STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 3, 2010

Phiri awatuliza Simba, atua na kuomba radhi * Aahidi ushindi Agosti 14



KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Phiri, alirejea nchini jana mchana kwa ajili ya kuendelea na kibarua chake cha kuwafundisha mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Bara na akawaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kwa kuchelewa kujiunga na timu.
Akizungumza mara baada ya kuwasili, Phiri alisema kuwa matatizo ya kifamilia yaliyokuwa yanamkabili ndio yalifanya achelewe kuripoti kambini na anaahidi kwamba hatarajii jambo hilo tena.
Phiri alisema kuwa haikuwa rahisi kwa yeye kuondoka na kuiacha familia yake bila ya kutatua matatizo aliyokuwa nayo (hakuyaweka wazi) na kwamba kwa muda wote alikuwa akiwafahamisha viongozi wa Simba kuhusu maendeleo yake.
"Najua kwamba nimechelewa, nawaomba mnisamehe, nitatumia muda uliobakia kuinoa timu ili ifanye vizuri katika Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa mapema mwakani," alisema kocha huyo ambaye alilakiwa na baadhi ya wanachama kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema kuwa pamoja na kuchelewa lakini pambano dhidi ya watani zao, anaamini watashinda kwa vile timu yao ni nzuri kuliko watani zao.
Simba na Yanga zinatarajiwa kupepetana kwenye pambano la Ngao za Hisani kuzindua msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mechi itakayochezwa Agosti 14.
Phiri aliondoka jijini Dar es Salaam na kuelekea Zanzibar kuungana na timu ambayo imeweka kambi tangu wiki iliyopita ikiwa chini ya makocha Syllersaid Mziray, Suleiman Matola na Amri Said.
Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Godfrey Nyange 'Kaburu' aliliambia gazeti hili kwamba mkataba wa kocha huyo umebakiza miezi michache na baada ya kumalizika uongozi utafanya upya mazungumzo naye kabla ya kuongeza mkataba mwingine.
Simba iliyopangwa kuanza ligi kwa kucheza na African Lyon, itacheza mechi ya kirafiki na Express ya Uganda Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru.

Chuji, Kaseja warejeshwa Stars





KIPA mahiri wa klabu ya soka ya Simba na kiungo nyota wa Yanga ambao waliondolewa kwenye timu ya taifa na Mbrazil, Marcio Maximo, wamerejeshwa kikosini humo na kocha mpya wa timu hiyo, Mdenmark, Jan Poulsen.
Akizungumza katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu alipowasili nchini Jumamosi usiku kwa ajili ya kurithi mikoba ya kocha Mbrazili Marcio Maximo aliyemaliza muda wake, Poulsen, alisema kuwa alipata taarifa za wachezaji hao na wengine waliowahi kuichezea timu hiyo, lakini ameamua kuwarejesha wawili hao ili kuwapa nafasi ya pili.
"Nimewapa nafasi ya pili ya kuonyesha vipaji vyao, hata kwangu pia, nidhamu ni sehemu ya vigezo vya wachezaji ninaowahitaji, kama watashindwa kuendana na sera zangu nitawaondoa, Boban (Haruna) sijamwita kwa sababu kwa sasa hana timu anayoichezea," alisema kocha huyo.
Mdenmark huyo alisema kwavile yeye ni mgeni na hawafawahamu wachezaji, alianza na wachezaji wa kikosi kilichocheza na timu ya taifa ya Brazili katika mechi ya kirafiki kwa kujua kwamba lazima ndio watakaokuwa wachezaji bora zaidi, kisha akaomba pia majina ya wachezaji wa vikosi vya nyuma na akaulizia kiwango cha kila mmoja hivi sasa na ndipo alipowabaini Kaseja, Chuji na Boban na wengineo.
Alisema wachezaji ambao walikuwepo katika kikosi kilichocheza na Brazil lakini hajawaita, imekuwa hivyo kutokana na kushuka kwa viwango vyao lakini endapo watarejesha viwango vyao atawaita tena huku akianza pia kuangalia vipaji vipya.
Alisema kuwa mipango yake ya muda mfupi ni kuhakikisha Stars inafuzu kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika na kutwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji.
Hata hivyo, alisema hajaja na miujiza na kwamba mafanikio hayapatikani mdomoni bali kila mdau kwa nafasi yake kujituma na kutimiza jukumu lake.
"Mafanikio haya yote hayawezi kupatikana kwa maneno, Kenya nao wanasema wanayataka, Uganda pia wanasema hivyo hivyo, lililo muhimu ni wachezaji kujituma, tunatakiwa tushirikiane kuanzia wachezaji, wadhamini, klabu... sio mimi peke yangu nitakayefanikisha," alisema kocha huyo.
Aliitaja mipango yake ya muda mrefu kuwa ni kuendesha mafunzo mbalimbali kwa makocha wa nchini na kusimamia maendeleo ya timu za vijana ambazo ndio msingi wa mafanikio ya nchi zote zilizoendelea katika mchezo huo.
Alisema kuwa wachezaji 27 aliowaita wataripoti kambini leo jioni na kuanza mazoezi kesho kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Misri 'The Pharaos' itakayofanyika katika jiji la Cairo Agosti 11.
Kikosi kamili alichokiita ni Kaseja, Jackson Chove, Shabani Kado, Shadrack Nsajigwa, Salum Kanoni, Stephano Mwasika, Juma Jabu, Idrissa Rajab, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kevin Yondani, Aggrey Morris na Erasto Nyoni.
Wachezaji wengine ni Nurdin Bakari, Abdulhalim Humoud, Henry Joseph, Chuji, Nizar Khalfan, Jabir Aziz, Kigi Makasi, Abdi Kassim 'Babi', Uhuru Suleiman, Suleiman Kassim, Mrisho Ngassa, John Bocco, Mussa Hassan 'Mgosi', Jerryson Tegete na Danny Mrwanda.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga, amewataka wadau kumpa ushirikiano kocha huyo mpya na kuongeza kwamba mafanikio hayaji kwa njia ya mkato.
Tenga alisema kuwa kocha huyo atafanya kazi kwa muda wa miaka miwili na akasisitiza kuwa Tanzania haina desturi ya kubadilisha makocha kama nguo.
Alisema pia kwa sasa, kocha huyo atasaidiwa na makocha Juma Pondamali na Syllvester Marsh.
Kaseja alipopigiwa jana alikataa kuzungumzia chochote kuhusiana na maamuzi ya kocha huyo mpya. "Nimesikia taarifa hizo, ila sina chochote cha kusema," alisema.

'Vigogo', Mawaziri wa JK 'chali' CCM







MAWAZIRI kadhaa wa Serikali ya Awamu ya Nne na wabunge wengi waliomaliza muda wao, wameshindwa kuongoza katika mchakato wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilizopigwa juzi kuteua wagombea wa ubunge, ingawa wanachosubiri ni kwa sasa ni hatma yao katika vikao vya juu vya chama hicho.

Baadhi ya mawaziri walioanguka katika kinyang'anyiro hicho ni aliyekuwa Mbunge wa Nkenge,Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diosdorus Kamala pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera wa Korogwe Mjini, huku kukiwa na taarifa kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, naye ameshindwa kuongoza katika Jimbo la Mbulu.

Mbali na hao, wabunge wengine maarufu wameanguka akiwemo aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, John Malecela wa Mtera, ambaye ameshindwa kushika nafasi ya kwanza ambayo ingempa nafasi ya moja kwa moja ya uteuzi, ingawa wakati mwingine matokeo hayo hubadilishwa na vikao vya juu vya CCM.
Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Mkoa huo, John Barongo,Malecela alimbwagwa na Katibu wa CCM wilaya ya Tarime, Livingstone Lusinde ambaye ameongoza kwa kupata kura 5,810 huku Malecela akiwa na kura 5,379.

Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje ambaye ameliogoza jimbo hilo kwa miaka 20, ameangushwa na Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Gregory Teu,Lubeleje aliyeambulia kura 4,830 huku Teu akiongoza kwa kura 7,777.

Jimbo la Chilonwa, matokeo ya awali yanaonesha Hezekiah Chibulunje anaongoza kwa kura 5,267 ambapo Joel Mwaka akiwa na kura 3,848, katika kata 8 kati ya kata 13.

Barongo alifafanua kuwa, kwa upande wa Jimbo la Kondoa Kaskazini, matokeo ya awali yalionesha kuwa Zabein Mhita alikuwa akiongoza ra 6,211, Mohamed Rashid akiambulia kura 2,116.

Jimbo la Kondoa Kusini, matokeo ya awali ya kata 11 kati ya kata 20, mtangazaji wa zamani wa TBC, Juma Nkamia alikuwa akiongoza kwa kura 4,249 huku akifuatiwa na Paschal Degera kura 632 huku aliyekuwa Katibu wa Bunge, Damian Foka akiambulia kura 545.

Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene alikuwa akiongoza kwa kupata kura 8,824 akifuatiwa na Acray Galawika mwenye 2,537.Jimbo la Bahi, Donald Mejiti aliongoza kwa kupata kura 2,627 akifuatiwa na Omar Baduel mwenye kura 2,268.

Jimbo la Dodoma Mjini ambalo lilikuwa na wagombea 19, Peter Chiwanga alikuwa akiongoza kwa 3,183 katika kata 18 kati ya kata 37, huku akifuatiwa na David Malole mwenye kura 2,479 naaliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Adam Kimbisa akipata kura 2,141.

Kwa upande wa Dar es Salaam, matokeo mengi yalikuwa hayajafika katika ofisi za wilaya. Matokeo ya awali katika Jimbo la Temeke yanaonesha kuwa Abass Mtemvu alikuwa anaongoza katika kata nne za Miburani, Sandali na Mtoni.

Alifuatiwakwa mbali na Salimu Chicago wakati Hiza Tambwe katika kata hizo aliambulia nafasi ya tatu. Katika Jimbo la Kigamboni, Faustine Ndungulile alikuwa anaongoza katika kata za Vijiweni, Kimbiji na Mbagala Kuu.

Katika jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu anaongoza na kuwaacha wapinzani wake kwa mbali huku katika Jimbo la Ukonga, Godwin Barongo anaongoza katika kata za Gongo la Mboto, Ukonga, Pugu na Kitunda.

Kwa upande wa Jimbo la Kinondoni aliyekuwa anaongoza ni Idd Azzan ambaye matokeo ya awali katika kata za Kijitonyama, Kigogo, Hananasif pamoja na Mwananyamala huku Shy-Rose Bhanji akimfuatia kwa karibu. Kura za majimbo ya Segerea, Kawe na Ubungo yanatarajiwa kutolewa leo.

Mkoani Kilimanjaro, Mbunge aliyemaliza muda wake katika Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro, ameanguka baada ya kushika nafasi ya pili kwa kubwagwa na Wakili Crispin Meela.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM mkoani Kilimanjaro, Stephen Kazidi alisema katika Jimbo la Vunjo, Kimaro alipata kura 3,194, Meela kura 7,162 huku wagombea wengine akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Taifa, James Kombe akipata kura 1,110 na Thomson Moshi kura 788.

Jimbo la Moshi Mjini aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiusa katika Manispaa ya Moshi, Buni Ramole alishinda kwa kura 1,554 huku wagombea wengine na kura zao katika mabano wakiwa Thomas Ngawaiya (1,539), Justine Salakana (1,152), Gibson Lyamuya (269) na Joseph Mtui (208). Wengine ni Onesmo Ngowi (127), Peter Njambi (110), Athumani Mwariko (109) na Askofu Pius Ikongo (91).

Jimbo la Moshi Vijijini, Dk. Cyril Chami aliongoza kwa kupata kura 9,196 huku mpinzani wake wa karibu, Ansy Mmasi akipata kura 2,791.

Jimbo la Mwanga, Mbunge anayemaliza muda wake, Profesa Maghembe alipata kura 10,743, Joseph Thadayo kura 6,889 na Karia Magalo alipata kura 252.

Hata hivyo, Katibu huyo wa CCM Mkoa, amesema Ngawaiya ameandika barua akilalamika kwamba baadhi ya wanachama wamezuiwa kupiga kura jambo lililomnyima kura ambazo zingempa ushindi.

Jimbo la Rombo, Kazidi alisema Basil Mramba ameongoza kwa kura 8,389, Netburga Masikini kura 2,946, Lemunge Lesfory kura 854 na Stambul Vitus kura 779.

