STRIKA

USILIKOSE

Tuesday, March 11, 2014
Mawakala wa wachezaji kutahiniwa April 3
MTIHANI
kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa
na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Aprili 3
mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (FIFA).
Kwa
wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni
mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani
huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya mtihani huo ni
maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF.
Tanzania
ina mawakala watatu tu wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala
hao ni Ally Saleh, John Ndumbaro na Mehdi Remtulla.
Babi apewa unahodha Malaysia
![]() |
Babi (kushoto-mbele) akiwa na kitambaa cha unahodha |
Babi alipewa unahodha huo wiki iliyopita alipoingoza timu hiyo katika mchezo dhidi ya 'vibonde' wa ligi hiyo Perlis na kupoteza mchezo huo wa ugenini kwa kulala mabao 2-1.
Kiungo huyo wa zamani wa Taifa Stars, aliiambia MICHARAZO kuwa nidhamu na kiwango bora cha soka alichokionyesha tangu atue katika timu hiyo ndicho kilichofanya apewe cheo hicho na kusema anamshukuru Mungu.
"Ninajisikia fahari kupewa cheo hicho baada ya viongozi na wachezaji kuridhika na uwezo wangu uwanjani na nidhamu kubwa niliyonayo ni furaha kwangu hasa ikizingatiwa nipo ughaibuni," alisema Babi.
Kuhusu mechi yao ya Ijumaa, Babi alisema walifungwa kimchezo katika pambano hilo la ugenini lililochezwa kwenye uwanja wa Darul Aman mjini Alor Setar, likiwa pambano lao la tatu mfululizo kupoteza. Wako katika nafasi ya tisa wakiwa na pointi nne tu.
"Tumefungwa kimchezo na kwa muda kulikuwa na mgogoro wa kiuongozi ambao kwa sasa umeisha na tunajipanga kwa mechi yetu ya Ijumaa hii tutakayocheza nyumbani," alisema Babi, nahodha wa zamani wa Yanga.
UiTM itaumana na DRB-Hicom katika mechi ambayo Babi ametamba kwamba timu yake wataibuka na ushindi katika mechi hiyo itakayochezwa uwanja wa Mini UiTM, katika mji wa Shan Alam.
Babi aliyewahi kuzichezea pia Mtibwa Sugar, Azam na KMKM kabla ya kutimkia Malaysia alikosaini mkataba wa mwaka mmoja, alisema ligi ya nchi hiyo ni ngumu na imejaa ushindani tofauti na alivyofikiria mwanzoni.
Ajali yachukua roho ya mmoja wengine wajeruhiwa
![]() |
Gari la Hood likiwa limepinduka na majeruhi wakipigania uhai wao |
![]() |
Abiria wakiwa hawaamini kama wamenusurika kifo |
AJALI zimeendelea kutikisa Tanzania, baada ya Basi
la Hood linalofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Mbeya, namba za usajili
T.488 AXV aina ya Scania kupata ajali mbaya leo asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na abiria wengine karibu 20 kujeruhiwa.
Ajali
hiyo imetokea majira ya saa tatu katika, barabara ya Same - Mwanga, Kijiji cha Kiverenge wilaya ya
Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo taarifa za awali zinasema kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi ya
mbele.
Kamanda
wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
ambapo amesema katika ajali hiyo alifariki Abiria mmoja aliyemtaja kwa jina la
Joshua Likumbia, Raia wa Kenya, ambaye alikuwa akisafiri kuelekea jijini Mbeya.
Kamanda
Boaz amesema majeruhi katika ajali hiyo ambao ni 16, akiwemo dereva wa Basi, Fadhili
Hashim wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na Hospitali ya Rufaa mkoani
Kilimanjaro, KCMC.
Kamanda
Boaz ameendelea kufafanua kuwa majeruhi hao nane wamelazwa Same huku wengine 8
wakikimbizwa mjini Moshi katika hospitali ya KCMC kutokana na hali zao kuwa
mbaya ambapo watatu kati yao wakia wamelazwa katika chumba cha wagonjwa
mahututi.
Ratiba ya VPL yapanguliwa tena
Na Boniface Wambura
BODI ya
Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeifanyia marekebisho ratiba ya Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) ambapo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya
Aprili 27 mwaka huu.
Marekebisho
hayo yamefanyika ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa, Taifa Stars, kujiandaa kwa mechi za mchujo la Kombe la Afrika 2015 ambapo itacheza
raundi ya awali Mei mwaka huu.
