STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 4, 2015

MATOKEO YA FA CUP HAYA HAPA

http://cdn1.theweek.co.uk/sites/theweek/files/styles/theweek_article_main_image/public/fa-cup_1.jpg?itok=vGlcL-92
http://i1.mirror.co.uk/incoming/article3558459.ece/alternates/s2197/Hull-v-Arsenal-FA-Cup-Final.jpg
Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Arsenal wapon dimbani kwa sasa Emirates

LIGI Kuu ya England wikiendi hii ilikuwa mapumziko na badala yake imeshuhudiwa mechi za raundi ya tatyu ya michuano mikongwe ya Kombe la FA iliyochezwa tangu Ijumaa na itaendelea hadi Jumanne.
Chini ni baadhi ya matokeo ya michuano hiyo wakati Arsenal ikiwa uwanjani nyumbani wakiongoza bao 1-0 dhidi ya wageni wao Hull City.
Ijumaa: 
Cardiff City     3-1   Colchester United    
Jana:
Charlton Athletic     1-2     Blackburn Rovers  
Rochdale     1-0     Nottingham Forest     
West Bromwich Albion 7-0  Gateshead     
Blyth Spartans     2-3     Birmingham City     
Rotherham United     1-5     AFC Bournemouth     
Huddersfield Town     0-1     Reading     
Tranmere Rovers     2-6     Swansea City     
Bolton Wanderers     1-0     Wigan Athletic
Millwall     3-3     Bradford City    
Derby County     1-0     Southport    

Brentford     0-2     Brighton & Hove Albion  
Fulham     0-0     Wolverhampton Wanderers      
Leicester City     1-0     Newcastle United   
Cambridge United     2-1     Luton Town     

Barnsley     0-2     Middlesbrough    
Preston North End     2-0     Norwich City     

Doncaster Rovers     1-1     Bristol City     
Leo:
Dover Athletic     0-4     Crystal Palace    
Sunderland     1-0     Leeds United    
Queens Park Rangers  0-3     Sheffield United   
Southampton     1-1     Ipswich Town    
Stoke City     3-1     Wrexham    
Manchester City     2-1     Sheffield Wednesday

Aston Villa     1 - 0     Blackpool    
Yeovil Town     0 - 2     Manchester United   
Chelsea     3 - 0     Watford     
  

Real Madrid yapigwa 2-1 ugenini na Valencia

Valencia players celebrate after earning a thrilling 2-1 victory over Real Madrid at the Mestalla
Valencia wakishangilia ushindi wao
Ronaldo paid no attention to the keeper's attempts to put him off and struck his penalty cleanly
Ronaldo akifunga penati
Real Madrid talisman Ronaldo evades a tackle from Valencia's Nicolas Otamendi during the game at the Metsalla
Ronaldo akikukuruka kuisaidia Real madrid ugenini kwa Valencia
VINARA wa Ligi Kuu ya Hispania, Real Madrid imejikuta ikipokea kipigo cha mabao 2-1 ugenini dhidi ya Valencia, ikiwa ni siku kadhaa tangu watiwe nuksi na AC Milan ya Italia kwa kuchapwa mabao 4-2 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa maalum iliyochezwa Dubai, UAE.
Real Madrid iliyokuwa imeshindwa mechi 22 mfululizo katika msimu huu ilizimwa na Milan na leo ikiwa ugenini licha ya kutangulia kupata bao katika dakika ya 14 kwa mkwaju wa penati lililofungwa na kinara wa mabao wa ligi hiyo, Cristiano Ronaldo ilishindwa kuhimili vishindo vya wenyeji wao.
Bao hilo lilikuwa la 25 kwa Ronaldo, baada ya Alvaro Negredo wa Valencia kuunawa mpira akiwa langoni mwake.
Wenyeji walirudi kipindi cha pili wakiwa wamecharuka na kujipatia bao la kusawazisha dakika ya 52 kupitia Barragan akimalizia kazi nzuri ya Jose Gaya kabla ya Nocolas Otamendi kuongeza bao la ushindi dakika ya 65.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo  Atlético Madrid wakiwa nyumbani walipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Levante, Sevilla ikiishinda Celta Vigo bao 1-0 nyumbani, Elche na  Villarreal  walitoka sare ya 2-2, huku Deportivo La Coruna wakiwa nyumbani waliitafuna Athletico Bilbao kwa bao 1-0 na Malaga kulala kwao mabao 2-1 dhidi ya Almería katika mechi zilizochezwa jana.
Kwenye nyingine za leo Getafe ikiwa nyumbani ililala mabao 2-1 dhidi ya Rayo Vallecano na kipigo cha Real Madrid kinaiweka katika nafasi ya kuenguliwa kileleni iwapo Barcelona inayotarajiwa kushuka dimbani hivi punde kama itaishinda Real Sociedad ya David Moyes watakaokuwa nyumbani kwao, kadhalika Espanyol itaikaribisha Eibar.
Real baada ya mechi 16 imesaliwa na pointi 39 Barcelona wenye michezo kama hiyo wakiwa na pointi 38 sawa na Atletico Madrid iliyotangulia kwa mchezo mmoja  (17) wakiwa na pointi kama hizo 38.

Didier Drogba kustaafu rasmi mwishoni mwa msimu

Atakapostaafu Didier Drogba atakuwa msaidizi wa Jose Mourinho kwenye benchi la ufundi.NYOTA wa Ivory Coast anayechezea klabu ya Chelsea Didier Drogba anatarajiwa kutangaza kustaafu kuichezea klabu hiyo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu akiwa amerejea Chelsea akitokea Galatasaray ya Uturuki .
Drogba ambaye kwa Chelsea anahesabika kama gwiji  ametengenezewa nafasi ya kubaki ndani ya klabu hiyo mara atakapostaafu ambapo ataendelea kuwepo chini ya kocha Mreno Jose Mourinho .
Drogba anatarajiwa kukaa kwenye benchi la Chelsea akiwa mmoja wa makocha wasaidizi wa Mourinho jukumu ambalo nyota huyu wa Afrika ameafiki kulichukua baada ya kukubali kuwa hawezi kuendelea kucheza katika kiwango cha juu .
Drogba amepanga kustaafu mwishoni mwa msimu huu .
Drogba amepanga kustaafu mwishoni mwa msimu huu .
Drogba alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Olympique Marseille mwaka 2003 ambapo aliichezea klabu hiyo kwa miaka 9 ambapo alifanikiwa kutwaa mataji kadhaa huku akijijengea sifa ya kuwa nyota wa mechi kubwa kutokana na uwezo wake w akufunga mabao muhimu kwenye mechi kubwa zikiwepo hatua za nusu fainali na fainali .
Atakapostaafu Didier Drogba atakuwa msaidizi wa Jose Mourinho kwenye benchi la ufundi.
Drogba alirudi Chelsea msimu huu baada ya kuondoka mwaka 2012 wakati klabu hiyo ilipotwaa ubingwa wa ulaya baada ya kuifunga Bayern Munich ya Ujerumani huku Drogba akifunga penati ya mwisho iliyoipa Chelsea ubingwa .

