
STRIKA

USILIKOSE

Monday, February 23, 2015
Irene Uwoya aibarishia Kisoda kufunika 2015
![]() |
Irene Uwoya |
Akizungumza na MICHARAZO, Irene anayefahamika kama 'Oprah' au Mama Krish, alisema kuwa kwa namna filamu hiyo ilivyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu ya kushirikisha nyota mbalimbali wa Tanzania na wale wa kimataifa ana imani ya kufunika 2015.
Irene alisema ingawa siyo vema kuanza kujisifia kabla hata filamu hiyo haijainguia sokoni, lakini anawataka mashabiki wake kuisubiri kuipokea kabla ya Pasaka kuweza kuthibitisha maelezo yake.
"Huwa sina utamaduni wa kupenda kujifagilia, lakini mashabiki wangu waisubiri 'Kisoda' waone utofauti, naamini itafunika kuliko hata 'Apple'," alisema Irene ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Apple Film Production.
Irene alisema kuna mambo yaliyokwamisha filamu hiyo kutoka mapema kama alivyokuwa amepanga, lakini mara baada ya kuhaririwa itaachiwa na kufanyiwa uzinduzi wake kabla ya Pasaka inayotarajiwa kuadhimishwa mwanzoni mwa Aprili.
Twiga Stars waingia kambini kujiwinda kimataifa
Kocha wa Twiga Stars |
Baadhi ya nyota wa Twiga Stars walioitwa kambini |
Kaijage ametangaza programu yake ya mazoezi itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye mchezo wa awali.
Twiga Stars ambayo imeingia kambini jana Jumapili na itakuwa kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF zilizopo Karume, imefuzu moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
Wachezaji walioitwa na kuingia kambini ni pamoja na Asha Rashid 'Mwalala', Esther Chaburuma 'Lunyamila', Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah, Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph, Dawa Haji Vuai, Belina Julius na Amina Ramadhani.
Mwili wa Mez B kuzikwa leo mjini Dodoma


MWILI wa msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Moses Bushagama maarufu kama Mez B aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita wakati akikimbizwa hospitalini unatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Wahanga wa Treni yaliyopo Mailimbili mjini Dodoma.
Taarifa
iliyotolewa na mama yake Mez B, Merry
Katambi alisema shughuli ya kumuaga
mwanae itafanyika Viwanja vya Nyerere Square Mjini hapa.
Mazishi hayo
kwenye viwanja vya Nyerere yataambatana na ibada ya kumuombea na yanatarajiwa
kuanza saa saba mchana.
"Mwanangu tutamzika Jumatatu (leo) katika
Makaburi ya wahanga wa Treni Mailimbili ila ibada pamoja na kuuga mwili wa
marehemu zitafanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere’’
Mez B
alikuwa ni mwanzilishi wa kundi la Chemba Squard ambapo alikuwa pamoja na Dar
Master, Noorah na Albert Mangwea huku akitamba na nyimbo za 'Kikuku cha Mama
Rhoda', 'Nimekubali' na 'Kama Vipi iliyomjengea jina kubwa kwa mashabiki wa muziki kabla ya 'kuzimika'.
Mourinho 'alianzisha' tena England, kisa sare na Burnley

Mourinho ameyasema hayo baada ya kutoka sare ya 1-1 na Burnley kwenye uwanja wa nyumbani wa Stamford Bridge ambapo amelaumu maamuzi ya mwamuzi Martin Alkinson.
Alkinson alimuonesha kadi nyekundu kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic na atakosa mechi ya jumamosi ya fainali ya kombe la ligi dhidi ya Tottenham baada ya kadi nyekundu ya dakika ya 69.
Mourinho anadai Ashley Barnes alitakiwa kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Martic na kulikosababisha kiungo wake amsukume mshambuliaji huyo wa Burnley na kuambulia kadi nyekundu.
Pia alitakiwa kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kitendo cha kumsukuma Branislav Ivanovic.
