STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 7, 2015

Mnyama ashindwa kutamba Tanga, Azam yarudi kileleni

* Kagera Sugar yaondoa gundu Shinyanga, Ndanda bado sana nyumbani

http://4.bp.blogspot.com/-HlzYMgUqY6E/VLYmO19_SFI/AAAAAAAAw04/Tum0BDfocyc/s1600/simba-mapinduzi_2015.jpg
Simba iliyong'ang'aniwa Tanga
http://api.ning.com/files/cPakA0chAEyfyqjZRP3k2djpZ9GyxNW23W69D7FY4fYhsuNz2vmH6gr7yEITcci18IdnTvIgOej4xydmYu8LtJiXW0uQDhCL/16.jpg
Kagera Sugar waliooindoa 'gundu' kwa kushinda uwanja wa Shinyanga
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVRbEIHy7_801zrOMtfyS9oWnAn9Wj6oTahWAMqqpwD5pn_QaYj-Kl6fpolmlrZ0fr5VQYOEkeiFe9NflY7atBcCjdsvEREiubcYjodwWeAlUxWTreYDXgIRhZmXPJQjkX7wMXw95djYBf/s1600/10847549_808297752551709_8272495318791573431_o-790072.jpg
Azam waliorejea kileleni kwa muda baada ya sare ya 2-2 mjini Morogoro
MDUDU wa sare ametawala katika viwanja vitano wakati wa michezo ya  Ligi Kuu Tanzania Bara zilizochezwa jioni ya leo, 'Mnyama', Simba alishindwa kufurukuta Tanga na Azam wakang'anganiwa Morogoro.
Simba ikicheza na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani walitoka suluhu, wakati Azam walitoshana nguvu na Polisi Moro kwa kutoka sare ya mabao 2-2.
Magoli katika pambano la mjini Morogoro, mabingwa watetezi walipata mabao yake kupitia kwa mapacha Kipre Tchetche  dakika 10 na Kipre Balou dakika 66 kwa frikiki.
Polisi walipata mabao yake kupitia Edward Christopher katika dakika ya 25 na Selemen Kassim Selembe' dakika ya 69.
Katika uwanja wa Chamazi, JKT Ruvu na Mbeya City walitoka sare ya bao 1-1, matokeo yaliyofana na yale ya mjini Mtwara kati ya Ndanda Fc dhidi ya wageni wao Stand United.
Wenyeji walishtushwa kwa bao la dakika ya 9 la wageni lililofungwa na Jibelele Abasilim kabla ya kuja kusawazisha katika dakika ya 53 kupitia kwa Nassor Kapama.
Mjini Mbeya, wenyeji Prisons ilishindwa kutamba Kwenye uwanja wa Sokoine, baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting.
Ruvu walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa Yahya Tumbo kwa tiktak kabla ya wenyeji kusawazisha dakika ya 36 kupitia kwa  Jacob Kalipalate na kuzifanya timu hizo zigawane pointi moja moja.
Kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga, Kagera Sugar waliondoa gundi baada ya kuicharaza Mgambo JKT bao 1-0. Bao hilo liliwekwa kimiani na Atupele Green.
Ushindi huo umeifanya Kagera kufikisha pointi 18 na kuzidi kuifanya ligi hiyo kuwa ngumu kutokana na klabu kufungana au kutofautiana kwa pointi chache, Azam wakirejea kileleni wakiiengua Yanga.
Licha ya timu zote kuwa na pointi 22 Azam wanaongoza kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, huku Mtibwa wakiporomoka kutoka  nafasi ya tatu hadi ya sita.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa pambano moja tu kwenye uwanja wa Taifa, Yanga ikivaana na Mtibwa Sugar katika mechi ya kisasi kwani Mtibwa waliitoa nishai Yanga kwenye uwanja wa Morogoro kwa kuifunga mabao 2-0 katika mechi ya ufunguzi wa ligi ya msimu huu uwanja wa Jamhuri.

TANZAIA: MUINGIZAJI WA KAOLE AFARIKI DUNIA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjks1hjwTP8Q0Vl_k4K4nOEkfxDXbksWhyphenhyphen_LlhSUdlCHbEDgzM3LilEiG4s2LvSiMzHxc61pDthJA1RIeyJiJp4BEPDQ5IprTuUcqUZHOKBl_-FIXPWjXog_TJAtWxSEe7t1CJXCxAHEtI/s1600/KaoneSanaa-cut-533.jpg
Baadhi ya wasanii waliowahi kuigiza na Mama Mashaka wakiwa na Januari Makamba. Wasanii hawa wamelifufua kundi kwa jina jipya la Kaone Sanaa Group
MSANII wa maigizo aliyewahi kuwika na kundi la Kaole Sanaa Group, Mwajuma Abdallah ‘Mama Mashaka’ amefariki dunia.
Mama Mashaka amefariki usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano za usiku katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala, jijini, Dar.Kwa habari zaidi tutaendelea kukujuza hapa.
GPL

BALAA TUPU LEO LIGI KUU YA ENGLAND

http://www.independent.co.uk/incoming/article9756138.ece/alternates/w620/Liverpool%20v%20Everton,%20Arsenal%20v%20Tottenham:%20The%20major%20talking%20points%20this%20weekend%20in%20the%20Premier%20League.jpghttp://news.bbcimg.co.uk/media/images/80827000/jpg/_80827370_newsplit.jpgWAKATI nahodha wa Manchester City Vincent Kompany akidai anaamini kuwa uzoefu wa sasa wa mabingwa hao unaweza kuwasaidia kukwea kileleni katika kiti walichokalia Chelsea katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, leo ni kama vita katika ligi hiyo.
Arsenal watavaana na wapinzani wa jadi wa London ya Kaskazini, Tottenham, wakati Liverpool watawafuata wapinzani wao wa jadi Everton.
City iliyopo katika nafasi ya pili leo itacheza mchezo wake wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Hull City kwenye uwanja wa Etihad ikiwa pointi tano nyuma ya vinara Chelsea, ambao watakuwa ugenini leo dhidi ya Aston Villa.
Kikosi hicho cha kocha Manuel Pellegrini kilikuwa pointi moja nyuma ya Liverpool wakati zimebaki mechi mbili kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita lakini iliweza kutwaa taji la Ligi Kuu.
Na Man City ilikuwa pointi nane nyuma ya Manchester United wakati zimebaki mechi sita kabla hawajatwaa taji la Ligi Kuu siku ya mwisho ya msimu wa mwaka 2011/12 wakiwa chini ya kocha wazamani wa timu hiyo Roberto Mancini.
"Hii ndio hali ya kawaida kwetu, alisema Kompany beki wa kati kutoka Ubelgiji, ambaye alikuwa mchezaji muhimu wakati timu hiyo ilipotwaa taji hilo mara zote.
"Kuwa pointi tano nyuma Januari au Februari ni jambo kubwa.
"Tunajisikia vizuri kuwa katika nafasi hiyo. Tumekuwa katika nafasi hiyo mara nyingi."
Huku Man United wakitawala misimu miwili iliyopita, Chelsea waliweza kufanya mambo kama Man City kama wapinzani wakubwa katika mbio za kuwania taji.
Man United wamekuwa wakipambana tangu kuondoka kwa Alex Ferguson mwaka 2013 na sio ama mbadala wake, David Moyes na Louis van Gaal, aliweza kuiweka timu hiyo katika mbio za ubingwa.
Ukiacha tambo hizo za Kompany, ligi hiyo leo itakuwa kama vita wakati viwanja kadhaa vitakavyotimua vumbi huku gumzo likiwa mechi za watani wa miji ya London na Liverpool.
Liverpool watakuwa ugenini kuvaana na Everton, kama itakavyokuwa kwa Arsenal watakaowafuata Tottenham Hotspur uwanja wa White Hart Lane.
Ratiba kamili EPL ipo hivi wikiendi hii:
Leo Jumamosi:
Tottenham     v    Arsenal   (Saa 9:45 alasiri)
Man City  v    Hull City (Saa 12:00 jioni)
Villa     v    Chelsea   (Saa 12:00 jioni)
Swansea  v    Sunderland  (Saa 12:00 jioni)
QPR  v    Southampton (Saa 12:00 jioni)
Leicester     v    Palace (Saa 12:00 jioni)
Everton   v    Liverpool (Saa 2:30 usiku)
Kesho Jumapili:
Burnley   v    West Bromwich (Saa 9:00 alasiri) 
Newcastle v   Stoke City (Saa 11:05).
West Ham  v   Man United