Jimbo la Same Magharibi, Dk. Mathayo David ameongoza kwa kura 14,281, sawa na asilimia 95, akifuatiwa na John Singo kura 608, Ali Kibwede kura 65 na Lameck Shogholo kura 61.

Jimbo la Hai, Mbunge anayemaliza Fuya Kimbita aliongoza kwa kura 3,725, akifuatiwa na Dastan Mallya (2,649), Aziz Waziri (2,384), Christopher Awinia (1,149), Masumba Meena (939), Lazaro Swai (728), Neema Massawe (456) na Gasper Ngido.

Katika Jimbo la Siha, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri alipita bila kupingwa ndani ya CCM.

Jimbo la Same Mashariki, Mbunge aliyemaliza muda wake, Anne Kilango Malecela, ameongoza kwa kupata kura 7,514 akifuatiwa na mpinzani wake mkubwa, Michael Kadede aliyepata kura 1,804.

Mkoani Singida, Singida Mjini, Mbunge aliyemaliza muda wake, Mohammed Dewji aliongoza kwa kishindo kwa kupata kura 8,997, sawa na asilimia 95, Hawa Ngulume kura 390 na Mariam Msawira 35.

Jimbo la Iramba Mashariki, Mgana Msindai ameshindwa baada ya kupata kura 3,005 huku aliyeongoza ni Salome Mwambu aliyepata kura 3,635, jimbo hilo lilikuwa na wagombea tisa.

Jimbo la Iramba Magharibi, aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Juma Kilimbah, amebwagwa pia baada ya kupata kura 3,788 ukilinganisha na aliyeongoza, Lameck Mwigulu mwenye kura 3,834.

Jimbo la Kwimba, Mbunge anayemaliza muda wake, Bujiku Sakila amekiri kushindwa na akizungumza kwa simu na gazeti hili jana kutoka Ngudu, makao makuu ya Wilaya ya Kwimba, alisema atakuwa tayari kumuunga mkono mgombea wa CCM, Shanif Mansoor ambaye ni Mhasibu wa CCM mkoa wa Mwanza.

“Kwanza nimeshindwa vibaya, lakini niseme kutoka rohoni mwangu kabisa ni mfumo wa uchaguzi wa kura za maoni ndiyo ulionifanya nishindwe, lakini sitakuwa na malalamiko makubwa maana nikiyatoa kitahitajika, “evidence,“ na mimi sikushindwa kwa kukosa sifa za kuwa Mbunge ila ni system ya uchaguzi ilivyokuwa, kulikuwa na rushwa sana hapa Kwimba
lakini mkamataji hakuwepo,” alisema.

Naibu Waziri huyo wa zamani aisema kwa jinsi alivyoona mazingira ya uchaguzi wilayani Kwimba, alisema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) hawakufanya kazi yao barabara ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi huo wa kura za maoni kwa madai kuwa rushwa katika jimbo hilo ilikuwa kubwa, kiasi cha kuifafanisha Takukuru na mtoto mdogo na wagombea watu wazima.

Jimbo la Ilemela, Mbunge wake, Anthony Diallo ameongoza kwa kupata kura 6,601. Wagombea wengine na kura zao ni Pastory Masota (2,159); John Buyamba (1,837); Samson Maganga (519); Darius Ngocho (450); DC mstaafu Jared Gachocha (365); Ashery Gasabire (357) na Shadrack Fereshi (343).

Katika Jimbo la Sengerema, kwa mujibu wa Katibu wa CCM, Maiko Kahuruda alisema jana kuwa mbunge ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alikuwa anaongoza kwa wingi wa kura akifuatiwa kwa karibu na Francisco Shejamabu.

Kwa Jimbo la Buchosa, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Dk. Charles Tizeba alikuwa anaongoza akifuatiwa na Eric Shigongo na Mbunge aliyekuwa anashikilia jimbo hilo, Samuel Chitalilo alikuwa wa tatu.

Jimbo la Misungwi, Kahuruda alisema Charles Kitwanga “Mawe Matatu” alikuwa akiongoza kwa kupata kura 9,104 katika kata tisa kati ya 27 zilipokewa matokeo yake huku akifuatiwa na Mbunge aliyemaliza muda wake, Jacob Shibiliti na Madoshi Makene akishika nafasi ya tatu.

Majimbo ya Sumve na Magu, matokeo yao yalikuwa yakiendelea kukusanywa, wakati katika Jimbo la Nyamagana, matokeo ya awali yaliyotolewa jana na Katibu wa CCM Wilaya, Musa Matoroka yalionesha kuwa Mbunge wa sasa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha alikuwa anaongoza kwa kupata kura 8,627, akifuatiwa na John Marogori aliyepata kura 2420.

Wagombea wengine na kura zao kwenye mabano ni Joseph Kahungwa (1,941); David Mtetemera (570); Wilson Swalala (492); Robert Masunya (396); Stephen Deya (286); Maseke Magaiwa (315); Stephen Deya (286); Abdi Chakechake(271); William Mvanga (220); Boniface Kahangara (162); na Ibrahim Lukumay (124).

Jimbo la Ukerewe, Mbunge aliyemaliza muda wake, Balozi Gertrude Mongella ameongoza kwa kura 6,666 na akifuatiwa na Josephat Lyato aliyepata kura 4,140. Wagombea wengine na kura zao kwenye mabano ni Msafiri Nyandiga (3,530); Oswald Mwizarubi (2,362); Mtani Chitanda (1,822); Deus Tungaraza (967); Ernest Kamando (642); Majige Munyu (284) na Mwibure

Kazi (104).

Jimbo la Busega, aliyekuwa anaongoza ni Dk. Titus Kamani ambaye alikuwa amemuacha mbali sana Dk. Raphael Chegeni

ambaye ni Mbunge anayemaliza muda wake.

Katika Jimbo la Busanda, Mbunge wa sasa, Lolensia Bukwimba alikuwa akiongoza. Jimbo la Nyang’hwale, Mbunge

anayemaliza muda wake, James Musalika ameshika nafasi ya tatu kwa kura 1,200 wakati DC wa Kilombero, Evarist Ndikilo

ana kura 3,125 na aliyeongoza ni Hussein Gulamali kwa kura 4,449.

Mkoani Shinyanga, Jimbo la Shinyanga Mjini, aliyeongoza kwa mujibu wa Katibu wa CCM Mkoa, Mohammed Mbonde, ni

Stephen Masele akiwaangusha wagombea wengine akiwamo aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na

Mbunge mtetezi, Dk. Charles Mlingwa na Mbunge mwingine wa Viti Maalumu, Joyce Masunga;

Jimbo la Solwa aliyeongoza ni Ahmed Salum; Jimbo la Meatu ni Salum Khamis ‘Mbuzi’; Jimbo la Kishapu ni Suleiman Nchambi’s na Jimbo la Bariadi Magharibi ni Andrew Chenge.

Katibu huyo wa CCM Mkoa aliwataja wengine waliongoza ni Emmanuel Luhahula (Bukombe); Peter Bunyungoli (MaswMashariki); Simon Robert (Maswa Magharibi); Martin Makondo (Bariadi Mashariki); Luhaga Mpina (Kisesa); James Lembeli (Kahama). Katika Jimbo Mbogwe, Augustine Masele anaongoza kwa kura nyingi.

Jimbo la Nkenge, Mbunge aliyemaliza muda wake, Dk. Diodorus Kamala ameanguka kwa kushika nafasi ya pili baada ya nafasi ya kwanza kuchukuliwa na Asumpta Mshamu.

Kamala ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, amepata kura 6,184 wakati Mshama amepata kura

9,055. Wagombea wengine ni Dickson Balyagati (4,123), Julius Rugemarila (771), Charles Katarama (410), Ismail

Suleiman (239) na Amani Kajuna kura 146.

Jimbo la Ngara, Mbunge wa sasa, Profesa Feetham Banyikwa alikuwa anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na kura 2,112,

wakati anayeongoza ni Deo Ntukamazima akiwa na kura 3,954 akifuatiwa na Alex Gashaga mwenye kura 3,838.

Jimbo la Chato, Mbunge wa sasa ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. John Magufuli alikuwa akiongoza kwa kura 8,305 akifuatiwa na Dk. Lukanima mwenye kura 810.

Jimbo la Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki amepita bila kupingwa.

Jimbo la Kyerwa, Mbunge aliyemaliza muda wake, Eustace Katagira ameongoza kwa kura nyingi. Hata hivyo, takwimu hazikuweza kupatikana haraka kutokana na tawi mojawapo katika Kata ya Businde kuendelea kukamilisha taratibu za uchaguzi kabla ya kuunganisha matokeo yote.

Jimbo la Karagwe ambalo pia mchakato wa kuunganisha takwimu uliendelea hadi jioni, matokeo yanaonesha mbunge aliyemaliza muda wake, Gosbert Blandes ameshinda kwa kura nyingi. Aliyeshika nafasi ya pili ni Karim na ya tatu ni Profesa Ngalinda.

Jimbo la Bukoba Vijijini ambako hadi jana jioni matokeo ya kata 20 kati ya 29 yalishapatikana, Jasson Rweikiza

ameongoza kwa kura 18,212. Mbunge aliyemaliza muda wake, Nazir Karamagi ameshika nafasi ya pili kwa kura 4,111 na

kufuatiwa na Novatus Nkwama mwenye kura 4,111.

Wagombea wengine ni Muzamir Kachwamba aliyepata kura 816 na Kamalu Mustafa amepata kura 600.

Mbunge wa sasa wa Biharamulo Magharibi, Oscar Mukasa ameongoza kwa kura nyingi akifuatiwa na Agricola Magoho na

Hamidu Nzomukunda.

Kwa upande wa Muleba Kusini, ingawa hadi jioni mchakato wa kuunganisha kura za kata zilizochelewa ulikuwa

ukiendelea, Profesa Anna Tibaijuka ndiye alitajwa kuibuka mshindi kwa kura nyingi akiwaacha mbali Mbunge wa sasa,

Wilson Masilingi aliyeshika nafasi ya pili. Nafasi ya tatu imeshikwa na Alfred Tibaigana.

Maswa Magharibi, Amani Nzugile Jidulalamabambasi, amefariki dunia jana wakati akiwa njiani kutoka Hospitali ya

Wilaya ya Maswa kwenda Rufaa Bugando kwa uchunguzi na matibabu zaidi baada ya kuwa amelazwa katika hispitali hiyo ya

wilaya tangu Julai 29, mwkaa huu.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk. Amos Mremi alisema mwanasiasa huyo alikuwa amelazwa kwenye hospitali hiyo

kutokana na uvimbe mkubwa uliojitokeza katika sehemu zake za siri na kutokana na hali yake ilivyokuwa ilibidi apewe

rufaa ya kweda Bugando kwa uchunguzi na matibabu, na jana akiwa njiani kwenda Mwanza pamoja na muuguzi mmoja kwenye

gari la wagonjwa, alifikishwa hadi katika mapokezi ya Bugando, lakini mara tu kufika hospitalini, iligundulika kuwa

amefariki dunia.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando, Dk. Charles Majinge alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba alifikishwa

mapokezi akiwa tayari amefariki dunia, mwili wake ulitarajiwa kurejeshwa wilayani Maswa kwa ajili ya mazishi.

Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa kiongozi wa UDP, alishika nafasi ya tatu nyuma ya Robert na Shibuda, miongoni mwa

wagombea tisa waliojitokeza.

Jimbo la Chalinze, aliyeongoza ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Said Bwanamdogo aliyepata kura 8,144 akifuatiwa na

aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Imani Madega mwenye kura 4,193; Mbunge aliyemaliza muda wake, Ramadhan

Maneno kura 3,623. Jimbo hilo lilikuwa na wagombea 10.

Jimbo la Bagamoyo, Mbunge wa sasa Dk. Shukuru Kawambwa ambaye pia ni Waziri wa Miundombinu, ameongoza kwa kura

6,576, akiafuatiwa Dk. Andrew Kasambala mwenye kura 1,061.

Wabunge waliomaliza muda wao, Dk. Ibrahimu Msabaha (Kibaha Vijijini), Dk. Zainabu Gama (Kibaha Mjini); Profesa

Idrisa Mtulya (Rufiji), nao wameanguka.