Mourinho anaamini haki haikutendeka ambapo walinyimwa penalti mbili kwani Michael Kightly aliunawa mpira wa shuti la Ivanovic katika dakika ya 33′ na nahodha wa Burnley Jason Shackell alimsukuma Diego Costa eneo la hatari dakika chache kabla ya mapumziko.
Chelsesa bao ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 60, wajkifuatiwa kwa mbali na Manchester City ambao walitoa kipigo cha 'Paka Mwizi' kwa Newcastle United kwa kuizabua mabao 5-0 na kufikisha pointi 55.
Kocha Southampton kumuadhibu Sadio Mane, kisa...!
![]() |
Sadio Mane akichuana na Coutinho katika mechi yao ya jana dhidi uya Liverpool na kulala nyumbani 2-0 |
Mane alikuwepo katika kikosi kilichowakabili wakali wa Merseyside kwa kufika baada ya nusu saa kupita kutoka muda waliopanga kufika, saa saba mchana.
Pia mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal anakabiliwa na adhabu nyingine ya kutozingatia muda.
“Alichelewa kwa dakika 25-30 kabla ya mechi”, amethibitisha Koeman.
“Tuna kanuni na maelekezo kwa wachezaji. Kila mtu anaweza kuchelewa siku moja asubuhi, lakini huwezi kuchelewa kufika saa saba wakati unacheza dhidi ya Liverpool.
“Hakutoa maelezo? Maelezo hayo ni baina ya kocha na mchezaji, lakini alichelewa.
‘Siwezi na sikubaliani na hilo. Kama ni kulipa faini alipe tu”
Mdudu wa sare ahamia Azam, yabanwa na Prisons
![]() |
Azam waliolazimishwa sare isiyo na mabao na Prisons-Mbeya |
Sare hiyo ya pili mfululizzo kwa Azam imetoa nafasi kwa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kutanua pengo lake la uongozi hadi kuwa pointi nne licha ya timu zote mbili kucheza mechi 15 kila mmoja.
Yanga inaoongoza ikiwa na pointi 31 baada ya kuvuna pointi 6 jijini Mbeya kwa kuzichapa Prisons na Mbeya City kwa mabao 3-0 na 3-1, wakati Azam kwa kupoteza pointi nne wamekusanya pointi 27.
Pambano hilo la Azam an Prisons lilichezwa usiku kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi na sare hiyo isiyo na mabao imewapa afueni maafande wa Prisons waliofikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi 15.
Sunday, February 22, 2015
Liverpool yaua, Spurs, Everton zabanwa nyumbani
Hivi ndivyo vita vya Liverpool na wenyeji wao Soputhmapton ilivyokuwa Victor Wanyama akichuana na Jordan Hendeson |
WAKATI klabu ya Tottenham Hotspur ikilamizika kupigana kiume kurejesha mabao mawili ili wasife nyumbani mbele ya West Ham Utd, Liverpool wameendelea kutoa dozi kwa kuicharaza Southampton kwa mabao 2-0 katika mfululzii wa Ligi Kuu ya England.
Spurs ikiwa nyumbani ilitanguliwa kufungwa mabao 2-0 kabla ya kuyarejesha baadaye na kuambulia sare ya mabao 2-2, shukrani za pekee zieende kwa Harry Kane aliyefunga bao la kusawazisha baada ya awali kukosa penati na mpira kumrudia na kuutumbukiza wavuni.
Katika mchezo mwingine timu ya mkiani ya Leicester City ilijitutumua na kulazimisha sare ya ugenini ya mabao 2-2 dhidi ya Everton kabla ya hivi punde Liverpool kuandikisha ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Southampton.
Mabao ya Phillipe Coutinho katika dakika ya tatu na jingine la kipindi cha pili lililofungwa na Raheem Sterling liliwapa vijogoo hao wa Anfield kupata ushindi huo uliowafanya wafikishe jumla ya pointi 45 na kulingana Spurs ingawa wameshindwa kuiengua Southampton katika nafasi ya tano wakati ligi ikiwa ipo raundi ya 26.
