Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo awali ilielezwa kuwa Simba ingecheza na Mtibwa Sugar kabla ya kuwepo kwa mabadiliko hayo. Taarifa toka ndani ya Simba zimesema maandalizi ya mechi hiyo yanaendelea vizuri, timu ikiwa kambini Zanzibar, chini ya Kocha wake mzoefu, Patrick Phiri kutoka Zambia. Kwa mujibu wa habari hizo, Simba huenda ikacheza mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa wiki ijayo kwa kumenyana na APR ya Rwanda. Mechi dhidi ya Gor Mahia itapigwa Jumamosi wakati mechi dhidi ya APR itapigwa Jumatano ijayo kwenye uwanja huo na ni maelekezo ya kocha Phiri.
STRIKA
USILIKOSE
Wednesday, September 3, 2014
Simba kuivaa Gor Mahia, APR Rwanda Dar
Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo awali ilielezwa kuwa Simba ingecheza na Mtibwa Sugar kabla ya kuwepo kwa mabadiliko hayo. Taarifa toka ndani ya Simba zimesema maandalizi ya mechi hiyo yanaendelea vizuri, timu ikiwa kambini Zanzibar, chini ya Kocha wake mzoefu, Patrick Phiri kutoka Zambia. Kwa mujibu wa habari hizo, Simba huenda ikacheza mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa wiki ijayo kwa kumenyana na APR ya Rwanda. Mechi dhidi ya Gor Mahia itapigwa Jumamosi wakati mechi dhidi ya APR itapigwa Jumatano ijayo kwenye uwanja huo na ni maelekezo ya kocha Phiri.
Ofisi ya Mkemia Mkuu yafichua siri nzito
![]() |
| Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Makosa ya Jinai na Vinasaba Gloria Omar (kushoto) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. |
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Makosa ya Jinai na Vinasaba Gloria Omar wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Alisema changamoto nyingine ni uhitaji wa mitambo mipya inayoweza kubaini dawa za kulevya zenye mchanganyiko na kemikali bashirifu pamoja na matengenezo ya jingo la maabara ya uchunguzi wa makosa ya jinai.
Omar alisema iwapo changamoto hizo zitatatuliwa kwa wakati ofisi yao itaongeza tija katika ufanikishaji wa kazi zake kila siku kama ilivyo kuwa hapo awali.
Mkurugenzi huyo alisema baadhi ya mashine zina muda mrefu na pia zinauzwa bei kubwa ufinyu wa bajeti unakwamisha kununua zingine hali ambayo inasababisha kutoendana na wakati kulingana na mabadiliko ya sampuli ambazo zinapatikana.
“ Ofisi yetu imepata mafanikio baadhi lakini changamoto ni kubwa kama nilivyozitaja hapo awali jambo ambalo kwa njia moja zinakwamisha malengo yetu” ,alisema.
Alitaja baadhi ya mafanikio ambayo yalipatikana kwa kipindi cha mwaka 2013 ni Ofisi hiyo kuchunguza majalada 208, utoaji ushahidi mahakamani umeimarishwa na takwimu zimehuhishwa kwa kutumia mfumo wa komputa.
Mafanikio mengine ni kushirika maonyesho ya kimataifa yanayohusu uzuiwaji usafirishaji wa dawa za kulevya na kushiriki katika shughuli za kikosi kazi cha kupambana na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Mkurugenzi huyo wa Idara ya Sayansi ya Makosa ya Jinai na Vinasaba alisema bajeti ya shilingi bilioni 1.4 imetengwa kwa ajili ya mitambo ya LCMS MS na GCMS MS kwa kipindi cha mwaka 2014/2015.
Aidha Omar alisema Ofisi ya Mkemia inapendekeza kuongezewa rasilimali watu pamoja na matumizi ya teknohama kwa kufanya mfumo mzima wa ununuzi, kutenga bajeti ya kotosha katika ofisi hiyo.
Mapendekezo mengine ni Serikali kuhakikisha kuwa inawapatia mashine za kisasa ambazo zitakuwa zikitoa majibu kulingana na wakati pamoja na mahitaji ya watu.
Kuhusiana na matokeo ya watu wanaopima vinasaba (DNA) kuonyesha asilimia 50 ya watu waliopima kuwa wanasingiziwa watoto alisema matokeo hayo ni sahihi jambo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa makini nini sababu yake.
Alisema kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kufanya vipimo anahitajika kufuata taratibu zote za kisheria pamoja na kulipa kiasi cha shilingi laki moja kwa kila sampuli moja.
Mwisho.
Azam, Yanga sasa kukipiga Sept 14 Ngao ya Hisani
![]() |
| Azam |
![]() |
| Yanga |
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, mchezo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa siku moja mbele tofauti na tarehe ya awali.
Mchezo huo utaambatana na shughuli za kijamii kama uchangiaji damu na maonyesho ya shughuli za wadau na maendeleo ya jamii Shirikisho la soka Tanzania (TFF) hutoa sehemu ya mapato ya mchezo huu kwa shirika/shughuli ya kijamii iliyochaguliwa kwa mwaka husika.
