Wadau,
Safari ya kupambana na ufisadi katika nchi hii ni ngumu sana. Leo kuanzia saa 5 hadi saa 8:30 mchana, Mhariri Mtendaji wa Jamhuri, Deo Balile, amehojiwa Makao Makuu ya Polisi kuhusu habari iliyochapishwa kwenye Jamhuri inayohusu “Ufisadi ujio wa marais 11” Kwa bahati nzuri, habari nzima wanaikubali kwamba ni ya kweli! Kasoro pekee eti ni matumizi ya barua ya Ikulu iliyokuwa na neno “Secret” ambayo ilikuwa na majina tu. Anashitakiwa kwa kosa la "Kuchapisha Nyaraka za Siri", jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Usalama, kifungu 5(1). Nimemwekea dhamana hadi Ijumaa saa 4 asubuhi. Angalizo: Huu ni mwendelezo wa Serikali kukwepa kuwashughulikia wezi na wafujaji wa fedha za umma zaidi ya Sh bilioni 8 kwenye Mkutano wa Smart Partnership, badala yake wameamua kuhangaika na neno moja tu “Secret”. Hivi kweli neno “secret” ni kero na hatari zaidi kuliko hoja yenyewe ya kile kilichoandikwa? Nawasilisha. Manyerere Jackton |
STRIKA

USILIKOSE

Wednesday, July 17, 2013
Mhariri Mtendaji 'Jamhuri' mbaroni, kisa...!
Ujangili Tanzania! Tembo 475 wauwawa majangili 1215 wanaswa
![]() |
Na Suleiman Msuya
WIZARA ya
Maliasili na Utalii kupitia Idara ya
Wanyamapori imesema zaidi ya tembo 475 wameuwawa na majangili kwa kipindi cha
mwaka 2012/13 ambapo watuhumiwa 1215 walikamatwa kwa makosa mbalimbali.
Mkurugenzi wa
Wanyamapori, Profesa Alexander Songoro pamoja na watuhumiwa hao pia jumla ya
bunduki 85 na risasi 215 za aina mbalimbali zilikamwata na kesi 670
zilifunguliwa katika mahakama za hapa nchini, ambapo kesi 272 zimekamilika kwa
washitakiwa 247 kulipa faini ya jumla ya
Sh175,002,420 na washitakiwa 71 kupewa adhabu ya vifungo vya jumla ya
miaka 99.
Alisema kesi 398
zenye jumla ya washitakiwa 897 bado zinaendelea katika mahakama mbalimbali
nchini ambapo wanaamini kuwa zitakamilika hivi karibuni.
"Kimsingi
ndugu zangu wanahabari hali ya ujangili ni kubwa sana kwani kwa kipindi cha
mwaka jana zaidi ya tembo 475 waliuuwawa hali ambayo inahitaji juhudi zaidi
ziongezeke ili kukabiliana na hali hiyo," alisema Profesa Songoro.
Alisema vita dhidi
ya ujangili ni ngumu hasa ukizingatia kuwa baadhi ya watanzania wanaamini kuwa
jukumu la kulinga wanyamapori ni la Serikali pekee hasa maofisa wanyama pori
jambo ambalo ni dhana potofu.
Songoro alisema ni
vema Watanzania wakatunza wanyamapori kwa kutambua kuwa asilimia 90 ya utalii
hapa nchini unategemea wanyamapori kwa watalii wengi kutmbelea maeneo yenye
wanyamapori.
Alisema utalii wa
wanyamapori ndio umebeba uchumi wa Taifa kwa kutoa huduma mbalimbali kama vile
madawa, vitabu na kujenga maabara na huduma zingine za kijamii.
Kaimu Mkurugenzi wa
Msaidizi Kitengo cha Kuzuia Ujangili, John Muya alisema migogoro inayotokea
katika maeneo ya hifadhi za wanayamapori inatokana ongezeko la binadamu na wanyama jambo ambalo linachangia kuwepo kwa mwingiliano
wa makazi .
Alisema binadamu
wamekuwa wakiingia na kuweka makazi katika maeneo ambayo wanyama wapo jambo
ambalo wakati mwingine linachangia vifo vya wananchi bila sababu za msingi.
Pia alisema ufinyu
wa watumishi katika mapori yenye kuhifadhi wanyamapori ni moja ya sababu nyingine
ya kukosekana kwa udhibiti wa wanyamapori ambao wanaingia katika makazi ya
watu.
Muya alisema
kuongezeka kwa ujangili wa nchini
kunachangiwa na Watanzania wenyewe ambapo kuna wenye fikra potofu juu ya
baadhi ya maeneo ya wanyama wanaouwawa ambapo tembo anaongoza.
Mganga wa Jadi Tanzania agundua dawa ya Ukimwi, NIMR kuijaribu
![]() |
Na Suleiman Msuya
TAASISI ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
imesema ipo kwenye majaribio ya dawa ya kudhibiti virusi vya Ukimwi ambayo
imegunduliwa na imewasilishwa kwenye taasisi hiyo na mmoja wa waganga wa jadi wa
hapa nchini.
Hayo yamebainishwa
na Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti NIMR Dk. Julius Massaga wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar
es Salaam.
Dk. Mssaga alisema
mganga huyo wa jadi aliyegundua dawa hiyo ambayo imepewa jina la warburgistat
aliitunza katika vifungashio vya kawaida ambapo NIMR wao wameweza kufanyia
maboresho kwa kuitengenezea kwenye mfumo wa vidonge.
Alisema kulingana
na taarifa za Mganga huyo wagonjwa 20 wa awali ambao walitumia dawa hiyo
wamepona kabisa na hamna madhara yoyote ambayo yamepatikana.
"Tunapenda
kuwaambia watanzania kuwa ipo dawa ya kudhibiti virusi vya ukimwi ambayo
iliwasilishwa NIMR na baada ya kuifanyia uchunguzi tunapata matumaini kuwa
inaweza kufanya kazi hiyo,'' alisema.
Mkurugenzi huyo wa
Kuratibu na Kukuza Utafiti NIMR alisema dawa hiyo wameiwasilisha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambapo
wanatarajia baada ya uchunguzi wataingiza sokoni ili iweze kutumika rasmi.
Alisema NIMR
imekuwa ikishirikiana na nchi zingine mbalimbali kama Afrika Kusini na
Swaziland katika kufanya utafiti dhidi ya dawa asili ambazo zimekuwa zikileta
matokeo makubwa kwa jamii.
Dk. Massaga alisema
NIMR inawakaribisha waganga wa jadi ambao wana amini kuwa wana dawa ambazo zinaweza kusaidia jamii ili wao waweze
kuzifanyia utafiti kwa uthibitisho zaidi.
