KLABU ya Liverpool ambayo ilikaribia kutwaa taji la UEFA Europa League kama sio kuteleza kwa Sevilla ya Hispania, imedaiwa inaongoza mbio za kuwania saini ya chipukizi wa kimataifa wa Uturuki na klabu ya Nordsjaelland, Emre Mor. Mor mwenye umri wa miaka 18, anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora wanaochipukia Ulaya kwasasa baada ya kuonyesha kiwango bora katika Ligi Kuu ya Denmark na kumfanya kuitwa katika kikosi cha Uturuki kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 inayoanza Juni 10 nchini Ufaransa.
Klabu za Manchester United, Borussia Dortmund na Ajax Amsterdam nazo zinatajwa kuwa zinamwania chipukizi huyo anayemudu kiungo mshambuliaji lakini Liverpool ndio inaelezwa kuwa inaongoza mbio hizo.
Dogo huyo amefunga mabao mawili na kusaidia mengine mawili mechi 13 alizoichezea klabu yake msimu huu.


LAZIMA iwashike. England imetangaza kikosi chake cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano ya Fainali za UEFA Euro 2016, huku chipukizi wa Manchester Utd, Marcus Rashford akijumuishwa katika kikosi hicho.
SIJUI ni mikosi au basi tu. Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low amemuacha mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus katika kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.
KAKATWA. Beki wa zamani wa Arsenal, Philippe Senderos ambaye amekuwa akihaha kurejea katika kiwango chake katika misimu ya karibuni, ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uswisi kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.
WAKATI klabu nyingine zikienda likizo kwa ajili ya mapumziko ya Ligi Kuu Bara, Mbeya City haijalala kwani inatarajiwa kufanya ziara ya kisoka Malawi.
BAADA ya kukosa penalti katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mahasimu wao, Real Madrid, beki wa Atletico Madrid Juanfran Torres amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo.

RAIS wa wa Jamhuri
STRAIKA Mbwana Samatta amweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuiwezesha timu yake kucheza michuano ya Ligi Ndogo ya Ulaya (UEFA Europa League) baada ya kuisaidia Genk ya Ubelgiji kufuzu hatua hiyo kwa kuilaza Charleroi.

NAHODHA wa Chelsea John Terry amemuunga mkono Jose Mourinho kufanikiwa kwenye
Klabu yake mpya Manchester United huku akimueleza kuwa Meneja huyo ndie
bora kupita yeyote aliewahi kucheza chini yake. 

MSHAMBULIAJI wa KImataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic amekuwa akihusishwa na kutaka kutua Manchester United ili kuungana na Kocha wake wa zamani, Jose Mourinho, lakini wakala wake wamesema klabu atakayojiunga nayo itashangaza wengi.
KLABU YA Tottenham Hotspur imetangaza kuwa itacheza mechi zake za Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani kwenye Uwanja wa Wembley.
WAKALA wa beki kisiki wa Barcelona, Dani Alves amekanusha taarifa kuwa mteja wake amesaini mkataba wa awali na Juventus, japo amekiri kuwa mabingwa hao wa Italia na klabu nyingine zinamwinda mchezaji huyo.
Benitez Akisaini Mkataba huo wa kumweka Newcastle United Miaka 3
Wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari juu ya kuongeza Miaka 3 kuifundisha Klabu hiyo ya Newcastle United
Kwenye Mkutano na Waandishi huko St. James Park