Kutokana
na marekebisho hayo, Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa Taifa) Machi
26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka huu
kwenye uwanja huo huo ni Yanga na Azam.
Machi 15
mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam Complex), na
Mtibwa Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza Machi
26 mwaka huu Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera
Sugar (Taifa).
Raundi ya
22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera vs Prisons
(Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga (Ali
Hassan Mwinyi). Machi 23 mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo
vs Mtibwa (Mkwakwani), Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs
Oljoro (Azam Complex).
Machi 29
mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti vs Oljoro (Azam
Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine), Kagera vs
Ruvu Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs Rhino
(Azam Complex), Azam vs Simba (Taifa), na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya
24 inaanza Aprili 5 mwaka huu kwa Kagera vs Simba (Kaitaba), Ashanti vs
Mbeya City (Azam Complex). Aprili 6 mwaka huu ni Coastal vs Mgambo
(Mkwakwani), Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Rhino vs
Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi), Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs
JKT Ruvu (Taifa).
Aprili 12
mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting (Mabatini),
Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine). Aprili 13
mwaka huu ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa),
Mbeya City vs Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri
Abeid).
Raundi ya
26 ni Aprili 19 mwaka huu kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali Hassan
Mwinyi), Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri,
Morogoro), JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh
Kaluta Amri Abeid), Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba
(Taifa).
Monday, March 10, 2014
Mpiga Drums Extra Bongo awashtua Wajumbe Bunge la Katiba
![]() |
Mpogoro Machine akikaanga chipa mazoezi ya Extra Bongo |
Mwanamuziki huyo alisema malumbano na muda unaopotezwa na wajumbe hao kwenye bunge hilo mjini Dodoma ni kutowatendea haki wananchi wanaosubiri kuona wanawasaidia kupata Katiba Mpya.
Mpogoro alisema anashindwa kufahamu iweje tangu wajumbe hao wakutane Dodoma karibu mwezi mzima unafika sasa wameshindwa kupata muafaka ili mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba uanze.
Alisema ni lazima wajumbe hao watambue kuwa wameteuliwa na Rais na kutumwa na wananchi kuhakikisha Tanzania inapata Katiba Mpya yenye kukidhi matakwa ya watanzania hivyo wafanye kazi yao.
"Malumbano yanayoendelea kwenye Bunge kiasi cha kushindwa kufanya kile walichotumwa kwa hakika ni kutomtendea haki Rais na wananchi waliowatuma kwenda kuipatia nchi katiba mpya,' alisema.
Kumekuwa na malumbano ya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo na kusababisha kila mara kuahirishwa kuanza kazi inayosubiriwa kwa hamu na watanzania kitu ambacho kimezua lawama kila kona ya nchi.
TFF yaiomba radhi serikali, ila yaapa kufa na 'wahuni' Taifa

TFF imeiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 1, mwaka huu. Imesema uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya Sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.
“Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine,”imesema taarifa ya TFF.
Kwa mujibu wa Serikali, viti 10 viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao na TFF imekubali kubeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa na ndiyo walioomba idhini ya kutumika uwanja huo kwenye mechi hiyo.
“Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu,”.
“Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi,”imesema taarifa ya TFF.
Japanese anogewa ughaibuni
![]() |
Japanese kikazi zaidi |
![]() |
Amina Ngaluma 'Japanese' akifurahia maisha Ughaibuni |
Akizungumza na MICHARAZO kutoka Thailand walipoweka maskani yao ya kudumu, Ngaluma alisema haoni ya sababu ya kurudi nyumbani kwa sasa wakati maisha yamemnyookea ughaibuni akiwa na bendi hiyo inayopiga muziki asilia na iliyoweka maskani ya kudumu nchini humo.
"Kwa kweli sifikirii kurudi nyumbani leo wala kesho, hii ni kutokana na kuona tofauti kubwa ya kuthaminika kwa wanamuziki kati ya huko na hapa tulipo tukiendeleza makamuzi na bendi ya Jambo Survivors," alisema Japanese aliyetamba na wimbo wa 'Mgumba II'.
Ngaluma alisema muziki wa Tanzania umeshindwa kuwanufaisha wanamuziki wake kutokana na kuwapo kwa unyonyaji kuanzia kwa wamiliki wa bendi mpaka wadau wanaousimamia kama wasambazaji na hata wananchi wanaowaibia wasanii kazi zao bila kujali wala kuwahurumia wanavyovuja jasho lao.