Mkurugenzi huyo
alisema pamoja na dawa hiyo pia wamefanikiwa kuboresha dawa za tiba asili kwa
ajili ya matumizi ya binadamu kama vile TMS 2001 tiba ya malaria, hepacure
inatibu ini, persician tiba ya kisukari, persivin tiba ya tezi dume, nimrex
tiba ya kikohozi na nimrevit kinywaji kinachoboresha afya ya kuongeza damu.
Pia alizitaja dawa
zingine ni mundex dawa ya kuongeza nguvu jinsia ya kiume, fukuza mbu dawa ya
kupakaa inayofukuza mbu,usambara balm dawa ya kupaka kwa ajili ya kutuliza homa
na mafua,usambara mosquito repellent mshumaa unafukuza mbu na takasa maji tiba
ya maji ya kunywa dhidi ya vimelea vya magonjwa yakiwemo ya kuhara na homa ya
matumbo.
Kwa upande mwingine
Dk. Massaga alisema NIMR inakabiliwa na changamoto mabalimbali kama kukosekana
kwa uhamasishaji na uwezeshaji katika eneo la kilimo cha miti dawa hali ambapo
inasababisha ukosefu wa dawa asili.
Changamoto nyingine
ni kukosekana na mitaala ya wataalamu wa tiba ya kisasa (madaktari, wafamasia
na manesi) ambao wamenyimwa fursa ya kuelewa kwa kina na kupata maarifa juu ya
tiba asilia na matumizi yake katika tiba.
Aidha changamoto
nyingine ni uhusiano mdogo kati ya watafiti, wataalamu wa tiba asilia na tiba
ya kisasa katika suala zima la tiba asili na kutokuwepo kwa orodha ya miti dawa
na taarifa ya matumizi yake katika tiba na maingiliano yake na dawa za kisasa.
Dk. Massaga alisema
pamoja na changamoto hizo NIMR inatarajia kusajili dawa na kiwanda kabla ya
uzalishaji katika mwaka huu wa fedha, kuanzisha uzalishaji wa kati wa dawa za
asili kulingana na mahitaji na kuuingiza dawa asali katika mfumo wa tiba.
Hata hivyo alisema
katika mwaka wa fedha wa 2013/14 serikali imetenga kiasi cha sh800 milioni kwa
ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuboresha tiba asilia pamoja na mitambo ya
kuzalishia dawa hizo.
Ambapo kwa sasa
serikali imeikabidhi NIMR mitambo midogo ya daraja la kwanza ya utendenezaji wa
dawa asili kwa matumizi ya binadamu na kujenga kiwanda cha daraja la kwanza cha
kisasa kwa ajili ya utafiti na utengenezaji wa tiba asili katika eneo la Mabibo
jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake
Mtafiti Mwandamizi wa NIMR Hamis Malebo alitoa wito kwa wananchi kuwa makini na
ongezeko la baadhi ya watu ambao wanajiita waganga wa jadi.
Alisema kwa muda
sasa hasa katika jiji la Dar es Salaam kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu wa
aina hiyo hali ambayo inahatarisha maisha ya wananchi ambao wamekuwa wakitumia
dawa hizo.
"Jamani kuweni
makini wapo watu (matapeli) ambao wapo tayari hata kutumia mapumba ya mbao
kuwapa watu kama dawa jambo ambalo si sahihi hata kidogo," alisema.
DAVID MAJEBELLE KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KINONDONI
MWILI wa mwandishi mkongwe David Michael Majebelle. aliyefariki alfajiri ya Jumapili iliyopita unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam Julai 18
Kwa mujibu
wa taarifa rasmi ya familia iliyotolewa leo, mwili huo utaletwa kutoka
katika hospilai ya Mwananyamala ulikohifadhiwa kisha kupelekwa
nyumbani kwake eneo la Sinza jirani na Lion Hotel ambapo heshima
za mwisho zitatolewa majira ya saa sita mchana kisha kulepekekwa katika
kanisa katoliki la Maria Mama wa Mwokozi lililopo Sinza na baadaye saa
tisa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni.
Marehemu
Majebele alizaliwa tarehe 03/05/1941 katika kijiji cha Ibiri, Wilaya ya
Tabora Vijijini, Mkoa wa Tabora, akiwa mtoto wa tatu (3) wa familia ya
watoto 10 wa Mzee Michael Kanyata Majebelle na Mama Theresia Malwa
Majebelle ambao wote kwa sasa ni marehemu.
SHULE
Alisoma
shule ya Msingi ya Bukene (1950) Puge, Wilaya ya Nzega, Mkoa wa Tabora
tangu mwaka 1951, Baadaye katika Shule ya Kati (Middle School) ya
Sikonge, Wilaya ya Sikonge, Mkoa wa Tabora, mwaka 1954 mpaka 1957.
Alijiunga na Tabora Boys School kwa masomo ya sekondari mwaka 1958 mpaka mwaka wa 1961.
Marehemu alikuwa mpenzi wa mpira wa miguu na aliwahi kushiriki kwenye mashindano ya SUNLIGHT CUP enzi zake.
KAZI
David
aliajiriwa na kampuni ya Almasi ya Williamson Diamonds Ltd ya Mwadui,
Shinyanga mwaka 1962 kama Public Relations Trainee. Mwaka 1963
alipelekwa Uingereza kusomea Stashahada ya Uandishi wa Habari/Upigaji
Picha za Uandishi.
Baada
ya kuhitimu alibaki nchini humo kwenye Kampuni ya The Anglo American
Corporation kupata uzoefu kable ya kurejea Mwadui kuendelea na kazi ya
Afisa Uhusiano wa kampuni ya Williamson Diamonds Ltd hadi Septemba 1967
alipojiuzulu na kuajiriwa na Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East
African Airways) na kituo chake cha kwanza kikiwa ni Uwanja wa Kimataifa
wa Embakasi – Nairobi. Oktoba 1971 alipewa uhamisho na kupelekwa London
Uingereza kuwa mwakilishi wa Shirika hilo kwenye uwanja wa Ndege wa
Kimataifa HEATHROW – London.
Julai
1974 alihamishwa kutoka Uingereza na kuletwa Tanzania kuwa Meneja Mauzo
wa Kampuni Tanzu ya Shirika lililojulikana kwa jina la SIMBA AIR.