Katika pambano hilo wenyeji walilalamika kunyimwa penati mbili za wazi baada ya wachezaji wao kufanyiwa madhambi langoni mwa Liverpool.
Mwadui Fc ndiyo mabingwa wa FDL2014-2015
![]() |
Kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelu 'Julio |
![]() |
Mabingwa wa FDL,. Mwadui Shinyanga walioizabua Wana Kimanumanu kwa bao 1-0 |
Mwadui imeibuka na ushindi huo katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi na kuzima ngebe za wapinzani wao waliotamba awali kushinda pambano hilo kudhihirisha kuwa Mwadui ni 'vibabu'.
Hata hivyo tambo hizo za Wana Kimanumanu zilizimwa kwa bao tamu la kichwa lililofungwa na Kelvin Sabato 'Kiduku' na kuwapa taji Mwadui ambao waliongoza katika kundi lao la ligi daraja la kwanza na kupanda Ligi Kuu msimu wa 2015-2016 mwaka mmoja baada ya kubaniwa na TFF msimu uliopita.
Mbali na Mwadui, nyingine zilizopanda ligi hiyo msimu ujao kuchukua nafasi ya timu nne zitgakazoshuka katika Ligi ya msimu huu inayozidi kushika kasi ni Africans Sports, Toto Africans na Majimaji-Songea.
Mnyama afa Shinyanga, Stand Utd yaifanyizia
![]() |
Kikosi cha Simba |
Kipigo hicho kimetolewa kwa Simba na timu ya Stand United katika pambano tamu lililochezwa kwenyue uwanja wa Kambarage na kuzima mbwembwe za vijana wa Msimbazi huku mashabiki wao wakiibua zogo.
Zogo hilo lililosababisha pambano hilo kusimama kwa muda ilitokana na imani kwamba lango la wapinzani wao lilikuwa limefukiwa 'vitu' ambavyo vilikuwa vikiwafanya vijana wao kushindwa kufunga mabao.
Bao pekee lililowaua Simba ya kocha Goran Kopunovic, liliwekwa kimiani na Mnigeria Absalim Chiibibele likiwa ni bao lake la tano msimu huu katika dakika ya 11 na kuwafanya Simba kuhaha kurirejesha bila mafanikio.
Kwa kipigo hicho Simba imesaliwa na pointi pointi 20 baada ya mechi 16 wakati Stand imefikisha pointi 18 baada ya mechi 16 pia na itavaana na Kagera Sugar katika mechi yao ijayo mjini Shinyanga.
Yanga 'watamu' kama Mcharo! Yaifumua Mbeya City
![]() |
Simon Msuva aliyeanza kufungua neema ya mabao Mbeya leo |
![]() |
Mrisho Ngassa akadhihrisha amerejea upya Jangwani |
![]() |
Amissi Tambwe akamaliza udhia kwa kufunga bao la tatu |
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulichezwa kwenye uwanja wa Sokoine na kuiwezesha Yanga kuibuka na ushindi huo mnono ulioifanya izidi kujizatiti kileleni ikiwa na pointi 31 baada ya mechi 15.
Simon Msuva alianza kufunga katika kipindi kwanza kabla ya Ngassa 'kuzawadiwa' bao mara baada ya kipindi cha pili kutokana na mbwembwe za kipa David Burhan wa Mbeya City kumpoza.
Kipa huyo Bora wa msimu wa 2012-2013, alirudishiwa mpira na Steven Mazanda na badala ya kuupiga mbele alijaribu kumpiga chenga Ngassa aliyeunasa kilaini na kutumbukiza wavuni kaundika bao la pili la Yanga.
Amissi Tambwe aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Haruna Niyonzima na kuiandikia bao la tatu, wakati huo tayari wenyeji alishapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Peter Mapunda.
