STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 9, 2016

Real Madrid yawinda rekodi mpya kwa Pogba

http://static.independent.co.uk/s3fs-public/thumbnails/image/2015/08/25/20/pg-64-pogba-1-getty.jpg
Paul Pogba anayeingia rada za Real Madrid
MWENDO wa noti tu. Klabu ya Real Madrid ipo tayari kumwaga mkwanja wa nguvu ili kuipiku Manchester United inayotaka kumrejesha kikosini, Paul Pogba anayekipiga Juventus.
Klabu hiyo imedaiwa ipo tayari kutoa Pauni Milioni 94 ili kunasa saini ya Pobga anayewindwa na klabu yake ya zamani Man United walio tayari kuvunja benki na kumwaga Pauni Milioni 78.
Kwa mujibu wa gazeti maarufu la michezo la Gazzetta dello Sport la Italia limesema kuwa, Real Madrid imepania kumnasa kiungo huyo fundi kutoka Ufaransa, licha ya kwamba katika mbio hizo pia Matajiri wa Manchester City wapinzani wakuu wa Man United nao wanammendea kimyakimya.
Iwapo Rela itafanikiwa kumnasa Pogba kwa kiwango hicho cha fedha itakuwa imevunja rekodi inayoshikilia kwa sasa ya kumnasa Gareth Bale misimu mizili iliyopita ilipomwaga kiasi cha Pauni Milioni 80.
Gazeti hilo limefichua kuwa, Mkurugenzi wa Juventus Giuseppe 'Beppe' Marotta wiki ijayo anatarajiwa kutua Hisapnia kwa ajili ya mazungumzo ya uhamisho wa Alvaro Morata, lakini pia suala la Pobga litagusiwa.
Mashetani Wekundu pia walikuwa wakimnyatia Moratta, lakini inaonekana wazi Jose Mourinho atachemsha mbele ya mabosi wake wa zamani Real Madrid.

http://img.kiosko.net/2016/06/09/it/gazzetta_sport.750.jpg
gazeti lililodokeza mipango ya Real kutaka kuvunja rekodi ya kumnyakua Pogba

Rodriguez azigonganisha Manchester City, United

https://metrouk2.files.wordpress.com/2014/06/875x10001.jpg
James Rodriguez

KLABU ya Manchester City imeingia kwenye vita dhidi ya mahasimu wake, Manchester United katika mbio za kumwania nyota wa Real Madrid, James Rodriguez.
Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia amekuwa akiwindwa pia na mabingwa wa Ufaransa, PSG, lakini duru la kispoti zinadokeza kuwa, Rodriguez ambaye kusalia kwake Santiago Bernabeu ni majaliwa anawindwa na mabingwa hao wa zamani wa England.

City chini ya kocha mpya, Pep Guardiola imevutiwa na Mfungaji Bora huyo wa Kombe la Dunia 2014 na kwamba wapo tayari kumwaga kitita ili kumnyakua.
Klabu za PSG na Bayern Munich iliyo chini ya Kocha mpya, Carlo Ancelotti aliyewahi kumnoa Rodriguez wakati akikinoa kikosi cha Blancos, nao wanatajwa kumnyemelea mkali huyo ambaye amekuwa hana raha Real Madrid kutokana na kuishia benchini.
Rodriguez ambaye ni nahodha wa Colombia kwa sasa yupo kwenye vita ya kuisaidia timu yake kufanya vema katika michuano ya Copa America 2016 inayochezwa Marekani.

Paul Pogba awaota kina Pele, Diego Euro 2016 watamkoma!