Lilipovunjika Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East African
Airways)’
David
Majebelle alijiunga na Shirika jipya la Ndege la Tanzania (Air
Tanzania) kama Meneja Mauzo. Mwaka 1978 aliacha kazi katika Shirika hilo
na kujiunga na wamiliki wa magazeti ya AFRICA NEWS na baadaye NEW
AFRICA mpaka mwaka wa 1990 kituo chake kikiwa Uingereza. Baada ya pale
alianzisha Kampuni yake binafsi kwa jina la MEDIA ADVERTISING CO.Ltd
iliyojihusisha na Uhusiano, Matangazo, Upigaji Picha ikiwemo za magazeti
mbalimbali kama;
The Financial Times of London, New Africa African Business, Profit Magazine ,The African Review na magazeti ya hapa nyumbani
Kadri
umri wake ulivyokwenda aliandamwa na magonjwa ya kisukari na shinikizo
la damu. Ilibidi apunguze kasi ya kushughulikia Kampuni hiyo mpaka
alipoifunga.
FAMILIA
David Michael Majebelle alifunga ndoa mwaka 1975. ameacha mke na watoto wane (4), wa kiume mmoja na wa kike watatu.
UMAUTI
Katika
miaka miwili ya mwisho wa maisha yake, marehemu amekuwa akisumbuliwa na
kisukari na shinikizo la damu. Jumatano iliyopita alifanyiwa vipimo
huko hospitali ya Agha Khan ambako aligundulika kuwa amepata “multiple
mild strokes”. Jumamosi kuamkia Jumapili iliyopita alifariki dunia.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.
Raha ya milele umpe ee Bwana; na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani, Amina.
Dude ndiye 'Yahaya' wa Lady Jaydee

MSANII
wa filamu za bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ anatarajia kucheza kama
‘Yahaya’ katika video ya wimbo huo, ulioimbwa na mwanadada Judith
Wambura ‘Lady Jaydee’.
Mwanadada huyo ameanza kushuti video ya wimbo huo juzi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Lady Jaydee alisema anawashukuru mashabiki wake
kwa kumpokea vizuri katika tasnia ya muziki ukiwa ni pamoja na mapokezi
ya ngoma hiyo.
“Kiukweli
sikutegemea kama Watanzania wananikubali kupita kiasi kama
walivyonionesha katika wimbo huu wa ‘Yahaya’, naomba wakae mkao wa kula
kupokea video yake ambapo Dude atacheza kama Yahaya,” alisema.
Alisema
anawaomba watanzania waendelee kumpa sapoti katika kazi zake
zinazofuata ikiwa ni pamoja na kukaa mkao wa kula kwaajili ya video ya
wimbo huo ambao unafanya vizuri kwasasa katika vituo mbalimbali vya
redio.
Msiba mwingine katika tasnia ya muziki Tanzania
![]() |
Kwa mujibu wa mmoja wa wanamuziki wenzake, Ramadhani Kisolo, ni kwamba Jino Moja aliyekuwa akipigia makundi ya mtaani baada ya kutemwa na Jahazi, alifariki saa 7 mchana na bado haijafahamika atazikwa lini kwa sababu ndugu na jamaa bado walikuwa wakipanga mipango ya mazishi yake.
Taarifa zaidi za msiba wa mwanamuziki huyo aliyekuwa akitajwa sana katika nyimbo za kundi la Jahazi tutazidi kuwaletea
Kivuli cha van Persie chamtesa Rooney United
Wayne Rooney |
Kwa mujibu wa duru za soka nchini England zinasema, Rooney amekuwa akiumia kucheza kama chaguo la pili ndani ya United katika safu ya ushambuliaji nyuma ya Mholanzi huyo aliyeibuka Mfungaji Bora wa EPL ikiwa ni msimu wake wa kwanza tangu atue Old Trafford akitokea Arsenal mwaka uliopita.
Chanzo cha karibu cha mchezaji huyo kimenukuliwa kikisema kuwa, Rooney 'amechukia na kuchanganyikiwa' baada ya kocha mkuu wa timu hiyo David Moyes kueleza wazi bado ataendelea kumuamini van Persie kama ailivyokuwa kwa mtangulizi wake.
Mchezaji huyo anayelipwa pauni 250,000 kwa wiki anaamini enzi zake baada ya miaka tisa ndani ya OT iliyomsajili kwa kitita cha pauni Milioni 26 akitokea Everton, ambapo tangu atue United ameifungia mabao 198 mpaka sasa.
Rooney amekuwa akiwinda na klabu mbalimbali baada ya kubainika hana amani OT licha ya klabu yake kusisistiza kuwa mchezaji huyo HAUZWI.
Cavani auma jongoo kwa meno, atua rasmi PSG akivunja rekodi ya uhamisho Ufaransa
![]() |
Edinson Cavani |
MSHAMBULIAJI nyota wa Uruguay aliyekuwa akiwinda na timu za Real Madrid, Manchester City na Chelsea, Edinson Cavani, ameamua kuuma jongoo kwa meno kwa kuzitosa timu hizo na kutua PSG ya Ufaransa kwa donge nono la karibu Euro Milioni 64 (Sh Milioni 126) kwa mkataba wa miaka mitano.
Dau lililomhamisha nyota huyo toka Napoli mpaka Ufaransa imemfanya avunje rekodi ya dau la uhamisho nchini humo lilililokuwa likishikiliwa na Radamel Falcao alipohamia Monaco hivi karibuni akitokea Atletico Madrid ya Hispamia aliyesajiliwa kwa donge nono la Euro Milioni 60.
Mchezaji huyo alifanikisha usajili wake huo kwa mabingwa hao wa Ligue 1 jana na kumfanya auange na mchezaji mwenzake wa zamani wa Napoli, Ezequiel Lavezzi.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay amefunga magoli zaidi ya 20 kwa kila msimu katika misimu mitatu iliyopita ya Serie A, Ligi Kuu ya Italia na kuisaidia Napoli kumaliza kwenye nafasi ya pili msimu wa 2012-13, hivyo kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuanzia hatua ya makundi.
Juzi, rais wa klabu hiyo De Laurentiis alinukuliwa kwamba kama PSG isingetangaza dau hilo isingekuwa tayari kumuachia mshambuliaji huyo ambaye aling'ara kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo PSG ilifika Robo Fainali.
Cheka aonywa kucheza mechi ya 'ndondo'
![]() |
Bondia Francis Cheka |
Cheka na Mmarekani huyo wanatarajiwa kuvaana Agosti 30 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kuwania mkanda wa WBF katika mchezo wa raundi 12 uzito wa Super Middle (kilo 75).
Hata hivyo, kuna taarifa kwamba Cheka anayeshikilia taji la Mabara la IBF atapanda ulingoni mwanzoni mwa Agosti dhidi ya Mmalawi Chimwemwe Chiotcha katika pambano lisilo la ubingwa.