Bao hilo la Mapunda limeitibua rekodi ya kipa Ally Mustafa 'Barthez'ambaye alikuwa amecheza muda wa dakika 704 bila kuruhusu wavu wake kutikiswa. Dakika hizo ni 630 za mechi sita na 74 za leo kabla ya Mapunda kumtungua kufuatia mabeki wake kushindwa kuokoa.
Kwa ushindi huo Yanga imejikita kileleni ikiwa na pointi 31 baada ya mechi 15 ikijiandaa kuondoka nchini kwenda Botswana kurudiana na BDF XI katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Simanzi! Christopher Alex hatunaye duniani!
![]() |
Christopher Alex (wa tatu toka kulia) enzi za uhai wake akiwa na kikosi kilichoing'oa Zamalek mwaka 2003 |
Kwa mujibu wa taarifa ambazo MICHARAZO imezipata mapema zinasema kuwa, kiungo huyo aliyekuwa akiugua kwa muda mrefu amefariki akiwa kalazwa katika Hospitali ya Milembe, iliyopo mkoani Morogoro.
Alex, anayekumbukwa kwa kupiga penati ya mwisho ya Simba iliyowavua ubingwa Zamalek ya Misri katika pambano la Ligi ya Mabingwa kati yao iliyochezwa mwaka 2013, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kifua.
Mama mzazi wa Alex amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambaye alikuwa akiishi naye na kumuuguza kwa msaada wa wasamaria wema wakiwamo wadau wa soka.
Wakati klabu yake ya zamani ikiwa 'Ãmemsusa', mashabiki wa klabu hiyo na wengine wa soka walikuwa bega kwa bega na mama huyo kwa kuchangia fedha za matibabu, harambe kubwa ikiendeshwa na kituo cha Cloud's FM
Marehemu Christopher Alex, alizaliwa Septemba 12, 1975, na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Uhuru na kumaliza katika shule ya Chamwino huko Dodoma mwaka 1993.
Alianza kucheza mpira kwenye timu ya daraja la nne ya Chamwino Utd na baadaye daraja la tatu akiwa na kikosi cha Aston Villa nayo ya Dodoma.
Mwaka 1999-2001, aliitumikia klabu ya CDA ya Dodoma, kabla ya kutimkia klabu ya Reli ya Morogoro mwaka 2002, na baadaye kujiunga na Wekundu wa Msimbazi Simba.
Marehemu ameacha mtoto mmoja aitwaye Alex.
MICHARAZO inatoa pole kwa ndugu, jamaa na familia nzima ya marehemu Alex kwa msiba huo na kuwaombea Subira kwa Mungu kwa kukumbuka kuwa 'Kila Nafsi Itaonja Mauti'
Mungu aiweke roho ya marehemu Alex Mahali Pema Ameen!
Bingwa wa FDL kujulikana leo Chamazi
![]() |
Mwadui Shinyanga |
Africans Sports 'Wana Kimanumanu' |
Awali mchezo huo wa fainali ulikuwa umepangwa kufanyika kwenye
dimba la Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF imepelekea mchezo huo kuhamishiwa
Chamazi.
Mchezo huo wa fainali utaanza saa 10 kamili jioni, na utaonyeshwa moja
kwa moja na kituo cha Azam TV ili kuwapa nafasi wapenzi na wadau wa soka waliopo
mbali na hasa mikoani kuweza kushuhudia mchezo huo.
Bingwa wa Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza atazawadiwa Kombe pamoja na
medali, huku mshindi wa pili akipata kikombe na medali pia.
Viingilio vya mchezo huo ni tsh.5,000 kwa jukwaa kuu na tsh. 3,000 kwa majukwaa
ya mzunguko.
Mo Farah aweka rekodi ya dunia
![]() |
Mwanariadha Mo Farah akimaliza mbio na kuweka rekodi mpya Birmingham |
LONDON, England
MWANARIADHA Muingereza Mo Farah amevunja rekodi ya dunia ya mbio za
ndani za Maili Mbili katika mbio za Birmingham Indoor Grand Prix.