Ndanda Fc yainyoa Prisons na kutoka mkiani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSvHwYqtPQMuzPoWUu4QCWVjjgvVwLySqdBYExhW-LxDkl-tjqI3X__y-_vwNzmO6A72piQEbxsK79AqJ8vub5o2bTvjx1VL8FqSFT_-uMryVYDTOmZZVv18G_WiMV4YrQE_D_be0p_aWy/s1600/20140913_160438.jpg
Ndanda
BAO pekee lililofungwa na Jacob Massawe katika dakika ya 35 imeisaidia Ndanda Fc ya Mtwara kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons Mbeya na kung'oka mkiani mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya, limeweza kuifanya Ndanda kufikisha pointi 9 na kutoka mkiani wakiiachia Prisons-Mbeya wakiwapokea wakati ligi ikitarajiwa kuendelea tena wikiendi ijayo.
Kocha wa Ndanda Mewja Abdul Mingange amesema amepokea ushindi huo kwa furaha baada ya vijana wake kujituma uwanja na kuibuka washindi huku kocha wa Prisons-David Mwamaja amesema wamekubali kipigo kwa vile vijana wake walifanya makosa yaliyotumiwa na wenzao kupata ushindi huo.
Kwani katika dakika za lala salama wenyeji walipoteza nafasi ya kusawazisha bao hilo baada ya kukosa mkwaju wa penati.
Kwa matokeo hayo Prisons wamekaa mkiani wakiwa na pointi saba wakati Ndanda wakichupa hadi nafasi ya 12 katika msimamo huo wakiwa juu ya Mbeya City yenye pointi nane.

Yanga yazidi kutisha Zenji yaua tena ikifuzu robo fainali

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2014/12/IMG_0557-0.jpgWAKATI mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, KCCA ya Uganda ikipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtende, Yanga imeendeleza undava wake baada ya kuinyoa Polisi kwa mabao 4-0.
Yanga ilipata mabao yake kupitia kwa Andrey Coutinho aliyefunga mawili na mengine kuwekwa kimiani na Kpeh Sean Sherman na Simon Msuva.
Coutinho alifunga baoa lwa kuongoza dakika ya 27 kabla ya Mliberia kuongeza la pili dakika ya 33 na kufanya timu ziende mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili Yanga waliendelea kuonyeshja dhamira yao kwamba wanalitaka taji hilo linaloshikiliwa na KCCA, baada ya Coutinho kuongeza la tatu kwa mkwaju wa adhabu ndogo dakika ya 56 na Msumva kufunga bao la nne la mchezo wa leo na la nne kwake katika michuano hiyo dakika kumi kabla ya mchezo kumalizika.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo, KCCA iliwalaza Mtende mabao 3-0 na Shaba ililala kwa bao 1-0 kwa Taifa ya Jang'ombe ambao walikandikwa mabao 4-0 na Yanga katika pambano lao lililopita.
Pambano linaloendelea kwa sasa ni kati ya Mabingwa wa Zanzibar KMKM inayoumana na mabingwa wa Tanzania Bara., Azam na matokeo kwa sasa bado 1-0, Azam wakiongoza dakika ikiwa ya 73.

Prisons-Mbeya, Ndanda nani kumcheka mwenzake leo?!

Prisons-Mbeya
Ndanda Fc
WAKATI vigogo vya Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Yanga, watetezi Azam na vinara Mtibwa Sugar wakiwa visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi na kulazimisha mechi zao kuchezwa katikati ya wiki, leo ligi hiyo itahsuhudia pambano moja ambalo litazikutanisha timu 'vibonde' Prisons-Mbeya itakayoikaribisha Ndanda ya Mtwara.
Pambano hilo litakalochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ndilo pambano pekee la ligi hiyo kwa leo baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupangua ratiba na kuahirisha mechi za 'vigogo' ili washiriki vema kwenye michuano ya Mapinduzi iliyoanza siku ya Alhamisi.
TFF ilipangua mechi nne zilizokuwa zichezewe jana na leo zinazohusu timu hizo ambazo sasa zitalazimika kucheza katikati ya wiki kwa wiki inayoanza kesho na wiki ijayo kabla ya mashindano hayo kumalizika Januari 13.
Hata hivyo pambano la Prisons-Mbeya na Ndanda lililokuwa liwe miongoni mwa michezo miwili iliyokuwa imepangwa kucheza leo zenyewe zitaendelea na ligi hiyo, huku kila timu ikiwania pointi tatu kujiondoa maeneo ya mkiani.
Ndanda inayocheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza ipo mkiani ikizibeba timu zote ikikusanya pointi sita tu katika mechi nane ilizocheza itaivaa Prisons ikiwa na kumbukumbu ya kuchezea kichapo toka kwa Mbeya City waliokuwa wakiburuza mkiani tangu ligi iliposimama Nov 9.
Timu hiyo ilikung'utwa bao 1-0 na Mbeya City ambayo leo itakuwa miguu juu kutokana na pambano lao la dhidi ya Yanga kuahirishwa hadi katikati ya wiki.
Wenyeji wao yaani Prisons wapo nafasi ya 13 wakiwa na pointi saba wakitoka kulazimishwa suluhu kwa mabingwa wa zamani Coastal Union katika pambano la wiki iliyopita lililochezwa kwenye uwanja wa huo wa Sokoine.
Timu hizo zinazofundishwa na makocha wazawa David Mwamaja wa Prisons na Meja Abdul Mingange watakuwa na kazi za kuhakikisha vijana wao wanapata ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri kadri ligi inavyozidi kushika kasi.
Prisons ni miongoni mwa timu mbili ambazo zimeshinda pambano moja katika ligi ya msimu huu ikiwa sambamba na Simba ambayo itavaana na Mgambo katikati ya wiki.
Kucheza kwao kwenye uwanja wa nyumbani unaweza kuwa na faida kwao, iwapo kama watagangamala vinginevyo wanaweza kuwapokea Ndanda nafasi ya mikiani kwani iwapo Ndanda itashinda itafikisha jumla ya pointi 9 zinazoweza kuwafanya kuiporomosha hata Simba waliopo nafasi ya tisa kwa sasa.
Hata hivyo kwa namna Prisons inavyocheza soka lake inaweza kuipa mtihani Ndanda iliyoimarisha kikosi chao kwenye usajili wa dirisha dogo, licha ya kuanza kwa kipigo mbele ya Mbeya City.
Baadhi ya wachezaji waliongezwa katika kikosi cha Ndanda kupitia dirisha dogo ni viungo wa zamani wa Yanga, Omega Seme, Kiggi Makassy, Stamili Mbonde na Raymond Zabron wote kutoka Villa Squad, Issa Said, MOhammed Masoud 'Chile' na Zubeir Ubwa waliokuwa huru.