Hata hivyo, Rais wa TPBO, Yasin Abdallah 'Ustaadh', alisema kwa mujibu wa mkataba na taratibu za ngumi, Cheka hawezi kucheza mapambano mawili ndani ya mwezi mmoja na hivyo kutoa tahadhari mapema.
Ustaadh alisema Cheka alishasaini mkataba wa pambano hilo dhidi ya Mmarekani tangu Mei mwaka huu na kwa taratibu ndani ya mwezi mmoja hawezi kupigana pambano jingine la sivyo yatamkuta kama ya Karama Nyilawila.
Nyilawila aliyekuwa bingwa wa WBF, alipoteza mkanda wake kutokana na ratiba ya pambano lake la utetezi kuingilia na mechi isiyo na mkanda dhidi ya Cheka mapema mwaka jana.
"TPBO tunahofia yasitokee yaliyotokea kwa Nyilawila, Cheka alisaini mkataba tangu Mei kwa ajili ya pambano hilo, hivyo wanavyoibuka watu na kusema kuwa bondia huyo atapigana na Mmalawi ndani ya mwezi huo ni kutaka kuvuruga pambano hilo la kimataifa ambalo litamsaidia kumtangaza Cheka," alisema.
Alisema kama kuna watu wanataka kumsaidia Cheka wamlete Chiotcha ili ampe mazoezi katika kambi yake kujiandaa na pambano hilo la WBF au wasubiri akishapigana na Mmarekani.
Ustaadh alisema imefika wakati wadau wa ngumi washirikiane kuwasaidia mabondia wao kufanya vyema kwenye mechi za kimataifa ili kurejesha heshima katika mchezo huo hasa yanapokuwapo na mapambano yanayotambuliwa duniani.
Aliongeza Chiotcha ni bondia hatari hivyo kama atapigana na Cheka katika kipindi kilichotangazwa anaweza pengine kumjeruhi Cheka na hivyo kushindwa kupigana na Derrick.
Aliongeza siku ya pambano hilo la Cheka na Derrick, mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wataonyeshana kazi kuwania mkanda wa WBF-Afrika, huku Alphonce Mchumiatumbo atapigana na De Andre McColl wa Marekani.
Stars, The Cranes kurudiana Julai 27
MECHI ya marudiano kati ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya wenyeji wao Uganda (The Cranes) ambayo ni ya kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN) itafanyika Julai 27 kwenye Uwanja wa Mandela jijini Kampala imeelezwa jana.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Angetile Osiah, alisema jana kuwa Chama cha Soka cha Uganda (FUFA) kimesema kwamba mchezo huo utachezwa jioni na maandalizi yake yanaendelea vizuri.
Osiah alisema kuwa katika kujiandaa na mchezo huo, Stars ilielekea Mwanza tangu Jumapili asubuhi kuweka kambi na itaondoka nchini kuelekea Kampala Julai 24 mwaka huu.
Alimtaja mchezaji, Mudathir Yahya, kuwa ameshachukua nafasi ya kiungo, Mwinyi Kazimoto, ambaye ametoroka katika kambi ya Taifa Stars tangu Jumamosi usiku na kuelekea Qatar kusaka klabu ya kuichezea soka la kulipwa.
"Safari hii timu itaanzia safari yake Mwanza kwenda Kampala na haitarudi Dar es Salaam kuanzia safari yake," alieleza Osiah.
Stars ilifungwa goli 1-0 dhidi ya Uganda katika mechi yake
ya kwanza iliyofanyika nchini ambapo wadau wengi wa mchezo huo akiwamo Rais wa TFF, Leodegar Tenga, walielezea kusikitishwa na kiwango kibovu kilichoonyeshwa na kikosi hicho.
Hata hivyo, Tenga alisema kuwa huu ni wakati wa kuwapa moyo wachezaji wa Taifa Stars na anaamini wana uwezo wa kuifunga Uganda nyumbani kwao na kusonga mbele lakini ni lazima wajiamini.
Bao pekee ya Uganda inayofundishwa na Mserbia Sredojevic Milutin 'Micho' lilifungwa na Denis Iguma katika dakika ya 47 ya mchezo huo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Mshindi kati ya Stars na The Cranes atafuzu kushiriki katika fainali za tatu za CHAN zitakazofanyika Afrika Kusini mapema mwakani.
Tayari wenyeji Afika Kusini (Bafana Bafana) na Ghana wameshakata tiketi ya kushiriki fainali hizo.
NIPASHE
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Angetile Osiah, alisema jana kuwa Chama cha Soka cha Uganda (FUFA) kimesema kwamba mchezo huo utachezwa jioni na maandalizi yake yanaendelea vizuri.
Osiah alisema kuwa katika kujiandaa na mchezo huo, Stars ilielekea Mwanza tangu Jumapili asubuhi kuweka kambi na itaondoka nchini kuelekea Kampala Julai 24 mwaka huu.
Alimtaja mchezaji, Mudathir Yahya, kuwa ameshachukua nafasi ya kiungo, Mwinyi Kazimoto, ambaye ametoroka katika kambi ya Taifa Stars tangu Jumamosi usiku na kuelekea Qatar kusaka klabu ya kuichezea soka la kulipwa.
"Safari hii timu itaanzia safari yake Mwanza kwenda Kampala na haitarudi Dar es Salaam kuanzia safari yake," alieleza Osiah.
Stars ilifungwa goli 1-0 dhidi ya Uganda katika mechi yake
ya kwanza iliyofanyika nchini ambapo wadau wengi wa mchezo huo akiwamo Rais wa TFF, Leodegar Tenga, walielezea kusikitishwa na kiwango kibovu kilichoonyeshwa na kikosi hicho.
Hata hivyo, Tenga alisema kuwa huu ni wakati wa kuwapa moyo wachezaji wa Taifa Stars na anaamini wana uwezo wa kuifunga Uganda nyumbani kwao na kusonga mbele lakini ni lazima wajiamini.
Bao pekee ya Uganda inayofundishwa na Mserbia Sredojevic Milutin 'Micho' lilifungwa na Denis Iguma katika dakika ya 47 ya mchezo huo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Mshindi kati ya Stars na The Cranes atafuzu kushiriki katika fainali za tatu za CHAN zitakazofanyika Afrika Kusini mapema mwakani.
Tayari wenyeji Afika Kusini (Bafana Bafana) na Ghana wameshakata tiketi ya kushiriki fainali hizo.
