![]() |
| Kikosi cha Simba kitakachoanza kibarua cha Mapinduzi Cup dhidi ya Mtibwa Sugar usiku wa kesho |
| Mtibwa Sugar watakaivaa Simba kesho usiku katika Mapinduzi Cup |
![]() |
| Yanga safari hii imekubali kushiriki kamili gado |
MSIMU mpya wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi unatarajiwa kuanza rasmi kesho kwa michezo mitatu 'Mnyama' Simba akitarajiwa kushuka dimbani Usiku kuvaana na Mtibwa Sugar, huku Azam wakitarajiwa kuvaama na KCCA ya Uganda Ijumaa.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa ni kwamba kesho mechi ya kwanza itawakutanisha JKU na Mafunzo majira ya saa 9 alasiri kabla ya Polisi-ZNZ kuvaana na Shaba jioni.
Yanga ambayo imekuwa 'ikisumbua' ushiriki wake katika michuano hiyo safari hii imekubali kikamilifu kushiriki na wenyewe wataanza kibarua Jumamosi kwa kuvaana na Sports Club Villa ya Uganda.
Jumla ya makundi matatu yamegawanywa yakiwa na timu nne kila moja nayo ni;
Kundi A: SC VILLA, YANGA, POLISI, SHABA.
Kundi B: KCCA, AZAM, KMKM na MTENDE.
Kundi C: SIMBA, MTIBWA, JKU, na MAFUNZO.
RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP IKO HIVI:
Alhamisi 1 Januari 2015:
Saa 9:00 JKU vs MAFUNZO.
Saa.11:00. POLISI VS SHABA.
Saa 2:15. SIMBA VS MTIBWA.
Ijumaa 2 Jan 2015
Jioni saa 10:00 KMKM VS MTENDE KUNDI B
Usiku Saa 2:00 KCC VS AZAM. KUNDI B
Jumamosi 3Jan 2015.
Jioni Saa 10:00 JKU VS MTIBWA KUNDI C
Usiku Saa 2:00 YANGA VS SC.VILLA KUNDI A
Jumapili 4 Jan 2015
Jioni saa 9:00 KCC VS MTENDE KUNDI B
Jioni saa 11:00 KMK VS AZAM. KUNDI B
Usiku saa 2:15. MAFUNZO VS SIMBA KUNDI C
Jumatatu 5 Jan 2015
Jioni saa 10;00 SC VILLA VS SHABA KUNDI A
Usiku saa 2:00 YANGA VS POLISI KUNDI A
Jumanne 6 Jan 2015
Jioni saa 9:00 AZAM VS MTENDE KUNDI B
Jioni saa 11: 00 MTIBWA VS MAFUNZO KUNDI C
Usiku saa 2:15. SIMBA VS JKU KUNDI C
Jumatano 7 Jan 2015
Jioni saa 9;00 POLISI VS SC VILLA KUNDI A
Jioni saa 11:00 KCC VS KMKM KUNDI B
Usiku saa 2:15. YANGA VS SHABA KUNDI A
Alhamisin 8 Jan 2015.
Jioni saa 10:00 WINNER B VS RUNNERS A.
Usiku saa 2:00 WINNER A VS BEST LOOSER 1
Ijumaa 9 Jan 2015
Jioni saa 11:00 WINNER C VS BEST LOOSER 2
Usiku saa 2;00 RUNNERS B VS RUNNERS C.
Jumapili 11 Jan 2015.
SEMIFINAL 1
Jioni saa 10:00. WINNER 1 VS WINNER 2
SEMIFANAL 2
Usiku saa 2:00 WINNER 3 VS WINNER 4
Tarehe
13/1/2015 itakuwa fainali ya michuano hiyo itakayofanyika usiku katika
uwanja wa amaan Zanzibar. kuhitimisha michuano hiyo.
























PAMBANO la kukata na shoka baina ya Yanga na Azam limemalizika matokeo yakiwa ni yale yale ya mabao 2-2 na kuendelea kuwa nyuma ya Mtibwa Sugar wanaoongoza msimamo.
TIMU ya soka ya Mbao ya Mwanza imekamata uongozi wa Kundi B la michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya jana (Desemba 27 mwaka huu) kuizamisha JKT Rwamkoma ya Mara mabao 2-1.
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Pedro amedai kuwa mchezaji mwenzake Lionel Messi ndiyo mchezaji bora kuliko yeyote duniani na anastahili kushinda tuzo ya Ballon d’Or mbele ya Cristiano Ronaldo. Messi amewahi kushinda tuzo hiyo kwa mara nne mfululizo kabla ya Ronaldo kuingilia kati na kunyakua tuzo hiyo mwaka jana ikiwa ni mara ya pili kwa upande wake.





KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon, Volke Finke ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 27 kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayofanyika huko Guinea ya Ikweta. 