Wabunge wa zamani waliopeta katika kinyang'anyiro hicho ni Adam Malima (Mkuranga); Abdul Malombwa (Kibiti) na

Abdulkarim Shah (Mafia)

Wagombea wapya waliochomoza na Silvesta Koka (Kibaha Mjini); Hamidu Abuu (Kibaha Vijijini); Seleman Jafo (Kisarawe)

na Dk.Seif (Rufiji).

Hata hivyo, baada ya matokeo hayo kutangazwa, aliyekuwa Mbunge wa Kibaha Mjini, Dk. Gama aliwasilisha barua kwa

Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Sauda Mpambalyoto akipinga matokeo ya jimbo lake kwa madai ya uchaguzi kutawaliwa na

mchezo mchafu na rafu za hapa na pale kwa baadhi ya wagombea.

Jimbo la Kasulu Mjini, Neka Raphael ameongoza kwa kura 672 akifuatiwa na Gidion Bunyaga (510); Askofu Gerald Mpango (306); Twalib Mangu (270) na Agnes Nyowola (225).

Jimbo la Kasulu Vijijini, Daniel Nsanzugwanko alikuwa akiongoza kwa kura 1,560 akifuatiwa na Kafonogo Mayengo (625) na Patrick Nyembele (420).

Jimbo la Manyovu, Albert Obama alikuwa akiongoza kwa kura 770; James Japhet (667); Eliadory Kavejuu (300); Betwel Ruhega (300) na mbunge anayemaliza muda wake, Kilontsi Mporogomyi (260).

Jimbo la Muhambwe, Jamal Tamim alikuwa akiongoza kwa kura 2,921 akifuatiwa na Richard Kigaraba (); Mbunge wa sasa, Felix Kijiko (1,523); mbunge wa zamani Arcardo Ntagazwa (577) na Edgar Mkosomali (922).

Mkoani Iringa, hatima ya wabunge Joseph Mungai, Monica Mbega, Jackson Makweta, Profesa Raphael Mwalyosi, Benito

Malangalila na Yono Kevela, kurudi kwa mara nyingine tena katika vikao vya Bunge lijalo, kutategemea zaidi maamuzi ya juu ya vikao vya CCM, baada ya taarifa za awali kuonesha kuwa wameshindwa kura za maoni.

Hata hivyo, mpaka tunakwenda mitambani ofisi za chama za majimbo hayo zilikuwa hazijatoa taarifa rasmi, na Katibu wa CCM wa Mkoa, Mary Tesha alipoulizwa, alisema ofisi yake inaendelea kupokea matokeo kutoka katika majimbo yote ya uchaguzi.

Taarifa za awali za uhakika kutoka katika majimbo hayo zinaonesha kwamba wakati Mahamudu Mgimwa ameibuka kidedea katika Jimbo la Mufindi Kaskazini lililokuwa likiongozwa na Mungai, Deo Sanga (Jah People) ameibuka kidedea katika Jimbo la Njombe Kaskazini lililokuwa likiongozwa na Makweta.

Mbega (Iringa Mjini) ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro atalazimika kurudi haraka iwezakanavyo mkoani humo

kuendelea na majukumu mengine ya kiserikali baada ya kushindwa katika kura hizo zilizompa ushindi aliyekuwa Katibu

Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela.

Mwakalebela anaongoza kwa kuwa na kura 3,897, Mbega 2,989 na Yahaya Msigwa 1,217. Ludewa, Mbunge wa sasa Profesa

Mwalyosi amebanwa na Deo Filikunjombe ambaye matokeo ya awali yanaonesha amepata kura zaidi ya 6,000 huku Profesa

Mwalyosi akipata kura zaidi ya 4,000.

Dalali maarufu Kevela wa Njombe Magharibi, naye anadaiwa yuko katika wakati mgumu dhidi ya Mbunge aliyemtangulia

Thomas Nyimbo, huku taarifa kutoka Jimbo la Mufindi Kusini nazo zimethibitisha kwamba Benito Malangalila naye

ameshindwa kuongoza katika kura za maoni za jimbo hilo. Mendradi Kigola anaongoza katika jimbo hilo.

Katika Jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto ameshindwa kumpiku Mbunge aliyemaliza muda wake, Profesa Peter Msolla

aliyepata zaidi ya kura 18,000 dhidi ya kura zake zinazodaiwa kuwa zaidi ya 3,000.

Jimboni Makete, mbunge aliyemaliza muda wake, Dk. Benelith Mahenge amejihakikishia kurudi bungeni kwa awamu ya pili,

kama ilivyo kwa Njombe Kusini kwa Naibu Spika, Anne Makinda.

Kutoka Isimani, Katibu wa CCM wa wilaya ya Iringa, Luciano Mbosa alisema jana kwamba William Lukuvi ameshinda kura hizo kwa kujinyakulia kura 7,996 dhidi ya kura 533 za Festo Kiswaga, 286 za Leonard Mwali na Yahaya Mtete aliyepata kura 176.

Huko Kalenga, Mbosa alisema shughuli ya ujumlishaji kura inaendelea hata hivyo taarifa za awali zinaonesha kwamba Dk William Mgimwa amepata kura 2,819 akifuatiwa na Abbas Kandoro aliyepata kura 2,353 na Hafsa Mtasiwa aliyepata kura

1,553.

Mkoani Mbeya, Mbarali, Mbunge anayemaliza muda wake, Estherina Kilasi amekuwa wa tatu akiwa na kura 614, huku

akiongoza Modestus Kilufi kura 1,521 na wa pili ni Burton Kihaka (1,322). Ileje ni Aliko Kibona (5,844), Ambonesigwe

Mbwaga (2,200) na Godfrey Msongwa (2,004).

Lupa, Mbunge aliyemaliza muda wake, Victor Mwambalaswa ameongoza kura 6,135 dhidi ya aliyewahi kuwa Mbunge na

Waziri, Njelu Kasaka (4,135). Songwe, Mbunge aliyemaliza muda wake, Dk. Guido Sigonda amepata kura 780; aliyeongoza

ni Philipo Mulugo (7,100); Paul Ntwina (1,618) na Hamad Juma (962).

Kyela, Mbunge ambaye alikuwa kinara katika mapambano ya ufisadi, Dk. Harrison Mwakyembe ameongoza kwa kura 7,681 dhidi ya George Mwakalinga (574) na Elias Mwanjala (512).

Rungwe Mashariki, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya ameongoza kwa kupata kura 4,240 dhidi ya Stephen Mwakajumulo (228). Rungwe Magharibi, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa ameongoza kwa kura 6,974, dhidi ya Richard Kasesela (5,843) na Frank Magoba (1,379).

Mbeya Mjini, Mbunge aliyemaliza muda wake, Benson Mpesya ameongoza dhidi ya Mbunge wa Kuteuliwa, Thomas Mwang’onda kwa kupata kura 5,586 dhidi ya kura 3,362.

Mbeya Vijijini, Mbunge aliyemaliza muda wake, Mchungaji Luckson Mwanjale ameongoza kwa kura 7,353 dhidi ya kura 1,902 za Andrew Saile.

Mkoani Tabora, Jimbo la Urambo Mashariki, Samuel Sitta alikuwa akiongoza kwa kura 6,130 dhidi ya Masoud Maswanya

mwenye kura 2,432 na Ali Karavina kura 464. Jimbo la Urambo Magharibi (sasa Kaliua), Profesa Juma Kapuya anaongoza

kwa kura 5.656 dhidi ya Ramadhan Kalla mwenye kura 751.

Jimbo la Nzega, Hussein Bashe alikuwa akiongoza kwa kura 6,815 na Lucas Selelii ambaye niMbunge aliyemaliza muda

wake, ana kura 1,420.

Jimbo la Bukene, Mbunge aliyemaliza muda wake, Teddy Kasella-Bantu ana kura 1,968 na Suleiman Zeddy ana kura 1,727.

Sikonge ni George Kakunda anaongoza kwa kura 1,570 dhidi ya Mbunge anayemaliza muda wake, Said Nkumba mwenye kura

1,365.

Tabora Mjini, Ismail Aden Rage anaongoza kwa kura 4,145 dhidi ya Mwanne Mchemba ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu

mwenye kura 2,985 na mbunge wa jimbo hilo, Siraju Kaboyonga ana kura 835.

Mkoani Lindi, Jimbo la Mchinga, Said Mtanda alikuwa akiongoza katika kata nane kati ya 10, kwa kuwa na kura 3,768

dhidi ya kura 1,577 za Mbunge aliyepita, Mudhihir Mudhihir.

Jimbo la Nachingwea, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe ameongoza kwa kura 5,887, akifuatiwa na DC wa

zamani wa Bukoba Mjini, Albert Mnali (3,912), Elias Masala (1,844), Maokola Majogo (1,191), Ally Mpelemba (450),

Fulgence Mpelembe (126) na Benito Ng’itu (266).

Mkoani Katavi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amepita bila kupingwa katika Jimbo la Mlele (zamani Mpanda Mashariki),

lakini wabunge watatu wa zamani wameanguka.

Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeshy Hillaly ameongoza kwa kupata kura 867 dhidi ya Mbunge wa Viti Maalumu, Elieta

Switi 155; Edson Makallo (54); James Kusulo (26); Frolence Mtepa (25); Emmanuel Msingezi (18); Joseph Malikawa

(38).

Jimbo la Nkasi Kaskazini, ameongoza Mohamed Keissy (1,557); Hiporitus Matete (1,173), DED wa Kilosa, Ephrem

Kalumalwendo (1,003), mbunge anayemaliza muda wake, Ponsiano Nyami (695), S. Khamsin (319) na V. Konga (51). Jimbo

la Nkasi Kusini, aliyeongoza ni Desderius Mipata (719); Joseph Walingozi (348); Emmanuel Sungura (45); J. Mwanansau

(23); Joseph Kitakwa (58).

Jimbo la Kwela, ameongoza Ignas Malocha (5,772); Meja January Kisango (1,772); Didas Mfupe (1,669); Steven

Chambanenje (796); Patrick Maufi (329); Solomon Jairos (66) na Bendicto Chapewa (227). Jimbo la Kalambo, Josephat

Kandege ameongoza kwa kura (5,597) dhidi ya Ludovick Mwananzila (4,061) na Paul Mwanandeje.

Mkoani Mtwara, Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia ameongoza katika Jimbo la

Mtwara Vijijini huku Vita Kawawa akiongoza Jimbo la Namtumbo.Mkoani Tanga, Bendera ameshindwa na Yussuf Nasir kwa

kupata kura 2,258 dhidi ya Nasir aliyeongoza kwa kura 2,513.

Pangani, Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, ameshinda Mbunge aliyemaliza muda wake, Risherd Abdallah kwa kura 4,391 dhidi ya 2,442.

Tanga Mjini, Omar Nundu ameongoza kwa kura 7,445 dhidi ya Harith Mwapachu aliyepata kura 2,156 ambaye ni Mbunge aliyemaliza muda wake.

Wakati huo huo, aliyekuwa Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Charles Mwera ameshindwa kutetea kiti hicho baada ya kubwagwa na mwanachama mwenzake, Mwita Waitara ambapo Waitara alipata kura

131 akifuatiwa na Mwera aliyepata kura 113. Wagombea John Heche kura 92 na Philipo Nyanchini aliyepata kura 10.

Upande wa Viti Maalumu kwa wagombea wa Chadema Tarime aliyeshinda ni Mary Nyagabona aliyepata kura 58 na kuwashinda Ester Matiko aliyepata kura 54, wengine ni Tekra Johanes kura nne na Mwenyekiti wa Wanawake wa Chadema Taifa, Leticia Mosore hakupata kura.

Tuesday, July 27, 2010

DC mikononi mwa Takukuru *Anawania ubunge viti maalum *Akamatwa na wapambe wake, fedha gesti

MKUU wa Wilaya ya Kasulu, Betty Machangu, ni miongoni mwa mavuno mapya ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) katika operesheni ya kukamata wagombea ubunge wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kugawa fedha.

Machangu alikamatwa juzi na maofisa wa Takukuru mkoani Kilimanjaro pamoja na vigogo wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wa mkoani wa Kilimanjaro
na wa Wilaya ya Moshi Vijijini.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye amejitosa kwenye kinyang’anyiro cha kusaka ubunge kupitia viti maalum mkoani Kilimanajro, alikamata na kuhojiwa kisha kuachiwa.