Yanga na Azam kwa sasa zipo kwenye maandalizi ya pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na ushindani ulioibuka baina ya timu hizo kwa siku za karibuni.
Yanga kujipima kwa Wakenya leo
![]() |
| Thika United |
BAADA ya kupata ushindi katika mechi tatu mfululizo za kujipima nguvu dhidi ya timu za visiwani Zanzibar, Yanga ya kocha Marcio Maximo itakuwa kibaruani leo itakapowakabili Thika Utd ya Kenya.
Thika United inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, imeshatua
jijini Dar tayari kwa mechi hiyo itakayokuwa ya kwanza ya
kwanza ya kirafiki ya kimataifa kwa Maximo.
Pia ni mechi ya kwanza kwa Yanga na Maximo kucheza kwenye dimba la Taifa, litakalotumika kwa mchezo huo ambao mashabiki wangependa kuona vipaji vyao vipya vilivyosajiliwa na kukimbizwa Pemba kwenye kambi.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga wanaotarajiwa kuwa kivutio leo ni Geilson Santana 'Jaja' na ,Andrey Coutinho toka Brazil, Edward Charles na Said Juma waliosajiliwa hivi karibuni pamoja na vifaa vingine vya zamani.
Viingilio vya mchezo huo ni: VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/= Orange Tshs 10,000/=
Bluu & Kijani Tshs 5,000/=
Viingilio vya mchezo huo ni: VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/= Orange Tshs 10,000/=
Bluu & Kijani Tshs 5,000/=
Jumba la Big Brother Laungua moto uzinduzi waahirishwa
M-Net na kampuni ya production ya Endemol wamethibitisha kuungua kwa
moto jumba la mashindano ya Big Brother Huko South na kutoa taarifa kuwa
mashindano haya yamehairishwa mpaka itakapotolewa taarifa zaidi.
Hakuna mtu aliyumia wala kupoteza maisha na mpaka sasa haijajulikana chanzo cha moto ni nini. M-Net na Endemol wameshaanza kutafuta jumba la kufanyia show ya mwaka huu na kutafuta vifaa vipya baada ya camera na editing instruments kuungua moto.

Hakuna mtu aliyumia wala kupoteza maisha na mpaka sasa haijajulikana chanzo cha moto ni nini. M-Net na Endemol wameshaanza kutafuta jumba la kufanyia show ya mwaka huu na kutafuta vifaa vipya baada ya camera na editing instruments kuungua moto.

Lady Jaydee Balozi wa Uzazi wa Mpango wa Maria Stopes
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST), Uller
Muller (kulia) akikabidhi kisanduku chenye vifaa vinavyohusika na
masuala ya uzazi wa mpango kwa Balozi mpya wa Marie Stopes ambaye pia
ni msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady
jaydee' katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo katika ofisi za
MST, jijiji Dar es Salaam jana
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura 'Lady Jaydee',
ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Marie Stopes,katika kampeni za uzazi wa
mpango.
Akitangazwa rasmi kuwa balozi mpya msanii Jay Dee aliibua shangwe na nderemo zilizotoka kwa baadhi ya wazazi na watu waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ofisi za MST zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Jay Dee sasa anaungana na Marie Stopes kwenye kampeni ya “Chagua Maisha” ambayo inalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa rasmi, Jaydee alisema kuwa amefurahi sana kupata nafasi hiyo ambayo anaamini ataitendea haki kulingana na nafasi yake kwa jamii.
“Nina furaha kubwa kuchukuka nafasi hii ya kipekee kama Balozi wa Marie Stopes kwa sababu wanafanya mengi kuwawezesha kina mama kusimama na kujitegemea, na pia naamini nitafanya kazi nzuri kwa ushirikiano na Marie stopes ili kuiwezesha Jamii kufikia na kuelewa vyema lengo la Uzazi wa mpango''. alisema Jay dee
Lengo kuu la Kampeni hii ya Chagua Maisha nikuhakikisha kila Mtanzania ana haki ya kuchagua mfumo wa uzazi wa mpango ili kulinda afya zao na kutimiza malengo yao ya kimaisha, hususan mabinti wadogo”.
Akitafakari sababu zilizompeleka kuungana na kampeni hii, Lady Jaydee alieleza: “siku zote nilikuwa naamini kuwa wanawake wana uwezo wa kubadilisha Tanzania kimaendeleo. Hivyo niliumizwa moyo sana nilipoambiwa hivi leo kuwa Wanawake wengi hupoteza maisha, na wasichana wengi wanalazimishwa kuacha masomo kutoka na ujauzito. Mimi nimeamua kusaidiana na Marie Stopes kuelimisha jamii nzima wanaweza kubalili fikra na hatima zao, kwa kutumia uzazi wa mpango”.
Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kwenye idadi ya vijana, 54% wakiwa chini ya umri wa miaka 20. Vijana hawa wana uwezo wa kubadili na kukuza hali ya kiuchumi ya Tanzania ndani ya miaka 10 ijayo iwapo watapata msaada.