Farah, 31, aliondoka uwanjani baada ya kumaliza mbio hizo kwa
kutumia dakika 3.40 akiivunja rekodi iliyotanguliwa iliyowekwa na Muethiopia Kenenisa
Bekele.
Hiyo ni rekodi ya kwanza kuwekwa na mwanariadha huyo bingwa mara
mbili wa Olimpiki.
"Hii ina maana kubwa kwangu, " alisema Farah. "Napenda
kuliwakilisha taifa langu, kutoa kitu fulani kwa watu wote. Siamini. "
Maandalizi ya kabla ya kuanza kwa mbio hizo za Jumamosi
yalitawaliwa na malumbano dhidi ya mchezaji mwenzake Muingereza Andy Vernon.
Farah alidai kuwa Vernon alihoji uraia wake baada ya bingwa huyo
mara mbili wa Olimpiki kushinda mbio za Ulaya za mita 10,000 mwaka 2014, huku Vernon
akielezea kuwa huo ulikuwa ni upotoshaji mkubwa.
Pamoja na suala hilo lakini Farah hakutetereka kwani alitawala
mbio hizo zilizofanyika jijini Birmingham, na kuwaacha Mkenya Paul Koech na
Mmarekani Bernard Lagat na kushinda mbio hizo.
"Ni (malumbano na Vernon) ndio yaliyonihamasisha mimi,
nilitaka kufanya hivyo, " alisema Farah.
Simba, Yanga Azam katika vita nyingine VPL
Kikosi cha Simba kitakachokuwa mjini Shinyanga, |
Azam watakuwa uwanja wa nyumbani wa Chamazi |
Kikosi cha Yanga kilichopo ugenini jijini Mbeya kuvaana na Mbeya City |
Vinara Yanga wenyewe watakuwa kwenye uwanja wa Sokoine kwa mara nyingine tena kupepetana na wenyeji wao Mbeya City, ikiwa ni siku chache baada ya kugawa dozi ya mabao 3-0 dhidi ya Prisons.
Simba walioanza kushika kasi katika ligi hiyo baada ya kuchechemea kwa muda mrefu, pia ipo ugenini mkoani Shinyanga kwa ajili ya kupepetana na Stand United kwenye uwanja wa Kambarage.
Mabingwa watetezi Azam watakuwa uwanja wa nyumbani wa Azam Complex, Chamazi kuikaribisha Prisons-Mbeya baada ya katikati ya wiki kubanwa mbavu na Ruvu Shooting na kutoka suluhu ya 0-0.
Yanga watakuwa na hamu ya kuendeleza rekodi yao ya kushinda mfululizo, ingawa Mbeya City ambayo imekuwa haina msimu mzuri safari hii ikiwa imeapa kumaliza uteja kwa wapinzani wao hao.
Mbeya City iliyopanda ligi kuu msimu uliopita, haijawahi kuifunga Yanga zaidi ya kulazimisha sare au kuambulia vipigo, kitu ambacho Kocha wake, Juma Mwambusi anaamini leo watavunja mwiko.
Hata hivyo Yanga imetamba kutaka kutoa dozi kwa lengo la kuongeza morali kabla ya kuondoka nchini kwenda Botswana kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI.
Yanga inayoongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 28, mbili zaidi ya Azam yenye 26 itarudiana na BDF wiki ijayo mjini Gaborone baada ya wiki iliyopita kuwacharaza mabao 2-0.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema hawaoni cha kuwazuia kuvuna pointi nyingine tatu jijini Mbeya wakati kikosi chao kimeandaliwa vema na kina morali mkubwa.
Muro alisema anafahamu Mbeya City ni timu ngumu na itataka kutumia vema uwanja wa nyumbani, lakini Yanga imejipanga kutoka na pointi zote ili kujikita zaidi kileleni kabla ya kwenda Botswana.
Wakati Yanga na Mbeya wakiwindana hivyo, Simba wenyewe wakiwa na furaha ya ushindi wa mabao 2-0 iliyopata ugenini mjini Morogoro dhidi ya Polisi wataivaa Stand United wakiwa na tahadhari kubwa.