NIPASHE
Golden Bush Fc yaonja kipigo Ligi Kinondoni
Kikosi cha Golden Bush Fc |
TIMU ya soka ya Golden Bush Fc inayoshiriki Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Kinondoni kwa mara ya kwanza jana imeonja machungu ya vipigo baada ya kukubali kulazwa bao 1-0 na Kijitonyama Fc.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa timu hiyo inayocheza ligi hiyo kwa mara ya kwanza na uongozi wa timu hiyo umesema ni changamoto kwao kujipanga vyema kwa mechi ijayo dhidi ya Shein Rangers.
Kabla ya hapo Golden Bush inayonolewa na makocha Shija Katina na Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' ilikuwa imeshinda mechi nne na kuongoza kundi lao linalotumia uwanja wa Itihad.
Hata hivyo huenda timu hiyo imeteleza baada ya ligi hiyo kusimama kwa muda mrefu na kuipunguzia kasi timu hiyo ambayo hivi karibuni ilifanikiwa kumvutia wakala wa soka wa kimataifa toka Msumbiji, Ashraf ambaye alitangaza kumchukua mchezaji mmoja wa klabu hiyo ili kwenda kucheza soka la kulipwa nchini mwake.
IKwa mujibu wa uongozi wa klabu hiyo watarekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi yao ya jana ili kuweza kufanya vyema kwa mechi zao zilizosalia ambapo inahitaji kushinda mechi tatu ili kujihakikisha kusonga mbele kwenye ligi hiyo kuwania kupanda Daraja la Tatu.
Tabora bado wauenzi mchezo wa bao
Juma Shoka Salumu
Dilunga Kushoto akicheza mchezo wa bao na Salumu Dilunga wakati walipokuwa
maeneo ya Changamoto Mkoa wa Tabora jana mchezo huo uliozoeleka kuchezwa
mikoa ya pwani imeleta chachu kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Tabora
Tuesday, July 16, 2013
Waliokufa Darfur waagwa, JWTZ lakana ongezeko la vifo
WAKATI miili ya wanajeshi saba wa Tanzania waliouwawa huko Darfur, Sudan wakiagwa kwa heshima nchini humo na kuanza mipango ya kurejeshwa nchini kwa ajili ya mazishji yake, Jeshi la Watanzania Tanzania, JWTZ, limekanusha taarifa za kuwepo kwa ongezeko la vifo vya askari wake.
Msemaji wa jeshi hilo. amenukuliwa hivi punde na Clouds FM kwamba hakuna askari mwingine aliyefariki japo alikiri mmoja wa majeruhi wa tukio hilo hali yake ni tete kiasi cha kuhamishwa hospitali aliyokuwa akipewa huduma na wenzake 9 na kupelekwa Khartoum kwa matibabu zaidi.
"Hatujui hizi taarifa zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii wanazipata wapi wakati sisi ndiyo wenye kuhusika na tukio, ila ukweli ni kwamba hakuna idadai iliyoongezeka ya vifo na jeshi halina sababu ya kuficha kitu," alisema Kanali Kapambala Mgawe Msemaji wa JWTZ.
Kanali Mgawe alisema hali za majeruhi wengine tisa zinaendelea vyema kiasi cha kuweza kutembea wenyewe japo mwenzao mmoja amehamishiwa Khartoum kwa matibabu zaidi na kuwataka watanzania wasiwe na hofu wala kuziamini taarifa hizo zinazoandikwa na kuwekwa kila muda katika mitandao hiyo.
"Watanzania hawana haja ya kuwa na hofu hali za askari wetu zinaendelea vyema japo mmoja hali yake siyo nzuri sana na kulazimika kuhamishiwa mjini Khartoum kwa matibabu zaidi na wenzake tisa tunashukuru kwani wanaendelea vyema," alisema.
Hapo chini ni baadhi ya picha za miili ya wanajeshi hao ikitolewa heshima na wanajeshi wenzao, sambamba na majeruhi waliolazwa baada ya tukio hilo la kushambuliwa na waasi wakati katika msafara wao wa kulinda amani katika jimbo hilo la Darfur.
The
African Union – United Nations Mission in Darfur (UNAMID), held a
memorial ceremony, in Nyala, the capital of South Darfur, to honor the
seven fallen peacekeepers who lost their lives in the 13 July attack in
South Darfur. The bodies are scheduled to be repatriated to Tanzania,
the home country of the fallen peacekeepers. In addition to the seven
killed, 17 military and police personnel were wounded, among them two
female Police Advisors, all of whom are recovering from their injuries
in UNAMID’s hospital in Nyala, South Darfur. Photo by Saidi Msonda,
UNAMID.






On
14 July 2013, following a 13 July attack in which seven military
peacekeepers of the African Union - United Nations Mission in Darfur
(UNAMID) were killed and 17 military and Police personnel wounded, among
them two female Police Advisers, Joint Special Representative Mohamed
Ibn Chambas visited the wounded peacekeepers at UNAMID’s hospital in
Nyala to provide encouragement and support. Photos by Albert González
Farran, UNAMID.


Casillas amkwamisha Kaseja kutua Mtibwa Sugar
![]() |
Juma Kaseja |
![]() |
Hussein Sharrif 'Casillas' |
KUKWAMA kwa kipa Hussein Sharrif 'Casillas' kujiunga na Fc Lupopo baada ya klabu yake ya Mtibwa kushindwa kuafikiana dau na timu hiyo ya DR Congo kumemfanya 'Tanzania One', Juma Kaseja kushindwa kutua Manungu kuichezea timu hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu.
Kaseja aliyetemwa na Simba baada ya kuitumikia miaka karibu 10, alikuwa akitajwa kuwa mbioni kusajili wa Mtibwa, lakini Mkurugenzi wa klabu hiyo, Jamal Bayser aliiambia MICHARAZO muda mchache uliopita kuwa, mpango huo umekufa baada ya Casillas kukwama kutua Lupopo.
Casillas alifuzu majaribio katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya DR Congo na alikuwa katika maandalizi ya kuondoka kwenda kujiunga na timu hiyo wakati klabu hizo mbili zikifanya mazungumzo ya mwisho kuhusu dau la uhamisho wake.
Hata hivyo Bayser alisema kuwa mazungumzo hayo ya Casillas kuhamia Lupopo yamekwama baada ya Wakongo kushindwa kuafiki dau walilokuwa wakilitaka na hivyo kipa huyo atasalia Mtibwa kwa msimu ujao na kwa maana hiyo hawana mpango na kipa mpya.
Bayser alisema walikuwa na dhamira ya kumnyakua Kaseja iwapo mazungumzo baina yao na Lupopo yangeenda vyema kwa Casillas kuondoka, lakini kw ahali ilivyo wamesitisha mipango ya kumsajili Kaseja ambaye alimtaja kama kipa bora ambaye kila timu inatamani iwe naye.