Akiwa amesimama Pamoja na Lady Jaydee, Bi Muller alikuwa na haya ya kusema: “Leo hii nchini Tanzania, mmjoa kati ya kila Wanawake wane chini ya umri wa miaka 19 wamekwisha kuwa wazazi na asilimia 20% ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20 wamo katika ndoa za kulazimishwa.
Zaidi ya hayo, kama binti akipata ujauzito hata kwa kubakwa, anafukuzwa shule na huo ndio unakuwa mwisho wa elimu yake. Haya siyo mazingira mazuri ambayo vijana wetu wanahitaji iwapo wana matumaini ya kukuza uchumi wa taifa letu na kuliweka kuwa katika kipato cha kati (middle income). Wanawake wana uwezo mkubwa wa kuchangia kukua kwa taifa letu, hivyo ni jukumu letu kuwapa fursa hizo”.
“Nina imani kubwa kuwa tutafanikiwa”, aliongeza Lady Jaydee, “tunataka kila mmoja atambue kuwa ana haki ya kuchagua muda na wakati wa kupata watoto, na pia idadi ya watoto wanaowataka. Marie Stopes na taasisi nyingine zinaweza kukusaidia kumaliza masomo yako na kuhakikisha kuwa una maliza elimu na kuwa na mwanzo mzuri wa maisha, kabla hujaamua kuwa mzazi. Name nitaanza kueneza ujumbe huu Jumamosi hii kwenya Nyama Choma Festival, Dar es Salaam!”
Tukio hili la Lady Jaydee kutembelea Hospitali ya Marie Stopes jijini Dar es Salaam litaonyeshwa jumapili tarehe 07 Septemba kwenye East Africa TV. Kituo hiki kilichopo Mwenge ni miongoni mwa hospitali 11 za Marie Stopes nchini Tanzania. Zote hizi zinatoa huduma za uzazi wa mpango kwa Wanawake bure kabisa bila malipo yoyote.
Akitangazwa rasmi kuwa balozi mpya msanii Jay Dee aliibua shangwe na nderemo zilizotoka kwa baadhi ya wazazi na watu waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ofisi za MST zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Jay Dee sasa anaungana na Marie Stopes kwenye kampeni ya “Chagua Maisha” ambayo inalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa rasmi, Jaydee alisema kuwa amefurahi sana kupata nafasi hiyo ambayo anaamini ataitendea haki kulingana na nafasi yake kwa jamii.
“Nina furaha kubwa kuchukuka nafasi hii ya kipekee kama Balozi wa Marie Stopes kwa sababu wanafanya mengi kuwawezesha kina mama kusimama na kujitegemea, na pia naamini nitafanya kazi nzuri kwa ushirikiano na Marie stopes ili kuiwezesha Jamii kufikia na kuelewa vyema lengo la Uzazi wa mpango''. alisema Jay dee
Lengo kuu la Kampeni hii ya Chagua Maisha nikuhakikisha kila Mtanzania ana haki ya kuchagua mfumo wa uzazi wa mpango ili kulinda afya zao na kutimiza malengo yao ya kimaisha, hususan mabinti wadogo”.
Akitafakari sababu zilizompeleka kuungana na kampeni hii, Lady Jaydee alieleza: “siku zote nilikuwa naamini kuwa wanawake wana uwezo wa kubadilisha Tanzania kimaendeleo. Hivyo niliumizwa moyo sana nilipoambiwa hivi leo kuwa Wanawake wengi hupoteza maisha, na wasichana wengi wanalazimishwa kuacha masomo kutoka na ujauzito. Mimi nimeamua kusaidiana na Marie Stopes kuelimisha jamii nzima wanaweza kubalili fikra na hatima zao, kwa kutumia uzazi wa mpango”.
Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kwenye idadi ya vijana, 54% wakiwa chini ya umri wa miaka 20. Vijana hawa wana uwezo wa kubadili na kukuza hali ya kiuchumi ya Tanzania ndani ya miaka 10 ijayo iwapo watapata msaada.
Akiwa amesimama Pamoja na Lady Jaydee, Bi Muller alikuwa na haya ya kusema: “Leo hii nchini Tanzania, mmjoa kati ya kila Wanawake wane chini ya umri wa miaka 19 wamekwisha kuwa wazazi na asilimia 20% ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20 wamo katika ndoa za kulazimishwa.
Zaidi ya hayo, kama binti akipata ujauzito hata kwa kubakwa, anafukuzwa shule na huo ndio unakuwa mwisho wa elimu yake. Haya siyo mazingira mazuri ambayo vijana wetu wanahitaji iwapo wana matumaini ya kukuza uchumi wa taifa letu na kuliweka kuwa katika kipato cha kati (middle income). Wanawake wana uwezo mkubwa wa kuchangia kukua kwa taifa letu, hivyo ni jukumu letu kuwapa fursa hizo”.