Xavi aiponda CAS kutupa rufaa ya Barcelona

http://cdn.inquisitr.com/wp-content/uploads/2014/10/Xavi-On-His-Way-To-Man-Utd.jpg
Xavi
KIUNGO mahiri wa Barcelona Xavi, ameiponda Mahakama ya Michezo ya Kimataifa-CAS kwa uamuzi wake wa kutupilia mbali rufani ya klabu hiyo wakipinga adhabu ya kufungiwa kusajili na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.
Barcelona walipewa adhabu hiyo kutokana na kupatikana na hatia ya kusajili wachezaji chini ya umri wa miaka 18 kutoka nje ya Hispania na baadae kukata rufani CAS ambayo katika maamuzi yake ilitupilia mbali. Uamuzi huo utaifanya Barcelona kushindwa kusajili mchezaji wa aina yeyote kwa mwaka huu na Xavi anadhani adhabu hiyo haijatenda haki.
Xavi ambaye ni nahodha wa Barcelona amesema wote wameshangazwa na uamuzi huo wa CAS kwani walitegemea kupunguza adhabu hiyo ambayo inaonekana kuwa kali kuliko kosa lenyewe.
Hata hivyo Xavi anaamini kuwa Barcelona bado ina vipaji vya kutosha vya kuifanya kuwa tishio katika kila mchezo wanaocheza.

Bingwa Malembeka Cup kunyakua RAV4

http://thechronicleherald.ca/sites/default/files/imagecache/ch_article_main_image/articles/2006_Toyota_RAV4_08web.jpgDIWANI wa Kata ya Msongola, Jimbo la Ukonga, Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam Angelina Malembeka amesema mshindi katika kombe la Malembeka ataibuka na gari aina RAV4 na mshindi wa kila Kata atapa pikipiki moja aina ya Honda.
Malembeka aliyasema hayo jana wakati akizungumza jijini Dar es Salaam ambapo alibainisha kuwa katika mashindano hayo timu 89 kutoka katika Kata nane.
Alisema lengo la kuandaa mashindano hayo ni kuhakikisha kuwa vijana ambao wana vipaji katika jimbo hilo wanatumia ipasavyo na kuwasaidia kupata soko katika timu kubwa.
Diwani huyo ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wa Wilaya ya Ilala alisema katika mashindano hayo kila kata inashiriki ambapo mshindi ataibuka na pikipiki moja aina ya Honda.
Katibu huyo wa Madiwani wa Ilala alisema baada ya timu kushindana katika ngazi ya Kata timu tatu bora zitaingia katika hatua ya pili ambapo ziicheza hadi msindi wa jumla apatikane.
"Nimeandaa mashindano ya mpira wa miguu ambapo timu 89 kutoka Kata nane zimeshiriki na bingwa atapata RAV4 na washindi wa kata watapata pikipiki," alisema Malembeka.
Malembeka alisema jitihada zake ni kuhakikisha kuwa michezo yote ambayo ipo inachezwa katika Jimbo na Kata yake ambapo kwa kuanza ameanza na mpira wa miguu na bao.
Alisema bao ameanza katika Mitaa tisa ya Kata yake ya Msongole ambapo kwa sasa yupo katika mkakati wa kuandaa mashindano.

CHAMIJATA WAALIKWA CHINA, DIWANI AWAPA BAO

[DSC08287+[800x600].JPG]
Mwenyekiti wa CHAMIJATA, Mohammed Kazingumbe
CHAMA cha Michezo ya Jadi Tanzania (Chamijata) kimesema kimepata mwaliko kushiriki mashindano ya kurusha mishale ambayo yatafanyika nchini China kuanzia Machi 28 hadi 20 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chamijata Tanzania Mohammed Kazingumbe wakati akizungumza na jijini Dar katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam.
Alisema Chamijata imekuwaikipata mialiko mara kwa mara katika nchi za China na Korea Kusini hivyo kwa mwaka huu mwaliko wa kwanza ni kutoka China na mialiko mingine ipo ambayo ni kwenda Korea Kusini mwezi Septemba.
Mwenyekiti huyo alisema kwa sasa wanahangaika kutafuta wafadhili ili waweze kupeleka timu na viongozi wa Chamijata wakati huo ukifika.
"Tumepata mwaliko wa kwenda China katika mashindano ya kurusha mishale ambayo yatafanyika Machi 28 hadi 30 hivyo jithada na mikakati yetu ni kuhakikisha kuwa tunashiriki," alisema Kazingumbe.
Kazingumbe alisema Chamijata ina imejipanga vilivyo ili kuhakikisha kuwa michezo ya jadi inarejea katika hadhi yake ya awali ambapo amewaomba wadau kuwasaidia kufanikisha hilo.
Mwenyekiti huyo alisema Chamijata katika kuhakikisha kuwa inakuza mchezo huo itatumia kitabu ambacho wamekiandika chenye maelezo kwakina kuhusu mchezo wa bao.
Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Msongola Angelina Malembeka ametoa msaada wa mabao matatu kwa Chama cha Michezo ya Jadi Tanzania (Chamijata) ikiwa ni jitihada zake za kuendeleza mchezo huo.
Malembeka ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wa Manispaa ya Ilala alikabidhi mabao hayo jana katika ofisi za Chamijata zilizipo Temeke jijini Dar es Salaam.
Alisema ameamua kutoa msaada huo kwa Chamijata kutokana na kuona kwa muda mrefu mchezo huo umeshindwa kuvuma hivyo kwa kuanzia mabao hayo yatawasaidia.
Diwani huyo alisema pia katika kuendeleza mchezo huo amegawa mabao katika mitaa tisa ya Kata yake lengo likiwa ni kuendeleza mchezo huo kuanzia Mitaa hadi ngazi ya Taifa.
"Jamani naomba mpokee mabao haya ila naahidi kuendelea kuwasaidia pale msaada utakapo hitajika kwani mimi ni mdau  wa michezo hasa michezo ya jadi," alisema Malembeka.
Malembeka alisema iwapo michezo ya jadi itapewa kipaumbele ni dhahiri kuwa jamii itadumisha tamaduni zake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chamijata Gamaliel Mhanga alimshukuru Diwani huyo kwa msaada wa mabao hayo ambapo aliwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia chama hicho.
Mhanga alisema Chamijata imejipanga kutekeleza mipango yake mbalimbali ya kuboresha na kuendeleza michezo ya jadi kwa kushirikiana na wadau kama Diwani Malembeka.