"Mazungumzo yetu na Fc Lupopo juu ya kuwapa Casillas yamekwama na hivyo kipa huyo atasalia Mtibwa na kwa maana hiyo hatuna haja ya kumuongeza kipa yeyote mpya kama ambavyo tulikuwa tumepanga tukimfikiria Kaseja," alisema Bayser.
Bayser aliongeza pia klabu yao haina mpango wowote wa kusajili mchezaji kutoka nje ya nchi na badala yake wataendelea kuwaamini vijana wazawa kama walivyofanya msimu uliopita na kumaliza ligi wakiwa katika nafasi ya tano.
Kwa wiki moja sasa kulikuwa na tetesi kwamba huenda Kaseja aliyetemwa Simba angetua Mtibwa Sugar au Coastal Union, kabla ya Coastal kuweka bayana kuwa haina mpango naye.
Dereva wa Bodaboda afa, wengine wajeruhiwa katika ajali

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi, Handeni.
DEREVA
mmoja wa Bodaboda amefariki dunia papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa
kwenye ajali baada ya pikipiki mbili kugongana usukani kwa usukani huko
kwenye eneo la Mzundu wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP Constantine Massawe, amemtaja Dereva huyo
wa Bodaboda kuwa ni Ismail Mhando(30), mkazi wa Kabuku wilayani Handeni. Amesema
kuwa ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mzundu wilayani Handeni
mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo katika uchunguzi wa awali wa tukio
hili Polisi walibaini kuwa imesababishwa na mwendo kasi kwa kila mmoja
na kutokuwa makini barabarani.
Amesema
marehemu Mhando akiendesha pikipiki yenye nambari za usajili T.256 AYM
akitokea Kabuku kwenda Mzundu akiwa amempakia dada mmoja aitwaye Salama
Bakari, aligongana na pikipiki nyingine iliyokuwa ikitokea Mzundu kwenda
Kabuku yenye namba za usajili T.584 CCS. Alisema
pikipiki hiyo ikiendeshwa na Sudi Nassoro ilikuwa imepakia abiria
wawili maarufu kama mshikaki na ilikua ikitokea katika kijiji cha Mzundu
kwenda Kabuku wilayani humo.
Kamanda
Massawe amesema majeruhi wanne wa ajili hiyo wamelazwa katika Hospitali
ya Wilaya ya Handeni kwa matibabu zaidi na hali zao amesema zinaendelea
vizuri.
Kamanda
Massawe ametoa wito kwa Madareva wote wa Bodaboda kuwa makini
wanapokuwa barabarani na kujiepusha na upakiaji abiria zaiidi ya mmoja
ili kuepuka matukio ya ajali zinazowahusisha watu wengi kwa wakati
mmoja.
Amewataka
kila mmoja wao kuwa mlinzi wa mwingine na kutoa taarifa pale
wanapomuona mwenzao mmoja anavunja sheria na kutotii sheria bila ya
shuruti ili achukuliwe hatua ili kuwanusuri wengine wanaofanya kazi zao
vizuri.
Kifo mkweli ahadi! Fundi anusurika kifo licha ya kuchomwa chuma kichwani
Liu Fenghe akiwa hospitali na chuma kichwani
FUNDI majengo Liu Fenghe wa nchini China, amenusurika kifo baada ya kuchomwa na chuma kichwani na kuzama inchi 8 ambazo ni sawa na sentimita 20.
Liu alikuwa akiongea na rafiki yake na kwa bahati mbaya alidondokewa na chuma hicho kilichomchoma kichwani.
Rafiki yake Liu aitwaye Zhang anasema: "Ilikuwa ghafla. Kabla sijafanya chochote Liu alikuwa katika dimbwi la damu."Inadhaniwa kuwa chuma hicho kilidondoka kutoka ghorofa ya 25 ya jengo walilokuwemo mafundi hao mpaka kusababisha maafa hayo.
Madaktari walimfanyia upasuaji wa haraka katika hospitali iliyopo jimbo la Shanghe nchini China na kueleza kuwa Liu hayupo tena katika hatari japo bado haijajulikana ni lini ataweza kurudi kazini.
Fabregas azikata maini Arsenal, Man United
![]() |
Cesc Fabregas |
SIKU moja tu baada ya klabu ya Manchester United kutangaza kuongeza dau ili kumnasa nahodha wa zamani wa mahasimu wao Arsenal, Cesc Fabregas, kiungo huyo ameikata maini timu hiyo.
Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Hispania anayeichezea Barcelona alikuwa chaguo la kwanza la David Moyes baada ya kumkosa Thiago Alcantara, pia alikuwa akiwindwa na klabu yake ya zamani. Hata hivyo kocha wa Barcelona, Tito Vilanova amefichua kuwa, aliongea na kiungo huyo na kumwambia kuwa kwamba anahitaji kuendelea kubaki Camp Nou.
Jana iliripotiwa kwamba United walituma ofa ya kwanza ya kiasi cha £25.9 million kwa ajili ya kumsajili Fabregas, ambaye amefeli kupata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu aliporudi akitokea Arsenal.
Lakini akiongea na waandishi wa habari leo mchana, Vilanova amesema wazi kwamba Fabregas bado anataka kubaki kwenye klabu yake hiyo ya utotoni, na hana mawazo ya kuondoka.
"Ninafahamu kwamba tumepokea ofa kadhaa kutoka kwa vilabu tofauti. Niliongea na Cesc na ameniambia kwamba anataka kubaki.
"Cesc hana mawazo ya kuondoka kwenda klabu nyingine. Anajua ushindani ni mkubwa hapa na ana ndoto za kuendelea kuwa hapa na kufanikiwa.
MIUJIZA! Mtoto azaliwa na Tasibhi shingoni mwake
Maelfu
ya watu walifika hospitali binafsi ya uzazi kwenye jiji la Kotaworo
eneo la Bida, iliyopo jimbo la Niger Jumapili, kwa lengo la kwenda
kumshuhudia mtoto wa kike aliyezaliwa akiwa amevaa Tasbihi inayotumika katika utajo wa Mwenyezi Mungu shingoni mwake.
Inaelezwa
kwamba mama wa mtoto huyo ambaye ana miaka ya kati, Adijat, alikimbizwa
hospitali karibu na nyumbani kwa Mohammed Bello Masaba, mida wa saa 8
mchana na baada ya pilika za uzazi alifanikiwa kujifungua mtoto huyo.
Kwa
mujibu wa mmiliki wa hospitali hiyo ya uzazi, Alhaji Abubakar Baiwa
Shasha ambaye ndiye aliyesimamia zoezi hilo la kujifungua alisema;
“Nilishtuka nilipoona mtoto anatoka akiwa na Tasbihi shingoni mwake, na wakati wa uzazi mtoto alizaliwa tasbihi hiyo ilikuwa nyeusi," alisema Shasha.