Zidane kumrithi Ancelotti Real Madrid

http://i.cbc.ca/1.2649728.1400694761!/cpImage/httpImage/image.jpg_gen/derivatives/16x9_620/zinedine-zidane.jpg
Zidane kushoto akiwa na Ancelotti
 MADRID, Hispania
GWIJI wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane ananolewa ili aje kuwa kocha wa baadaye wa klabu ya Real Madrid, alisema Carlo Ancelotti.
Zidane, ambaye kwa sasa ndiye anakinoa kikosi cha akiba cha Real Madrid cha Castilla, "ana viwango vyote " vinavyohitajika kushika usukani wa klabu, alisema Ancelotti alipozungumza na waandishi wa habari.
"Nafurahia kazi ya Zidane, anafanya vizuri sana, " alisema Ancelotti katika mahojiano hayo.
Baada ya mwanzo mgumu wa msimu, Castilla wako kileleni mwa ligi daraja la tatu ya Hispania.
"Anafanya vizuri sana katika mwaka wake wa kwanza wa kuifundisha timu hiyo. Ameichukua Castilla hadi katika nafasi ya kwanza na anatakiwa kuendeleza kazi hiyo nzuri.
"Kwangu ni wazi kuwa ana vigezo vyote vya kuwa kocha wa kuifundisha timu kubwa. Na ikiwemo Real Madrid," alisema kocha huyo Muitalia, aliyemteua gwiji huyo Mfaransa msimu uliopita.
Baada ya kushuhudia Castilla ikipoteza mechi zake tano kati ya sita za mwanzo, Zidane alibadili mambo na pamoja na ugeni wake katika kuifundisha timu hiyo, sasa amepoteza mchezo mmoja tu katika miezi minne iliyopita.
Timu hiyo inaweza kuongeza tofauti ya pointi endapo Jumapili kesho itashinda itakapocheza dhidi ya Athletic Bilbao.

MKWAKWANI PATACHIMBIKA NI COASTAL, SIMBA!

Simba
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/coastal-union1.jpg
Coastal Union
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/slides/AZAM%20FC.JPG
Azam Fc watakaoivaa Polisi Moro na mbinu za Kikongo
http://kabumbu.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/polisi-moro-KIKOSI.jpg
Maafande wa Polisi Moro watahimili vishindo vya Azam uwanja wa Jamhuri?
PATACHIMBIKA Mkwakwani! Ndivyo unavyoweza kusema wakati 'Mnyama' Simba watakaposhuka dimbani kuvaana na 'ndugu' zao, Coastal Union katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Aidha mabingwa watetezi Azam watakuwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro kuwafundisha Polisi Moro mbinu mpya za Kikongo watakapoumana kwenye mfululizo wa ligi hiyo.
Coastal Union iliyofumuliwa na Yanga bao 1-0 katikati ya wiki watakuwa na kazi ngumu ya kuwasimamisha Simba iliyozinduka tangu walipolambwa mabao 2-1 na Mbeya City.
Simba iliitandika JKT Ruvu mabao 2-0 katika pambano la kusisimua wiki iliyopita na hivo watavaana na Coastal wakiwa na ari na nguvu kubwa.
Ikiwategemea nyota wake wa KIganda, Emmanuel Okwi, Dan na nduguye Simon Sserunkuma itashuka dimba la Mkwakwani wakiwa na nia ya kuongeza pointi tatu ili wasogea maeneo ya juu baada ya kushindwa kuonja kwa muda mrefu tangu ligi ilipoanza Septemba 20 mwaka jana.
Mechi nyingine ya kutupiwa macho ni ile ya Azam dhidi ya Polisi itakayochezwa uwanja wa Jamhuri, ambapo Polisi wakiwa wanachekelea kuizima Mbeya City katika mechi hiyo iliyopita itataka kuwazima Azam wanatokea DR Congo walipoenda kushiriki michuano maalum.
Meneja wa Azam, Jemedari Said amesema kikosi chao kipo tayari kwa vita mbele ya Polisi, huku habari ambazo MICHARAZO inayo ni kwamba klabu hiyo imevamia tawi la Simba la Mpira Pesa la Magomeni Mikumi na kuwanunua mashabiki kuwapeleka Morogoro kwa ajili ya kuwapa sapoti katika mchezo huo.
Azam watakuwa wakihitaji ushindi ili kurejea kileleni angalau kwa muda baada ya Yanga watakaocheza kesho dhidi ya Mtibwa Sugar, kuwaengua katikatgi ya wiki baada ya kuwalaza Coastal.
Mabingwa watetezi hao wana pointi 21, moja pungufu na ilizonazo Yanga wenye 22 na waliokaa kileleni, huku Polisi wakiwa nafasi ya Nne wakiwa na pointi 18 sawa na ilizonazo JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar.
Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni pambano la kukata na Mundu kati ya Ndanda Fc dhidi ya Stand United katika mechi ya kisasi itakayochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, huku Mgambo JKT baada ya 'likizo' ndefu itashuka dimba la Kambarage Shinyanga kuvaana na 'wenyeji' wao Kagera Sugar waliohamia katika uwanja huo toka CCM Kirumba.
Maafande wa Prisons wakuwa uwanja wa nyumbani wa Sokoine, Mbeya kuwaalika Ruvu Shooting katika mchezo mwingine wa kisasi baada ya Prisons kuwatoa nishai wapinzani wao kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mabatini katika mechi ya ufunguzi wa duru la kwanza.
Baada ya kupokea kichapo toka kwa Simba, maafande wengine wa JKT Ruvu watakuwa uwanja wa nyumbani wa Chamazi kuwakaribisha wababe wa Simba, Mbeya City katika mechi kali ya kusisimua inayowakutanisha makocha wenye rekodi nzuri Fred Minziro na Juma Mwambusi.