RC Kandoro awaasa watanzania kudumisha amani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiIdCG8q41fcHcJCPLnyMeU3MtDBoF9jTL6h2bf2OUimm7yC_Vh8ffzBmmCqMQH8sY7P4hyPtWBRisvzPY30rSrB4mKD_jgGEot7YjrNC5oCAPJreK9Jkm785v1cnjdyKu_BU4vmpn-GUk/s800/2.JPG
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
Mwandishi MaalumMKUU wa Mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amewataka wananchi wa kudumisha amani kwani kinyume na uwepo wa amani hakuna maendeleo yatapatikana katika nchi na kwa wananchi.
Kandoro amesema hayo wakati akizungumza katika mkesha wa mani ambao uliandaliwa na viongozi wa dini wa Mkoa huo kutoka makanisa mbalimbali.
Alisema amani ya Tanzania haiwezi kudumu  kama vitendo vya uvunjifu wa haki, uonevu, ukosefu wa maadili na ukosefu wa ajira vitaendelea kuongezeka katika jamii.
"Suala la amani ni la kila mtu katika jamii hivyo kinachohitajika ni kila mmoja wetu kuwa sehemu ya kuhakikisha amani inakuwepo kwa nguvu zoake zote," alisema.
Kandoro aliwataka viongozi wa dini waache mahubiri ya kudai fedha zasadaka badala yake wafundishe waumini wao kufanya kazi kwa bidii ili mapato yao ndio watoe sadaka.
Alisema hivi sasa vijana wengi wapo vijiweni hawana kazi hivyo kinachohitajika ni juhudu kila mmoja wenu kwa kushirikiana na Serikali kuhamasisha jamii iweze kukituma katika kujitafutia kipato cha halali badala ya watu kutoa sadaka za ufisadi, rushwa na madawa ya kulevya.
Mkuu huyo wa mkoa alisema iwapo viongozi wa dini watasimamia haki taifa litastawi na kuwa mahali pa maendeleo na kuboresha uwajibikaji katika utumishi.
Akizungumza katika mkesha huo kwa niaba ya viongozi wa dini Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanzania, William Mwamalanga, alisema ni vyema viongozi wakazingatia maadili katika kutumikia Taifa na jamii ili kuondoa tabia ya ufisadi na rushwa iliozoeleka.
Mwamalanga alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa viongozi wa dini ambao wanawatetea watu ambao wamefaidika na fedha za Escrow waache kwani wanamkosea mungu.
Alisema mchakato wa kupiga vita ufisadi unahitaji ushirikiano wa wadau wote hivyo ni kosa kwa baadhi ya viongozi hasa wa dini kudiriki kutumia nafasi zao kutetea waovu.

New Family Group yaiomba serikali kudhibiti panya Road

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYt0VvknsAULCfXKblhX-k4MAqyoupcdtUtit8OCIsc5iad7xmCsz-Gdc5Tv6VcadL4wW6tpyDwCYkiHdNfytf3FXuXJ3WBuPq1ghcDLkP3-nf84TGXfrDG7o5SL2ZYf93aK0UwLJHqSpS/s1600/panya+Road.jpg
baadhi ya wanaodaiwa kuwa viongozi wa kundi la OPanya Road waliponaswa hivi karibuni
Mwandishi Maalum
KITUO cha New Familiy Group (NGFG) cha Mwasonga Temeke jijini Dar es Salaam kimeomba Serikali kushirikina na kituo hicho ili kuweza kuwahifadhi vijana ambao wanaonekana kuleta hofu katika Jiji wanaotambulika kwa jina la 'Panya rodi' ili waweze kulelewa kituo hapo.
Ombi hilo linakuja ikiwa ni siku moja vijana hao kutajwa kuwa wameibuka katika Wilaya ya Kinondoni na Ilala na kufanya matokio ambayo yanahatarisha amani kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa NHFG Omari Kombe alisema kikundi hicho ambacho kinaundwa na vijana wengi wa mitaani kutoka mikoani kipo kwa muda mrefu lakini udhibiti wake umekuwa wa kusuasua.
Kombe alisema wamekuwa wakiwasiliana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto pamoja na Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia ili kwa pamoja waweze kupata muafaka wa tatizo hilo ila mwitiko kwa upande wa Serikali umekuwa duni.
"Unajua kwa muda mrefu vijana hawa wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya uhalifu na hili la jana ni endelevu lakini njia ambayo inaweza kuwa ni suluhisho ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo na eneo ambalo linaweza kuwapatia mafunzo ya ufundi, ujasiriliamali na mengine ambayo yatakuwa na tija nao," alisema Kombe.
Kombe alisema NHFG ipo tayari kushirikiana na Serikali kwa kutoa eneo ambalo litajengwa kituo kikubwa mbapo watapata mafunzo hali ambayo inaweza kuleta amani kwa jamii.
Mwenyekiti huyo alisema NHFG ina eneo la heka 10 hivyo iwapo Serikali itaona ni jambo la msingi kujenga wao wapo tayari kushirikiana kwa maslahi ya vijana hao na nchi kwa ujumla.
Alisema iwapo vijana hao watashindwa kudhibitiwa kwa sasa ni ishara tosha kuwa nchi inatengeneza majambazi kwa miaka ijayo ambayo yatakuwa na uzoefu wa kutosha.
Kombe alisema vijana hao wameanza kutumiwa na kundi lingine la Mbwa Mwitu ambalo nalo limekuwa likiibuka kila mara katika maeneo  mbalimbali ya mji.
Alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Serikali hasa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kuwa matatizo hayo ya uwepo wa panga rodi na mbwa mwitu yanaisha.