Stand Utd imetoka kuwatoa nishai Mgambo JKT kwa kuicharaza mabao 4-1, kitu ambacho kinaonyesha namna gani wameanza kuizoea ligi hiyo wanayoicheza kwa msimu wao wa kwanza.
Katika pambano hilo kila timu itakuwa ikitegemea nyota wake, Simba ikitambia akina Emmanuel Okwi, Dan Sserunkuma, Eliasi Maguri na wengine huku Stand ikimtegemea Mnigeria Abasalim Chiibibele na Heri Mohammed wenye mabao manne kila mmoja katika ligi hiyo.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Oktoba 4, mwaka jana timu hizo zilizoshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wa Taifa.
Angalia msimamo wa Ligi Kuu ulivyo:
P W D L F A GD Pts
01. Yanga 14 08 04 02 18 07 11 28
02. Azam 14 07 05 02 22 12 10 26
03. Kagera Sugar 16 06 06 04 13 11 02 24
04. Simba 14 04 08 02 15 11 04 20
05. Ruvu Shooting 15 05 05 05 10 11 -1 20
06. Mtibwa Sugar 15 04 07 04 15 15 00 19
07. Coastal Union 16 04 07 05 11 11 00 19
08. Polisi Moro 16 04 07 05 12 14 -2 19
09. JKT Ruvu 15 05 04 06 14 15 -1 19
10. Ndanda Fc 16 05 04 07 14 18 -4 19
11. Mbeya City 14 04 05 05 09 11 -2 17
12. Mgambo JKT 14 05 02 07 08 15 -7 17
13.Stand Utd 15 03 06 06 13 18 -5 15
14. Prisons 14 01 08 05 10 15 -5 11
Wafungaji:
8- Didier Kavumbagu(Azam)
7- Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ame Ali (Mtibwa), Simon Msuva (Yanga),
5-Danny Mrwanda (Yanga), Kipre Tchetche (Azam)
4- Rama Salim (Coastal), Emmanuel Okwi (Simba), Nassor Kapama, Jacob Massawe (Ndanda), Heri Mohammed, Abasalim Chiibibele (Stand Utd) , Malimi Busungu (Mgambo)
3- Ally Shomari (Mtibwa), Frank Domayo (Azam), Atupele Green (Kagera)
2- Shaaban Kisiga, Dan Sserunkuma, Elias Maguli (Simba), Salum Kanoni, (Kagera Sugar) Aggrey Morris (Azam), Najim Magulu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Amissi Tambwe, Jerry Tegete, Mrisho Ngassa, Andrey Coutinho (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Mussa Said (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi),Yahya Tumbo (Ruvu Shooting)
Saturday, February 21, 2015
Chelsea wabanwa, Man Utd yafa, Arsenal raha
![]() | ||
Ben Mee akiisawazishia Burnley bao kwa kichwa |
![]() |
Oyooooooooooo! |
![]() |
hoi |
![]() |
Arsenal kwa raha zao |
![]() |
ilikuwa vita |
![]() |
QPR walip[okuwa wakizamishwa ugenini |
Chelsea wakiwa kwenye uwanja wao wa Stanford Bridge walitangulia kuandika bao la kuongoza lililofungwa na beki wake Branslav Ivanovic katika ya 14 na wageni Burnley kuchomoa bao hilo dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa Ben Mee.
Chelsea itajilaulumu kwa kushindwa kuibuka na ushindi nyumbani kutokana na kutawala mchezo huo na washambuliaji wake Eden Hazard na Diego Costa wakikosa mabao ya wazi.