Wenyeji Guinea ya Ikweta watozwa faini


256137B200000578-2941812-image-a-28_1423209530874
WENYEJI wa fainali za kombe la Mataifa ya Africa, Afcon 2015, Guinea ya Ikweta wametozwa faini ya dola laki moja kwa mtafaruku wa juzi usiku katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ghana ‘Black Stars’.
Hata hivyo CAF imesema Guinea ya Ikweta wataucheza mpambano wao wa kusaka Msindi wa Tatu dhidi ya DR Congo mchezo unaochezwa leo.
Plastic bottles and other debris litter the running track at the Malabo Stadium following the crowd disturbances
Mashabiki wa timu mwenyeji walifanya vurugu na kuwarushia chupa za maji wachezaji wa Ghana, Viongozi pamoja na mashabiki.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki hao, huku wachezaji wa Ghana wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali.
Vurugu hizo zilisababisha mechi kusimama kwa dakika 35, lakini Ghana walifuzu fainali kutokana na ushindi wa mabao 3-0.
Ghana wanasema katika vurugu zile watu wangeweza kufa, ingawa inaelezwa watu 14 walijeruhiwa akiwa raia wa Mali aliyeumia vibaya.

Nyosso, Morris wafungiwa kisa 'uhuni' uwanjani



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limefungua makucha yake na kumuadhibu beki ngangari wa Mbeya City, Juma Nyosso kwa kitendo cha kumshika mshambuliaji wa timu yake ya zamani, Simba Elias Maguri.
TFF imemfungia Nyosso adhabu ya mechi nane na klabu yake imesema itakata rufaa kwa mabai ni ya kionevu na yenye kuviza maendeleo ya soka hata kama ni kweli beki wao alifanya kitndo hicho kinavyotafrisiwa kuwa ni 'udhalilishaji'.
Nyosso anatuhumiwa kumfanya 'ubasha' Maguri timu zao zilipokutana January 28 na Simba kulala mabao 2-1.
Mbali na Nyosso pia TFF imemfungia mechi tatu beki mahiri wa Azam, Aggrey Morris kwa madaiu ya kumpiga kiwiko kilichomfanya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kuzimia uwanjani.
Morris anadaiwa kufanya tukio hilo wakati timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Taifa Januari 25 na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Beki mwingine George Assey anayedaiwa kumpiga kabali Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe yeye amewekwa kiporo kwa kushindwa kuhudhuria kikao cha kamati ya Nidhamu iliyotoa adhabu hizo.
Assey anayeichezea Ruvu Shooting alionekana akimniga na kumtoa damu Tambwe katikia mechi yao kwenye uwanja wa Taifa iliyoisha kwa sare isiyo na magoli.

Ancelotti awakosa Rodriguez, Ronaldo Madrid Derby

http://www1.pictures.zimbio.com/gi/James+Rodriguez+Club+Atletico+de+Madrid+v+xwEg2Ahj4GDl.jpg
Ameikosa Derby ya Madrid baada ya kuumia mguu
http://www.realmadridfootballblog.com/wp-content/uploads/2013/05/1530-cristiano-ronaldo-real-madrid.jpg
Ronaldo karudi
KOCHA klabu ya ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa James Rodriguez na Sergio Ramos watakosa mchezo wa La Liga dhidi ya mahasimu wao jiji Atletico Madrid leo Jumamosi, lakini cha kufurahisha ni kwamba nyota wake Cristiano Ronaldo atakuwepo katika mchezo huo.
Ronaldo alikosa mechi iliyopita kutokana na adhabu iliyotokana na kadi nyekundu na leoi atarejea kwenye mechi hiyo ya watani wa jadi wa jiji la Madrid litakalochezwa kwenye uwanja wa Estadio Vincente Calderon nyumbani kwa mabingwa watetezi wa La Liga, Atletico Madrid.
Ancelotti atawakosa wachezaji wake wawili Rodriguez na Ramos baada ya wawili hao walipata majeruhi katika mchezo wa majuzi wakiiitandika Sevilla kwa mabao 2-1, ambapo Ramos alipata majeruhi ya msuli wa paja huku Rodriguez akielezwa kuvunjika mguu wa  kulia baada ya kufunga bao la kuongoza.
Ancelotti sasa anakabiliwa na uhaba wa mabeki kutokana na beki wake wa kati Pepe naye kuwa nje kutokana na majeruhi ya mbavu.
Hata hivyo, Ancelotti ana matumaini chipukizi Raphael Varane na Nacho wataweza kumudu changamoto za Atletico iliyo chini Diego Simeone.
Akihojiwa Ancelotti amesema pamoja na kuwakosa mabeki wake kutegemea lakini bado ana imani na waliopo akiwemo Nacho na Varane kwamba wataweza kuhimilia mikikimikiki ya wapinzano wao hao.

NGOMA MPYA YA DAYNA NYANGE-PEPEA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjUuFc5y1TNmgfCZGwbKjGo5Ldf64JSg-nXbucI8rILy4V3TWdGcBsZGy6mQifc6PwViasH3kp8KW2grMPo2-LSLfgn0RISgGqbXqKAE6Wvd0zA9hAr6POtAkB-6j1DTJAND9HnpuhKiXfA/s640/dayna.JPG
Dayna Nyange katika pozi
BONYEZA HAPA KUUSIKILIZA WIMBO MPYA WA DAYNA NYANGE 
 Dayna Nyange - Pepea @Hulkshare:

Thursday, February 5, 2015

Real Madrid waitumia salamu Atletico Madrid La Liga

The Colombia playmaker wheels away in celebration after scoring a delightful opener for Real during Wednesday's encounter
James Bond akishangilia bao la kwanza la Madrid
Real doubled their lead on 36 minutes when substitute Jese (left) finished from close-range against Sevilla
Jesse akifunga bao la pili la wenyeji Santiago Bernabeu
Gareth Bale (left) was a constant menace to the Sevilla defence throughout the match at the Santiago Bernabeu
Gareth Bale akiwajibika uwanjani
VINARA wa Ligi Kuu ya Hispania, Real Madrid imetuma salamu kwa wapinzani wao wa jadi Atletico Madrid watakaovaana nao siku ya Jumamosi baada ya kuicharaza Sevilla kwa mabao 2-1 katika mfululizo wa ligi hiyo maarufu kama La Liga.
Mabao ya  James 'Bond' Rodriguez la dakika ya 12 na lingine la Jesse dakika ya 36 yalitosha kuwapa ushindi muhimu vijana wa Santiago Bernabeu kwenye uwanja wao wa nyumbani kabla ya kuwafuata Atletico katika mechi ya kisasi.
Wageni walijipatia bao la kufutia machozi dakika 10 kabla ya kumalizika kwa pambano hilo kupitia kwa Iago Aspas.
Ushindi huo umeifanya Real Madrid ambayo iliwakosa nyota wake kadhaa kiwamo nahodha Cristiano Ronaldo anayetumikia adhabu.ya kadi nyeekundu, kufikisha pointi 54 na kujikita kileleni huku nyuma yao wakiwa ni Barcelona wenye pointi 50, na saba zaidi ya wapinzani wao wa Jumamosi walipo nafasi ya tatu.