Noma! Ronaldo ndiye mchezaji tajiri duniani
NYOTA wa Ureno anayeichezea Real Madrid, Cristiano Ronaldo ndiye mwanasoka tajiri kuliko wote duniani.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Goal.com, nahodha huyo watimu ya taifa ya Ureno ndiye kinara katika
orodha hiyo iliyotangazwa leo.
Mkali huyo amerithi nafasi hiyo ya kwanza
iliyokuwa ikishikiliwa na David Beckham kwa muda mrefu kabla hajastaafu soka msimu uliopita.
Ronaldo ambaye alisaini mkataba mnono zaidi na Real
Madrid miezi kadhaa iliyopita amempita mshindani wake Lionel Messi na
mwanasoka anayelipwa zaidi kimshahara Wayne Rooney.
Samuel Eto'o ndiye Mwaafrika pekee aliyeingia kwenye listi ya wanasoka matajiri zaidi duniani.
Hii ndiyo orodha kamili:
1. Cristiano Ronaldo £122m
2. Lionel Messi £120.5m
3. Samuel Eto'o £70m
4. Wayne Rooney £69m
5. Kaka £67.5m
6. The Neymar family £66m
7. Ronaldinho £64m
8. Zlatan Ibrahimovic £57m
9. Gianluigi Buffon £52m
10.Thierry Henry £47m
2. Lionel Messi £120.5m
3. Samuel Eto'o £70m
4. Wayne Rooney £69m
5. Kaka £67.5m
6. The Neymar family £66m
7. Ronaldinho £64m
8. Zlatan Ibrahimovic £57m
9. Gianluigi Buffon £52m
10.Thierry Henry £47m
SOURCE: Goal.
Ronaldo azidi kuipaisha Real Madrid
![]() |
Ronaldo akiwajibika uwanjani |
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo usiku wa jana alisaidia timu yake kuzidi kujichimbia kileleni baada ya kufunga moja ya mabao yaliyoisaidia Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Levante.
Real Madrid imefikisha pointi 67 na kuwakimbia Atletico Madrid wenye pointi 64 timu zote zikiwa zimecheza mechi 29.
Ronaldo
alifunga bao hilo katika dakika ya 11 akiunganisha kona ya Angel Di Maria kabla ya kumtengenezea pande zote Marcelo aliyefunga bao la pili.
Bao la tatu la vinara hao lilitiwa kimiani na Karabellas dakika ya 81.
Katika mchezo huo Levente walipata pigo baada ya David Navarro kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumchezea vibaya Ronaldo katika dakika ya 49.
Barcelona ambayo juzi ilikandikwa na vibonde Real Valledolid ipo katia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 63 na kutishia amani utetezi wa taji lake la La Liga msimu huu.
Barcelona ambayo juzi ilikandikwa na vibonde Real Valledolid ipo katia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 63 na kutishia amani utetezi wa taji lake la La Liga msimu huu.
Maskini Yanga yakwama Misri, matuta yawatoa Afrika
LICHA ya kutolewa, lakini Yanga inastahili pongezi kwa kupigana kiume mbele ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Al Ahly baada ya kung'olewa kwa mikwaju ya penati katika pambano la marudiano lililochezwa usiku wa jana.
Yanga ilipambana kwa dakika 90 na kujikuta wakilala kwa bao 1-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1 na hivyo kuingia kwenye hatua ya upigaji wa penati ambapo ilionekana dhahiri walikuwa wakielekea kufuzu baada ya Deo Munishi Dida kudaka penati mbili za Wamisri.
Dida aliyeonyesha ushupavu mkubwa alidaka penati za Saed Mowaeb na Hossan Ashour huku zile za Abdalllah Said, Gedo, Mahmoud Trezeguet na Mohamed Nagieb zilimpita.
Hata hivyo Oscar Joshua alikosa penati naye na baadaye Bahanuzi aliyekuwa akimalizia mikwaju ya penati tano tano, alipaisha mkwaju wake wakati wachezaji wenzake wakijiandaa kushangilia kuwavua ubingwa Al Ahly na kuongezwa penati moja moja.
Katika hatua hiyo Mbuyi Twite alilizamisha jahazi la Yanga baada ya kukosa mkwaju wake na kuwafanya mabingwa watetezi hao kufuzu hatua ya pili na kutarajia kukutana na waarabu wenzao kutola Libya, Al Ahli Benghazi.