“Nina imani kubwa kuwa tutafanikiwa”, aliongeza Lady Jaydee, “tunataka kila mmoja atambue kuwa ana haki ya kuchagua muda na wakati wa kupata watoto, na pia idadi ya watoto wanaowataka. Marie Stopes na taasisi nyingine zinaweza kukusaidia kumaliza masomo yako na kuhakikisha kuwa una maliza elimu na kuwa na mwanzo mzuri wa maisha, kabla hujaamua kuwa mzazi. Name nitaanza kueneza ujumbe huu Jumamosi hii kwenya Nyama Choma Festival, Dar es Salaam!”
Tukio hili la Lady Jaydee kutembelea Hospitali ya Marie Stopes jijini Dar es Salaam litaonyeshwa jumapili tarehe 07 Septemba kwenye East Africa TV. Kituo hiki kilichopo Mwenge ni miongoni mwa hospitali 11 za Marie Stopes nchini Tanzania. Zote hizi zinatoa huduma za uzazi wa mpango kwa Wanawake bure kabisa bila malipo yoyote.
Vyombo vya Dola lawamani Haki za Binadamu
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHGG) imesema asilimia kubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu hapa nchini unaanzia pale mtu anapokamatwa na vyombo vya dola kwenye mahojiano pamoja na mahabusu.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Kisheria (CHGG) Nabor Assey wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam.
Assey alisema utafiti unaonyesha kuwa wengi wao wanakamatwa pasipo utaratibu, kudhalilishwa, kuteswa, kubambikiwa kesi, kuwekwa muda mrefu bila kufikishwa mahakamani na kuwepo mazingira magumu ya dhamana jambo linalokiuka haki za binadamu zilizoainishwa katika ibara ya12 mpaka 24 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na sheria zingine za nchi na mikataba ya kimataifa iliyoridhiwa.
Mkurugenzi huyo utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 50 ya watu wanaoshikiliwa maeneo mbalimbali nchini ni mahabusu ambao ama wanasubiri kufikishwa mahakani au kesi zao zinaendelea katika mahakama mbalimbali bado hawajahukumiwa.
“Napenda kuweka wazi kuwa hii ni Idara huru ya Serikali tunachokisema hapa ni katika juhudi za kusaidia serikali kutatua changamoto ambazo zinaikabili jamii yake hasa katika masuala ya haki za binadamu” alisema.
Assey alisema ni wazi kuwa vyombo vya dola hasa jeshi la polisi limekuwa likishutumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu hali ambayo inahitaji elimu zaidi ambayo inaweza kusaidia kutatua tatizo hilo.
Alisema ni vema dhana halisi ya jina la polisi (Pilice Force) kubadishwa na kuwa (Police Service) ili kuwapatia uelewa kuwa wanapaswa kutoa huduma na sio kutumia nguvu zaidi kama njia ya kukabiliana na tatizo.
Mkurugenzi huyo alisema pia kuna mapungufu katika mfumo wa sheria za jina za Tanzania akitolea mfano ibara ya 13(6) (e) ya Katiba ya Tanzania ya 1977 inakataza utesaji kwa watuhumiwa na kuelekeza mamlaka za nchi kutunga sheria kwa minajili hiyo.
Alisema bado kuna upungufu katika sheria kwani kifungu cha 29 cha sheria ya ushahidi sura ya 6 ya sheria za Tanzania kinakata ushahidi uliopatikana kwa shinikizo la aina yoyote kutumika kama ushahidi halali mbele ya mahakama.
Assey alisema pamoja na sheria hizo kuonyesha ukatazo bado hazijaonyesha ni hatua gani atachukuliwa mtumishi yeyote ambaye atabainika kufanya vitengo vinavyokiuka haki za binadamu.
Alisema Tume yao ipo katika mchakato wa kuhakikisha kuwa vyombo vya usalama vinapatiwa elimu yakutosha juu ya nini majukumu yao pale ambapo wanamshikilia mtu ambaye amefanya kosa.
Mkurugenzi huyo alisema jitihada hizo zinatakuwa zikishirikisha wananchi hasa kwa kudai haki zao ambazo hazipo kisheria ambao wanaonekana kuwa waathirika wakubwa kutokana na vyombo vya dola hasa Jeshi la Polisi.
Tuesday, September 2, 2014
Hatem Ben Arfa atimkia Hull City kwea mkopo
![]() |
| Kiungo Ben Hatem wakati akiitumikia Newcastle United |
MCHEZAJI Hatem Ben Arfa wa Newcastle United amejiunga na klabu ya Hull City kwa mkopo kwa kipindi kilicho baki cha
msimu akimaliza safari yake ndani ya klabu yake ya Newcastle.
Ben Arfa amekuwa katika wakati mgumu katika kikosi cha Newcastle, licha ya mchango wake mkubwa tangu alipojiunga nao.
Blind atua Mashetani Wekundu mtazame katika uzi mpya
![]() |
| Daley Blind aliyekamilisha uhamisho United |
Vilabu
hivyo vimefikia makubaliano kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa
miaka 24 mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani wiki iliyopita
ambapo United na Ajax walikubaliana ada ya uhamisho wake kufikia pauni
milion £14.2 hii ikiwa ni baada ya mawindo ya muda mrefu ya mashitani
wekundu.