Machangu anadaiwa kutoa rushwa kwa wajumbe wa UWT mkoa ili wamchague.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Alexander Budigila, aliwataja
watuhumiwa wengine kuwa ni Katibu wa UWT mkoa, Mariam Kaaya, Katibu wa
UWT wilaya ya Moshi, Hadija Ramadhani, mfanyabiashara wa Moshi
mjini, Hawa Sultani na dereva wa gari alilokuwa wakitumia, Swalehe
Twalibu.

Alisema Takukuru ilipokea taarifa kutoka kwa raia mwema za kuwepo vitendo vya rushwa katika nyumba ya kulala wageni ya Safari Resort, ambapo walikuwa wakigawa rushwa ya fedha na vitu kwa wajumbe kwa kila mmoja kuingia mmoja mmoja kuanzia majira ya saa 8:30 mchana.

Tarifa hiyo ilionyesha kuwa mgombea huyo na wafuasi wake walikuwa wakigawa fedha kiasi cha Sh. 100,000 na 50,000, kanga, asali na vipeperushi na kadi za wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT mkoa.

“Tuliizingira nyumba hiyo kuanzia majira ya saa nane hadi saa 10 ndipo tulipoingia ndani na kuwataka kufungua chumba namba 24 ambako
mgombea huyo na viongozi hao walikuwa wamejifungia huku dereva wa gari
lenye namba za usajili T 688 APQ aina ya Mitsubishi ambaye alikuwa anaimarisha ulinzi kwa kila anayefika,” alisema

Alisema walikaa kimya hadi saa 1:30 bila kufungua na ndipo maafisa wa
Takukuru walipojitambulisha na kugonga mlango kwa nguvu zaidi na
majira ya saa 2:15 usiku, ambapo ndipo walifanikiwa kuingia ndani na
kuwakuta watu wanne.

Alisema baada ya upekuzi walikuta Sh. 400,000 kwenye pochi ya katibu wa UWT, pea nne za vitenge, vipeperushi vya kumnadi mgombea
huyo, kadi za wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT mkoa ambazo zilitumbukizwa
kwenye chombo cha kuingiza maji chooni (tanki la chooni).

Alisema pia walikamata Sh.100,000 zikiwa kwenye pochi ya mgombea huyo, ambazo ziliwekwa kwenye bahasha na kuandikwa majina, lakini baada ya kuhisi watakamatwa walizitoa kwenye bahasha na
kuzichanachana na kisha kuzitupa chini ya uvungu wa kitanda.

Budigila alisema pia kwenye pochi ya katibu huyo walikuta vipeperushi
vya mgombea mwingine Regina Chonjo ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT mkoa na walifanikiwa kulikamata gari hilo ambalo ni mali ya mgombea huyo.

Machangu akizungumza na wanahabari alisema kuwa majira ya saa 10 ndio
alikwenda kwenye baa hiyo kwa lengo la kupata chakula cha mchana na kwamba baada ya kufika alitafuta mahali penye utulivu, ili azungumze
na viongozi na msaidizi wake kabla ya kwenda kwenye mkutano wa kampeni.

Alisema walikosa pa kukaa na kumua kwenda kukaa chumbani na hakukua na
rushwa yoyote iliyotolewa kwa kuwa kila mmoja alikuja na mkoba wake na
hata kama angetaka kutoa rushwa angewafuata majumbani mwao.


Takukuru yashikiria saba

Wakati huo huo, Takukuru inawashikilia na kuwahoji watu saba waliodaiwa kuwa mabalozi, wajumbe wa vijiji na makatibu wa CCM katika kata ya Shirimatunda ambao wanadaiwa walikuwa wakila na kunywa na mgombea
udiwani mmoja.

Habari zinasema baada ya maafisa wa Takukuru kufika watu hao walikimbia akiwemo mgombea huyo na kwamba walifanikiwa kuwakamata watu hao kati
ya 30 waliokuwa wamekaa na mgombea huyo wakiwa na kikao cha kushawishi
mgombea huyo kupitishwa.

Kamanda wa Takukuru mkoani hapa alisema uchunguzi wa kina wa matukio hayo yote unaendelea na baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Dodoma wataka
matokeo yafutwe

Baadhi ya wagombea udiwani wa Viti Maalum kupitia UWT katika Wilaya ya Dodoma Mjini, wametaka matokeo yafutwe na uchaguzi urudiwe kutokana na uchaguzi huo kutofanyika kwa haki.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi ya CCM mkoa, mmoja wa wagombea hao, Catherine Mbiligwa, alisema uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki kutokana na mmoja wa wasimamizi uchaguzi (jina tunalo) kutoa kauli za matusi kwa wagombea na wajumbe waliokuwepo kwenye uchaguzi huo.

Alisema moja ya sababu za kuomba uchaguzi huo kurudiwa ni kutokana na wagombea hao kutopata nafasi ya kuhesabu kura zao wala kuweka mawakala wao.

“Tulipojaribu kumuomba tuweke mawakala wetu kama haki yetu, tulifukuzwa kama mbwa na askari pamoja na katibu wa UWT wakishirikiana na msimamizi wa uchaguzi,” alisema.

Aidha, mgombea huyo alisema wakati wa kupiga kura pia hapakuwa na masanduku ya kutosha ya kuwekea kura, badala yake kura nyingine zililazimika kufungwa kwenye kanga za wajumbe.

Mgombea mwingine, Mwajuma Yame, alisema mbali na kutotendewa haki katika uchaguzi huo, pia hapakuwapo na uwiano wa nafasi za viti maalum kwa kila tarafa.

“Kila tarafa inatakiwa kuwa na madiwani watatu wa viti maalum, lakini tarafa zingine zina kata chache tofauti na Dodoma Mjini ambapo kuna kata takribani 20, lakini nafasi za viti maalum ni nne tu…Tunaomba uwiano,” alisema.

Akampeni harusini

Mgombea udiwani anaye maliza mda wake katika Kata ya Tambukareli Manispaa ya Dodoma, Edward Lamali, amejikuta akifanya kampeni katika ukumbi wa harusi.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Hall Cross, ambapo diwani huyo aliteuliwa na ndugu kutambulisha wageni pamoja na kuwapa nasaha maharusi katika maisha yao ya ndoa.

Diwani huyo alitoa utambulisho huo kama alivyoagizwa, lakini kabla ya kuhitimisha alianza kupiga kampeni kwa kuwataka wageni waalikwa kumpigia kura za maoni wakati utakapowadia.

Aliwaomba wamchague kwa mara nyingine ili aendelee kuyamalizia mambo ambayo alikuwa ameshaanza kuyatekeleza kwa kipindi kilichopita.

Mwangunga akumbana na Loliondo jimboni Ubungo
Mgombea wa ubunge Jimbo la Ubungo, Shamsa Mwangunga, amezidi kubanwa na wanachama baada ya kuambiwa kuwa kama alishindwa kuwasaidia Wamasai wa Loliondo mkoani Arusha wasinyang'anywe ardhi na mwekezaji, atawezaje kutatua kero zinazowakabili wananchi wa Mabibo, jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wanachama wa CCM alimbana mgombea Mwangunga ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii kwenye mkutano wa kujinadi wagombea uliofanyika Mabibo na kukutanisha matawi manne.

“Ukiwa kama Waziri wa Maliasili na Utalii ulishindwa kuwasaidia wafugaji hao ambao serikali ilidai kuwa waliingia eneo la hifadhi ya Taifa je, utaweza kutusaidia sisi?” alihoji mwanachama huyo.

Baada ya kuulizwa swali hilo, Mwangunga alishangaa kisha alimjibu kuwa wafugaji hao ndiyo waliovunja sheria na kuingia eneo la hifadhi hivyo serikali iliwaondoa kwa kuzingatia sheria.

Hata hivyo, mwanachama huyo alionekana kutoridhika na jibu hilo ingawa alilikubali na kukaa chini ili kumpa mwenzake aendelee kuuliza
swali lingine.

Maghari ya kifahari yatumika

Wakati huo huo, wagombea wa CCM wamezidi kuonyeshana ufahari wa kuwa na magari ya gharama wakati wa kampeni zao zinazoendelea maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam licha ya chama chao kuwataka wasitumie vyombo hivyo na badala yake wapande basi moja.

Baadhi ya magari hayo yaliyoonekana kuvinjari maeneo ya mikutano ni yenye namba za usajili, T 626 AEX aina ya Toyota Land Cruiser Prado, T 780 AZJ aina ya Nissan Patrol na T257 AQT Toyota Land Cruiser VX ambayo yalikuwa yakitumiwa na wagombea katika jimbo la Segerea.

Katika jimbo la Ubungo nalo, Mwangunga alionekana akiwa ndani ya gari lake aina ya Land Cruiser huku wagombea wenzake wakiwa kwenye basi la pamoja kama chama kilivyowataka kufanya.

Akizungumza na NIPASHE siku ya kwanza ya kuanza kampeni hizo, Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Abihudi Shilla, alisema wagombea wote hawaruhusiwi kutumia magari yao wala kuvaa suti au nguo nyingine tofauti na zile za chama.

Alisema chama kimeweka utaratibu huo ili wagombea wote waonekane wapo sawa kwa wanachama badala ya kila mmoja kufanya mbwembwe za kila aina ili kuwakoga wanachama.

Shy-Rose aibuka
na staili mpya

Mchakato wa kura za maoni kwa wagombea wa CCM Jimbo la Kinondoni umeendelea kuwa na vituko na moja ya matukio na vituko hivyo ni mmoja wa wagombea kutembea kwa gwaride mbele ya wanachama na kuwapigia magoti kuomba kura.

Mgombea huyo, Shy-Rose Bhanji, jana alitumia staili hiyo katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa alipokuwa akiomba kura kutoka kwa wanaCCM wakazi wa Kata ya Ndugumbi.

Bhanji alitembea kwa gwaride wakati wa kujitambulisha na kupiga magoti kabla ya kuondoka kwa gwaride na kushangiliwa kwa makofi mengi.

Akijibu swali aliloulizwa la jinsi gani ataweza kupambana na dawa za kulevya na kitu gani alichowafanyia vijana kichama, Bhanji alisema kuwa atatetea kero mbalimbali ikiwemo ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana, kusaidia wajane kwa kuunda vikundi vya maendeleo.


Kigamboni wazozana

Kampeni katika Jimbo la Kigamboni jana zilikumbwa na mzozo baada wagombea ubunge kutaka kuwabana makatibu wa matawi na wanachama wao kususia kikao cha kampeni.

Matukio hayo yametokea katika mikutano ya katika Kata za Kibada na Mjimwema wakati wagombea hao walipokwenda kujinadi kwa wanachama.

Katika kata ya Kibada, wagombea ubunge walifika katika eneo la mkutano majira ya saa 4:00 asubuhi, lakini walijikuta wakiwa peke yao bila ya kupokewa na wenyeji, baada ya viongozi na wanachama kutokuwepo eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo, baadhi walionekana kuja juu wakidai kuna dalili ya kuchezewa rafu, kwa sababu haiwezekani wasione hata mwanachama mmoja akiwa eneo la mkutano.

Juhudi za kusubiri wapiga kura ziligonga ukuta, baada ya mratibu wa kampeni hizo, Jimbo la Kigamboni, Sophia Kinega, kuwaagiza wagombea hao kujinadi mbele ya wanachama 50 pekee kati ya wapigakura 1,500 waliotakiwa kuwepo kwenye mkutano huo.

Akielezea tukio hilo, Mratibu huyo alisema hali hiyo ilisababishwa na makatibu wa matawi kususia kutoa taarifa kwa wanachama wao kwa sababu zisizoeleweka.

“Kwa kweli ni hali ya kusikitisha, nimewasiliana na katibu wa kata, lakini ameniambia makatibu wa matawi wamesusa na ndio maana hata wanachama hawakufika, jambo hili ni baya na ni lazima nilifikishe mbele,” alisema Kinega.

Mjumbe mmoja aliyejitaja kwa jina la Mohamed Namwogo, alisema kwa ujumla taarifa ya kuwepo kwa mkutano huo waliipata usiku na kusababisha wengi wao kushindwa kufika.


Nusura wapigane mkutanoni

Katika hatua nyingine, wagombea watatu nusura wapigane ngumi kwa madai kuwa mgombea mmoja alikuwa akieneza maneno yanayohusiana na ubaguzi wa kikabila.

Wagombea hao, John Kibaso na Magige Kiboko walimtuhumu Kazimbaya Makwega kwa kueneza maneno yanaoonyesha ishara ya kuwatenga kwa sababu wao wanatoka Mkoa wa Mara.