Sare hiyo imeifanya Chelsea kufikisha pointi 60 na kutoa fursa kwa wapinzani wao mabingwa watetezi Manchester City kupunguza pointi zilizokuwapo kwani mpaka muda huu wa mapumziko City wanaoongozxa mabao 3-0 dhidi ya Newcastle United.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Arsenal ikiwa ugenini imeshinda mabao 2-1, Manchester Utd ikipigwa 2-1 na Swansea City, wakati Aston Villa wameendelea kutetepa kwa kukubali kichapo cha 2-1 wakiwa nyumbani toka kwa Stoke City huku QPR wakilala ugenini 2-1 mbele ya Hully City na timu za Sunderland na West Bromwich wakitoka suluhu ya kutofungana.
Barcelona yazamishwa nyumbani na Malaga
![]() |
Juanmi akiitungua Barcelona leo |
![]() |
Messi hakufua dafu leo kwa Malaga siku chache kabla ya Barcelona kuvaana na Manchester City kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya |
Kipigo hicho cha nne kwa Barcelona msimu huu katika ligi hiyo kimezidi kuongeza ushindani wa mbio za ubingwa dhidi ya watetezi Real Madrid ambayo watashuka dimbani kesho wakiwa ugenini.
Bao pekee la wageni Malaga mbele ya Barcelona liliwekwa kimiani na Juanmi katika dakika ya saba ya mchezo huo na kungángánia hadi mwisho na kuwaacha Barcelona wakiwa hoi nyumbani.
Mechi nyingine inayochezwa hivi sasa Valencia wakiwa ugenini waongoza bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Cardoba.
Jahazi la Mtibwa lazidi kuzama, Coastal hoi, Kagera yaua
Mtibwa Sugar iliyoipokea kichapo cha nne mfululizo leo kwa Mgambo JKT |
![]() |
Kagera Sugar waliongára Kambarage kwa kuilaza Polisi Moro |
Polisi Moro wliopoteza mchezo wa pili leo mbele ya Kagera Sugar baada ya wiki iliyopita kulala kwa Simba 2-0 |
Ndanda iliyotakata nyumbani Mtwara kwa kuilaza Coastal Union 1-0 |
Kipigo hicho cha Mtibwa kimeifanya timu hiyo kuzidi kuporomoka kwenye msimamo wa ligi hiyo wakisaliwa na pointi zao 19 baad ya mechi 15.
Bao lililoizamisha Mtibwa katika pambano hilo lililochezwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga, liliwekwa kimiani na Malimi Busungu katika dakika ya 36 na kuifanya timu yao kufikisha pointi 17.
Katika mchezo mwingine ul;iochezwa Nangwanda Sijaona, wenyeji Ndanda waliinyuka Coastal Union kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Jacob Massawe katika dakika ya 79.
Aidha Kagera Sugar wakwia uwanja wa Kambarage Shinyanga wanaoutumia kama uwanja wao wa nyumbani, iliendelea kutakata baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Moro.
Bao hilo pekee lililowapa ushindi Kagera na kuzidi kujikita nafasi ya tatu ikifikisha pointi 24 liliwekwa kimiani na Rashid Mandawa ambaye anafikisha bao lake la saba katika ligi hiyo, bao moja nyuma dhidi ya kinara wa mabao kwa sasa wa ligi hiyo Didier Kavumbagu wa Azam.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo mitatu, Yanga wakiwa uwanja wa Sokoine Mbeya kupapetana na Mbeya City, Simba watakuwa wageni wa Stand Utd mjini Shinyanga na Azam watauamana na Prisons Mbeya uwanja wa Chamazi.
Mechi hiyo ya Azam na maafande itachezwa saa 2 usiku na kila timu imetamba kujiandikishia ushindi katika pambano hilo.
Friday, February 20, 2015
Yamoto Band watua UK tayari kwa shoo wa kesho
Kikosi kizima cha Yamoto Band ndani ya jiji la London tayari kwa makamuzi ya jumamosi hii ndani ya ukumbi wa Royal Regency Monor Park London
Yamoto Band Touchdown London this morning., safe and sound.Now let's Get it...Let's Goooo. ..Made in East Africa 2015 ,Yamoto band Live in London Royal Regency Banquite .