Kwa wastani Yanga ilikuwa imejiandaa kuweka rekodi kwa soka la uhakika na umakini mkubwa iliyooonyesdha katika mchezo huo kwa kuwabana wenyeji wao kwenye uwanja wa Border Guard mjini Alexandria.
Kipindi cha kwanza kiliisha kwa sare ya kutofungana kabla ya wenyeji kupata bao dakika za jioni baada ya mabeki wa Yanga kujichanganya kuokoa mpira uliokwamishwa na Sayed Moawad. dakika ya 71.
Ndipo ikaja hatua ya kupigiana penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa matokeo hayo yaliyofanya timu hizo kuwa nguvu sawa kwani Yanga ilishinda bao 1-0 nyumbani wiki iliyopita na zikaja penati na Yanga wakapata penati zao kupitia nahodha Nadir Cannavaro, Emmanuel Okwi na Didier Kavumbagu.
Kung'olewa kwa Yanga kumehitimisha safari ya timu za Tanzania kwenye michuano ya kimataifa baada ya awali Azam, KMKM na Chuoni kung'oka raundi ya awali katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Sunday, March 9, 2014
Manchester City yatupwa nje FA Cup
![]() |
City wakitunguliwa bao |
City ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Etihad, imejikuta ikinyukwa mabao 2-1 na Wigan na kushindwa kukutana na Arsenal kama wengi walivyokuwa wakitarajia na kuona ndoto za kocha huyo kutoa Chile zikitimia.
Mabao ya Jord Gomes kwa mkwaju wa penati dakika ya 27 na jingine la pili la dakika ya 47 lililofungwa na James Perch yalitosha kuizima wababe hao wa Manchester City licha ya Samir Nasir kufunga bao dakika ya 68 lililoshindwa kuisaidia timu yake.
Kwa ushindi huo sasa, Wigan inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza itaumana na Arsenal kwenye mechi ya Nusu Fainali, huku nusu fainali nyingine ikizikutanisha Hull City dhidi ya Sheffield United.
Ikulu yakana Rais kumtembelea mfungwa, yamtembelea Mkambara na wengine

Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtangazaji wa kituo cha
Televisheni cha Channel Ten na Magic Radio FM Bwana Salum Mkambala
aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa muhimbili
baada ya kuapata ajali na kujeruhiwa vibaya wiki iliyopita

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akijulia hali Ofisa wa Habari tume ya Uchaguzi Bi.Margareth Chambiri
aliyelazwa katika Tasisi ya MOI Hospitali ya Taifa Muhimbili.Bi.Chambiri
aliwahi kufanya kazi katika Televisheni ya Taifa TBC.Picha na Freddy
Maro-IKULU
Nusu Fainali FA ni Hull City vs Sheffield Utd, Arsenal vs Wigan (?)
![]() |
Kwa mujibu wa droo iliyotangazwa muda mfupi uliopita mechi za hatua hiyo zitacheza kati ya Aprili 12 na 13 kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
Tumaini ya mashabiki wengi kutaka kuona nusu fainali ya aina yake kati ya Arsenal na Manchester City ni kama inapotea kwani mpaka sasa City wakiwa nyumbani wameshanyukwa mabao 2-1 na Wigan japo imesalia dakika 10 pambano hilo kumalizika, Samir Nasir alifunga bao la Man City baada ya muda mwingi Wigan kuongoza 2-0.
Iwapo City itashindwa kupenya hatua hiyo itafanya ndoto za kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini wa kuiwezesha timu hiyo kutwaa mataji manne msimu huu baada ya awali kunyakua Kombe la Ligi (Capital One) na Jumatano ana kibarua kigumu mbele ya Barcelona kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya awali kulala 2-0 nyumbani wiki mbili zilizopita.
CS Sfaxien, Cotonsport, AS Vita nazo zafuzu Afrika, Yanga ipo dimbani wakiwakimbiza Ahly Niyonzima nje
![]() |
CS Sfaxien waliyofuzu hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika |
![]() |
AS Vita ya DR Congo |
Katika mechi yao ya kwanza mjini Addis Ababa, Dedebit ilifungwa mabao 2-1.
Nayo timu ya Coton Spors ilifungwa bao 1-0 ugenini wiki iliyopita nchini Burundi leo ikiwa nyumbani imeifanyia mauaji ya kutisha Flambeau de l'Est kwa kuifumua mabao 5-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 6-1.