Asamoah Gyan aleta hofu Ghana wakiwavaa wenyeji Afcon

http://megasignals.net/wp-content/uploads/2014/06/Asamoah-Gyan-Ghana-World-Cup-2014-Wallpaper.jpg
Nahodha wa Ghana, Asamoah Gyan
MALABO, Guinea ya Ikweta
MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Ghana, Christian Atsu anaweza kuwa nguzo muhimu katika mechi ya nusu-fainali ya Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Guinea ya Ikweta leo kama Asamoah Gyan atashindwa kucheza kutokana na majeraha, mchezaji mwenzake Jonathan Mensah alisema juzi.
"Sote tunafahamu nini Atsu anaweza kukifanya, inasaidia sana kuwa na wachezaji ambao wanaweza kuleta tofauti mchezoni," beki Mensah aliwaambia waandishi wa habari.
"Ana nafasi muhimu katika timu, anafanya kile anachotaka kufanya na anaongezeka ubora siku hadi siku. Tuna furaha yuko katika makali yake hivi sasa na ataisaidia timu."
Atsu (23), alifunga goli kali wakati kikosi cha Avram Grant kilipotinga katika hatua ya nusu-fainali kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Guinea mjini Malabo Jumapili lakini ni lazima wajiandae kuwakabili wenyeji leo bila ya nahodha wao mwenye ushawishi kikosini Gyan.
Baada ya kupona malaria na kufunga goli la dakika za lalasalama la ushindi wa Ghana katika mechi yao ya pili ya hatua ya makundi dhidi ya Algeria, Gyan aliumizwa kwa teke la kurukiwa tumboni kutoka kwa kipa wa Guinea, Naby Yattara.
Wakati Gyan akiwa shakani katika mechi ya nusu-fainali leo, Mensah anaamini Atsu, ambaye yuko kwa mkopo Everton akitokea katika klabu yake ya Chelsea, anaweza kufunika kutong'aa kwake kwenye ngazi ya klabu na kutamba kwenye timu ya taifa.
"Hisia inakuwa ni tofauti anapoichezea Everton. Tunamuachia anafanye kile anachoweza vyema, ni timu tofauti kabisa," alisema Mensah.
"Timu hii ya Ghana haina mfungaji maalum wa magoli, sote tunafunga tunapopewa nafasi, hilo ni jambo ambalo linalotusaidia sana."
Huku akisifu kuongezeka ubora kwa Atsu, Mensah pia alielezea umuhimu wa Gyan kwenye kikosi cha Black Stars.
"Ndani na nje ya uwanja Gyan ni kiongozi, yeye ni nahodha wa timu na wakati wowote anaokuwapo uwanjani huthibitisha yeye ni kiongozi wa kweli," alisema.
"Yeye ni mshambuliaji bora barani Afrika hivyo wakati wowote anaokuwapo uwanjani ni kama jumlisha mbili kwenye timu.
"Anajisikia maumivu. Amefadhaika sana, kwa sababu ndiyo kwanza alikuwa ameanza kurejea katika makali na kisha majeraha haya yamekuja. Tumezungumza na morali yake iko juu, lakini wakati huohuo hayuko fiti kwa asilimia 100.
"Yeye ni bonge la kiongozi na hata pale asipofunga, au kupata fursa ya kufunga, wakati wote hufanya kazi kwa ajili ya timu. Yeye ndiye kinara wetu na tuna furaha kuwa naye," aliongeza.
Iwapo Ghana wanaing'oa Guinea ya Ikweta na kukutana na Ivory Coast watarejesha kumbukumbu ya Fainali za mwaka 1992 zilizozikutanisha timu hizi na Ivory Coast kushinda kwa mikwaju ya penati.

JAHAZI LA BORUSSIA DORTMUND LAZIDI KUZAMA UJERUMANI

Borussia Dortmund keeper Roman Weidenfeller
Wachezaji wa Dortmund hawaamini kama wamezama teena nyumbani
Augsburg's Raul Bobadilla
Bobadilla akimtungua kipa wa Dortmund, Roman Weidenfeller
Borussia Dortmund coach Jurgen Klopp (centre)
Kocha Jurgen Kloop akiwa na wachezaji wake vichwa chini
JAHAZI la mabingwa wa zamani wa Ujerumani na wana fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya za mwaka juzi, Borussia Dortmund limezidi kutota baada ya usiku wa jana kugongwa nyumbani bao 1-0 na Augsburg na kuzidi kujichimbia mkiani mwa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga.
Bao pekee lililofungwa na Raul Bobadilla dakika tano baada ya kuanza kwa kipindi cha pili lilitosha kuwaacha vijana wa kocha Jurgen Kloop wakisalia mkiani wakiwa na pointi 16 tu baada ya kucheza mechi 19 huku wapinzani wao wakichupa hadi nafasi ya nne katika msimamo wakiwa na pointi 33.
Katika mechi 19 ilizocheza Dortmund imeshinda mechi nne tu na kuambulia sare nne huku ikipoteza mechi 11 na kuwa na wakati mgumu katika kupigana kusalia katika ligi hiyo, matoke ambayo ni  mabaya kwa timu hiyo kuwahi kutokea katika misimu ya karibuni.
Kloop ameiongoza timu yake katika mechi nane na kupata ushindi mmoja tu, kitu ambacho kimeacha maswali mengi kwa mashabiki wa timu hiyo iliyotetemesha ligi ya Ujerumani na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ujumla, japo ipo kwenye mechi za mtoano zitakazoanza wiki mbili zijazo ambapo Wajerumani hao watavaana na Juventus.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa jana Hoffenheim ilikubali kichapo nyumbani dhidi ya WErder Bremen kwa kulazwa mabao 2-1,  Hertha Berlin nayo ikalala 1-0 nyumbani mbele ya Bayer Leverkusen, huku FC Koln  na Stuttgart wakitoshana nguvu kwa suluhu isiyo na mabao na Paderborn ikanyukwa mabao 3-0 nyumbani na Hamburger SV.

Liverpool wafanya kweli Kombe la FA,

The Brazilian midfielder points to the sky after his goal put Liverpool into the FA Cup fifth round
Coutinho akimshukuru Mungu kwa kuifungia Liverpool bao lililowavusha Raundi ya Tano ya Kombe la FA usiku wa jana
Alberto Moreno (left) jumps for joy with Coutinho as Liverpool secure an FA Cup fifth round tie against Cyrstal Palace
Coutinho akipongezwa na Moreno
Clough, making just his third Bolton start, is tripped by Skrtel as referee Roger East looks on in the distance
Martin Skrtel akimchezea dogo wa Bolton rafu iliyozaa bao pekee la wenyeji wa mchezo huo wa marudiano
Eidur Gudjohnsen (left) puts Bolton into a 1-0 lead against Liverpool with a penalty in the 59th minute 
Eidur Gudjohnsen akifunga penati ya Bolton
KLABU ya Liverpool ilitoka nyuma dhidi ya Bolton Wanderers na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutinga Raundi ya Tano ya Kombe la FA.
Mechi hiyo ya marudiano ilichezwa usiku wa jana kwenye uwanja wa Macron nyumbani kwa Bolton ambao waliwashtua wageni wao kwa kutangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa EidurGudjohnsen katika dakika ya 59 baada ya dakika 45 za awali kumalizika timu hizi zikiwa nguvu sawa ya kutofungana.
Bao hilo lilifungwa kwa mkwaju wa penati baada ya Martin Skrtel kumchezea rafu Zach Clough, hata hivyo dakika nne kabla ya kumalizika kwa pambano hilo na huku wenyeji wakiamini wameungana na timu nyingine zilizowatoa nishai vigogo katika michuano hiyo, Raheem Starling aliisawazishia Liverpool bao hilo.
Sekunde chache kabla ya kumalizika kwa pambano hilo pengine wenyeji ambao walimpoteza mmchezaji wao mmoja baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano iliyofuatana na nyekundu, wakiamini wataenda kwenye muda wa ziada, Phillipe Coutinho aliiandikia bao la ushindi Liverpool na kuwafanya kusonga mbele na kukabiliana sasa na Crystal Palace Siku ya Wapendanao uwanja wa ugenini.
Kabla ya mechi hiyo ya FA, Liverpool  itakuwa na kibarua wikiendi hii kuvaana na wapinzani wao wa jadi Everton uwanja wa ugenini Goodson Park kisha kuwakaribisha Vijogoo wenzao wa London, Tottenham Hotspur uwnaja wa Anfield Jumanne ijayo.