Breaking News! Mwanamuziki Kachumbari afariki dunia

http://www.charlesmusicstore.com/images/percussion/hand_percussion/SantanaCongas.jpg
HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwanamuziki aliyewahi kutamba na bendi mbalimbali ikiwamo Chuchu Sound, Flowing Kachumbari amefariki dunia asubuhi hii.
Kwa mujibu wa kiongozi wa bendi ya African Minofu, Joseph Matei, ameiambia MICHARAZO kuwa mpiga tumba na dramu huyo amefariki asubuhi ya leo na kwa sasa wanafanya taratibu za mazishi yake.
MICHARAZO inaendelea kufuatilia na itawajulisha kinachoendelea.

Liverpool kumpa mkataba mnono Raheem Sterling

http://i3.mirror.co.uk/incoming/article3428044.ece/alternates/s2197/Raheem-Sterling.jpg
Raheem Sterling
KLABU ya Liverpool wanajipanga kuwafurahisha mashabiki wao kwa kutaka kumuongeza mkataba mwingine Raheem Sterling kufikia mwishoni mwa mwezi huu.
Mkataba huo utaigharimu klabu hiyo ya Anfield paundi milioni 25.
Majogoo hao wa jiji wanamatumaini ya kumbakisha Sterling kwa mkataba wa miaka mitano ambapo atakuwa analipwa paundi laki moja kwa wiki na tayari mazungumzo baina ya pande mbili yameshaanza baada ya taarifa za kushangaza kwamba nahodha Steven Gerrard anaondoka kwenda kucheza soka Marekani.
Mchezaji huyo amekuwa msaada mkubwa kwa klabu hiyo, licha ya kwamba kuondoka kwa Luis Suarez na kuwa majeruhi kwa Daniel Sturridge kumemfanya kupunguza makali yake.

Shilole aahidi makubwa 2015

MUIGIZAJI nyota wa filamu anayetamba kwenye muziki kwa sasa, Zuwena Mohammed 'Shilole' amewataka mashabiki wake kupata mambo makubwa na mazuri zaidi ndani ya mwaka 2015 kuliko ilivyokuwa mwaka uliopita.
Shilole anayetamba kwa sasa na wimbo mpya wa 'Malele' baada ya kusumbua hewani na nyimbo kama 'Lawama', 'Dume Dada', 'Chuna Buzi', 'Nakomaa na Jiji' na 'Nimemchukua' alisema amejipanga kuwapa raha zaidi mashabiki wake.
"Shishi Baby halali kwa kuwaza namna ya kuwapa burudani mashabiki wake, hivyo wajiandae kupata makubwa zaidi kuliko ilivyokuwa nyuma sawia na kusubiri kuniona nikirejea tena kwenye filamu baada ya kuwa kando kwa muda," alisema Shilole.
Mwanadada huyo alisema anajiandaa kushuti filamu yake mpya itakayofahamika kwa jina la 'Shilole in Dar' ambayo atairekodia Igunga Tabora baada ya awali kutamba na filamu kama 'Shilole', 'Fair Decision', 'Bed Rest', 'Black Sunday', 'Morning Alarm' na nyingine.

Kalapina auaga mwaka 2014 akitarajia makubwa 2015

http://api.ning.com/files/3QWN5yhdbaeQObObLezaYgpUwAXMvGqT*xDpp-v1dArxT1bAwibog9Yk4gMPCahJQX1EPtdr6KDsl-MHfQnB62aUwJ1fkvv5/PINA.jpg
Kalapina
RAPA na mwanaharakati, Karama Masoud 'Kalapina' amesema mwaka 2014 ulikuwa wa mapinduzi katika muziki wa kizazi kipya nchini na kutabiri mapinduzi zaidi kwa mwaka 2015 ulioanza.
Kalapina aliyeuaga mwaka 2014 kwa kuangusha shoo akishirikiana na Kikosi cha Mizinga  na wasanii wengine kama LWP, Big Dog Pose, Dopa Man na Country Boy, alisema kwa yeyote aliyefuatilia muziki wa Tanzania amebaini mwaka 2014 ulikuwa wenye mapinduzi makubwa na fani hiyo kupata mafanikio kwa wasanii walio wengi.
Hata hivyo alisema mafanikio hayo yanapaswa kuwa changamoto kwa wasanii wote kuongeza bidii ili kusonga mbele zaidi kubwa kulenga kuikomboa jamii katika hali iliyonayo ikizingatiwa mwaka 2015 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu.
"Mafanikio yaliyopatikana ndani ya 2014 ni chachu ya kupata mafanikio zaidi ndani ya 2015, muhimu tushirikiane na kuhakikisha tunaisaidia jamii katika kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu," alisema Kalapina.
Kalapina ambaye aliwahi kugombea udiwani kupitia chama cha CUF, aliwahi kudokeza kuwa mwaka huu atajitosa kuwania kiti cha Ubunge wa Kinondoni kwa lengo la kutaka kuwakomboa watanzania hususani wa jimbo hilo ambalo halijawahi kuongozwa na 'mzawa' wa eneo hilo