Mchezo mwingine uliochezwa DR Congo imeshuhudia AS Vita ikifuata nyayo za ndugu zao TP Mazembe kusonga mbele baada ya kuiondosha patupu Dyanamos ya Zambia kwa kuilaza bao 1-0.
Dynamos iliyolazimishwa suluhu katika mechi yao ya nyumbani ilishindwa kufurukuta kwa wenyeji hao na kujikuta wakilala 1-0 ugenini.
Yanga kwa sasa ipo dimba la Alexandria ikiumana na Al Ahly ambapo mpaka sasa hakuna timu iliyoona lango la wenzake na timu zimeenda mapumziko.
Kikosi cha Yanga kipo hivi;
Deo Munishi, Mbuyi Twite, Oscar Joshua, Nadir Cannavaro, Kelvin Yondani, Frank Dumayo, Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi.
Juventus haishikiki Italia, Inter nayo yang'ara
![]() |
Kwadwo Asamoah akiifungia Juventus bao pekee leo dhidi ya Fiorentina |
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Italia (Seria A) Juventus imeendelea kutamba kwenye ligi hiyo baada ya jioni hii kuifumua Fiorentina kwa kuilaza bao 1-0, huku Inter Milan nayo ikichomoza na ushindi kama huo dhidi ya Torino.
Bao la dakika ya 42 lililofungwa na Mghana, Kwadwo Asamoah lilitosha kuwapa pointi tatu 'kibibi' cha Turin na kuongeza pengo la pointi na timu inayowafuata nyuma yao, Roma kwa pointi 14 ambayo itashuka .
Juve imefikisha pointi 72 wakati Roma itakayoshuka dimbani baadaye kuumana na Napoli ikiwa na pointi 58.
Katika mechi nyingine Inter Milan iliilaza Torino kwa 1-0, huku Lazio ikilala nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya Atalanta, Chievo ikishinda mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Genoa, Parma ikiifumua Hellas Verona mwaka 2-0 na Sampdoria ikishinda nyumbanio mabao 4-2 dhidi ya Livorno na Bologna na Sassuolo zikitoka suluhu.
Hull City, Sheffield Utd zaifuata Arsenal Nusu Fainali FA
![]() |
Hull City na Sunderland walipoumana leo |
![]() |
Huree tumefuzu mmoja wa wafungaji wa Sheffield Unitd akishangilia bao lake lililoivusha timu hiyo ya daraja la chini kutinga hatua hiyo ya Nusu Fainali tangu Wycombe Wanderers kufanya hivyo mwaka 2001. |
Katika mechi ya kwanza Ryan Flynn aliifungia Sheffeld bao la kuongoza dakika ya 65 kabla ya dakika mbili baadaye John Brayford aliongeza la pili na kufuzu hatua hiyo baada ya miaka mingi, huku katika mechi ya pili Sunderland ilibanwa na wenyeji wao na kukubali kipigo hicho cha aibu na kuiondosha patupu.
Mabao ya Curts Davies katika dakika ya 68 kabla ya Meyler akaongeza la pili dakika ya 72 na Fryatt akafunga la tatu na kuihakikishia Hull City ikifuzu Nusu Fainali.
Mechi nyingine ya kuhitimisha robo fainali za michuano hiyo, Manchester City wenyewe wapo njiani sasa wakiumana na Wigan Athletic ambao wameshatangulia kupata mabao 2-0 ikiwa ni kipindi cha pili.
JKT Ruvu yaifumua Mtibwa Sugar Chamazi
JKT Ruvu walioifumua Mtibwa leo |
Mtibwa sugar iliyopoteza matumaini ya kuwnaia ubingwa na sasa kupigana kubakia katika ligi |
Mabingwa hao wa zamani wa Tanzania, walishindwa kuwabana vijana wa Fred Felix Minziro na kupoteza mchezo huo ulioufanya uongozi wa Mtibwa kukiri kwamba mbio za ubingwa kwao ndiyo basi tena.
Nahodha Husseni Bunu aliifungia JKT Ruvu bao dakika ya 34 bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kusawazisha bao kupitia kiungo mkongwe, Vincent Barnabas katika dakika ya 70 kabla ya dakika tano baadaye Amos Mgisa kumaliza udhia kwa kuipatia JKT bao la pili./
Kwa ushindi huo JKT Ruvu imefanikiwa kufikisha pointi 25 licha ya kusalia kwenye nafasi ya 9 ikiwa nyuma ya Mtibwa waliolingana nao pointi ila wanatofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Al Ahli Benghazi yafuzu raundi ya pili Afrika
* Ndiyo ikayocheza na Yanga au Al Ahly
* TP Mazembe yapenya kwa kishindo
* Raja Casablanca yatolewa kwa matuta

AL Ahli Benghazi ya Libya jioni hii imeifumua Berekum Chelsea ya Ghana kwa mabao 2-0 na kufuzu raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikisubiri mshindi kati ya Yanga ya Tanzania au Al Ahly ya Misri.