Wakijiachia na mmoja wa mabosi wake |
Enock Bella akiosha maji |
Wacheza filamu nchini waonywa
Mlela akipeana mkono na Katibu Mtendani wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisoo |
WASANII wa filamu nchini wameshauriwa kutumia taaluma waliyonayo kupanua wigo wa filamu nchini na kuitangaza Tanzania duniani kote kwa kuzingatia matumizi mazuri ya lugha ya Kiswahili katika filamu wanazozitengeneza.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Joyce Fisoo, juzi alipokutana na wasanii waliotarajia kuondoka jana kwenda Uingereza kurekodi filamu ya 'Sabasi' na Kampuni ya Didas Entertainment iliyopo nchini humo.
Fisoo alisema kuwa baadhi ya wasanii nchini wamekuwa makontena yanayopitisha biashara haramu kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine hivyo kuwaomba wasanii wanaokwenda Uingereza kuachana na tabia hiyo bali watumie fursa waliyoipata kuiwakilisha Tanzania vizuri na kutengeneza filamu bora itakayowawezesha kujulikana na kufungua fursa za kushirikishwa katika filamu na nchi nyingine duniani.
Aidha, Fisoo aliwataka wasanii hao kuheshimu sheria, kanuni na taratibu za Uingereza kwani kwa kufanya hivyo watakuwa mabalozi bora na kutoa nafasi kwa wasanii wengine kupata fursa hizo.
Naye Mama wa Didas Entertainment, Nuru Idrisa, aliwataka wasanii wa Bongo Movie waliopata nafasi ya kurekodi filamu na Didas Entertainment kujiheshimu na kuvaa mavazi ya staha yatakayostiri miili yao muda wote watakaokuwa nchini Uingereza kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamelinda heshima ya nchi.
Akitoa neno la shukrani, msanii wa Bongo Movie, Yusuph Mlela, aliishukuru Bodi ya Filamu kwa kuwa bega kwa bega na wasanii na kuwaahidi wadau wa filamu nchini kazi bora na yenye tija katika jamii.
Filamu ya 'Sabasi' inatarajiwa kurekodiwa hivi karibuni nchini Uingereza na Kampuni ya Didas Entertainment na kuwashirikisha wasanii Mlela, Esha Buhet na Husna Athumani, na ni filamu ya pili kurekodiwa na kampuni hiyo na kuwashirikisha wasanii kutoka Tanzania. Filamu ya kwanza kurekodiwa na kampuni hiyo iliyowashirikisha wasanii kutoka Tanzania ni ile ijulikanayo kwa jina la 'Mateso Yangu Ughaibuni'.
Balotelli alianzisha tena Liverpool
![]() |
Muunganiko wa picha zilizochapishwa na Daily Mail zinazomuonyesha Balotelli na nahodha wake, Steven Gerrard |
![]() |
Balotelli akifunga penati yake |

Kitendo chake cha kulazimisha kuipiga penati hiyo kimemtibua nahodha wa timu ya Liverpool Steven
Gerrard anayemshutumu kwa utovu wa nidhamu.
Balotelli alifunga penalti hiyo na
kuiwezesha Liverpool kuibuka washindi wa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Ndogo ya Ulaya, katika uwanja wa
Anfield.Hali hiyo ilijitokeza baada ya kushindwa kuelewana na
nahodha wa mchezo huo Henderson na Daniel Sturridge juu ya nani abebe
jukumu la kupiga penalti hiyo.Gerrard amesema: "Henderson ni nahodha na Balotelli kwa kiasi fulani alionyesha kumkosea adabu katika hali hiyo."
Gerrard ambaye kwa sasa ni majeruhi, alikuwa mchambuzi katika matangazo ya mchezo huo kwenye televisheni ya ITV ya nchini Uingereza.
Katika mechi nyingine timu ya Tottenham Hotspur ililazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Fiorentina wakati Everton wakipata ushindi mnono wa mabao 4-1 ugenini dhidi ya Young Boys ya Uswisi.
Subscribe to:
Posts (Atom)