Sikinde wajiandaa kurekodi video albamu mpya

Baadhi ya wanamuziki wa Sikinde, Hemba akiwa kati
BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Mlimani Park 'Wana Sikinde' inatarajia kuanza kurekodi video ya albamu yao mpya mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza na MICHARAZO, mmoja wa viongozi wa Sikinde, Abdallah Hemba alisema kuwa, video hiyo itarekodiwa mara tu baada ya aalbamu yao kutolewa studio ilipokuwa inamaliziwa.
Hemba ambaye ni mmoja wa waimbaji waandamizi wa bendi hiyo, alisema ingawa mpaka sasa bado hawajaju kampuni itakayofanya kazi ya kuitengeneza video hiyo, lakini shughuli za kuirekodi itafanyika ndani ya mwezi huu wa Januari.
"Tutaanza kuirekodi mara baada ya albamu kutoka studio na tungependa kukamilisha mapema video hiyo kabla ya kumalizika kwa mwezi huu wa Januari ili kuachia kwa pamoja 'audio'," alisema.
Hemba alisema Sikinde imepania kutengenezea video nyimbo zote saba, japo ni chache zitakazoachiwa hewani ili kuitambulisha albamu hiyo yenye nyimbo kama 'Jinamizi la Talaka', 'Kibogoyo', 'Za Mkwezi', 'Nundu ya Ng'ombe', 'Kukatika kwa Dole Gumba', 'Deni Nitalipa' na 'Tabasamu Tamu'.

Waumini wacharangana mapanga Kanisani!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgkQiBrgXpc7OYa4fHMTrSZrxZw26vlnPuP1xF5VeGfDOcZJuF2RgOV6eYR-YyP-BSQHjXM6kJObZF3EMjfHwfFUljOOKPIeu7-bAyd8amki1xouRA83NFnrSQDou7LZ1fuJiJfljZjHgNl/s1600/jesus.jpg
Warioba Igombe, Morogoro
WAUMINI wawili wa Kanisa la Moravian mkoani Morogoro wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao, baada ya kukatwakatwa mapanga katika vurugu zilizoibuka kanisani.
Inadaiwa kuwa, waumini hao walikatwa mapanga hayo na Jackson Mnyilimi, baada ya kutokea fujo kanisani hapo.
Akizungumzia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Paulo alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo ambazo zilitokea jana katika Kijiji cha Makelele Tarafa ya Malinyi wilayani Ulanga.
Alisema tayari mtuhumiwa aliyefanya vurugu hizo anashikiliwa na polisi ili sheria ichukue mkondo wake, baada ya kuhusishwa na tukio hilo la kujeruhi waumini hao.
Aliwataja waliojeruhiwa ni Maria Silumbwe (47) na Aron Silumbwe (20), wote ni wakazi wa Malinyi.
“Tukio hilo lilitokea wakati waumini wa Kanisa hilo wakiingia kanisani, ndipo kundi la mzee Ntony Mnyelemi (53), ambaye ni Mwenyekiti wa Kanisa hilo, liliwanyang’anya ngoma wanakwaya wa kanisa hilo na kusababisha kutokea kwa fujo kanisani hapo,” alisema Paulo.
Kamanda Paulo alisema kwa mujibu wa taarifa za awali, chanzo cha vurugu hizo ni mgogoro wa uongozi wa Kanisa hilo, ambapo baadhi ya waumini hawamtaki mchungaji mpya aliyetokea Mbeya aitwaye Johnson Silumbwe (50).
Alifafanua, wakati polisi wakimshikilia Mnyilemi, wahutuhumiwa wengine wanaohusishwa kufanya vurugu hizo walitoroka na jeshi hilo linaendelea kuwatafuta.
Alisema watakapopatikana watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Naye, Mwandishi Claudia Kayombo anaripoti kutoka Dar es Salaam kuwa, Kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la Misheni Mashariki limevitaka vyama vya siasa kutoa wagombea waadilifu kwa kuwa, viongozi wa kisiasa wanayo nafasi kubwa katika kuleta mabadiliko kwa taifa kupitia maono, sera na uadilifu wao.
Katibu Mkuu wa jimbo hilo, Mchungaji Emmaus Mwamakula alitoa kauli hiyo juzi wakati akitoa salamu za mwaka mpya 2015 kwa Watanzania.
“Natoa mwito kwa vyama vya siasa watoe wagombea waadilifu kwa kuwa, viongozi wa kisiasa wanayo nafasi kubwa katika kuleta mabadiliko kwa taifa kupitia maono, sera na uadilifu wao.
“Kwa kuwa mwaka tunaouanza ni wa uchaguzi katika nchi yetu, ninapenda kutumia nafasi hii ili kugusia kuhusu uongozi mpya utakaochaguliwa katika ngazi za udiwani, ubunge na urais.”
“Kwa kuwa, mchakato wa uchaguzi unaanzia ngazi za uongozi wa vyama husika ambao ndiyo wenye majukumu ya kuwachuja wagombea wao, ningependa kutoa mwito hasa kwa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu za vyama vya siasa nchini kuhakikisha kuwa, vinateua majina ya watu walio waadilifu miongoni mwa watakaojitokeza kugombea kupitia vyama vyao.
“Ni dhahiri kuwa, kila chama kinao mfumo au chombo kitakachowasaidia kumjua mgombea mwenye sifa na mwadilifu,” alisema.
Alibainisha kuwa, vyama ambavyo vitaruhusu rushwa kuamua mshindi katika michakato yao ya ndani kwa kuwapitisha wagombea waliotoa rushwa kwa wajumbe wakati wa michakato, vitakuwa vinajijengea mazingira ya kushindwa kwa kuwa, wananchi watawakataa wagombea wa aina hiyo wakati wa uchaguzi.
Alisema uongozi ni kazi yenye heshima sana katika jamii yoyote, maana mwanzilishi wa uongozi ni Mungu mwenyewe.
Hata hivyo, alisema katika miaka ya hivi karibuni imejengeka tabia miongoni mwa wanasiasa na wale wanaowafanyia kampeni kuacha kutangaza sera zao na kuanza kujihusisha na kampeni chafu kwa njia ya kuwachafua wenzao.
“Tungependa jamii itambue kuwa, mtu yeyote anayetumia fedha nyingi katika kuwachafua wenzake wakati wa kampeni, anakuwa amekosa sifa za uongozi.
“Tunatoa mwito kwa watakaojitokeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuepuka kutumia lugha za vitisho na matusi dhidi ya wapinzani wao, iwe kabla au wakati wa kampeni,” alitanabaisha Mchungaji Mwamakula.
Aidha, alitoa mwito kwa asasi za kiraia kuelimisha jamii katika kipindi cha uchaguzi.
“Nitumie nafasi hii pia kutoa mwito kwa asasi mbalimbali kwa jamii kuwekeza katika elimu ya uraia wakati wote wa uchaguzi, kwa kuchapisha wasifu na historia fupi za wagombea ili wapiga kura na wananchi waweze kuwafahamu.
“Mpango huu utawasaidia wananchi kuwafahamu wagombea wengi, wakiwemo ambao uwezo wao wa kujitangaza kupitia vyombo vya habari utakuwa ni mdogo.