http://bolavip.cdnfsn.com/img/rankings/x/n1406834042.jpg
Paul Pogba
MBONA mtamkoma. Kiungo nyota wa Juventus aliyewahi kukipiga kwa Mashetani Wekundu, Manchester United, Paul Pogba amefunguka kwa kudai kuwa anataka akumbukwe kwa soka lake kama ilivyokuwa kwa kina Diego Maradona wa Argentina na Pele wa Brazil.
Pogba ambaye atakuwa na jukumu la kuisaidia nchi yake kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya (Uefa Euro 2016) inayofanyika kwao Ufaransa, alisema kuwa,  amepania kufikia malengo yake hayo kwa kujituma na kuhakikisha kila siku anaimarika.
Kiungo huyo aliyeiwezesha Juventus kunyakua mataji manne ya Ligi Kuu ya Serie A na kucheza fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana, amekuwa akizidi kuimarika na kuwa mmoja ya nyota wanaomezewa mate kwa ubora wake wa soka.
Pogba aliondoka United kuelekea kwa Kibibi Kizee cha Turin mwaka 2012 na akihojiwa na runinga ya ESPN, Pogba alisema  kwasasa hadhani kama ameshafanya lolote la maana katika soka kwa vile bado kuna mataji mengi hajawahi kushinda ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia na hata Euro.
Hivyo amesema kuwa atapambana kiume katika ushiriki wake wa soka ili kuona anafika kule ambako kina Diego na Pele walifikia kiasi cha kubaki kuwa gumzo licha ya kustaafu kitambo na kuibuka kwa nyota mbalimbali duniani kwa sasa.

Adidas yaiomba radhi Colombia kwa kuchapia tangazo

Tangazo lililozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii hasa twitter ambapo Adidas ilishambuliwa kabla ya kuliondoa na kuomba radhi
WAUNGWANA. Kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas imeonyesha uungwana kwa kuomba radhi kwa kosa la kuliandika vibaya jina la Colombia katika matangazo yake yanayohusu jezi mpya wanazotumia timu ya taifa ya nchi hiyo katika michuano ya Copa America 2016.
Tangazo hilo ambalo linawaonyesha wachezaji wa Colombia wakiwa katika jezi nyeupe liliondolewa baada ya mitandao ya kijamii kushambulia kwa kwa kuliandika vibaya jina la nchi hiyo ambapo badala ya kuandika Colombia waliandika Columbia.
Katika taarifa yake kampuni hiyo yenye makao yake makuu huko Portland, Oregon imedai kuwa wanathamini ushirikiano wao na Shirikisho la Soka la Colombia na kuwaomba radhi kwa makosa hay
o yaliyofanyika. Kampuni hiyo imekuwa ikitengeneza sare za Colombia tangu mwaka 2011.

Neymar Jr matatani kwa udanganyifu, kuburuzwa kortini


MSAMBWENI. Straika nyota wa Brazili anayeichezea klabu ya Barcelona, Neymar Jr, ameingia matatani baada ya Waendesha Mashitaka nchini Hispania kutaka ashitakiwe kwa kosa la udanganyifu.
Waendesha Mashitaka hao kutoka Mahakama ya Juu ya Makosa ya Jinai Hispania, wanamtuhumu Neymar na baba yake kuficha ukweli wa thamani halisi ya uhamisho wake kutoka Santos kwenda Barcelona.
Barcelona ilitangaza kumnunua Neymar kwa kitita cha Euro Milioni 57 mwaka 2013, huku wazazi wake, Neymar da Silva Santos na Nadine Goncalves sa Silva Santos wakivuta mkwanja wa haja wa Euro Milioni 40 na klabu yake ya zamani Santos wakipata Euro Milioni 17.
Lakini waendesha mashtaka hao wamesema ada ya uhamisho ya nyota huyo ilifikia kitita cha Euro Milioni 83, ingawa pande zote mbili zimekanusha kufanya jambo lolote baya kwenye uhamisho huo.

Tattoo zamponza msela, apasuliwa mara 25 kuzifuta usoni

Akianza matibabu
zilipokuwa zikiondolewa kwa operesheni maalum
Picha tofauti kuelekea kuziondoa tattoo zake usoni
http://www.smh.com.au/content/dam/images/1/m/u/g/a/image.related.articleLeadwide.620x349.1mug6.png/1320183665650.jpg
Alivyo sasa bila Tattoo
AMA kweli ujanja mwingi mbele kiza. Hebu soma kisanga kilichompata huyu jamaa ambaye alikuwa kinara wa kundi moja la wakora nchini Ujerumani.
Msela huyo kwa kutaka kujifanya anaenda na wakati alijichora tattoo kadhaa mwilini mwake, lakini mwishoni wa yote amejikuta akipata maumivu na kutoboka kiasi kikubwa cha fedha baada ya kufanyiwa upasuaji mara 25 ili kuzifuta tattoo hizo za usoni.
Inaelezwa jamaa huyo, Bryon Widner alitumia kiasi cha Pauni 20, 233 ambazo ni kama Shs. 63.9 Milioni, huku akisimulia namna alivyopata maumivu makali kwa ajili ya kusafisha uso wake kuondoa tattoo hizo.
Widner alisema kuwa, alipitia maumivu makali sana ili kusafisha sura yake na kuzitoa tattoo hizo na alitumia muda wa miezi 16 katika operesheni hizo 25 ili kuweka sawa sura yake.
Upasuaji huo wa kuondoa tattoo hizo za usoni kati ya tattoo kibao alizojichora mkora huyo ulifanywa na Dk Bruce Shack wa Vanderbilt University Medical Center kilichopo mjini Nashville.
Kitu cha kufutia ni kwamba licha ya kadhia zote hizo, kwa sasa Widner amesafishika sura yake akiwa hana kovu lolote usoni, jambo linalompa faraja.