Tukio hilo lilitokea katika kituo cha Kata ya Mjimwema kabla ya kuanza kwa mkutano, ambapo wagombea hao walionekana kupandwa na hasira na kutishia kumtwanga ngumi kwa maelezo kuwa wamechoshwa na maneno yake.

“Haiwezekani bwana kila akisema utamsikia huyu mtu wa Musoma, sasa u-Musoma wetu unakuja vipi hapa, usitubabaishe bwana,” alisema Kibaso kwa hasira na kumfuata Makwega sehemu aliyokuwa amesimama.

Baada ya kuona hali imekuwa mbaya, baadhi ya wagombea waliingilia kati na kuwaingiza ndani ya gari wagombea hao na kuwasihi wapunguze jazba kwani wote ni wamoja.

Hata hivyo, wagombea wote walijinadi mbele ya wanachama na kuelezea mikakati na mipango yao ikiwa watachaguliwa.

Chanzo:GAZETI LA NIPASHE

Rais wa Tandale aja na filamu ya Mbagala


=============================


KIBAO cha 'Kwetu Mbagala' kinachozidi kutamba nchini cha msanii Naseeb Abdul 'Diamond' a.k.a 'Rais wa Tandale' kinatarajiwa kutengenezewa filamu itakayopewa jina hilo hilo la 'Mbagala'.
Akizungumza na Blog hii, Diamond, alisema tayari ameshaanza maandalizi ya kufyatua filamu hiyo ambayo itawashirikisha wasanii nyota wa fani hiyo akiwemo Jacqueline Wolper.
Diamond alisema lengo la kutoa filamu hiyo ni kutaka kufafanua ukweli juu ya kibao chake ambacho kimekuwa kikilalamikiwa na baadhi ya wapenzi na mashabiki wa fani hiyo wakazi wa eneo hilo la jijini wakidai amewadhalilisha.
"Baada ya kibao changu cha 'Mbagala' kutamba, natarajia kuja na filamu yenye jina hilo ambayo itawashirikisha wasanii kadhaa nyota, akiwemo Wolper, mimi mwenyewe na wengineo ambao wataifanya iwe ya kiwango," alisema Diamond.
Aliongeza kuwa kutoka kwa filamu hiyo kutamaliza 'ubishi' juu ya ukweli kama kibao chake cha 'Mbagala' kilikuwa kinalenga kuwadhalilisha wakazi wa Mbagala au alitumia jina hilo kupata vina vya wimbo huo, ilihali alikuwa akilenga maskani yake ya Tandale alipokulia.
"Mengi yamesemwa juu ya kibao hiki, lakini itakapotoka filamu yake ndio watu watajua mimi sikuwa na nia mbaya ya kusanifu kitongoji hicho, ila nililazimika kutumia jina lake kufikisha ujumbe juu ya mkasa wa kimapenzi na eneo letu nililokulia la Tandale," alisema

RATIBA LIGI KUU YA VODACOM 2010-2011







IFUATAYO NI RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM, VPL- 2010-2011 ILIYOTOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA, TFF, AMBAYO INATARAJIWA KUANZA AGOSTI 21, MWAKA HUU;


JUMAMOSI, Agosti 21
African Lyon v Simba
Polisi Dodoma v Yanga
AFC v Azam
Majimaji v Mtibwa Sugar
Toto African v Ruvu Shooting
Kagera Sugar v JKT Ruvu

JUMAMOSI, Agosti 28
Majimaji v African Lyon
Polisi Dodoma v Mtibwa Sugar
Kagera Sugar v Ruvu Shooting
Toto African v JKT Ruvu

JUMAMOSI, Septemba 4
Polisi Dodoma v Toto African
JKT Ruvu v Majimaji
African Lyon v AFC

JUMAMOSI, Septemba 11
AFC v Yanga
Azam v Simba

JUMATANO, Septemba 15
Kagera Sugar v Azam
Mtibwa Sugar v Yanga
Simba v Ruvu Shooting

Jumamosi Septemba 18
Toto African v Azam
Yanga v Majimaji
Ruvu Shooting v AFC
Mtibwa Sugar v Kagera Sugar

JUMAPILI, Septemba 19
Simba v Polisi Dodoma

JUMATATU, Septemba 20
African Lyon v JKT Ruvu

JUMATANO, Septemba 22
Ruvu Shooting v POlisi Dodoma
Yanga v Kagera Sugar
Majimaji v AFC

ALHAMISI, Septemba 23
JKT Ruvu v Mtibwa Sugar

IJUMAA, Septemba 24
Azam v African Lyon

JUMAMOSI, Septemba 25
Simba v Toto African
Majimaji v Polisi Dodoma

JUMAPILI, Septemba 26
Yanga v Ruvu Shooting

JUMATATU, Septemba 27
African Lyon v Kagera Sugar
AFC v Toto African

JUMANNE, Septemba 28
Azam v JKT Ruvu

JUMATANO, Septemba 29
Mtibwa Sugar v Simba

JUMAMOSI, Oktoba 2
Mtibwa Sugar v Toto African
Ruvu Shooting v African Lyon
Kagera Sugar v Polisi Dodoma
AFC v JKT Ruvu
Majimaji v Azam

JUMAMOSI, Oktoba 16
Simba v Yanga

JUMATANO, Oktoba 20
Simba v AFC
Mtibwa Sugar v Azam
Polisi Dodoma v African Lyon
Toto African v Kagera Sugar
Ruvu Shooting v Majimaji

ALHAMISI, Oktoba 21
JKT Ruvu v Yanga

JUMAMOSI, Oktoba 23
JKT Ruvu v Simba
Ruvu Shooting v Mtibwa Sugar
AFC v Polisi Dodoma
Toto African v African Lyon

JUMAPILI, Oktoba 24
Azam v Yanga
Kagera Sugar v Majimaji

JUMATANO, Oktoba 27
Toto African v Majimaji
Mtibwa Sugar v AFC
Yanga v African Lyon
Polisi Dodoma v Azam
Kagera Sugar v Simba

ALHAMISI, Oktoba 28
JKT Ruvu v Ruvu Shooting

IJUMAA, Oktoba 29
African Lyon v Mtibwa Sugar

JUMAMOSI, Oktoba 30
Azam v Ruvu Shooting

JUMAPILI, Novemba 7
Polisi Dodoma v JKT Ruvu
AFC v Kagera Sugar
Majimaji v Simba
Yanga v Toto

2011
JUMAMOSI, Januari 15
Azam v Kagera Sugar
Toto African v Polisi Dodoma
Majimaji v JKT Ruvu
AFC v African Lyon
Ruvu Shooting v Simba

JUMAPILI, Januari 16
Yanga v Mtibwa Sugar

JUMANNE, Januari 18
Simba v Azam

JUMATANO, Januari 19
Mtibwa Sugar v Polisi Dodoma
Ruvu Shooting v Kagera Sugar

ALHAMISI, Januari 20
African Lyon v Majimaji

IJUMAA, Januari 21
Yanga v AFC
JKT Ruvu v Toto African

JUMAMOSI, Januari 22
Yanga v Polisi Dodoma

JUMAPILI, Januari 23
Simba v African Lyon

JUMATATU, Januari 24
Azam v AFC

JUMATANO, Januari 26
Ruvu Shooting v Toto African
Mtibwa Sugar v Majimaji
JKT Ruvu v Kagera Sugar

JUMATANO, Februari 2
Azam v Toto African

JUMAMOSI, Februari 5
Majimaji v Yanga
Kagera Sugar v Mtibwa Sugar
AFC v Ruvu Shooting
Polisi Dodoma v Simba
JKT Ruvu v African Lyon

JUMAPILI, Februari 13
AFC v Majimaji
Mtibwa Sugar v JKT Ruvu
Polisi Dodoma v Ruvu Shooting

JUMATANO, Februari 16
African Lyon v Azam
Toto African v Simba
Kagera Sugar v Yanga

JUMAPILI, Februari 20
Kagera Sugar v African Lyon
Toto African v AFC
Polisi Dodoma v Majimaji
JKT Ruvu v Azam

JUMATANO, Februari 23
Toto African v Mtibwa Sugar
African Lyon v Ruvu Shooting
Polisi Dodoma v Kagera Sugar

JUMAPILI, Februari 27
Simba v Mtibwa Sugar

JUMATATU, Februari 28
Ruvu Shooting v Yanga

JUMANNE, Machi 1
JKT Ruvu v Ruvu Shooting

JUMATANO, Machi 2
Azam v Majimaji

JUMAMOSI, Machi 5
Yanga v Simba

JUMATANO, Machi 9
Kagera Sugar v Toto African
African Lyon v Polisi Dodoma
Majimaji v Ruvu Shooting

JUMAMOSI, Machi 12
AFC v Simba
Yanga JKT Ruvu

JUMAPILI, Machi 13
Azam v Mtibwa Sugar

JUMATANO, Machi 16
African Lyon v Toto African
Polisi Dodoma v AFC
Majimaji v Kagera Sugar
Mtibwa Sugar v Ruvu Shooting

JUMAMOSI, Machi 19
Majimaji v Toto African

JUMAPILI, Machi 27
Simba v Kagera Sugar

JUMATANO, Machi 30
Yanga v Azam
Ruvu Shooting v JKT Ruvu
AFC v Mtibwa Sugar

JUMAPILI, Aprili 2
Simba v JKT Ruvu

JUMATATU, Aprili 3
African Lyon v Yanga

ALHAMISI, APrili 7
Azam v Polisi Dodoma

JUMAMOSI, Aprili 9
JKT Ruvu v Polisi Dodoma

JUMAPILI, Aprili 10
Mtibwa SUgar v African Lyon
Kagera Sugar v AFC
Toto African v Yanga
Ruvu Shooting v Azam
Simba v Majimaji

Wanamichezo wauota ubunge 2010

MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Ismail Rage anaongoza orodha ya wanamichezo waliojitosa kwenye mchakato wa kuwania kuteuliwa kuwa wagombea na viti vya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 31.
Rage anawania jimbo la Tabora Mjini kwa tiketi ya CCM, ambalo linashikiliwa kwa sasa na Juma Kaboyoga ambaye anakitetea kiti hicho.
Wanamichezo wengine wanaotaka ubunge ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo Netiboli, CHANETA, Shy Rose Bhanji anayewania Jimbo la Kinondoni, Seneta wa zamani wa Yanga, Nasor Duduma na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake katika klabu hiyo Imani Madega wao wamejitosa kwenye mbio hizo wakiwania Jimbo la Chalinze.
Wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Frrdirick Mwakalebela, aliyejitosa jimbo la Iringa Mjini, mkimbiaji bingwa wa zamani, John Bura aliyejitosa Jimbo la Karatu, Mkurugenzi wa Simba, Aziz Aboud aliyeomba katika jimbi la Morogoro Mjini.
Phares Magese, Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Kikapu nchini, TBF, aliyejitosa Jimbo la Kigamboni.
Pia katika kinyang'anyiro hicho cha mbio za siasa, Mtangazaji wa Mtangazaji wa Channel Ten, Cyprian Msiba amejitosa Jimbo la Mwibara.
Majina ya wagombea wateule wa viti vya ubunge ndani ya CCM yanatarajiwa kutangazwa Agosti 1 baada ya kukamilika kwa kura za maoni za wanachama wa chama hicho.