Saturday, January 3, 2015

New Alert! Polisi yawanasa Panya Road 36

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRFCKTrOSS6jQnrp-2w6J_KAENIsfm6tqqgJBEGvkXRlu4ZT6sIiNADLj1Mp7001DbrJDkTOTAD64AZsWES5iZkPYt7wtn1J0jgKfMpgrWCV7iFj1Z-88iz0YGNxnvpUE5rzYqkilwbLX8/s1600/4.jpg
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Suleiman Kova
JESHI la Polisi nchini linawashikilia vijana 36 wa kundi maarufu Panya Road wanaodaiwa kufanya vurugu na kupora mali za watu na kusababisha taharuki katika jiji la Dar es salaam huku baadhi ya wananchi wakitoa maoni tofauti kuhusiana na tukio hilo.
Akitoa ufafanuzi wa taharuki hiyo msemaji wa jeshi la polisi SSP ADVERA BULIMBA ambaye mbali na kuwatoa hofu wananchi kuwa hali hiyo haitajitokeza tena amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na vikundi vyovyote vinavyotaka kuvuruga amani ya nchi na kwamba endapo polisi wasingewadhibiti vijana hao mapema tangu wakiwa makaburini baada ya kumzika mwenzao aliyeuwawa na wananchi baada ya kuiba hali ingekuwa mbaya zadi.
  Kufuatia tukio hilo waandishi wa habari wamezunguka maeneo mbalimbali ya jiji yaliyodaiwa kukumbwa na tafrani hiyo ambapo baadhi ya wananchi wa maeneo ya magomeni ambako vurugu zilianzia wameelezea namna zilivyoanza hadi kusababisha watu kuanza kukimbia hovyo na wengine kuacha maduka yao wazi  na taarifa kusambaa maeneo mengine.
Katika maeneo ya mwananyamala na ubungo baadhi ya waliozungumzia sakata hilo wameitaka serikali kuangalia makundi ya vijana na ikiwezekana wapatiwe elimu ya ujasiriamali bure ili waweze kuendesha maisha huku wengine wakishauri vijana wasiokuwa na kazi mitaani wapelekwe jeshini wakafundishwe stadi za kazi pamoja na uzalendo ili kuepuka vitendo hivyo.
Taharuki hiyo ilitokea usiku wa tarehe mbili chanzo kikiwa ni kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la MOHAMED AYUB kuuwawa na wananchi tarehe mosi mwaka huu katika maeneo ya tandale kwa mtogole kwa tuhuma za wizi ambapo tarehe 2 maziko yalifanyika na taarifa zilizolifikia jeshi la polisi zilidai kuwa baada ya maziko vijana wenzake walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi.
  via..ITV

Kocha afichua Ronaldo kurudi Manchester Utd

http://img2.timeinc.net/people/i/2012/specials/sma/athletes/cristiano-ronaldo-1-435.jpg
Ronaldo
KOCHA Msaidizi wa zamani wa klabu ya Manchester United, Mike Phelan amesema kuwa nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anaweza kusikiliza kama klabu hiyo ikijaribu kumnunua tena.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno ametengeneza mahusiano mazuri na mashabiki wa klabu hiyo katika kipindi alichoichezea kabla ya kujiunga na Madrid kwa kitita cha paundi milioni 80.
Phelan anaamini kuwa Ronaldo anaweza kurejea United kwani alifurahia katika kipindi chote alichokuwepo hapo kwasababu ndio maisha yake ya soka yalipoanza kung’ara.
Pamoja na hayo Phelan anadhani kwasasa itakuwa mapema mno kwa Ronaldo kurejea Old Trafford hususani kutokana na mafanikio aliyopata na hadhani kama klabu hiyo inaweza kumruhusu.

Equatorial Guinea kumpa ulaji Becker

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2e/Esteban_Becker_Churukian.jpg/150px-Esteban_Becker_Churukian.jpg
Kocha Becker
WENYEJI wa michuano ya Mataifa ya Afrika, AFCON inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Januari 15, Guinea ya Ikweta wanajiandaa kumpa ulaji kocha Estaban Becker kuchukua mikoba iliyoachwa wazi na Andoni Goikoetxea waliyemtema.
Chama cha soka nchini humo, kiliamua kutomuongeza mkataba kocha huyo Goikoetxea uliomalizika Desemba 31 mwaka jana.
Rais wa chama hicho Andres Jorge Mbomio amedai kuwa wameamua kutomuongeza mkataba kocha huyo baada ya kukiuka masharti ya mkataba wa kwanza kwa kushindwa kusafiri na kikosi cha timu kwenda Ureno Desemba 16.
Guinea Ikweta iliyookoa jahazi la michauno huyo kwa kuipokea Morocco waliogoma kwa dai la tishio la ugonjwa wa Ebola, ina wiki mbili kuandaa kikosi chao kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ambapo wao watafungua dimba na Congo Brazzaville Januari 17 mwaka huu.