Wednesday, June 8, 2016

Man City kumekucha! Yaingia vita ya kumwania Aubameyang

https://i.guim.co.uk/img/media/aa83556e4ff4a53c273d8fc73c14e1e6bd7105d7/0_80_3000_1800/master/3000.jpg?w=620&q=85&auto=format&sharp=10&s=53bd60055f2d7d1fab6d5d30c9526dd8KLABU ya Manchester City inadaiwa ipo mbioni kuingia kwenye orodha ya timu zinazomwania straika wa Borussia Dortmund ma Mchezaji Bora wa Afrika 2015, Pierre-Emerick Aubameyang.
City wana matumaini ya kumsana nyota huyo wa kimataifa wa Gabon mwenye umri wa miaka 26 katika kipindi hiki cha kiangazi. Aubameyang anatajwa kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora Ulaya baada ya kuonyesha kiwango kikubwa Dortmund akifunga mabao 39 katika mashindano yote msimu uliopita.
Meneja mpya wa klabu hiyo, Pep Guardiola anafahamu vyema kipaji cha Aubameyang na ameona kuwa anaweza kumfaa katika mipango yake ya baadae. City wanadaiwa kuwa tayari kumsaidia Guardiola katika usajili kwa kujiandaa kuvunja rekodi ya usajili kwa kumleta nyota huyo Etihad.

Leseni za klabu zimeanza kutolewa na TFF, mshindwe ninyi

http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/04/Rais-wa-Shirikisho-la-Mpira-wa-Miguu-Jamal-Malinzi-akioneshwa-kukerwa-na-waamuzi-kuuza-mechi.jpg
Rais wa TFF, Malinzi
NA ALFRED LUCAS
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza kutoa fomu za Leseni za Klabu (Club Licensing) za Ligi ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na zile za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.
Klabu hizo zitatumiwa fomu hizo na kutakiwa kuzijaza na kuzirejesha kabla ya Juni 19, mwaka huu ikiwa ni siku 10 mara baada ya Bodi ya Ligi ya TFF (TPLB) kuwatuamia fomu hizo. Klabu itakayojaza fomu hizo kwa wakati ndiyo ambayo maombi yake ya leseni yatashughulikiwa mapema.
Tayari TFF imeteua Kamati ya Leseni ya Klabu (Club Licensing Committee) ambayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi ya leseni kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza na kutoa uamuzi wa kuzikubali au kuzikataa kwa kuzingatia Kanuni ya Leseni ya Klabu.
Wajumbe walioteuliwa kwenye Kamati hiyo inayoundwa kwa mara ya kwanza ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), David Kivembele, Hamisi Kissiwa na Prof. Mshindo Msolla.
Klabu zinatakiwa kuchukua fomu za maombi TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa kazi ambapo zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya Kanuni husika zitapatiwa leseni husika ili zishiriki michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016/2017.
Kwa klabu ambazo zitashindwa kukidhi matakwa ya leseni yanayolenga kuhakikisha mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangaji matokeo katika maeneo matano ya wachezaji (sporting), viwanja (infrastructure), utawala (administrative and personnel), umiliki wa klabu (ownership) na fedha (financial), hazitapa leseni hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki ligi.Klabu ambazo zitanyimwa leseni na kutoridhika na uamuzi huo, zitakuwa na fursa ya kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF. Kwa mujibu wa Ibara ya 5(3) ya Kanuni ya Leseni ya Klabu ya TFF, Kamati hiyo ndiyo itakayosikiliza rufani zinazopinga uamuzi wa Kamati ya Leseni ya TFF.

