MBONA freshi tu! Kocha wa klabu ya NEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa Jack Wilshere anaweza kuitumikia klabu hiyo kwa kipindi kirefu mbele ya safari huku akisisitiza kuwa kiungo huyo hana chochote cha kumuonyesha zaidi ya kuwa fiti. Wilshere ameenda kwa mkopo wa msimu mzima katika klabu ya AFC Bournemouth dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili majira ya kiangazi halijafungwa ikiwa kama sehemu ya mikakati ya kujijenga upya kufuatia kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara katika misimu miwili iliyopita. Akizungumza kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Southampton, Wenger alipuuza habari kuwa amekuwa haelewani na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye amekuwa akimtaja kuwa na uwezo mkubwa.
Kocha Wenger alisema alizungumza na Wilshere naye alimwambia hadhani kama ataweza kupata muda wa kutosha kucheza akibakia hapo kwa vile anataka kucheza zaidi msimu huu baada ya kupona majeruhi yake.
Wengeraliendelea kudai kuwa alimruhusu kuondoka kwasababu alikuwa hawezi kumuahidi muda wa kutosha wa kucheza kama alivyotaka mwenyewe.
USIYEMPENDA Kaja. Ndivyo ambavyo Osasuna watakuwa wanawaza sana, baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo yupo fiti na kesho huenda akashuka uwanjani kuvaana nao.




LIVERPOOL iliyoanza vema Ligi Kuu ya England msimu huu kwa kuikandika Arsenal kwa mabao 4-3 inatarajia kucheza mechi zake tatu zinazofuata ikiwa ugenini kitu ambacho si cha kawaida.














CHILE imetinga fainali za Copa America kwa mara ya pili mfululizo na watavaana na Argentina katiak mechi inayorejea fainali za mwaka jana ambapo ilibeba taji kwa ushindi wa bao 1-0.



WAMEPANIA si mchezo. Mabingwa wa soka Ulaya, Real Madrid wamethibitisha kuwa Alvaro Morata atarejea Santiago Bernabeu kipindi hiki cha kiangazi. Taarifa z klabu hiyo zinasema kuwa, hakuna kizuia kwa mkali huyo kurudia nyumbani.
WANAMCHUKUA. Klabu ya Manchester City, ipo hatua ya mwisho kumnasa straika wa kimataifa wa Hispania, Nolito kutoka Celta Vigo. 

Sept 10, 2016
Nov 05, 2016Bournemouth v Sunderland