Yanga yawabutua Coastal Union kwao, mkwakwani kimyaaaaa!

Cannavaro 6
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza nahodha wao Cannavaro kwa kufunga bao pekee la Yanga dhidi ya Coastal


Cannavaro akishangilia bao lake
Match Report: Coastal Union 0 – 1 Yanga, Yanga yakwea kileleni
Oyooooooooo! Cannavaro akishangilia bao lake
BAO pekee la Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' lilitosha kuwapa ushindi Yanga na kuwapeleka hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuizima Coastal Union kwenye uwanja wao wa nyumbani wa CCM Mkwakwani Tanga.
Yanga walipata ushindi huo katika mechi iliyojaa ufundi na ubabe ya kiporo kilicholeta mvuto wa aina yake kutokana na tambo na majigambo ya viongozi wa pande mbili kwamba kabla ya kuchezwa kwake.
Cannavaro amekuwa mhimili mkubwa wa Yanga kwa uhamasishaji wake, kujituma na kufunga mabao muhimu pale washambuliaji wa timu hiyo wanapozembea, aliweka kimiani bao hilo dakika ya 11 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kurushwa wa beki Mbuyu Twite ulioparazwa na Simon Msuva na kuipa Yanga pointi tatu zilizowafanya wafikishe 22, moja zaidi ya mabingwa watetezi ambao hata hivyo wana mchezo mmoja pungufu zaidi ya Yanga.
Licha ya Coastal Unio kucharuka kusaka bao la kusawazisha walienda mapumziko wakiwa nyuma na hata katika kipindi cha pili hali ilikuw ahivyo hivyo, huku Yanga ikimpoteza mshambuliaji wake Amissi Tambwe aliyeumizwa wakati wa mchezo kipindi cha kwanza na kushindwa kurudi uwanjani.
Kwa kipigo hicho Simba ambayo Jumamosi hii wana mtihani mwingine dhidi ya Simba, wamesaliwa na pointi zao 17 baada ya mechi 13 na kusalia kwenye nafasi ya saba mbele ya Simba wenye pointi 16 baada ya mechi 12.
Ligi hiyo itaendelea tena wikiendi hii kw amichezo kadhaa huku pambano la Yanga na Mtibwa Sugar likiwa limeahirishwa ili kutoa nafasi kwa wawakilishi wa Kombe la Shirikisho kujiandaa vema kabla ya kuvaana na BDF XI ya Botswana wiki ijayo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tembo wa Afrika watangulia fainali, waigonga Kongo 3-1


afcon
Gervinho akijaribu kumtungua kipa wa DRC, Kidiaba
Wachezaji wa Tembo wa Ivory Coast wakishangilia ushindi wao wa kutinga fainali za Afcon 2015
TEMBO wa Ivory Coast, wamedhihirisha dhamira yao ya kutaka ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika baada ya kugawa dozi nene kwa Chui wa DR Congo kwa kuwalaza mabao 3-1 katika mechi ya Nusu Fainali na kutinga Fainali za michuano hiyo itakayochezwa Jumapili.
Kikosi cha Ivory Coast kikiongozwa na nahodha wake, Yaya Toure kilifanikiwa kutinga hatua hiyo ya fainali kwa kulipa kiasi ilichowahi kupewa na wapinzani wao wakati wa mechi za makundi za kuwania kwenda Guinea ya Ikweta kwa kulazwa nyumbani kwao mabao 4-3.
Wafungaji wa mabao ya wanafainali wa mwaka 2012 walikuwa Yaya Toure katika dakika ya 21, Gervinho aliyeongeza la pili dakika ya 41 na  Kanon aliyemaliza udhia katika kipindi cha pili kwenye dakika ya 68.
Bao la kufutia machozi la Congo waliowang'oa watani zao wa jadi Congo-Brazzaville kwenye mechi ya robo fainali lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Mbokani dakika ya 24.

Kwa matokeo hayo Ivory Coast wanasubiri mshindi wa mechi ya leo kati ya mabingwa mara nne Ghana dhidi ya Guinea ya Ikweta ili kuumana nao kwenye fainali ya Jumapili itakayoamua bingwa mpya wa Afrika baada ya taji kiutokuwa na mwenyewe kufuatia Nigeria waliokuwa mabingwa kukwa kwenda Afcon 2015.
DR Congo wenyewe watakuwa wakisubiri kujua wataumana na timu ipi itakayopoteza mchezo wa leo ili kumenyana naye katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu itakayochezwa keshokutwa Februari 7.

Wednesday, February 4, 2015

ZAHIR ALLY ZORRO FT MWANA FA

VIJIMAMBO: ZAHIR ALLY ZORRO FT MWANA FA

Michuano ya Utalii Cup 2015 kutimka Feb 23 jijini Dar

http://www.mercurialsports.com/media/catalog/product/cache/1/image/9df78eab33525d08d6e5fb8d27136e95/t/r/tr1543f.jpgMICHUANO ya soka ya kuwania kombe la Utalii ‘Utalii Cup 2015’ inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 23, kwenye viwanja mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya michezo ya Bos Promotions, Samuel Peter, alisema maandalizi yanakwenda vizuri na bingwa atazawadiwa Ng’ombe.
Peter alisema mbali ya zawadi hiyo, washindi wa kwanza pia watapata nafasi ya kutembelea moja ya mbuga za wanyama zilizopo nchini.
Alisema lengo la michuano hiyo ni kuibua vipaji vya wanasoka chipukizi jijini Dar es Salaam na kutangaza utalii wa ndani kupitia mchezo wa soka.
Msemaji huyo alisema timu 12 zinatarajia kushiriki na zitapangwa katika makundi mawili ambapo nne za juu kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya robo fainali.
Peter alisema milango ipo wazi kwa timu ya daraja lolote inayotaka kushiriki mashindano hayo yatakayokuwa yakifanyika kila mwaka.
“Maandalizi yanakwenda vizuri na tayari tumeshaanza kutoa fomu kwa timu zinazotaka kushiriki na namba ya mawasiliano ni 0714 743276”, alisema.

