilizoingia 10 bora ya viwango hivyo kidunia kwani ni zile zile za mwezi uliopita zikiongozwa na Ujerumani ambayo ilitwaa Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu.
Nafasi ya pili inashikwa na Argentina ikifuatiwa na Colombia, Ubelgiji, Uholanzi, Brazil, Ureno, Ufaransa, Hispania na Uruguay.
Italia ipo nafasi ya 11 ikifuatiwa na Switzerland     wakati England ambayo Ligi Kuu yake ina wapenzi wengi barani Afrika, ikishika nafasi ya 13 katika viwango hivyo ambavyo hutolewa kila mwezi.