Serengeti Boys kambini kuisubiri Shelisheli

http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/2016/03/21/serengeti%20boys.jpg?itok=F-SUOdMWNA ALFRED LUCAS
TIMU ya soka ya taifa ya vijana U17 'Serengeti Boys' inataingia kambini Juni 13, 2016 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika Serengeti Boys ilicheza mfululizo michezo saba  ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
Haishangazi nchi nyingi za Ulaya, Asia na Marekani zimeulizia uwezekano wa timu hii kutembelea nchi zao kwa michezo ya kirafiki.
Awali timu ya Serengeti Boys ilipewa nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya rekodi zilizokuwa zinaiweka Tanzania katika viwango vya chini katika umri huo kwa nchi za Afrika Magharibi na Kaskazini zilikuwa juu zaidi na vilevile ukweli wa kwamba timu kama USA, Korea, Malasyia na India zilikuwa na bajeti kubwa iliyogharamiwa na Serikali zao na walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi cha kuomba magari kwa ajili ya vifaa vya mazoezi na mechi.
Serengeti Boys ilimaliza Mashindano ya AIFF katika nafasi ya tatu kwa kuifunga Malaysia mabao 3-0. Serengeti Boys na Bingwa Korea hawakupoteza mchezo hata mmoja na awali walipokutana walitoka sare ya 2-2.

Rais Obama ayakosa mazishi ya Muhammad Ali

http://cdn-mf1.heartyhosting.com/sites/mensfitness.com/files/styles/photo_gallery_full/public/ali_rotator.jpg?itok=CnLNStFo
Muhammad Ali enzi za uhai wake
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/06/382dab0f0ef23504d829de029e0e543f-702x336.jpgMWILI wa bingwa mara wa tatu wa Dunia kwa uzito wa juu, Muhammad Ali unatarajiwa kuzikwa keshokutwa Ijumaa, lakini cha kusikitisha ni kwamba hatazikwa na Rais wa Marekani, Barack Obama.
Muingiliano wa mazishi hao wa shujaa huyo na mwanaharakati wa kuwatetea watu weusi kupitia ngumi, kiasi kwamba leo Marekani inaongozwa na Rais mwenye asili ya Afrika na yale ya mahafali za binti wa Obama ndio sababu ya Obama kukosa mazishi hao.
Viongozi kadhaa kutoka sehemu mbalimbali duniani watakuwa miongoni mwa maelfu ya waombolezaji watakaohudhuria mazishi hayo huko Louisville, Kentucky ambako Ali alizaliwa mwaka 1942.
Ikulu ya Marekani imesema kuwa Obama na mkewe Michelle wanatarajiwa kuwa katika mahafali ya binti yao Malia huko Washington, DC.
Ali alifariki dunia wiki iliyopita hospitalini huko Phoenix, Arizona akiwa na umri wa miaka 74.
Hata hivyo familia ya Obama inatarajia kutuma barua kwa familia ya Ali ambayo itawasilishwa na mshauri mwandamizi wa Ikulu Valerie Jarrett ambaye anamfahamu Ali.
Msemaji wa familia ya Ali, Bob Gunnell amesema Obama alizungumza na mjane wa Ali, Lonnie katika simu kumpa pole kwa kifo hicho cha mumewe. Miongoni mwa viongozi watakaohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Mfalme Abdullah wa Jordan.

Jose Mourinho aanza mambo Man United

http://static.independent.co.uk/s3fs-public/styles/article_large/public/thumbnails/image/2016/06/08/13/eric-bailly-2.jpg
Eric Bailly
MBONA mtamkoma. Kocha Mkuu wa Manchester United, Jose Mourinho ameanza makeke yake baada ya klabu yake kumnasa beki wa Villarreal, Eric Bailly.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na United kwa ada ya Pauni Milioni 30 na kupewa mkataba wa miaka minne.
Akihojiwa Bailly amesema ndoto zake zimetimia za kujiunga na United na kucheza soka katika kiwango cha juu kama siku zote alivyotaka iwe.
Kocha Mourinho amesema Bailly ana nafasi kubwa ya kuja kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani.
Bailly alijiunga na Villarreal kwa kitita cha Pauni Milioni 4.4 Januari mwaka 2015 na kucheza katika kila mechi wakati Ivory Coast ikishinda taji la Mataifa ya Afrika wiki chache baadae.
Huo unakuwa usajili wa kwanza wa Mourinho toka atue Old Trafford huku pia wakitajwa kumwania pia mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic.