Cheka amlaumu meneja wake

BINGWA wa dunia wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na mashirikisho ya ICB na UBO Francis Cheka amemlaumu meneja wake Juma Ndambile kwa kushindwa kumuandalia mapambano. Aidha, amedai anajuta kuingia nae mkataba ambao "unamfunga" bila faida.
Akizungumza na Micharazo, Cheka alisema katika kipindi cha mwaka mmoja alioingia mkataba na meneja huyo, ameshakosa michezo kadhaa ikiwemo pambano la kimataifa lililokuwa lifanyike Uingereza pamoja na mengine ya ndani.
Cheka, alisema hajui ni kwa nini meneja huyo anashindwa kumsaidia katika hilo wakati anatambua kuishi kwake kunategemea ngumi.
"Kwa kweli huwa najuta kwa nini niliingia mkataba na meneja huyu kwa jinsi anavyonizibia riziki zangu wakati hanitafutii mapambano ya kuniwezesha kuingiza fedha na pia kupima kiwango changu," alisema Cheka.
Aliongeza kuwa hata suala la malipo ya mishahara aliyokubaliana naye imekuwa ikilegalega na kusisitiza huenda asiongeze mkataba mpya na meneja huyo mara mkataba wa sasa utakapomaliza Desemba mwaka huu.
Hata hivyo Ndambile alisema madai ya Cheka ni ya "kitoto" kwa sababu yeye ni meneja na sio promota.
Wakati akiingia mkataba na bondia huyo alimlipa mishahara ya muda wa miezi sita pamoja na fedha nyingine za ziada kwa ajili ya dharura, alisema Ndambile.
Aliasema alimlipa mishahara ya miezi sita ambayo ni shilingi milioni 1.2 na kumpa dola za kimarekani 1,500 za maandalizi ya michezo atakayoipata na hivyo kushangazwa na tuhuma kwamba anamzungumza kumlipa chake.
"Anachokisema ni utoto, mimi sio promota ni meneja wake na unajua kazi za umeneja, hivyo sijui anataka nimfanyie nini," alisema Ndambile.
"Pia amekuwa akipata mapambano kibao, lakini amekuwa akiyakwepa kiasi cha kuwakera hata wadhamini waliojitolea kwa ajili yake."
Alisema bado anaendelea kumtambua Cheka kama bondia wake na ataendelea kumsimamia atakapopata mapambano kama mkataba unavyojieleza.

Friday, July 23, 2010

Mtoto wa Balozi Chokala ajitosa kumrithi Kimbisa



MTOTO wa Balozi Mstaafu Patrick Chokala, Simon Mashiku Chokala (28), amejitokeza kuchukua fomu za udiwani katika Kata ya Kivukoni kwa lengo la kumrithi Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Adam Kimbisa aliyekuwa diwani wa kata hiyo aliyeamua kujiweka kando.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi mara baada ya kurejesha fomu ofisi ya CCM kata ya Kivukoni, Chokala alisema lengo la kutaka kuongoza kata hiyo yenye ofisi ya Rais (Ikulu), ni kutaka kubadilisha mazingira ya kata hiyo.
"Kama kijana nimeamua kuchukua fomu ya udiwani ili niweze kuiweka kata hii katika mazingira ya kisasa zaidi...Ikulu ipo katika kata hii hata wageni wengi wa nchi lazima waje hapa, hivyo nimejipanga kuiweka sawa," alisema Chokala.
Alisema pamoja na Meya Kimbisa kuifanyia makubwa kata hiyo, bado anahitaji kuifikisha mbali zaidi kwa sasa.
Chokala ambaye baba yake akiwa Balozi nchini Urusi mwaka 2005, alijitokeza kuwania urais kupitia CCM, lakini alijitoa katika kura za maoni.
Akizungumzia taaluma yake, Chokala alisema alimaliza elimu ya msingi katika Bunge jijini Dar na kisha kupata elimu ya sekondari nchini Kenya kabla ya kuchukua digrii ya biashara nchini Urusi.
Aidha, alichukua mafunzo ya kompyuta nchini Urusi wakati baba yake, Balozi Chokala akiiwakilisha nchi huko.
Chokala anachuana na wagombea wengine waliojitokeza kuwania kiti hicho akiwemo Mbunge wa Afrika Mashariki, Didas Masaburi.
Meya Kimbisa ameamua kuwaachia vijana kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo kwa madai anakwenda katika jimbo moja mkoani Dodoma kuwania Ubunge kupitia chama tawala.

Mwisho

Monday, July 19, 2010

Rage aupongeza uongozi mpya wa Yanga, amwagia sifa Nchunga



MWENYEKITI wa klabu ya soka ya Simba, Ismail Aden Rage, ameupongeza uongozi mpya wa watani zao Yanga na kumwagia sifa binafsi mwenyekiti mpya wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga, akidai ni mchapakazi na muadilifu.
Akizungumza na Micharazo kwa njia ya simu kutoka Tabora, Rage alisema amefurahishwa mno na umakini wa wanachama wa Yanga wa kumchagua Nchunga na Davis Mosha kuwa viongozi wao kwa madai ni watu makini na watakayoiletea mabadiliko klabu yao.
Rage alisema binafsi anamfahamu Nchunga kutokana na kuwahi kufanya naye kazi na kumtaja kama kiongozi mchapakazi na muadilifu.
"Nawapongeza wana Yanga kwa umakini wao wa kumchagua Lloyd Nchunga kuwa mwenyekiti wao, namfahamu ni muadilifu na mchapakazi na naamini ataendeleza mauhusiano mema baina ya klabu zetu mbili za Simba na Yanga," alisema Rage.
Rage alisema Simba na Yanga ni watani wa jadi na sio maadui na hivyo kuingia madarakani kwa Nchunga na Davis Mosha pamoja wengine waliochagulia watalichukulia jambo hilo hivyo na kujenga umoja na mshikamano kwa lengo la kuendeleza soka la Tanzania.
Nchunga, alichaguliwa kuwa mwenyekiti baada ya kuwabwaga wagombea wenzake watatu, Abeid Abeid, Mbaraka Igangula na Edger Chibula, huku Francis Kifukwe akijiondoa wakati wa kujinadi, wakati Mosha alishinda umakamu mwenyekiti kwa kumshinda Constatine Maligo,.
Uchaguzi huo wa Yanga ulifanyika juzi kwenye uwanja wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam, ambapo wagombea wengine nane kati ya 28 akiwemo Ally Mayay walichaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.

M

Rage achukua na kurudisha fomu Tabora Mjini





MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Tabora, Ismail Aden Rage, mapema leo asubuhi amekuwa mtu wa kwanza kuchukua na kurudisha fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza kwa simu kutoka Tabora, Rage, alisema alichukua fomu hiyo ya kuwania kiti hicho kinachoshikiliwa na Juma Siraju Kaboyoga majira ya saa 2;55 asubuhi na kuijaza kabla ya kuirudisha saa 5:30.
Rage alisema kuwa alikuwa ni mtu wa kwanza kujitokeza kuchukua fomu hiyo na pia amekuwa wa kwanza kuirudisha na matumaini yake ni kuibuka mshindi katika uteuzi wa CCM ili aweze kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31.
"Nimekuwa mtu wa kwanza kuchukua na kurudisha fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Tabora Mjini, nikichukua muda wa saa tatu kuchukua na kurudisha fomu hiyo na tumaini langu kama ilivyokuwa uchaguzi wa mwaka 2000, naamini nitashinda," alisema Rage.
Katika uchaguzi huo wa mwaka 2000, Rage aliwania uteuzi wa CCM katika jimbo hilo na kuibuka na ushindi wa kishindo, lakini utaratibu wa chama chake uliliengua jina lake na kumpitisha aliyekuwa mshindi wa pili, Henry Mgombelo aliyekuja kuibuka mshindi wa kiti hicho.
Rage alisema ni yake ya kujitosa katika jimbo hilo ni kuipeperusha bendera ya CCM dhidi ya wapinzani na pia kutaka ridhaa ya wananchi ili awatumikie kama ambavyo amekuwa akijitolea kwa hali na mali kwao hata kabla ya kuwa mbunge.
Alisema kwa vile katiba ya nchi na demokrasia ndani ya chama chake inamruhusu yeyote kuwania uongozi naye haoni sababu ya kujiweka nyuma na haswa kusukumwa kwake na nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.
Rage aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wazazi-Tabora mwaka 2004 na kukitetea kjiti chake tena mwaka jana, alisema anaamini chama chake kitampa ridhaa ya kuongoza na wananchi wa Tabora Mjini hawatamuangusha Oktoba mwaka huu.
Mtetezi wa kiti hicho cha Ubunge wa Jimbo la Tabora, Juma Kaboyoga, ndiye aliyekuwa mtu wa pili kuchukua fomu majira ya saa 5:40, ingawa haikufahamika kama aliwahi kurejesha au la.

Mwisho

Wawili waiacha bendi ya Kalunde



Wanamuziki wawili wa bendi ya Kalunde ambayo iko chini ya ukurugenzi wa Deo Mwanambilimbi, wameondoka kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanya shughuli za muziki
Akizungumza na Micharazo, mkurugeni huyo aliwataja wanamuziki hao kuwa ni mwimbaji Sarafina Mshindo aliyetimikia Marekani na Bonny Kamplobo (solo) ambaye amekwenda Thailand.
Mwanambilimbi alisema wanamuziki hao wameondoka baada ya kupata baraka za uongozi wa bendi na kwamba watakapomaliza mikataba yao huko waliko watarudi kuendelea kazi katika bendi hiyo.
"Sarafina anaweza kukaa Marekani kwa muda mrefu, kutokana na mkataba alioupata, lakini Kamplobo
atarudi baada ya mwezi mmoja ujao kwani atakuwa anamaliza mkataba," alisema Mwanambilimbi.
Aliongeza kuwa Kamplobo amechukuliwa na Kanku Kelly ambaye kwa sasa wanafanya naye kazi ya muziki huko Thailand na kwamba ana uhakika mkataba ukiisha atarudi Kalunde.
Alifafanua kuwa wanamuziki hao wameondoka wakati bendi hiyo ikikamilisha albamu ya kwanza ya
'Hilda' ambayo baadhi ya nyimbo zake ni 'Itumbangwewe', 'Fikiria' na 'Umenigusa Nikakugusa'.
"Hii ndio albamu ya kwanza ya bendi ya Kalunde ingawa watu wengi huwa wanadhani kwamba Uchona ni albamu ya bendi, lakini ukweli ni kwamba bendi ilianzishwa wakati albamu hii ipo tayari mitaani," alisema.
Mwanambilimbi alizitaja baadhi ya nyimbo za albamu hiyo ambazo pia zimesaidia kuiweka juu bendi hiyo kuwa ni 'Siwezi Sema', 'Mwana Mpotevu', 'Chekacheka', 'Masikitiko' na 'Anitha'.
Bendi hiyo imekuwa ikitoa burudani kila Ijumaa katika ukumbi wa New Africa Hotel na kisha humalizia shughuli za burudani Jumapili, katika ukumbi wa Giraffe Ocean View, Mbezi Beach.

Pentagon, Shikito hawarudi Levent

WAIMBAJI wawili nyota wa bendi ya Extra Bongo 'Next Level', Athanas Thomas 'Shikito' na Ramadhan Mhoza 'Pentagon', wamesema kuwa hawana mpango wa kurejea katika bendi yao ya zamani.
Kabla ya kujiunga na Extra Bongo, waimbaji hao walikuwa kwenye bendi ya Levet Musica ya mjini Morogoro ambayo mwenzao Suzuki waliyekuwa naye Extra Bongo ameamua kurejea Levent.
Waimbaji hao wamemwambia mkurugenzi wao Ally Choki kuwa hawawezi kurudi Levent kwa sababu wana imani na uongozi wa Extra Bongo na hamu ya kuona mchango wao unasaidia bendi hiyo kusonga mbele.
Kauli ya waimbaji hao vijana imekuja wakati Extra Bongo leo ikitarajiwa kutua mjiji Morogoro kwa ajili ya onyesho moja linalofanyika katika ukumbi wa Savoy mjini humo.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam, 'Pentagon' na 'Shikito' walisema kuwa sasa hawaoni kama kuna sababu ya wao kurudi tena Levent wakati mambo ndani ya Extra Bongo yakianza kunoga.
"Wakati mwingine kuhama kutoka bendi moja hadi nyingine ni kunamnyima mwanamuziki uzoefu, mimi na mwenzangu tumeamua kubaki Extra Bongo hadi kieleweke," alisema 'Shikito'.
Kwa upande wake 'Pentagon' alisema uongozi wa Extra Bongo hauna sababu ya kuwa na shaka juu yao kwamba huenda wakabaki Morogoro baada ya onyesho lao la leo.
Akizungumzia kauli hiyo, Ally Choki alisema yeye na viongozi wenzake wameipokea kwa moyo mkunjufu akisema kuwa safari ya mafanikio daima haikosi vikwazo wakati mwingine vya kuvunja moyo.
"Kwa kweli ni kauli ya kutia moyo, mimi pia nawaamini na kuwategemea sana wanamuziki wangu, natamani tuwe pamoja daima ili tufanikiwe kuivusha na kuifikisha mbali bendi yetu," alisema.