Ikiwa uwanja wa nyumbani Benghazi ilipata ushindi huo muhimu na kufanikiwa kufuzu raundi ya pili kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya wiki iliyopita kulazimisha sare ya 1-1 ugenini.
Sasa timu hiyo itataka kujua itaumana na nani kati ya Yanga iliyopo ugenini kuwakabili mabingwa watetezi wa taji hili Al Ahly katika mechi inaytotarajiwa kucheza muda mfupi ujao mjini Alexandria, Misri.
Katika mechi ya kwanza Yanga ikiwa nyumbani jijini Dar es Salaam iliifumua Al Ahly kwa bao 1-0 na hivyo usiku huu itahitajika kupigania sare ya aina yoyote kuingia hatua hiyo ya pili na kukumbana na mwarabu mwingine.
Nao mabingwa wa zamani wa Afrika, TP Mazembe ikiwa nyumbani imepata ushindi wa kishindo baada ya kuicharaza Les Astres ya Cameroon mabao 3-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 ugenini na wapinzani wao hao.
Nao vijogoo wa Morocco Raja Casablanca pamoja na kushinda nyumbani bao 1-0 dhidi ya Horoya ya Guinea imejikuta iking'oa raundi ya kwanza kwa kunyukwa kwa mikwaju ya penati 5-4.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Conakry, Raja walifungwa bao 1-0 na hivyo ushindi wa leo uliifanya kuwa sare ya 1-1 na kulazimishwa kupigiana penati na kushindwa na wapinzani wao.

AFC Leopards yatupwa nje Kombe la Shirikisho Afrika
![]() |
AFC Leopards |
KLABU kongwe ya Kenya, AFC Leopards jioni hii imeyaaga mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Supersport ya Afrika Kusini.
Katika mechi hiyo ya marudiano iliyochezwa uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi Leopards imejikuta ikikwama kusonga mbele kwa Wasauzi baada ya wiki iliyopita kukubali kipigo cha mabao 2-0 ugenini na hivyo kung'olewa mashindanoni kwa jumla ya magoli 4-2.
Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao maara baada ya kipindi cha pili kuanza baada ya kufanikiwa kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nguvu sawa ya bila kufungana.
Bao hilo lilifungwa na dakika ya 48 kupitia James Situma, lakini wageni walisawazisha dakika ya 54 kupitia Thuso Phala kabla Supersport kuongeza la pili kupitia kwa Sameehg Doutie katika dakika ya 79 na kuwafanya Leopards kucharuka ili kuepuka kipigo cha nyumbani.
Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 90 wakati Allan Wanga kulisawazisha bao hilo na kufanya matokeo kuwa 2-2, matokeo ambayo hata hivyo hayakuwasaidia Wabaluya kusonga mbele dhidi ya wageni.
Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo Bizertin ya Tunisia nayo ilifuzu raundi ya pili baada ya kuinyuka Desportivo Huila ya Angola kwa mabao 2-0.
Watunisia walikuwa nyumbani na ushindi huo umeifanya kutinga raundi nyingine kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya wiki iliyopita kushinda 1-0 ugenini nchini Angola.
Simba yabanwa Mbeya, Prisons yaendeleza rekodi
![]() |
Prisons |
Simba |
Simba ambayo ilikuwa ikihitaji ushindi ili angalau kuendelea kuwepo kwenye mbio za kuwania ubingwa, ilishindwa kufurukuta katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine-Mbeya.
Ikiwa na nyota wake wote wakiwamo waliokuwa na timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa Namibia kucheza mechi ya kirafiki na wenyeji wao, Simba haikuweka kuvunja mwiko wa Maafande hao wa Magereza ambao hawajapoteza mchezo wowote katika duru hili la pili la ligi.
Kwa sare hiyo Simba imeendelea kujiimarisha kwenye nafasi ya nne kwa kujikusanyia pointi 36 nyuma ya Yanga yenye pointi 38 ila ikiwa na michezo mitatu mkononi.