Malinzi amlilia Stephen Keshi aliyefariki leo

http://stargist.com/wp-content/uploads/2014/05/Stephen-Keshi-Stargist.jpg
Keshi enzi za uhai wake
NAHODHA na Kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi amefariki dunia ghafla leo Jumatano na kuleta mshtuko mkubwa kwa mashabiki wa soka nchini humo na kwingineko Afrika.
Nchini Tanzania  Rais wa Shirikisho la Soka(TFF), Jamal Malinzi naye ni miongoni mwa walioshtushwa na kifo hicho na kuweka bayana alivyopokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo0 wa Keshi (54) na kutuma salamu zake za pole. Rais Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Soka Nigeria (NFF), Amaju Pinnick, familia ya marehemu Keshi pamoja na ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata kuwa nahodha wa kikosi cha Taifa Nigeria ‘Super Eagles’.
Katika rambirambi ambazo zimefika pia katika Ofisi za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Rais Malinzi amesema kuwa japo Keshi ametangulia mbele za haki, mchango wake kwenye soka hautasahaulika kwani atabaki kuwa alama ya maendeleo ya mchezo wa soka.

Benteke ambeep Klopp, atasepa kama atamzingua

http://i3.mirror.co.uk/incoming/article6908832.ece/ALTERNATES/s615b/Liverpool-vs-Bordeaux-Europa-League-Group-Stage.jpg
Benteke
ANAONDOKA. Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ubelgiji, Christian Benteke amesema anataka kubakia Liverpool, lakini amekiri anaweza kuangalia mahali pengine kama hatakuwepo katika mipango ijayo ya Kocha Jurgen Klopp.
Strika huyo aliyepo na kikosi chao kwenye fainali za Kombe la Ulaya Euro 2016, alijiunga na Liverpool akitokea Aston Villa kwa kitita cha Pauni Milioni 32.5 kiangazi mwaka jana.
Mkataba wake ulikuwa wa miaka mitano lakini amekuwa akishindwa kuonyesha cheche zake Anfield tangu Kocha Klopp alipomrithi Branden Rodgers.
Nyota huyo bado anapenda kuendelea kubakia hapo, lakini kama atakuwa nje ya mipango ya Klopp anaweza kuangalia mahali pengine atakapoweza kupata nafasi ya kucheza.
Akihojiwa Benteke amesema akiwa na umri wa miaka 25 sasa sio kwamba ni mkubwa sana au mdogo lakini muhimu ni kupata muda mwingi wa kucheza.

Didier Kavumbagu anukia Mbeya City

Didier Kavumbagu (kulia) akiwa na nyota wenzake wa Azam FC
NYOTA wa timu ya Taifa ya Burundi ‘Intamba Mu rugamba’ Didier Kavumbagu anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kutangazwa kujiunga na kikosi cha Mbeya City Fc ya jijini Mbeya kinachoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara muda wowote kuanzia sasa.
Katibu Mkuu wa City, Emmanuel Kimbe, mchana huu ameidokeza mtandao wa mbeyacityfc.com kuwa mazungumzo ya kumnasa nyota huyo wa timu ya taifa ya Burundi aliyekuwa akicheza kwenye kikosi cha Azam Fc ya jijini Dar es Salaam msimu uliomalizika yako kwenye hatua nzuri na tayari wakala wa mchezaji huyo amekwishaainisha yale yote muhimu yanayohitaji kwa ajili ya kuipata huduma yake likiwemo suala la kipengele cha kumruhusu kwenda kufanya majaribio nje ya nchi endapo yatapatikana.
“Tulianza mchakato wa kumpata Kavumbagu mapema kabisa, baada ya kukwama kwenye dirisha dogo Januari mwaka huu, tulikubaliana kuwa hitimisho litakuwa kwenye majira haya ya kiangazi, tayari nimezungumza na wakala wake, tuko kwenye hatua za mwisho kwa sababu ameshaanishia yale yote yanayohitajika, kwa maana hiyo basi, endepo tutamalizia vizuri hatua iliyobaki, muda wowote kuanzia sasa tunaweza kumtangaza kama mchezaji wetu," alisema Kimbe.
Akiendelea zaidi Kimbe alisema kuwa, Kavumbagu ni moja ya nyota walio kwenye orodha ya kocha Kinnah Phiri aliyoomba wasajiliwe ili kuiimarisha timu kwenye eneo la ushambuliaji akilenga kuwa wachezaji wenye uwezo wa kufunga kufuatia tatizo la umaliziaji lililoikuba City  kwenye michezo kadhaa ya mzunguko wa pili wa ligi  licha ya kucheza vizuri kwenye maeneo mengine.
“Tunayo majina  kadhaa ambayo kocha wetu ameomba wasajiliwe kulingana na mahitaji aliyonayo, Kavumbagu anaweza kuwa  wa kwanza kati yao,wengine watafuata kwa mujibu wa taratibu zetu, tunataka kufanya usajili makini ili kuimarisha timu na hatimaye tuwe na kikosi kitakachotupatia matokeo mazuri msimu ujao  hii ni baada ya mapito msimu uliopita”.
Kavumbagu  alianza kuichezea timu ya taifa ya Burundi mwaka 2009 na alikuwa mmoja wa nyota waliokiwakilisha kikosi hicho  kwenye michezo ya kutafuta kufuzu Kombe la Mataifa Afrika 2012 na kufunga mabao 2.
Kwa upande  mwingine   Kimbe  amedokeza kuhusu nyota ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha City msimu ujao, na kusema kuwa  ni vizuri kuendelea kusubiri  kwa sababu muda si mrefu  taarifa  juu ya hilo itatolewa.