Dady, J-Mupa wote pamoja



WASANII wanaokuja juu kwenye muziki wa kizazi kipya ambao kila mmoja anatamba na kibao chake, Leonard Fidelis 'Dady' na Juma Mussa 'J-Mupa' wanajiandaa kutoa albamu ya pamoja ya nyimbo 16.
Wakizungumza na Micharazo, wasanii hao, walisema albamu hiyo ya pamoja itakuwa na mchanganyiko wa miondoko tofauti ya R&B, Ragga na Hip Hop.
Dady anayetamba na kibao cha 'Ni Gani', alisema ana uhakika hiyo ya pamoja itawaweka kwenye matawi ya juu, kutokana na ukweli kwamba muda mrefu wamekuwa wakijitahidi kutoka bila mafanikio.
Lakini sasa wameangukia mikononi mwa meneja wao mpya waliyemtaja kwa jina la Nassa na kwamba wana imani atasaidia kuhakikisha wanatoka upya na tena kwa kishindo.
"Baada ya kusota kitambo, hatimaye nimeachia kazi mpya iitwayo Ni Gani, huku nikiwa katika maandalizi ya kutoa albamu pamoja na mshirika wangu, J-Mupa, tutakayeshea nyimbo 16," alisema.
Dady alisema baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ya pamoja ni kibao chao cha pamoja walichokitoa mwaka 2006 cha 'Uvumilivu', 'Upungufu', 'Inatosha', 'Rudi', 'Ni Gani', 'Namsaka' na nyinginezo.
Kwa upande wake J Mupa, anayetamba na 'Mzuri Yupi', alisema albamu yao hiyo huenda ikaleta mapinduzi kutokana na jinsi wanavyoumiza kichwa kuiandaa.
"Ni albamu bab' kubwa muhimu ni wapenzi na mashabiki kutupa sapoti ya kutosha ili tufanikiwe kutoka na kuwapa burudani murua," alisema J-Mupa ambaye pia hujihusisha na masuala ya filamu.

Diamond yaja na Power 2010


Diamond Musica yaja na Power 2010

BENDI ya Diamond Musica 'Vijana Classic', imeachana na mipango ya maandalizi ya kuzindua albamu ya pili ya 'Mapenzi Kitu Gani', badala yake sasa imeelekeza nguvu katika kuandaa albamu ya tatu.
Mkurugenzi msaidizi wa bendi hiyo Perfect Kagisa, ameliambia Micharazo Mitupu kuwa kwa vile nyimbo zao albamu ya pili zilishasikika sana redioni, kwenye televisheni na katika kumbi mbalimbali, haina haja kuizindua.
"Tumeamua kuandaa albamu nyingine kwa sababu pia bendi yetu ilifanya mabadiliko kwa kuleta wanamuziki wapya, ndipo tukaona kuwa tuanze pia na vitu vipya," alisema Kagisa.
Kagisa alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo bendi hiyo imezikamilisha kwa ajili ya albamu ya tatu kuwa ni 'Power 2010', 'Kovu', 'Supu ya Kongolo' na 'Abdulkarim'.
Alisema wanamuziki wa bendi hiyo wanajiandaa kushuti video ya wimbo wa 'Power 2010' na kwamba kazi hiyo ya kushuti itafanyika wiki ijayo ili uanze kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya televisheni.
"Hii intro ya Diamond Musica, ndio maana tumeamua kuanza nayo na kisha nyimbo nyingine zitafuata katika mpangilio wetu wa kurekodi nyimbo za albamu ya tatu," alisema.
Diamond Musica ilitua jijini Dar es Salaam zaidi ya miaka mitatu iliyopita ikitokea Zimbabwe ikiwa na albamu ya kwanza iliyopewa jina la 'Swali' ambayo hata hivyo, haikuitambulisha vyema bendi hiyo.
Baada ya hapo wanamuziki walikuna vichwa na kuibuka na albamu ya pili ya 'Mapenzi Kitu Gani' na kuifanya uanze kukwea matawi ya juu, lakini hadi sasa albamu hiyo haijazinduliwa.
Hata hivyo, mkurugenzi huyo alisema kuwa licha ya kuandaa albamu nyingine, zile za albamu ya pili zitaendelea kupigwa kwenye kumbi za burudani na kuuzwa madukani kama kawaida.

Ndumbaro bado alia na Boban



WAKALA wa kimataifa wa wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, Damas Ndumbaro, amezidi kulia na kiungo Harun Moshi 'Boban' akidai mchezaji huyo ana desturi ya kutoheshimu mikataba kama alivyofanya kwa kuitosa klabu ya GIF ya Sweden.
Akihojiwa na kituo kimoja cha redio, Ndumbaro alisema pamoja na Boban kujitetea kuwa kilichomkimbiza Sweden ni kukiukwa kwa mkataba baina yake na klabu hiyo, lakini ukweli ni kwamba inaonekana suala la kutoheshimu ni kawaida ya kiungo huyo mahiri.
Ndumbaro alisema kwa kumbukumbu zake kutaka kuvunja mkataba dhidi ya GIF ni mara ya tatu kwa Boban, kwani alishawahi kufanya hivyo pia alipoenda kucheza soka la kulipwa Arabuni na pia Ethiopia.
"Hili sio jambo la bahati mbaya ni wazi ni Boban ana kawaida ya kutoheshimu mikataba kwani alishawahi kuvunja alipoenda Arabuni na kuiponza klabu yake ya Simba kulipa gharama za huvunjwaji huo wa mkataba huo, pia alifanya hivyo alipokuwa Ethiopia," alisema Ndumbaro.
Wakala huyo alisema dai kwamba labda Boban hakuuelewa mkataba huo wa miaka miwili si sahihi kwa vile alisimamiwa na mwakilishi wa Academy yake anayezungumza kiswahili na ndipo aliposaini na kuanza kuitumia klabu hiyo.
Ndumbaro alisema pengine yale mazoea na kuwakosa 'washkaji' zake wa vijiweni kama anavyokuwa nchini ndio kilichochangia kiungo huyo kurejea nchini ghafla, ingawa Boban alinukuliwa akisema kuwa malipo kiduchu ndicho kilichomrejesha Bongo.

Mwisho

Boban awagawa wadau wa soka nchini



UAMUZI wa kiungo nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Harun Moshi 'Boban' kuamua kurejea nchini kwa kuvunja mkataba na klabu yake ya GIF ya Sweden umewagawa wapenzi na wadau wa soka nchini baadhi wakimuunga mkono wengine wakimshangaa.
Baadhi ya wadau wamedai kitendo cha Boban kurejea ghafla nchini na kuiacha timu yake ya GIF ni kuonyesha jinsi wachezaji wa Kitanzania wavumilivu au kuwa tayari kucheza soka la kulipwa kama wenzao wa mataifa mengine.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya fedha ya klabu ya Simba Onesmo Wazir 'Ticotico'alisema hata kama kulikuwa na matatizo yaliyomkera Boban alipaswa kuzungumza na wakala wake kuona namna ya kutatua ikiwemo kuhamishwa klabu nyingine ya nje kuliko kurejea nchini.
"Unajua nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje huja kwa nadra sana na ilipaswa Boban kutumia nafasi hiyo kuangalia mbele katika kipaji chake badala ya kukimbilia kurejea nchini ili kuendelea kuchedza soka la sifa kwa klabu za Simba na Yanga," Ticotico alisema.
Hata hivyo Kocha Mkuu wa timu ya TMK United, Kennedy Mwaisabula, alisema binafsi haoni sababu ya Boban kulaumiwa, iwapo hakuona faida ya kuendelea kucheza soka la kulipwa katika klabu hiyo ya Sweden kutokana na kuonyesha hakuufahamu vema mkataba wake.
Mwaisabula alisema huenda wakala wake, Damas Ndumbaro hakuwa muwazi kwa kiungo huyo na yeye alipoona mambo yapo ovyo hakuona sababu ya kuendelea kuwepo huko, huku akisema uamuzi wa kurejea nchini kucheza soka sio wa ajabu kwani ni suala lake binafsi.
"Sioni sababu ya kumshutumu na kumdhalilisha Boban, kurudi kwake ni sahihi na hasa baada ya kukaa nae kwa saa zima na kuzungumza nae akieleza kila kitu na sio kweli kama kaikimbia baridi au kuwakumbuka washkaji zake," alisema Mwaisabula.
Kocha huyo aliyewahi kuzinoa Yanga na Bandari Mtwara, alisema huenda Boban ameona soka la Bongo linalipa kuliko huko Sweden kwani kabla hajaenda huko tayari alishakuwa na uwezo wa kiuchumi akimiliki nyumba na gari la kisasa.
Mwaisabula alisema pia Boban hatakuwa mchezaji wa kwanza kucheza soka la nyumbani badala ya nje ya nchi akiwataja, Tresot Mputu wa DR Congo, Mohammed Abutrika wa Misri aliodai pamoja na uwezo wa kisoka hawajahi kuwaza au kwenda kucheza soka la kulipwa licha ya kuwindwa na klabu mbalimbali maarufu za Ulaya.

Mwisho

Njoroge apigiwa ramli Jangwani



HATMA na uwepo wa beki wa kimataifa wa Yanga, Mkenya John Njoroge ndani ya klabu hiyo bado haieleweki, kutokana na uongozi wa klabu hiyo kudai unasubiri maamuzi ya kocha wao, Kostadin Papic
Njoroge aliyetua Yanga akitokea Tusker ya Kenya, kwenye usajili wa dirisha dogo msimu uliopita, amekuwa akitajwa ataachwa ili kutoa nafasi ya kusajiliwa kwa kipa Mserbia, Ivan Knezevic kutekeleza kanuni mpya ya usajili inayosisitizwa na Shirikisho la Soka nchini, TFF.
Kanuni hiyo ya usajili inaelekeza klabu zote za ligi kuu kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano, kitu ambacho ndicho kinachomchanganya kocha wa Yanga, kuamua nani abaki na nani aondoke klabuni hapo.
Msemaji wa Yanga, Louis Sendeu aliliambia Micharazo kuwa, pamoja na kwamba usajili wao unaelekea kukamilika vema, lakini hadi sasa haijafahamika nani na nani katika wachezaji wageni watakaokuwa kwenye kikosi hicho hadi kocha wao atakapoamua.
Sendeu alisema kutokana na hilo, ndio maana inakuwa vigumu kwao kuweka bayana kama itamuacha Njoroge au la ambaye ilielezwa awali angeungana na mastaa wengine wa kigeni waliotupiwa virago katika timu hiyo.
"Aisee ni vigumu kuweka bayana juu ya hatma ya Njoroge, tunasubiri suala hilo liamuliwe na kocha na nasisitiza kuwa lolote linaweza kutokea katika usajili huo mpya wa timu yetu ambao utatangazwa wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukamilika," alisema Sendeu.
Tayari uongozi wa Yanga umejinasibu kuwasainisha wachezaji wanne kutoka Ghana, kipa Yew Berko, mlinzi, Isaac Bokye, kiungo Ernest Boake na mshambuliaji Kenneth Asamoah, huku ikidaiwa kukaribia kumalizana na kipa Knezevic aliyetua wiki iliyopita kwa majaribio.
Iwapo kipa huyo atasajiliwa ili kuziba nafasi ya Obren Curcovic basi ni lazima kati ya Waghana wanne au Njoroge, mgeni pekee aliyebakishwa kikosi kilichopita mmojawao jina lake likatwe.
Yanga inayoendelea na mazoezi yao katika uwanja wa Uhuru, imedaiwa tayari imewanasa Nsa Job, Yahya Tumbo, George Minja, Chacha Marwa, Stephano Mwasika, Omega Sunday na Salum Telela kwa ajili ya kikosi kipya kuungana na nyota wengine walisalia msimu uliopita.