“Ila nilishangaa baada ya muda tasbihi hiyo ilibadilika na kuwa nyeupe huku kukiwa na watu wengine wamezunguka.”
“Mara
baada ya habari hiyo kusambaa mjini, maelfu ya watu walifika kwenye
hospitali hiyo ya uzazi huku wakisema “Allahu Akibar; Allahu Akibar
(Mungu ni Mkubwa) huku wakifika na kumgusa mtoto huyo.”
Juhudi
za kumpata Baba wa mtoto huyo aitwaye Isah, ambaye anatokea eneo la
Loma ndani ya Jimbo la Kwara zilishindikana baada ya kukataa
kuongea na mtoa habari.
Mwanachuo mmoja wa Kiislamu, Malam Idiris Ndajiwo alisema, kuzaliwa kwa mtoto huyo akiwa na kitu kama hicho inaonyesha
ukuu wa Allah (SW). Kuzaliwa kwa mtoto huyu leo, kwenye mji huu na eneo hili
(Kutaworo) ni kitu kikubwa kwa Waislamu. Hii hakika inakuja kuonyesha
kwamba Allah ndiye mwenye kupanga kwa lolote kutokea kwa yeyote kwenye
ulimwengu huu.”
Pigo! Jaji Chipeta afariki dunia
![]() |
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Buxton Chipeta enzi za uhai wake |
HABARI zilizopatikana hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania,Buxton Chipeta amefariki dunia muda mfupi uliopita.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia, Jaji Chipeta alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari ambapo ilifikia wakati akalazimika kukatwa vidole kadhaa vya miguuni.
Enzi za uhai wake, Jaji Chipeta aliweza kujijengea heshima katika kazi yake na kufikia kuwa mmoja wa majaji wanaoheshimika mno hapa nchini.
Pia Jaji Chipeta aliwahi kuwa miongoni mwa majaji wa Tume ya kurekebisha Sheria yeye akiongoza kanda ya Dar es Salaam.
MICHARAZO inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao na kuwaombea kwa Allah Subhana Wataala kuwa na subira na uvumilivu kwa kuamini kuwa kila nafsi itaonja mauti na kurejea kwa aliyetuumba. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia, Jaji Chipeta alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari ambapo ilifikia wakati akalazimika kukatwa vidole kadhaa vya miguuni.
Enzi za uhai wake, Jaji Chipeta aliweza kujijengea heshima katika kazi yake na kufikia kuwa mmoja wa majaji wanaoheshimika mno hapa nchini.
Pia Jaji Chipeta aliwahi kuwa miongoni mwa majaji wa Tume ya kurekebisha Sheria yeye akiongoza kanda ya Dar es Salaam.
MICHARAZO inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao na kuwaombea kwa Allah Subhana Wataala kuwa na subira na uvumilivu kwa kuamini kuwa kila nafsi itaonja mauti na kurejea kwa aliyetuumba. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema.
Walimu Shule ya Msingi King'ongo wawalia wazazi, kisa utoro wa wanafunzi
UONGOZI wa Shule ya Msingi King'ongo, iliyopo Kata ya Saranga, wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, umelia na vitendo vya utoro uliokithiri kwa wanafunzi wanaosoma shule hiyo hasa wale wa darasa la saba na kuwaomba wazazi wa wanafunzi hao kuingilia kati kuwasaidia.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Flora Salila alitoa kilio hicho katika mkutano wa pamoja kati yao na wazazi wa wanafunzi wa darasa la saba uliofanyika juzi shuleni hapo.
Mwalimu Salila, alisema uongozi wao umekuwa katika wakati mgumu kutokana na vitendo vya utoro kwa wanafunzi na hasa wa darasa la saba, ambapo kuna wakati hufikia mpaka wanafunzi 58 kati ya 268 wa darasa hilo la saba kutoonekana shuleni.
Mwalimu huyo alisema vitendo hivyo huenda vinachangiwa na wazazi kutojenga utamaduni wa kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni na kuwapa wakati mgumu walimu ambao hujaribu kutatua tatizo hilo la utoro bila mafanikio kwa kukosa ushirikiano na wazazi.
"Lazima niwaeleze ukweli kuwa, utoro ni tatizo sugu shuleni kwetu hasa hawa wa darasa la saba kwa mfano karibu wanafunzi 58 miongoni mwa 268 wa darasa hilo hawakuwepo shuleni wakati wa upigaji wa picha za maandalizi ya mitihani, hii siyo jambo zuri, wazazi tusaidieni," alisema.
Aliongeza kwa jumla ya wanafunzi 1762 waliopo shuleni hapo kwa siku watoto kati ya 100-200 huwa hawafiki shuleni na kuhoji wazazi wenye watoto hao wanafanya nini katika kuwasaidia walimu kuwaondoa watoto katika vitendo hivyo vinavyochangia kudumaza taaluma.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Demetrius Mapesi alisema ni lazima wazazi washirikiane na walimu kutatua utoro shuleni hapo iwapio wanataka shule yao iendelee kushika nafasi ya pili katika Kata ya Saranga.
Mapesi alisema wazazi wamekuwa wakishindwa kufuatilia nyendo za watoto wao na kuishia kuwatumia lawama walimu pale watoto wao wanapofanya vibaya kwenye mitihani wakati jukumu hilo ni la lazima kwao kabla ya walimu kufuatia hasa wanapokuwa shuleni.
"Wazazi badilikeni, kutofuatilia nyendo za watoto wenu ndiyo chanzo cha kuharibika kwa vijana, dunia ya sasa imeharibika na haiaminiki, ukijifanya upe bize na kazi ujue unazalisha watoto machangudoa, vibaka na hata mashoga, mtakuja kumlaumu nani," alihoji Mapesi.
Mwisho
Polisi Dar wawanasa watuhumiwa wa ujambazi, mbakaji
![]() |
wanachuo walipoandama baada ya tukio la kuvamiwa na kupigwa risasi kwa wenzao na majambazi waliokamtwa na jeshi l polisi |
WATU wanne wanaodaiwa kuwa majambazi wamenaswa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika na tukio la ujambazi lililotokea Juni 21, mwaka huu, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), katika eneo la bweni la Yombo One.
Aidha mtu mwingine anayedaiwa kumlewesha kwa dawa za kulevya kisha kumbaka kabla ya kumpora mfanyabiashara nyumbani kwake naye katiwa mbaroni na jeshi hilo baada ya kuendesha msako dhidi yake.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Ally Mlege, alisema watuhumiwa wanne waliohusika na tukio la Chuo Kikuu, walikamatwa na jeshi hilo Julai 8, mwaka huu, kwenye kituo cha Daladala Ubungo.