David Moyes amuita Steven Gerrard Real Sociedad

https://s.yimg.com/bt/api/res/1.2/fw0doU3LIH0xHkBkFbvYfA--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9ZmlsbDtoPTM3NztpbD1wbGFuZTtweG9mZj01MDtweW9mZj0wO3E9NzU7dz02NzA-/http://media.zenfs.com/en_GB/Sports/Eurosport/1382031-29636997-2560-1440.jpg
David Moyes akipeana mkono na Steven Gerrard
MENEJA wa zamani wa Manchester United, David Moyes amemfungulia milango Steven Gerrard kujiunga na klabu ya Real Sociedad mwishoni mwa msimu huu.
Moyes alikuwa na msimu mbaya wakati akiinoa United msimu wa 2013-2014 hali iliyopelekea kutimuliwa lakini sasa amepewa nafasi nyingine kwa kupewa kibarua cha kuinoa klabu hiyo ya Hispania.
Baada ya Gerrard kutangaza uamuzi wake wa kuondoka Liverpool baada ya mkataba kumalizika, Moyes amempa nafasi ya kufikiria kujiunga na Sociedad ili kupata changamoto mpya.
Moyes mwenye umri wa miaka 51 amesema Gerrard amecheza kwa mafanikio katika klabu yake hiyo na timu ya taifa ya Uingereza hivyo itakuwa ngumu kuziba pengo lake na kama angependa kwenda Hispania kucheza soka anajua kuwa anaweza kumpigia simu.
Naye meneja wa Southampton Ronaldo Koeman pia amedai kuwa katika kikosi chake kutakuwa na nafasi ya Gerrard kama atataka kujiunga nao.

Arsene Wenger awakata maini wanaotamani aondoke Arsenal

http://www.arsenal.com/assets/_files/scaled/510x250/aug_10/gun__1281108157_20100806_wenger_membersday1.jpg
Kocha Arsene Wenger
KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amewakata maini wanaodhani fujo wanazomfanyia zinaweza kumfanya aiteme timu hiyo.
Wenger amesisitiza kuwa asingeweza kuondoka katika timu hiyo hata kama wangeshindwa kunyakuwa Kombe la FA msimu uliopita. 
Arsenal walimaliza ukame wao wa vikombe wa miaka tisa kwa kuifunga Hull City kwa mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Wembley Mei mwaka jana. 
Akiulizwa na wanahabari kama angeondoka kwa kushindwa kunyakuwa Kombe la FA, Wenger amesema isingewezekana kwani hakuona umuhimu huo. 
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa katika mechi 1000 alizoisimamia Arsenal ameshinda 600 hiyo inamaanisha ana wastani wa ushindi kwa asilimia 60 hivyo haoni sababu ya kujiuzulu kwani anafanya kazi yake vyema. 
Wenger amesema anaheshimu mkataba wake na ataendelea kuutumikia mpaka hapo wakati wake utakapofika.

Huyu ndiye Mwanasheria Mkuu Mpya wa Serikali

Mwanasheria Mpya wa Tanzania, George Mcheche Masaju
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na: 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM. 
3 Januari, 2015

Simba yaona mwezi Mapinduzi, Mtibwa yabanwa

Kikosi cha Simba

Hekaheka katika pambano la Mtibwa na JKT (Picha: ZanziNews)
BAO la shuti kali la umbali wa mita 40 lililowekwa kimiani na kiungo Said Ndemla limeiwezesha Simba kufufua matumaini yao katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuibuka na ushindi mbele ya Mafunzo.
Simba ambao ilitoka kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa katika pambano lao la kwanza ilishuka dimbani ikiwa inaongozwa na kocha wake mpya, Mserbia Goran Kapunovic na ilienda mapumziko ikiwa suluhu dhidi ya timu hiyo ya visiwani Zanzibar.
Katika kipindi cha pili kilikuwa chenye kasi zaidi kwa timu zote na Simba ilipata bao pekee lililofungwa na Ndemla katika dakika ya 54 baada ya kuipokea pasi ya Hassan Kessy na kufumua shuti kali lililomshinda kipa Hashim Haruna na kuwapa faraja mashabiki wa Msimbazi ambao walikuwa hawana raha baada ya timu yao kupokea kipigo cha Mtibwa ikiwa ni siku chache tangu ilale kwenye ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar.
Katika pambano jingine la michuano hiyo lililochezwa mapema, Mtibwa Sugar na JKU zilishindwa kutambiana baada ya kwenda sare ya 1-1 huku Mtibwa ikijilaumu kwa kukosa penati iliyopotezwa na Mussa Hassan Mgosi aliyetangulia kuifungia Mtibwa bao kabla ya JKU kurejesha kupitia kwa Amour.
Michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa pambano la mapema litakalowakutanisha mabingwa watetezi KCCA ya Uganda dhidi ya Mtende kisha Yanga kuvaana na  Polisi Zanzibar jioni na usiku kushuhudia Azam ikipepetana na KMKM.

Kagera yashindwa kuzing'oa Yanga, Azam, Coastal yapigwa kidude

http://tplboard.co.tz/assets/uploads/files/ded5f-kagera-sugar1.png
Kagera Sugar walioshindwa kutamba mbele ya Ruvu Shooting
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/HMB_39851.jpg
Coastal Union waliopigwa kudude kimoja na JKT Ruvu
TIMU ya soka ya Kagera Sugar imeshinda kuzipiku Yanga na Azam kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare isiyo na mabao kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi dhidi ya wenyeji wa Ruvu Shooting, huku Coastal Union ikikubali kipigo nyumbani.
Kagera ilikuwa na nafasi ya kuzipiku Yanga na Azam ambazo zipo visiwani Zanzibar zikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi kwani kama ingeshinda mchezo wa leo ingefikisha pointi 16 na kulingana na Mtibwa Sugar na kuziondoa mabingwa hao wenza walio na pointi 14.
Hata hivyo suluhu hiyo imeisaidia timu hiyo kujimarisha kwenye nafasi ya nne ikilingana na Yanga na Azam na kutofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, Coastal Union ilikubali kipigo cha bao 1-0 nyumbani Mkwakwani mbele ya maafande wa JKT Ruvu inayonolewa na kocha Fred Felix Minziro.
Ushindi huo umeifanya Ruvu uliotokana na bao la dakika ya 38 lililofungwa na Samuel Kamuntu umeifanya ikwee hadi nafasi ya sita ikiwa nyuma ya Polisi Moro wanaolingana nao pointi 13 baada ya maafande hao wa Morogoro kupata sare isiyo na magoli na Stand United katika pambano jingine lililochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri.
Wagosi wa Kaya wenyewe wameporomoka kwa kipigo hicho hadi nafasi ya sita wakiwa na pointi 12 baada ya mechi tisa walizocheza.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa pambano moja tu kati ya wenyeji Prisons Mbeya dhidi ya Ndanda Fc ya Mtwara wanaouguza kipigo cha bao 1-0 ilichopewa katika mechi yao ya wiki iliyopita dhidi ya Mbeya City.