Prisons yenyewe imejiongeza pointi moja na kufikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi ya 20.
Taifa Stars sasa kutumia jezi za Adidas
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas
kupitia msaada wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya
michezo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema kwamba kufuatia makubaliano hayo TFF ilipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars), zikiwemo jezi ambazo zilianza kutumika kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek.
Amesema
vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo
utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema kwamba kufuatia makubaliano hayo TFF ilipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars), zikiwemo jezi ambazo zilianza kutumika kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek.
“TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini,”amesema Malinzi.
Mwezi uliopita, Malinzi alikwenda makao makuu ya CAF, Cairo nchini Misri kujitambulisha baada ya kurithi kiti cha Leodegar Tenga Desemba mwaka jana na akiwa huko alikutana na Rais wa CAF, Issa Hayatou aliyeahidi kumpa sapoti kubwa.
Yanga tupeni raha Watanzania, funga Ahly leo
ROHO zikiwadunda baadhi ya mashabiki wa kandanda nchini kuhuisiana na pambano la marudiano baina ya Yanga na Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kocha msaidizi wa mabingwa hao watetezi wa Tanzania, Charles Mkwasa amesisitiza timu yao haitapaki basi badala yake itashambulia mwanzo-mwisho.
Yanga inavaana na Alhy wiki moja baada ya kuwadonyoa bao 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo katika mechi ya leo Jangwani wanahitaji sare yoyote ili kufuzu hatua ya 16 Bora.
Mechi hiyo inachezwa kwenye uwanja wa Mexx, mjini Alexandria badala ya Cairo kama ilivyokuwa ikifahamika awali, kitu kinachoelezwa kama hila za wapinzani wao kutaka kuwachanganya akili kabla ya mechi hiyo itakayochezwa majina ya saa 2 usiku kwa hapa kwetu na itaonyeshwa live kupitia mtandao wa Yanga.
Kocha Msidizi wa Yanga, Mkwasa alisema mchezo wa leo utakuwa mgumu kutokana na Yanga kuwafunga wenyeji wao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam na kudai itakuwa kosa kama Yanga itaingia uwanjani na mkakati wa kujihami.
Badala yake kocha huyo alisema Yanga itashambulia huku ikiwa makini kwenye ulinzi, ili kuhakikisha inailiza tena Ahly nyumbani kwao na kuweka rekodi Afrika.
"Naamini hawa jamaa watacheza mchezo wa kutushambulia ili kupata goli la mapema," alisema Mkwasa.
"Tunalifahamu hilo lakini ili kuwapa wakati mgumu ni lazima tumiliki mpira na kuwashambulia muda wote na kutowapa nafasi ya kupanga mashambulizi."
Aidha, Mkwasa alisema katika mikanda ya hivi karibuni waliyoiangalia Al Ahly imeonekana kuwa inatumia zaidi mawinga na mabeki wa pembeni kupiga krosi katika mashambulizi yake lakini wamejipanga kudhibiti mchezo huo.
Mkwasa alisema kila mchezaji wa Yanga yupo kwenye hali nzuri kimchezo na wapo tayari kwa mpambano wa leo.
"Unajua ushindi wa nyumbani umewapa wachezaji hali ya kujiamini," alisema. "Wapo tayari kwa mchezo na kwa kweli kama tutafanikiwa kufanya tulichokipanga kwenye mazoezi yetu, ni wazi tutasonga mbele kwenye mashindano haya."
Akizungumzia kikosi cha leo, Mkwasa alisema kupanga ni kazi ya kocha mkuu, Hans van Pluijm. Hata hivyo alisema hakitabadilika sana kulinganisha na mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita.
Kwenye mchezo huo ambao goli pekee lilifungwa na naodha Nadir Haroub 'Canavaro' kikosi kilichoanza kilikuwa:
Deogratias Munishi 'Dida', Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Canavaro, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngasa, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi.
Katika mchezo wa leo, Yanga ina anasa ya hata kutofungwa si zaidi ya bao 1-0 na ikasonga mbele angalau kwa njia ya matuta
MICHARAZO MITUPU na watanzania kwa ujumla inaitakia kila la heri Yanga katika mechi hiyo ya leo ili kuweza kufanya vyema na kuwapa furaha mashabiki wa soka ambao wamechoka kuona timu zao zikiwa wasindikizaji katika michuano ya kimataifa.