Sasa
imethibtishwa kua Blind atakuwa akiichezea United msimu huu baada ya
kufanikiwa vipimo vya afya na kukubali maslahi ndani ya mshahara wake na
kigogo hicho cha Premier League.
Miyeyusho kuyeyushana na Emilio Mkwakwani Nov 5
| Miyeyusho na Emilio katika pozi |
| Wakitunishiana misuli |
Mabondia hao watapambana katika pigano la uzito wa Feather (kilo 57) siku ya Novemba 5 kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mratibu wa pambano hilo Anthony Rutta alisema maandalizi yameanza kwa kumalizana na mabondia hao wenye sifa zinazolingana kwa sasa katika medani ya ngumi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
"Mabondia Francis Miyeyusho na Emilio Norfat wanatarajiwa kupanda ulingoni kupigana kwa mara ya kwanza Novemba 5 na watasindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi siku hiyo," alisema Rutta.
Rutta alisema itakuwa mara ya kwanza kwa Miyeyusho kupanda ulingoni mkoani Tanga sawa na ilivyo kwa Emilio anayeshikilia nafasi ya pili nchini katika uzito huo wa Feather kati ya mabodia 60.
Emilio anashikilia kwa sasa taji la Afrika Mashariki na Kati la WPBC na rekodi zinaonyesha amecheza michezo 27 akishinda 23 na kupoteza minne, wakati Miyeyusho amecheza 51 ameshinda 38 na kupoteza 11 na kudroo miwili..
Pambano la mabondia hao litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) ambalo Rutta ndiye Katibu Mkuu wake.
Falcao katika uzi mpya baada ya kutambulishwa Old Trafford
| Falcao akiwa katika uzi mpya wa Mashetani Wekundu |
![]() |
| Akiteta na Kocha msaidizi, Ryan Giggs |


Ndege yaanguka Serengeti na kuua abiria wote

Ndege iliyopotea mapema jana ikitokea Mwanza kuelekea Magadi nchini Kenya, imepatikana huko eneo la Serengeti Mara, na abiria wote watatu waliokuwa kwenye ndege hiyo imetaarifiwa wamekufa.
WWF yatoa mafunzo kwa watumishi wa Manispaa ya Kinondoni
SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la WWF, limeendesha mafunzo kwa watumishi wa idara mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni , kuhusiana na ueneaji wa hewa ukaa na matumizi sahihi ya nishati jadidifu nchini.Mafunzo hayo yametolewa na Mratibu kutoka WWF. Teresia Olemako aliyesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanakuwa na ufahamu juu ya kukabiliana na madhara ya hewa ukaa na umuhimu wa kutumia nishati jadilifu.
Alisema mafunzo hayo yanahusu watumishi kutoka mikoa mitatu ambayo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha ambao majiji na miji yao imeingia katika shindano la kimataifa la kukabiliana na utunzaji wa mazingira ambalo litafanyika mwakani kwa kushirikisha nchi 18 duniani, Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza.
Olemako alisema juhudi za WWF kwa kushirkiana na ICLEI ni kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya nishati jadilifu kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira ambao unachangia kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi kote duniani.
“WWF tumejipanga kushirikiana na watumishi wa mikoa hiyo niliyoitaja hapo juu kuhakikisha suala la kupunguza hewa ukaa na kuhimiza matumizi ya nishati jadilifu ni moja ya majukumu yao ambao watatumia mafunzo hayo kuwapatia wananchi elimu zaidi”, alisema.
Mratibu huyo wa Programu ya Nishati Jadilifu alisema mradi huo utakuwa ukitambaulika kwa kauli mbiu ya (Chakula, Nishati, Taka Ngumu na Maji) kutumika kama njia mbadala ya kukabiliana na uharibifu mazingira katika maeneo husika.
Alisema nishati jadilifu ikitumika ipasavyo itakuza uchumi wanchi pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na ukweli haina madhara na ipo kwa wakati wote hivyo ni vema kila mmoja kuwa balozi mzuri katika kuelimisha jamii.
Akizungumzia juu ya shindano hilo alisema ni vema kwa mikoa husika kufanya kila liwezekano ili kuweza kuleta ushindani wa kweli jambo ambalo linaweza kupelekea Tanzania kuibuka na ushindi ambao utakuwa kichochoe cha utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati jadilifu kuongezeka zaidi.
Aidha alisema kutokana na tathmin iliyofanywa na WWF inakadiriwa hadi mwaka 2025 jiji la Dar es salaam litakuwa na wakazi zaidi ya mil. 6.2 huku mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka mara mbili zaidi ya sasa jambo ambalo linahitaji kufanyika maandalizi mapema kabla hali haijawa mbaya.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Injinia Mussa Natty, alisema kila idadi ya watu inapoongezeka, miundombinu na mahitaji ya kibinadamu pia huongezeka hivyo kuifanya jamii kuboresha mahitaji muhimu.