Kamanda Mlege, alisema jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata watu hao wakiwa na silaha aina ya SMG ikiwa na risasi moja, laptop mbili aina ya Toshiba, simu aina ya Samsung, panga moja na nyundo.
Alisema baada ya mahojiano, majambazi hayo yalikiri kuhusika katika tukio la unyang’anyi lililotokea UDSM.
Afande Mlege, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Dolisera Gerald (22), Leonard Mathias (21), Leonard Leopard (32), Gerald Moses (23), ambao licha ya kukiri kuhusika katika tukio hilo pia walikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya kihalifu sehemu tofauti jijini.
Wakati huo huo Kamanda Mlege alisema jeshi hilo limemtia mbaroni mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, Ezekiel Matiti (35), kwa tuhuma za kumlewesha dawa za kulevya mkazi wa Makongo Juu, jijini humo, Aida Kiangi.
Kwa mujibu wa Mlege baada ya mtuhumiwa kumlewesha Aida, alimpeleka nyumbani kwake (Makongo Juu) na kumuingiza ndani na kumbaka na kisha kumuibia runinga, pamoja na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. milioni nane.
Aidha aliongeza kuwa, katika tukio lingine, polisi inawashikilia Michael Pascal (35), Donald Joseph (43), Kulwa Adamson (43), na Ally Akiri (41), na watuhumiwa wengine watano, kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la kurushiana risasi na askari polisi eneo la Kunduchi Mtongani.
Hussein Javu atamani soka la kulipwa
![]() |
Hussein Javu (kulia) akikabana na Aggrey Morris wa Azam katika moja ya mechi za igi Kuu |
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya Mtibwa Sugar, Hussein Javu amesema anatamani kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchini bila kujali kama ni Afrika au barani Ulaya, ili kutimiza ndoto zake za tangu utotoni.
Javu, aliye katika kikosi cha pili cha taifa 'Young Taifa Stars' alisema ipo mipango anaiweka sawa ili kutimiza ndoto hizo za kucheza soka la kulipwa akiwa tayari kutua kokote hata kama ni nchi jirani za Kenya, DR Congo au Msumbiji.
Alisema kwa sasa anamsikilizia wakala wake kuona mipango hiyo inakwendaje, ingawa alisisitiza kuwa bado ana mkataba wa kuitumikia timu yake ya Mtibwa hadi mwakani.
Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa wakitajwa kama miongoni mwa wachezaji wapya wa Yanga, ingawa mwenyewe anakanusha kuwa hajasaini kokote zaidi na kujitambua kama mchezaji wa Mtibwa kulingana na mkataba aliokuwa nao na klabu hiyo aliyojiunga nayo tangu mwaka 2007 katika kikosi cha vijana, alisema kiu ya kucheza soka la kulipwa ni kubwa kiasi cha kutoelezeka.
"Hakuna kitu ninachokitamani na kulilia kama kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, kuna mipango inafanywa lakini siwezi kuiweka wazi kwa sasa kwa vile ni mapema, ila nitafarijika sana kama nitaenda hata Kenya tu," alisema.
Javu anayemhofia dimbani beki wa zamani wa Simba aliyehamia Coastal Union Juma Nyosso, alisema kiu yake ya kucheza nje ya nchi imeongezeka baada ya kuona mafanikio ya wachezaji wenzake wa timu ya taifa, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na watanzania wengine wanaocheza soka hilo barani Afrika katika nchi za DR Congo, Kenya, Msumbiji na Angola.
Pia aliweka bayana kwamba mbali na kiu ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, pia angependa kuichezea timu mojawapo kubwa nchini kati ya Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikimuwinda ili kumsajili.
Maugo, Mwakyembe kutimka J4 ijayo kwenda Urusi
Mada Maugo |
Rais wa TPBO-Limited, Yasin Abdallah 'Ustaadh', aliiambia MICHARAZO mabondia hao wataondoka Julai 23, ambapo Maugo ataenda kupigana na Movsur Yusupov na Mwakyembe ataonyeshana kazi na Apti Ustarkhanov kwenye michezo itakayochezwa kwenye ukumbi wa Trade &Intertainment uliopo mji wa Kasiysk, nchini Russia.
Ustaadh alisema watanzania hao watapigana na Warusi hao katika michezo ya kilo 75 (Super Middle Weight) itakayokuwa na raundi nane kila mmoja.
Rais huyo wa TPBO alisema mpinzani wa Maugo rekodi yake inaonyesha kuwa amecheza mapambano matatu na yote ameshindwa moja likiwa kwa KO wakati mpinzani wa Mwakyemba amecheza mechi mbili na kushinda moja na mwingine kupigwa.
"Pamoja na rekodi ndogo za wapinzani wao, lakini ikumbukwe kuwa mabondia wa Russia na kwingineko Ulaya huwa hawachezi ngumi za kulipwa bila kucheza ngumi za ridhaa na kufikia hatua ya kushiriki michuano ya Olimpiki kwa maana hiyo Maugo na Mwakyembe wakitarajiwe wepesi Russia," alisema Ustaadh.
Ustaadh aliongeza kuwa tayari mabondia hao wa Tanzania wameshaombewa visa za kwenda nchini humo gharama zote zikilipwa na TPBO-Limited na wataondoka nchini wakiongoza na wakala wao kutoka Kenya, Thomas Mutua atakayeondokea Kenya na kukutana na mabondia hao Dubai.
Monday, July 15, 2013
CHADEMA KUFUTWA? TENDWA ALIPUKA
MSAJILI wa Vyama vya Siasa Tanzania, John Tendwa ameibuka na kusema sasa anaandaa kalamu yake kukifuta Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.
Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari muda mfupi uliopita Tendwa amesema CHADEMA wanataka kuanzisha kikundi cha mgambo ambacho ni kinyume na sheria, katiba ya nchi na sheria za usajili wa vyama.
Msajili huyo amesema kwamba kama madai ya CHADEMA ni kuanzisha kikundi cha kujilinda dhidi ya Green Guard wa CCM madai hayo hayana msingi wowote kwani kama CHADEMA wana taarifa kwamba Green Guard wanahatarisha amani basi wanapaswa kuripoti suala hilo polisi ili lifanyiwe kazi kwa mujibu wa sheria.
Tendwa amezidi kuonya kwamba uamuzi wake ni wa mwisho na atakapoifuta CHADEMA maamuzi yake hayapingwi popote kisheria.
Source: JF
Subscribe to:
Posts (Atom)