YANGA, COASTAL UNION NI VITA TUPU LEO MKWAKWANI

Wagosi wa Kaya, Coastal Union waliopania kuwatia maumivu vijana wa Jangwani leo Mkwakwani
Yanga waliopa kuondoa 'gundu' Mkwakwani kwa kuinyoa Coastal Union
COASTAL Union wametangaza vita ya dakika 90 dhidi ya Yanga katika mechi pekee ya leo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, inayopchezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, huku Yanga wenyewe akitamba kuwa wameenda Mkwakwani kuchukua pointi tatu kwa wenyeji wao.
Timu hizo zinakutana kwenye mchezo nhuo wa kiporo huku kila moja ikitoka kulazimishwa sare isiyo na mabao nyumbani katika mechi zao za mwishoni mwa wiki.
Yanga ilibanwa na Ndanda Fc kwenye uwanja wa Taifa, wakati Coastal ikiwa nyumbani ilishindwa kufurukuta kwa Mtibwa Sugar, hali inatyofanya pambano la leo kuwa kama vita ya kusaka pointi tatu kwa timu zote.
Coastal kupitia Msemaji wake, Oscar Assenga, amesema kuwa kikosi chao kipo tayari kuwatoa nishai Yanga, wakati Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro akisema wameenda Tanga kuchukua pointi tatu kwa vile timu yao ni bora kuliko wapinzani wao.
Coastal inayonolewa na kocha James Nandwa kutoka Kenya itakuwa na kibarua kigumu kwa wapinzani wao licha ya kwamba kwa muda sasa Yanga haijaonja ushindi Mkwakwani dhidi ya Wagosi wa Kaya ama Mgambo JKT.
Mara ya mwisho Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani ilikuwa Novemba 12, 2012 iliposhinda 2-0.
Katibu Mkuu wa Coastal Kassim El Siagi alisema angetaka mashabiki wa soka kuthibitisha ipi timu ya soka la kweli la uwanjani na timu za magazetini ambao namna wanavyopambwa unaweza kusema ni Barcelona ilihali ni timu ya kawaida ionayoshindwa kuzifunga hata timu ndogo kama Ruvu Shooting na Ndanda FC.
Hata hivyo Yanga wameapa kufanya kweli leo baada ya kushuhudia safu yake ya ushambuliaji katika mechi tatu ilizocheza za Ligi Kuu ikifunga moja tu walipoilaza Polisi Moro.
Mashabiki wa Yanga pamoja na timu yao wapo mjini Tanga tangu majuzi kwa ajili ya pambano hilo ambalo litatoa taswira mpya ya msimamo wa Ligi Kuu timu mojawapo ikipata ushindi, Yanga ikiweza kurejea kileleni baada ya kutemeshwa muda mrefu na Mtibwa Sugar na baadaye Azam.
Kadhalika Coastal ikishinda inaweza kukwea hadi nafasi ya pili na kuwaengua Yanga waliopo katika nafasi hiyo kwa sasa wakiwa na pointi 19, mbili nyuma ya Azam wanaoongoza na pointi zao 21.
MSIMAMO LIGI KUU ULIVYO KWA SASA
                             P   W    D    L    F    A   GD   Pts
01. Azam              11  06  03  02  15  08  07   21
02.  Yanga            11  05  04  02  12   07  05  19
03. Mtibwa Sugar  11  04  06  01  13  07  06   18
04. Polisi Moro      13  04  06  03   10  09  01  18
05. JKT Ruvu        13  05  03  05   13   13  00  18
06. Ruvu Shooting13  05  03   05   09   10  -1  18
07. Coastal Union 12  04  05   03  10   08  02  17
08. Simba            12  03  07   02   13   11  02  16
09. Mbeya City     12   04  03  05  08   10  -2   15
10. Kagera Sugar 13  03  06  04   10   11   -1  15
11. Mgambo JKT  11  04  02  05   06    10  -4  14
12. Ndanda Fc     13  04  02   07  12    17  -5  14
13. Stand Utd      13  02  05   06   08   16  -8  11
14. Prisons          12  01  07   04   09   11  -2   10

