![]() |
| Manuel Pellegrini |
![]() |
| Claude Puel |
![]() |
| Victor Wanyama aliyetua Spurs |
Klabu hiyo ilidaiwa ilikuwa mbioni kumpa ajira Kocha Pellegrini mwenye miaka 62 ili kuziba nafasi ya Ronald Koeman aliyetimkia Everton, hata hivyo mpango huo umefutwa na sasa inaelezwa njia nyeupe kwa Mfaransa, Claude Puel wa klabu ya Nice.
Imeelezwa Southampton imeachana na Pellegrini na kumgeukia Puel anayeinoa Nice kutokana na kubaini katika mazungumzo yao Kocha huyo kutoka Chile hawezi kuendana na falsafa ya klabu hiyo katika suala zima la maendeleo ya soka la vijana.
Mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa na shauku kubwa ya kumuona bosi huyo wa zamani wa Real Madrid na Villareal, aliyetwaa taji la Ligi Kuu ya England miaka miwili iliyopita akitua klabu kwao ili kuchukua nafasi ya Kocha Ronald Koeman aliyewakacha na kuhamia Everton mapema mwezi huu kwa ajili ya msimu ujao.
Southampton inahaha kusaka kocha wakati kiungo wake Mkenya Victor Wanyama akiwa ametimka zake Tottenham Hotspur aliposaini mkataba wa miaka mitano kwa ajili ya msimu ujao na kumpa nyota huyo fursa ya kukipiga Ligi ya Mabingwa Ulaya.











CHILE imetinga fainali za Copa America kwa mara ya pili mfululizo na watavaana na Argentina katiak mechi inayorejea fainali za mwaka jana ambapo ilibeba taji kwa ushindi wa bao 1-0.



WAMEPANIA si mchezo. Mabingwa wa soka Ulaya, Real Madrid wamethibitisha kuwa Alvaro Morata atarejea Santiago Bernabeu kipindi hiki cha kiangazi. Taarifa z klabu hiyo zinasema kuwa, hakuna kizuia kwa mkali huyo kurudia nyumbani.
WANAMCHUKUA. Klabu ya Manchester City, ipo hatua ya mwisho kumnasa straika wa kimataifa wa Hispania, Nolito kutoka Celta Vigo. 

Sept 10, 2016
Nov 05, 2016Bournemouth v Sunderland
SIMANZI. Habari zilizotufikia muda huu zinasema kuwa, basi la Tahmeed linalofanya safari zake kati ya Dar na Tanga limeungua lote kwa moto mapema leo katika kijiji cha Komkoma.