Mwisho

Diamond kutangaza utalii wa ndani



MSHINDI wa tuzo tatu za muziki nchini na Balozi wa Malaria, Naseeb Abdul 'Diamond' ameingia makubaliano ya mwaka mmoja na waandaaji wa shindano la Miss Utalii Tanzania kwa nia ya kuhamasisha utalii wa ndani sambamba na kuendelezxa vita dhidi ya malaria.
Habari zilizopatikana jijini na kuthibitishwa na Rais wa Miss Utalii, Gideon Chipungahelo, zinasema lengo la kamati hiyo kumshirikisha Diamond ni kuunganisha nguvu za sanaa ya muziki na urembo wa kitalii katika kuunga mkono juhudi za serikali za kukuza sekta ya utalii na utamaduni pia vita dhidi ya ugonjwa hatari wa malaria nchini na Africa kwa jumla.
Katika makubaliano ya awali kati ya wawili hao ni kwamba Diamond atafanya ziara ndefu maalum ya uhamasishaji itakayofahamika kwa jina la Diamond Tanzania Kamwambie Tour-Malaria Inaua Utalii ni Maisha'.
Pia msanii huyo aliyengara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Awards-2010, atatunga kibao maalum kwa ajili ya Miss Utalii Tanzania 2010 ambao ataimba na kurekodi pamoja na warembo wote wa Miss Utalii Tanzania wanaoshiriki fainali za mwaka 2010.
Kibao hicho ndicho kitakachotumika katika fainali za shindano hilo zitakazofanyika Septemba mwaka huu kwa kushirikisha jumla ya warembo 60 toka kanda na mikoa mbalimbali.
Washindi wa fainali hizo za Taifa watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia na ya kimataifa 2010 na 2011 yakiwemo ya Miss Heritage World 2011,Miss Tourism University World 2011,Miss Globe International 2010,Miss United Nation 2010,Miss Tourism World 2010 na Miss University africa 2011.
Rais wa Miss Utalii alithibitisha kuwepo kwa makubaliano hayo na Diamond, ingawa msanii huyo mwenyewe hakuweza kupatikana kufafanua juu ya suala hilo.

Mwisho

Mabingwa Ngumi EA kusakwa wiki ijayo





TIMU mbili za taifa za mchezo wa ngumi wa ridhaa zinatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya ngumi ya Mabingwa wa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati itakayofanyika jijini Arusha kuanzia Julai 26 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Mashanga Makore, alisema, Tanzania kama mwenyeji wa michuano hiyo itawakilishwa na timu mbili zilizopewa majina ya Tanzania A na B zitakazokuwa na wachezaji karibu 39.
Makore alisema timu ya taifa A itakuwa na wachezaji 19 wakati ile ya pili yaani Taifa B itakuwa na mabondia 20.
"Kutokana na uwenyeji wetu wa michuano ya ngumi ya Mabingwa wa Mabingwa wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, tunatarajiwa kuwakilishwa na timu mbili na tayari timu hizo zimeshaanza mazoezi tangu wiki iliyopiuta kujiandaa na michuano hiyo," alisema Makore.
Makore alisema mazoezi ya timu hizo yanaendelea chini ya makocha wazawa, ambao wanawasiliana kila mara na kocha mkuu wa timu hizo, Mcuba Geovanis Hultado ambaye yupo mapumziko nchini kwao.
Katibu huyo alisema imani ya BFT ni kuona Tanzania inafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo, ikizingatiwa kuwa wao ni wenyeji na pia itawakilishwa na timu nyingi tofauti na wapinzani wao.
Kuhusu maandalizi ya michuano hiyo, Makore alisema yanaendelea vema ikiwemo timu zote tano za Afika Mashariki kuthibitisha ambazo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.


Mwisho

Nukuu kali za kukumbukwa Kombe la Dunia 2010





JOHANNESBURG, Afrika Kusini
MAKOCHA na wachezaji wamekuwa wakizungumzwa mara kwa mara, si kwa sababu ya viwango vyao uwanjani pekee, bali pia kwa sababu ya kauli zao za nje ya uwanja. Zifuatazo ni nukuu kali za kukumbukwa zilizowahi kutolewa nao wakati wa michuano ya mwezi mmoja ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

Milovan Rajevac
* "Nyie watu, hebu tumieni akili. Yeye si shujaa, yeye ni muongo mkubwa. Ni mkono gani wa Mungu? Ule ni mkono wa shetani," kocha wa Ghana, Mserbia Milovan Rajevac, alisema kuhusy mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez, ambaye alizuia kwa mikono mpira uliokuwa ukivuka mstari wa goli katika dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza kwenye mechi yao ya robo fainali ya Kombe la Dunia.
‘Mkono wa shetani’ wa Suarez uliinyima Ghana nafasi ya kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Dunia.


Patrice Evra
* "Tunajihisi kama taifa dogo la mchezo wa soka na hili linaumiza. Hakuna cha kuelezea zaidi ya kusema kwamba hili ni balaa," nahodha wa Ufaransa, Patrice Evra, akielezea kwa uwazi hitimisho la kiwango chao kibovu katika fainali zilizomalizika za Kombe la Dunia 2010. Ufaransa, sio tu ilimaliza ikiwa mkiani katika kundi ambalo ilitarajiwa kuwa kinaea, lakini pia ilikumbwa na kashfa ya wachezaji wake kugomea mazoezi kufuatia kutimuliwa kikosini kwa mshambuliaji Nicolas Anelka.

Jean-Louis Valentin
* "Hawataki kufanya mazoezi, ni kashfa. Najiuzulu, naachoa ngazi kwenye shirikisho. Hapa sina zaidi cha kufanya. Narudi zangu Paris," Mkurugenzi wa timu ya Ufaransa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, Jean-Louis Valentin, alisema baada ya wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa kugomea mazoezi kufuatia kutimuliwa kikosini kwa Anelka.

Diego Maradona
* "Hii ilikuwa ni (kama) ngumi kutoka kwa Muhammad Ali. Sikuwa na nguvu yoyote ile. Siku niliyostaafu soka ingeweza kufanana na hii, lakini hii ya leo ni mbaya zaidi," Maradona alisema baada ya Argentina kupata kipigo kikali cha 4-0 kutoka kwa Ujerumani, kipigo kibaya zaidi kwao katika fainali za Kombe la Dunia tangu waliposhindiliwa kwa magoli 6-1 katika mechi ya michuano hiyo dhidi ya Czechoslovakia mwaka 1958.

Dunga
* "Siku zote tunatakiwa kushinda, lakini hata tunaposhinda, hawatufurahii kwa madai kwamba hatuchezi soka la kuvutia. Tukicheza soka la kuvutia, hawafurahi kwa sababu hatushindi kwa magoli mengi kama sita au saba hivi. Tukishinda kwa magoli sita au saba, wanaibuka tena na kusema wapinzani wetu ni dhaifu," alisema kocha wa Brazil, Dunga, akidai kwamba hata siku moja, vyombo vya habari huwa haviridhiki.

Gennaro Gattuso
* "Miaka minne iliyopita tuliheshimiwa kwa kuwa mabingwa, leo hii tunacheza hovyo kama mabeberu ya mbuzi vile," kiungo wa Italia, Gennaro Gattuso, alisema katika tathmini isiyo ya kawaida ya kujishutumu binafsi kwa kiwango cha hivyo kiichoonyeshwa na timu yao iliyokuwa ikitetea ubingwa wa fainali za Kombe la Dunia na kumaliza ikiwa mkiani katika Kundi lao.

Howard Webb
* "Anashindwa hata kuwaongoza watoto wake mwenyewe. Sijui anamudu vipi jukumu la kuongoza mchezo wa soka uwanjani," mke wa refa aliyechezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia, Howard Webb, alisema kabla ya mechi hiyo ya fainali iliyozikutanisha timu za mataifa ya Hispania na Uholanzi.

Cristiano Ronaldo
* "Maholi, kama gwiji mmoja wa soka alivyowahi kuniambia, huwa yanafuatana ... wakati mwingine, kadri unavyojaribu kuhaha ili ufunge, hayaji, na wakati yanapokuja, yanakuja mengi kwa wakati mmoja," alisema mchezaji wa bei mbaya zaidi duniani, Cristiano Ronaldo wa Ureno, kuelekea mechi yao ufunguzi ya hatua ya makundi ya Kombe la Dunia. Kiwango cha Ronaldo katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia kilikuwa cha hovyo, huku mshambuliaji huyo akifunga goli moja pekee.

Roger Milla
* "Kwa hakika hakuna anayeweza kucheza kama mimi! Mauno yangu yalikuwa ya kwanza, tena ya ubunifu kabisa. Unahitaji kunengua kiasili, kuchezesha nyonga. Yote ni kuhusiana na uasili wa mguso binafsi, na inatakiwa uwe na mshawasha kutoka moyoni, iwe ni kitu chako mwenyewe. Na hakika, vilevile unapaswa kufunga goli kwanza, usisahau jambo hilo!" alisema Roger Milla kuhusiana na ushangiliaji wake wa goli kwa kukata viuno.
Mauno ya Milla kwenye kibendera cha kona kila mara alipofunga goli yalikuwa maarufu kama magoli yake aliyoifungia Cameroon wakati nchi hiyo ilipotinga robo fainali za Kombe la Dunia mwaka 1990.

England v Ujerumani
* "England walianzisha soka, lakini Ujerumani wanashinda soka", ulisema utani wa zamani uliotumika wakati wa fainali za Kombe la Dunia kuelezea ushindi wa kishindo wa Ujerumani wa 4-1 dhidi ya mahasimu wao wa jadi katika hatua ya 16-Bora ya Kombe la Dunia.

Sepp Blatter
"Itakuwa ni upuuzi kutolifungua tena jalada la mapendekezo ya kutaka kutumiwa kwa teknolojia ya goli," alisema Rais wa FIFA, Sepp Blatter, baada ya makosa ya marefa kuwagharimu England na Mexico.


Felipe Melo
* "Mimi ni mzoefu wa kupenda. Watu wanaweza kufikiri kuwa kuwa nina sura mbaya, lakini ninapenda kutuma kadi na maua kwa mke wangu na ninapenda pia kutumiwa," beki mpambanaji wa Brazil, Felipe Melo, akisema kuwa yeye si mtu mbaya ‘kiivyo’.

Oscar Tabarez
* "Soka ni kama blanketi fupi, ama litatosha kukufunika kichwani au miguuni," kocha wa Uruguay, Oscar Tabarez, alisema kuhusiana na udhaifu wa mabeki wa Korea Kusini kabla ya mechi yao ya hatua ya mtoano ambayo Uruguay walishinda dhidi ya Waasia hao.

Carlos Marchena
* "Sawa, ni pweza," alisema beki wa Hispania, Carlos Marchena, katika muonekano wa kukasirika wakati alipotakiwa kuelezea maoni yake kuhusiana na utabiri wa pweza uliodai kwamba Hispania watashinda katika mechi yao ya fainali dhidi ya Uholanzi. Pweza huyo maarufu alitabiri kwa usahihi matokeo ya mechi zote saba za Ujerumani wakati wa fainali za Kombe la Dunia.

Felipe Melo
* "Najua kwamba wakati mwingine huwa napitiliza. Ni jambo ambalo huwa nalifikiria muda wote na ninajua kwamba hili ni jambo linalohofiwa na Wabrazili wote. Baba yangu siku zote amekuwa akinisisitiza kuhusu jambo hili, haachi kunikumbusha," alisema kiungo wa Brazili, Felipe Melo, kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia, kuhusiana na umuhimu wa yeye kuepuka kadi nyekundu. Hata hivyo, alitolewa uwanjani katika mechi yao ya robo fainali dhidi ya Uholanzi kwa kumkanyaga mpinzani wake.

Dunga
* "Wakati wakionyesha vipande vya picha za video za fainali za mwaka 1970, unachoona ni sehemu nzuri tu. Kuanzia mwaka mwaka 1958, wanaonyesha vipande vya sehemu nzuri tu, na kuanzia mwaka 1962, pia wanaonyesha vipande vya sehemu nzuri tu. Kama tukichukua vilevile vipande vya sehemu nzuri tu za timu ya Brazil ya sasa, mashabiki wataamini kwamba ndio timu bora kabisa. Lakini leo hii, wanaonyesha vipande vingi vya picha za matukio mabaya kama ilivyo kwa matukio mazuri." Dunga akilalamikia kumbukumbu za timu ya Brazil ya mwaka 1970 na kudai kwamba haikuwa timu nmzuri sana kama inavyoonyeshwa kwenye televisheni.


Marcelo Bielsa
* "Wote tunajifunza kutokana na makosa tunayofanya na kutoka kwenye makosa tuliyoyashuhudia yakifanywa na watu wengine, na kujaribu kuepuka kuyarudia. Huu ni mchakato wa kufanya makosa na kuepuka kuyarudia tena, kuona namna wengine wanavyofanya makosa ili kuyaepuka makosa kama hayo, ni mchakato ambao hausimami, na hauwezi kupimika." kocha asiyetabirika wa Chile, Marcelo Bielsa, akizungumzia umuhimu wa kujifunza kutokana na makosa.
--------------