Natty alisema kutokana na hali hiyo WWF inapaswa kuongeza juhudi zaidi za kutoa elimu na kusaidia utekelezaji wa miradi ambayo inaweza kuwa na tija kwa Taifa na wananchi wake kwa vizazi vijavyo kwani kutokufanya hivyo kunaweza kuwa sababu ya kuleta mitafaruku mijini.
Mkurugenzi huyo alisema miradi kama hiyo ikiwa endelevu ni wazi kuwa kila mwanajamii atakuwa balozi mzuri wa kuhitaji mbadilo chanya ambao hayatamuathiri yeye na kizazi chache.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza WWF Tanzania kwa kushirikina na WWW Sweden kwa kuja na mradi huu na manispaa yangu ikawa moja wapo naamini tutaufanyia kazi vizuri kwani sisi Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla tumeathirika sana na mabadiliko ya Tania nchi”, alisema.
“Pia kila mmoja wetu ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es salaam, anahitaji kuwajibika katika sehemu yake ili kuhakikisha mahitaji muhimu ya kibinadamu yanapatikana jirani na jamii ili kuiondoa jamii katika hali ya umasikini unaosababisha ukataji na uharibifu wa misitu”, alisema.
Naye Mwanasheria wa Jiji, Philip Mwakyusa aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe alisema jiji limeupokea mradi kwa mikono yote na watatoa ushirikiano kwa WWF ili iweze kutekeleza mradi huo kwa mafanikio makubwa na ya yenye tija kwa jiji.
Arsenal yamnyakua Welbeck wa Man Utd
KOCHA
Arsene Wenger amefanya jambo la maana katika kutatua tatizo la safu
yake ya ushambuliaji baada ya kukubali kumsaini kwa Pauni Milioni 16
mshambuliaji wa England, Danny Welbeck.
Kocha
huyo wa Arsenal, alikuwa Italia kuthibitisha ahadi ya kucheza mechi
hisani, ameonyesha hisani inaanzia nyumbani baada ya kuwapiga bao Spurs
kwa kumsaini mshambuliaji huyo wa Manchester United.
Welbeck,
anayeondoka Old Trafford baada ya kushindwa kumvutia kocha Louis van
Gaal tangu Mholanzi huyo awasili msimu huu, awali alitolewa kwa mkopo wa
muda mrefu wa msimu kwa Pauni Milioni 3.
Lakini
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akalazimishwa kuuzwa moja kwa
moja aka pate mwanzo mzuri mpya na kuisaidia Arsenal kuilazimisha United
kupunguza bei kutoka Pauni Milioni 18 walizotaka awali kabla ya
mchezaji huyo kusaini Mkataba wa miaka mitano.
Ajali yaua baba, mtoto akiwa hoi kwa majeraha
MTU
mmoja aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili
T. 495 ALM aina ya Nissan Pick Up amefariki dunia katika ajali mbaya,
huku mtoto wake akijeruhiwa vibaya maeneo ya Nane Nane jijini
Mbeya usiku wa kuamkia jana majira ya saa saba za usiku.
Dereva
huyo aliyefariki dunia amefahamika kwa jina la Boniface Mwasoba
alifariki dunia baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka katika
maeneo hayo ya Nane Nane achali iliyopelekea pia kujeruhiwa kwa mtoto
wake anayefahamika kwa jina la Willy Boniface Mwasoba mwenye miaka 7 na
mwanafunzi wa shule ya msingi Mkapa na amelazwa katika hospitali ya
Rufaa jijini Mbeya.
Mpaka
sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika japokuwa polisi bado
wanaendelea na uchunguzi ili kubaini, lakini kamanda wa polisi mkoa wa
Mbeya, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa
wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto kwa kuzingata
sheria na alama za usalama wa barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza
kuepukika.
Monday, September 1, 2014
Ebu angalia usajili kabla ya dirisha kufungwa usiku wa leo
![]() |
| WAKATI dirisha la usajili kwa klabu barani Ulaya likifungwa usiku wa leo, chini ni baadhi ya wachezaji waliohama na kutua katika klabu zao mpya mpaka sasa tukielekea ukingoni. |
Dunga amrejesha Robinho kikosini
KOCHA mpya wa timu ya
taifa ya Brazil, Dunga amemuita mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya
Real Madrid, Manchester City na AC Milan, Robinho kuziba pengo la
majeruhi Hulk wa Zenith kwa ajili ya mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya
Colombia na Ecuador. Dunga ambaye alitaja kikosi chake cha kwanza toka achukue mikoba kwa mara ya pili kutoka kwa Luiz Felipe Scolari baada ya Kombe la Dunia, amemchukua nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye ameichezea nchi hiyo mechi 92.
Robinho amerejea nyumbani Brazil kucheza katika klabu ya Santos ambayo ndio alianzia kucheza soka lake baada ya AC Milan kumuuza kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Dunga aliyewahi kuinoa Brazil katika miochuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 kabla ya kutimuliwa sasa anaelekea katika mchezo dhidi ya Colombia utakaochezwa jijini Miami Ijumaa hii akiwa na wachezaji 10 pekee waliokuwepo katika kikosi cha Scolari.