MWANASHERIA MKUU AKATA MZIZI WA FITINA MAHAKAMA YA KADHI

http://www.thecitizen.co.tz/image/view/-/2604484/highRes/932159/-/maxw/600/-/d4xms2z/-/AG_Masaju.jpg
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akizungumza na wanahabari
http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/5.jpg
Viongozi wa Kiislam wakizungumza na wanahabari kupinga tamko la Jukwaa la Wakristo waliopinga Mahakama ya Kadhi kujadiliwa bungeni hivi karibuni
TEC
Viongozi wa Jukwaa la Wakristo wakitoa msimamo wao wa kupinga Mahakama ya Kadhi kujadiliwa bungeni ikiwa kama sehemu ya msimamo wao wa kuikata tamaa mahakama hiyo ianzishwe nchini
WAKATI viongozi wa Kikristo wakiendelea kushupaa na kuipinga kwa nguvu Mahakama ya Kadhi inayoliliwa na Waislam nchini Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju ameweka wazi kwamba hakuna jambo baya juu ya uwepo wa mahakama hiyo kama inavyolazimishwa kuaminishwa.
Kwa mujibu wa gazeti la NIPASHE, limedokeza kuwa wakati muswada wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ukitarajiwa kujadiliwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, amesema haitakuwa na athari yoyote hasi nchini.
Masaju alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE jijini Dar es Salaam akifafanua juu ya muswaa huo hasa baada ya kuwapo kwa dalili za mvutano kuhusu uanzishwaji wa mahakama hiyo.
Alisema tatizo lililopo ni kwamba serikali haijachukua hatua madhubuti kuwaelimisha wananchi namna ambavyo mahakama hiyo itakuwa inaendesha kazi zake.
“Suala la Mahakama ya Kadhi limekuwapo tangu zamani na ilikuwa ahadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Serikali hatuoni kwa nini suala hili lisifanikiwe,” alisema.
Masaju alisema Watanzania lazima watambue kuwa Mahakama ya Kadhi itahusu mambo ya Waislamu wenyewe ambayo ni mirathi, ndoa na talaka.
“Sioni kwa nini isifanikiwe kwa sababu mahakama hii haiwahusu watu ambao siyo Waislamu na pia haitakuwa ya kulazimisha,” alisema.
Alisema Mahakama hiyo kwa sababu itakuwa inashughulikia masuala binafsi kama ndoa na talaka ambayo serikali haishughuliki nayo.
Alisema serikali imekuwa ikishughulika na masuala ya jinai kama vile wizi, watu wanaokula rushwa hivyo mambo binafsi kama ya talaka haishughuliki nayo.
Aliongeza kuwa kujiunga katika Mahakama ya Kadhi itakuwa ni hiari hata miongoni mwa Waislamu na gharama za uendeshaji wake serikali haitahusika.
Masaju alisema suala hilo kama wananchi wakielimishwa haliwezi kuleta mgogoro kwa kuwa ni kitu cha kawaida na linafanyika katika baadhi ya nchi.
Alisema kimsingi suala hilo linakuzwa na baadhi ya vyombo vya habari na kusisitiza kuwa Watanzania ni wamoja na watabaki kuwa wamoja.
Aliongeza kuwa watu ambao hawataki mahakama hiyo wataenda kwenye mahakama nyingine za kawaida.
“Pamoja na Mahakama ya Kadhi kuamua masuala hayo, mahakama za kawaida zitabaki kuwa na mamlaka ya kusikiliza masuala ya talaka, mirathi na ndoa,” alisema.
Alisema wakati wa Bunge Maalum la Katiba Waislamu walitaka suala hili liingizwe katika Katiba mpya, lakini serikali iliona yasiingizwe kwa sababu ni ya imani za dini na hivyo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliahidi serikali itapeleka muswada bungeni.
Akijibu swali la kwamba huenda kuwasilishwa bungeni kwa muswada huo sasa kunalenga kuvuruga Watanzania kuacha kufikiri masuala muhimu yaliyopo mbele kama uchaguzi mkuu, Masaju alisema siyo kweli.
Alifafanua kuwa masuala yote kama ya kura ya maoni kuamua Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu yote yana umuhimu na yataenda sambamba.
“Wakristo ni majirani wa Waislamu, Waislamu na Wakristo wanaishi pamoja, katika baadhi ya familia wengine kuna Waislamu na Wakristo, mwanasheria mmoja aliniuliza ni amri ipi iliyokuu kuliko yote akasema, mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, mpende jirani yako kama nafsi yako, Waislamu ni jirani zetu,” alisema.
Masaju alisema kutugwa kwa sheria hii ni kuwezesha Mahakama ya Kadhi kufanya kazi kwa kufuata utaratibu bila kuingilia mambo mengine ya serikali.
“Hii siyo mara ya kwanza kutunga sheria. Mtusaidie kama taifa, sioni sababu Watanzania kupigana na kupinga suala la Mahakama ya Kadhi na kusababisha kuvunjika kwa amani,” alisema.
Aliongeza kuwa Zanzibar wana Mahakama ya Kadhi, hivyo itakuwa jambo la kushangaza kwa nini Tanzania Bara kusiwe na mahakama hiyo hali ambayo italeta manung’uniko kwa Waislamu waliopo bara.
Alisema kwa waliosoma Chuo Kikuu cha Sheria Dar es Salaama suala la mahakama ya Kadhi hufundishwa kwa mwaka mzima ili kulielewa vizuri.
Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatumika hata Zanzibar, hivyo siyo jambo zuri bara kusiwe na Mahakama ya Kadhi kwani itawafanya Waislamu waliopo bara wasononeke.
“Tumeona Waislamu wanaona na Wakristo, hiki ni kitu cha kawaida kabisa hakuna sababu ya kulipinga, sisi wote tunategemeana, sisi ni ndugu, binadamu tunaoishi pamoja.
Suala la Mahakama ya Kadhi limekuwa likizungumzwa sana bungeni tangu Augustino. Mrema alipopeleka hoja binafsi akidai Mahakama hiyo mwaka 1998.
Tangu wakati huo mwaka 1998 - 2000 iliundwa kamati ndogo ya Bunge kulishughulikia suala hilo chini ya Mwenyekiti wa wakati huo, Arcado Ntagazwa, aliyekuwa mbunge wa Muhambwe  na baadaye liliibuliwa tena mwaka 2002 na Thomas Ngawaiya aliyekuwa mbunge wa Moshi Vijijini na likashughulikiwa na Kamati ya Katiba, Utawala na sheria chini ya Mwenyekiti wa wakati huo, Athumani Janguo akiwa mbunge wa Kisarawe.
Baadaye suala hilo lilirudishwa serikalini chini ya Tume ya Kurekebisha Sheria kati ya 2006 -2008. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mwenyekiti Profesa Ibrahimu Juma.
Viongozi wa Kikristo wamekuwa wakipinga kuwepo kwa Mahakama hiyo, huku Waislam wakiililia kwa kudai ni haki yao katika kushughulikia kesi zinazowahusu waumini wake ambao misingi yao ipo kwa muongozo wa Qur'an na Mafundisho ya Mtume Muhammad SAW.
Msimamo wa AG Masaju unaendana na ukweli kuwa yapo mataifa yenye waislam wachache lakini yana Mahakama hiyo ya Kadhi na kuwa wanachama wa OIC jambo jingine linalopingwa nchini na viongozi wa Kikristo na mambo yao yanaendelea bila ya hofu wala tatizo kama inavyoelezwa kama njia ya kukwamisha jambo hilo nchini.

Manchester United yaing'oa Cambridge Utd kwa kuinyuka 3-0

Mata finished off Di Maria's cross from six yards out to break the deadlock and put Manchester United ahead
Juan Mata akifunga bao la kuongoza la Manchester United
Wilson came off the bench to score Manchester United's third goal in the 73rd minute to finish off Cambridge United
James Wilson akifunga bao la tatu
Argentine defender Rojo doubled Manchester United's lead over Cambridge United in the 32nd minute at Old Trafford
Marcos Rojo akiiandikia Mashetani Wekundu bao la pili
Elliott and his Cambridge United team-mates react in despair after seeing his shot flick the outside of the post and go wide
Hayaaa! Tom Elliot akisikitika kwa kukosa bao la wazi
Manchester United's Argentine winger Angel di Maria tries to break down the Cambridge United defence
Angel di Maria akimtoka mchezaji wa Cambrigde United
WAKIWA kwenye kiwango bora kuliko mchezo uliopita na huku wakicheza kwa tahadhari kubwa, Manchester United wamefanikiwa kuichapa Cambridge United kwa mabao 3-0 na kutinga hatua ya Tano ya michuano ya Kombe la FA.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford, Manchester United waliolazimishwa suluhu bila kutarajiwa na timu hiyo ya Daraja la Pili katika mechi ya wiki iliyopita uwanja wa ugenini, walienda mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-0.
Kiungo Mshambuliaji Juan Mata alianza kuiandikia wenyeji bao katika dakika ya 25 akimalizia krosi pasi ya Angel di Maria kabla ya Marcos Rojo kuongeza la pili kwa kichwa akimalizia mpira uliopigwa na Robin van Persie katika dakika ya 32.
Wageni walikaribia kuwatungua Mashetani Wekundu baada ya 'kinda' Tom Elliott, kushindwa kufunga mara mbili akiwa peke yake na lango kutokana na makosa ya mabeki wa Manchester United.
Mtokea benchi James Wilson aliyempokea van Persie aliihakikisha Manchester United nafasi ya kusonga mbele kwa kufunga bao la tatu kwa mkwaju mkali wa mguu wa kushoto katika dakika ya 73 baada ya kunyezewa pasi murua na  Ander Herrera.
Kwa ushindi huo Manchester United sasa watavaana na timu ya Preston North End ambayo ilipata ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Sheffield United katika mechi nyingine ya marudiano ya michuano hiyo baada ya awali kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza. Mechi ya timu hizo itachezwa Jumatatu ya Februari 16.
Katika pambano jingine la marudiano Sunderland ikiwa ugenini ilitakata kwa kuisasambua Fulham kwa mabao 3-1 na kutinga raundi ya Tano wakikaribiana na Bradford City katika mechi itakayochezwa Jumapili ya Februari 15. Katika mechi yao ya kwanza timu hizo zilitoka 0-0.
Timu ya Bradford City ndiyo iliyoing'oa Chelsea kwenye michuano hiyo katika raundi hiyo ya nne kwa kuilaza vinara hao wa Ligi Kuu ya England mabao 4-2 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Stanford Bridge wiki iliyopita.