Yanga ndiyo tiumu pekee ya Tanzania kusalia kwenye michuano hiyo mwaka huu baada ya Azam, KMKM na Chuoni za Zanzibar kung';olewa kwenye mechi ra awali za michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Atletico Madrid yashinda ugenini na kuiporomosha Barca
![]() |
Villa akipongezwa na wachezaji wenzake |
Villa alifunga mabao hayo ndani ya dakika mbili dakika ya 62 na 64 na kuiwezesha timu yake iliyocheza bila 'muuaji' wake Diego Costa anayetumikia kadi nyekundu kufikisha p[ointi 64 kulingana na Real Madrid ambayo ina mchezo mmoja mkononi ambao itaucheza leo.
Timu hizo zinatofautiana uwiano wa mabao Madrid ikiizidi Atletico mabao matano tu na kuitangulia watetezi wa ligi hiyo Barcelona ambao jana walichezea kichapo cha bao 1-0 toka kwa Real Vallodolid kwa pointi moja kwani yenyewe ina pointi 63.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo Jumapili, Grenada ilijipatia ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya wageniu wao Villarreal.
Kipute cha ligi hiyo kitaendelea tena leo kwa michezo kadhaa ambayo inaweza kuiongeza pengo la pointi baina ya vinara Real Madrid dhidi ya wapinzani wake waliopo ndani ya Tatu Bora.
AC MIlan bado mwaka wa tabu Italia yanyukwa tena
![]() |
Di Natale alipowatungua Milan jana |
Bao pekee lililoizamisha Milan iliyomweka benchi mshambuliaji wake nyota, Mario Balotelli na kumuingiza kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Robinho, liliwekwa kimiani na Antonio di Natalie katika dakika ya 67 akimaliza kazi nzuri ya Bruo Fernandes.
Kwa kipigo hicho Milan imeendelea kusalia na pointi 35, ikiwa ni kama nusu ya pointi ilizonazo vinara na watetezi wa ligi hiyom Juventus yenye pointi 69 na inayotarajiwa kushuka dimbani leo kukamilisha mchezo wake wa 27.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana Catania na Cargliari zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
Simba katika mtihani mgumu Mbeya leo
Simba |
![]() |
Wenyeji Prisons |
Simba ambayo ilishika nafasi ya tatu msimu uliopita nyuma ya Yanga na viongozi wa ligi kuu msimu huu Azam, ipo hatarini kukosa tena moja ya nafasi mbili za juu kutokana na kuachwa na Azam kwa tofauti ya pointi tano zikiwa zimebakiwa mechi sita.
Wekundu wa Msimbazi pia wameachwa kwa tofauti ya pointi tatu na Yanga ambayo ina mechi tatu mkononi katika nafasi ya pili. Azam ina mechi mbili za ziada.
Hivyo ni ushindi tu ambao utaendeleza ndoto ya Simba ya kucheza angalau Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika mwakani, lakini inakutana na Prisons ambayo imeshinda mechi tatu mfululizo zilizopita.
Kocha wa Prisons, David Mwamaja alinukuliwa toka Mbeya akisema kuwa amekiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha kinaibuka na ushindi dhidi ya Simba ili kiendelee kusalia kwenye ligi kuu msimu ujao.
Licha ya kutopoteza mchezo wowote katika mechi sita za duru la pili, Prisons ipo pointi nne tu juu ya janga la kushuka daraja na ushindi dhidi ya Simba leo utaisaidia kupiga hatua kubwa katika kutimiza lengo la klabu na Mwamaja.
“Tunaiheshimu Simba kwa sababu ni klabu kongwe nchini lakini hatuiogopi na kamwe wasitarajie mteremko katika mechi yetu ya kesho (leo).," alisema Mwamaja.
"Tunazihitaji pointi tatu muhimu dhidi yao ili tujiweke sehemu nzuri katika msimamo wa ligi.”
Naye Zdravko Logarusic, kocha mkuu wa Simba, alisema ana matumaini makubwa ya kushinda mechi ya leo.
Alisema kuifunga Prisons ni sehemu ya mikakati ya kushinda mechi zao zote sita zilizobaki ili kuwa katika nafasi za juu kadri iwezekanavyo katika msimamo wa ligi hiyo.
Mechi nyingine itakayopigwa leo ni kati ya JKT Ruvu itakayoikaribisha Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Chamazi ikiwakosa wachezaji wake kadhaa akiwamo Mussa Mgosi na Salvatory Ntebe walioadhibiwa na TFF
Subscribe to:
Posts (Atom)