Baada ya kukwaana na Colombia, Brazil itachuana na Ecuador huko East Rutherford jijini New Jersey Septemba 9 mwaka huu.
Messi aanza na gundu, yathibishwa yu majeruhi
NYOTA wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi huenda
akawa nje ya dimba kwa kipindi kifupi baada ya kudaiwa kuumia paja jana wakati wa Ligi Kuu ya Hispania.Klabu ya Barcelona imetoa taarifa ikidai kuwa nyota wake huyo amepata majeraha ya paja katika mchezo waliopata ushindi mwembamba dhidi ya Villarreal jana.
Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, imedai Messi aliumia msuli wa nyuma ya paja katika mguu wake wa kulia lakini sio majeraha makubwa sana.
Pia ilithibitisha kuwa mshambuliaji wao mwingine Munir El Haddadi naye aliumia nyama na vipimo vya wote wawili vinatarajiwa kufanyika leo kujua ukubwa wa matatizo ya nyota wake hao.
Kuna hatari kubwa Messi akakosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Argentina na Ujerumani unaotarajiwa kuchezwa keshokuwa.
Beki Manchester City Micah Richards atimkia Fiorentina
![]() |
| Micah Richards |
Richards, 26 tayari ameshawasili Italia na anatarajiwa kuwa Mwingereza wa 24 kuichezea klabu hiyo mara atakapokamilisha usajili wake.
Beki huyo alikuwa mchezaji muhimu ya kikosi cha City kilichonyakuwa taji la Ligi Kuu mwaka 2012 lakini amejikuta akikosa nafasi ya kucheza chini ya meneja Manuel Pellegrini aliyeibebesha ubingwa msimu uliopita.
City pia bado wanasiliza ofa kwa wachezaji wao Matija Nastastic, John Guidetti na Scott Sinclair ambao wanaonekana kutokuwepo katika mipango ya Pellegrini.
Richards ambaye ni mzaliwa wa Birmigham alifanikiwa kucheza mechi mbili pekee za Ligi Kuu msimu uliopita na alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.
TFF ya Malinzi yaanza kumeguka, Mtawala abwaga Manyanga
| Evodius Mtawala (kulia) akiwa na viongozi wenzake wa TFF kabla ya kubwanga manyang'a |
TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, aliyekuwaMkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya Kisheria
katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Evodius Mtawala, ameachia
ngazi katika nafasi hiyo.
Mtawala Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Simba, alikuwa na hali ya kutokuelewana na uongozi wa shirikisho hilo
na ndiyo chanzo cha kung'atuka TFF.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, alithibitisha
kuachia ngazi kwa Mtawala lakini akasema ni kutokana na sababu mbalimbali za
taaluma yake ya uanasheria.
“Ni kweli Mtawala hataendelea kufanya kazi TFF
lakini ameamua kuchia ngazi mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali alizodai
kwamba ni kujikita na taaluma yake zaidi kwa sasa, lakini mambo mengine juu ya
hilo yatabaki kuwa siri baina yake na mwajiri wake.
“Ila mpaka makubaliano ya mwisho yalieleza
kuwa itakapofika mwisho wa mwezi wa nane (jana 31, Agosti) atakuwa tayari
ameshakabidhi ofisi na kuendelea na masuala ambayo alidai anahitaji kujikita
zaidi kulingana na taaluma yake,” alisema Mwesigwa.
Rasmi Chicharito mali ya Real Madrid
![]() |
| Akiwa na jezi yake mpya ya Real Madrid na Rais wa klabu hiyo Perez |
| Wakati akichukuliwa vipimo vya afya na kubainika yupo fiti |
| Akiangunga saini ya kuichezea klabu hiyo bingwa ya Ulaya |
Chichirito ambaye hakuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu tangu alipotua akitokea kwao Mexico, amejiunga na Madrid akimpisha Ramadel Falcao aliyetokea Monaco aliyetua Old Trafford kwa mkopo vilevile.
Mshambuliaji huyo alitua Ol Trafford mnamo mwaka 2010 na amenyakuliwa na Madrid ili kuchukua nafasi ya Alvaro Morata ambaye aliuzwa Juventus.
Rais Kikwete atuma Salamu za rambirambi Mbeya
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa
Abbas Kandoro kuomboleza vifo vya watu 10 vilivyotokea Mbalizi, Mkoani
Mbeya tarehe 29 Agosti, 2014 baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota
Hiace maarufu kama Daladala Na. T 237 BFB kugongana na lori aina ya
Tata Na. T 158 CSV. Katika ajali hiyo, watu saba wengine walijeruhiwa
na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
“Nimesikitishwa
na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya watu 10 na wengine saba
kujeruhiwa katika ajali hii iliyotokea siku chache baada ya ajali
nyingine kutokea Mkoani Tabora iliyoua watu 19 na wengine 81
kujeruhiwa”, amesema Rais katika salamu zake.