CAF yamfungia mwamuzi aliyewabeba wenyeji Afcon 2015

http://ww1.hdnux.com/photos/34/36/27/7464396/5/628x471.jpg
Refa Seechurn Rajindraparsad

https://s.yimg.com/bt/api/res/1.2/RFZ6duPBZw4ebZ6b797g2A--/YXBwaWQ9eW5ld3M7cT04NTt3PTYzMA--/http://media.zenfs.com/fr_FR/Sports/Eurosport/1405900-30114704-640-360.jpg
Polisi wakimlinda mwamuzi Rajindraparsad asipewe kichapo na wachezaji wa Tunisia baada ya kutoa penati tata kwa wenyeji dakika za lala salama
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemsimamisha mwamuzi Seechurn Rajindraparsad aliyevurunda pambano la Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya wenyeji Guinea ya Ikweta na Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) kutakiwa kuomba msahama kwa vurugu zilizofanywa na wachezaji wa nchi hiyo.
Mwamuzi huyo kutoka Mauritius alitoa penati ya utata dakika za lala salama za pambano hilo na kuwapa wenyeji bao la kusawazisha lililofanya mchezo huo kuongezewa muda wa dakika 30 na Guinea ya Ikweta kushinda kwa mabao 2-1 na kutinga nusu fainali.
Wachezaji wa Tunisia walionyeshwa kukerwa na maamuzi hayo kiasi cha askari Polisi kulazimika kumuokoa na kumlinda ili asidhuriwe.
Katika taarifa yake iliyotolewa juzi, CAF imetangaza kuondoa mwamuzi huyo kwa kuchezesha ovyo mechi hiyo na kusimamisha kwa muda wa miezi sita sambamba na kumuondoa kwenye orodha ya Caf ya waamuzi wa Daraja A kutokana na kikao cha Kamati ya waamuzi.
Mwamuzi huyo licha ya 'kubanyanga' mchezo huo ambao ulionekana wazi wenyeji wameondoshwa mashindanoni, huku TFT ikitakiwa kuomba radhi kwa vitendo vilivyofanywa na wachezaji wa timu yao ya taifa  siku ya mchezo huo.
TFT tayari imeshaadhibiwa kiasi cha Dola za Kimarekani 50,000 kwa utovu wa nidhamu wa wachezaji wa timu yao ya taifa na maafisa wake, ingawa CAF kupitia kamati ya Waamuzi inakiri kwamba mwamuzi wa pambano hilo alivurunda kwa kuchezesha chini ya kiwango jambo ambalo CAF haipo tayari kuona madudu kama hayo katika michuano yake.

Bayern Munich wang'ang'aniwa nyumbani Bundesliga

http://i1.eurosport.com/2015/02/03/1408140-30159502-1600-900.jpg
Thomas Mullier akipambana dhidi ya wachezaji wa Schalke 04
http://b.smimg.net/15/06/640x480/bayern-munich-arjen-robben.jpg
Mfungaji wa bao la Bayern Munich, Arjen Robbin akishangilia
MABINGWA watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich wameshindwa kutamba nyumbani baada ya kung'ang'aniwa na Schalke 04 na kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mfululizo wa ligi hiyo nchini Ujerumani.
Bayern wakiwa kwenye uwanja wao wa Allianz Arena, walijikuta wakishindwa kufurukuta mbele ya wageni wao ambao walionekana kudhamiria kuendeleza aibu kwa mabingwa hao ambao walikuwa wametoka kupokea kipigo chao cha kwanza katika ligi hiyo wakiwa ugenini dhidi ya Wolfsburg waliowachapa mabao 4-1.
Baada ya kumaliza dakika 45 za awali wakiwa nguvu sawa, wenyeji walianza kuandikisha bao la kuongoza dakika ya 67 kupitia kwa Arjen Robben akimalizia kazi nzuri ya Xabi Alonso.
Hata hivyo bao hilo lilidumu kwa dakika tano tu kwani Schalke walisawazisha kupitia kwa Benedikt Howedes na kuwafanya wenyeji waliocheza pungufu kwa muda mrefu baada ya beki wake tegemeo Jeremy Boateng kulimwa kadi nyekundu dakika ya 17 tu ya mchezao kuhaha kusaka bao la ushindi bila mafanikio.
Kwa matokeo hayo Bayern wameendelea kukalia kiti cha uongozi wa Bundesliga wakiwa na pointi 46 baada ya mechi 19 huku wapinzani wao wakipanda hadi nafasi ya nne wakiwa na pointi 31.
Katika michezo mingine ya ligi hiyo iliyochezwa juzi, Borussia Monchengladbach walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Freiburg uliowapeleka hadi nafasi ya tatu wakifikisha pointi33, huku Hannover 96 na Mainz 05 wakishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 1-1 kama ilivyokuwa katika mchezo wa timu za Eintracht Frankfurt na 'wababe' wa Bayern Munich Wolfsburg

Ivory Coast iliyokamilika kuvaana na DR Congo leo Afcon

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/8/8a/Cheick_Ismael_Tiote_9030.JPG
Cheikh Tiote
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiW4t072rDsv7i065sgWdPt51mT1c0i-lbQg5kDT8bcTMgvICAFJ60KLvXsHnqWGDAQuuaknHY-9zn2a2NQntbalajJRXyMoLk2UvQJpJ2JWD4e_ihAo2feQ84Jv6kUFeZT8wKM4xMN2T0/s1600/IMG_9994.JPG
Kikosi cha Ivory Coast kitakachokabuiliana na DR Congo leo kwenye nusu fainali ya kwanza ya AFCON 2015
TIMU ya taifa ya Ivory Coast imemkaribisha kwa mikono miwili katika mazoezi ya timu hiyo mchezaji wake Cheick Tiote kabla timu hiyo leo haijashuka dimbani kucheza  mchezo wao wa nusu fainali wa Mataifa ya Afrika.
Ivory Cioast baada ya kuitoa  Tunisia katika hatua ya robo fainali, inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa mashindano hayo makubwa kwa nchi barani Afrika.
Cheick Tiote huenda leo Jumatano akawemo katika kikosi cha Ivory Coast cha nusu fainali dhidi ya Jamhuri ya Watu wa Kongo.
Kiungo huyo mahiri wa Newcastle United hajapangwa katika kikosi cha kocha wake Herve Renard  tangu alipoichezea timu hiyo kwa mara ya mwisho wakati ilipocheza na Mali katika mchezo wa  Januari 24 kutokaana na maumivu ya kifundo cha mguu.
Hatahivyo, kocha wa timu hiyo Renard ana matumaini makubwa kuwa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, atarejea uwanjani na wanafuzu kwa fainali zao za sita ndani ya miaka sita katika mashindano hayo.
"Tiote alianza mazoezi mepesi na yumo katika orodha ya kikosi cha leo Jumatano kitakachoshuka dimbani.
"Kwa kweli ni vigumu kwake kuanza mchezo huo, lakini yumo katika kikosi hicho.
Ivory Coast wanaangalia kutwaa taji lao la kwanza la AFCON tangu mwaka 1992 huko Equatorial Guinea, huku kocha Renard akiwa na matumaini kibao ya kujaribu bahati ya kulitwaa taji hilo tena baada ya kufanikiwa kufanya hivyo alipokuwa akiifundisha Zanzibar mwaka 2012.
Kesho Alhamisi kutakuwa na nusu fainali ya pili itakayozikutanisha Ghana na wenyeji Equatorial Guinea ambao watakuwa wakicheza mbele ya wapenzi wao.