Rais
Kikwete amesema mfululizo wa ajali hizi unaonyesha dhahiri kuendelea
kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa umakini miongoni mwa madereva, hivyo
jitihada zaidi zinatakiwa kufanywa kusimamia kikamilifu Sheria ya
Usalama Barabarani na kufuatiliwa kwa karibu kwa mienendo ya
wanaoendesha vyombo vya moto, ili ajali hizi ziweze kupunguzwa na hata
kudhibitiwa kabisa katika barabara zetu.
“Naomba
upokee salamu zangu za rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kutokana
na ajali hiyo, na kupitia kwako naomba unifikishie salamu zangu za pole
kwa wafiwa wote kwa kupotelewa ghafla na wapendwa wao”Ameongeza.
Rais
Kikwete amesema anatambua machungu waliyo nayo wanafamilia, ndugu na
jamaa wa watu waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo, lakini anawaomba
wote wawe wavumilivu na wenye subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya
ndugu na jamaa zao.
“Ninawaombea
kwa Mola majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea
katika hali zao za kawaida ili waweze kuungana tena na familia, ndugu
na jamaa zao”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika salamu zake.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
31 Agosti,2014
Manchester United yamnasa Falcao kilaini
![]() |
| Add caption |
KLABU ya Manchester
United imezipiga bao klabu za Arsenal na Manchester City zilizokuwa zikidaiwa kumnyemelea mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia,
Radamel Falcao baada ya nyota huyo kutua kwao kwa mkopo akitokea Monaco ya Ufaransa.
Falcao, 28 amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka muda
mrefu kiangazi hiki kutoka Monaco ambao walimsajili kwa paundi milioni
50 mwaka jana.
Toka ametua Monaco Falcao amefanikiwa kufunga mabao 11
katika mechi 20 huku akikaa nje nusu msimu kutokana na majeruhi ya goti
yaliyomsababisha pia kuikosa michuano ya Kombe la Dunia.
Mahasimu wa
United katika Ligi Kuu Manchester City walishindwa kumuwania nyota huyo
kwa sababu hawakuweza kumhakikishia namba katika kikosi chao.
Falcao pia
alikuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na Arsenal, mabingwa wa Italia
Juventus na mabingwa wa Ulaya Real Madrid.
Sunday, August 31, 2014
Chelsea yazidi kujiimarisha, Kagawa arejea Dortmund
KLABU ya Chelsea imezidi kujiimarisha baada ya kukamilisha uhamisho wa Loic Remy kwa dau la Pauni Milioni 8 kutokaq QPR, huku Mjapan Shinji Kagawa wa Manchester United akirejea klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund.
Remy
aliyekuwa anatakiwa pia na Arsenal, anakwenda kuziba nafasi ya Fernando
Torres aliyehamia AC Milan kwa mkopo wa muda mrefu.
Uhamisho
huu ni faraja kwa Remy ambaye sasa anakwenda kujiunga na klabu
inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kocha Mreno, Jose Mourinho alihitaji
mshambuliaji baada ya kumtoa kwa mkopo Torres.Katika kuelekea mwisho wa kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, Shinji Kagawa ambaye hakuwa akipewa nafasi kubwa ndani ya Mashetani WEkundu amerejea Ujerumani kuichezea Dortmund.
Kiungo huyo amerejea Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 6.3, miaka miwili tu tangu aondoke klabu hiyo ya Ujerumani.
Kagawa atasaini Mkataba wa miaka minne na Dortmund, ambayo ilimuuza Mjapani huyo United mwaka 2012 kwa Pauni Milioni 12.
![]() |
| Shinji Kagawa akikabidhiwa uzi wake mpya wa Dortmund baada ya kuondoka Manchester Utd |
![]() |
| Remy akisaini mkataba wa kujiunga na Chelsea |
![]() |
| Akionyesha uzi mpya wa klabu yake ya Chelsea |
Arsenal bado haijatulia, Sanchez aendelea kufunga
![]() |
| Sanchez akifunga bao la Arsenal |

ARSENAL imeendelea kugawa pointi bada ya kulazimishwa sare ya pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Engaland dhidi ya timu ya Leicester City uwanja wa ugenini.Vijana wa Arsene Wenger walilazimisha sare ya 2-2 na Everton kabla ya leo kupata sare ya 1-1 kwa Leicester City waliotanguliwa kufungwa bao katika dakika ya 20.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Alexis Sanchez kabla ya Leonardo Ulloa kulirejesha dakika mbili baadaye.
Kwa matokeo hayo Arsenal wameongeza kibindoni pointi moja na kufanya wafikishe tano baada ya mechi tatu na itarejea nyumbani kuisubiri mabingwa watetezi Manchester city katika mechi ya ligi hiyo wiki mbili zijazo yaani Septemba 13.
Bao la Sanchez ni la pili katika mashindano baada ya katikati ya wiki kufunga bao pekee lililoivusha Arsenal hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Subscribe to:
Posts (Atom)

