Simba kweli imepania yasajili nyota wapya kimyakimya

Wachezaji wa Simba wakishanglia moja ya mabao yao katika ligi iliyoisha hivi karibuni
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgIabpUQ1LhhV7WT0QDrMFTU3RkBUGjZcb9Vzjfhh_C9h79PB8OF127G0bCOqwCFY_EuUeS78PmeexLHfJ4mkxmuUUdFOynFb0SGf62Nh03pY0fyVpwyoksIU9nPXaSzZzdtkrBZOR1EHE/s1600/_FDA0288.JPG
Rais wa Simba, Evans Aveva na Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zakari Hanspoppe
KLABU ya Simba wajanja kwelikweli. Baada ya viongozi wa klabu hiyo kubaini kuwa, wanachama wao wana hasira kwa sababu timu yao haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara tangu mwaka 2011-2012, wameamua kufanya yao.
Wakienda na mwendo wa kimya kimya, viongozi hao wamefanya usajili kamambe bila makeke, kitu ambacho wapinzani wao Yanga na Azam ni lazima wakae chonjo kwa ligi ya msimu ujao.
Viongozi wa Simba ambao wanadaiwa wapo mbioni kuleta vifaa vya kimataifa kutoka Zimbabwe na Malawi, wamewanyakua nyota kadhaa wa klabu mbalimbali za Ligi Kuu Bara wakiwamo kutoka Mtibwa Sugar na Mwadui FC.
Wachezaji hao wameshasaini na kupewa mikataba yao, licha ya kwamba zile mbwembwe ambazo zimezoeleka kipindi kama hiki kwa klabu hiyo katika usajili zimewekwa kando ili kuhakikisha wachezaji wanaowataka wanawatia mkononi.
Micharazo inayo majina ya wachezaji wanne wapya waliosainiwa Msimbazi akiwamo kiungo mmoja fundi, ambaye katika ligi iliyomalizika alifanya yake akiifungia mara kadhaa Mtibwa mabao muhimu.

Kazi hiyo inafanywa kwa ushirikiano mkubwa baina ya matajiri wa Simba na Kamati ya usajili ya klabu hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Zakaria Hanspoppe kwa mapendekezo ya kocha Jackson Mayanja na Benchi lake la Ufundi.
Mkali mwingine ni kiberenge kilichowahi kutamba Azam Fc, huku beki aliyekuwa akiwindwa na timu hiyo kutoka Mwadui, Idd Mobby ikielezwa amepotezewa, kwa sababu analetwa fundi mmoja toka Malawi atakayechukua nafasi ya Juuko Murshid.

Friday, June 3, 2016

Kweli imebaki Stori kwa Rich Mavoko (Official Video )

Ngeleja wenzake wapewa kifyagio na Malinzi

http://www.theworldfolio.com/img_db/timthumb.php?src=img_db/old/13226688671.jpg&w=800&z=1
Mhe. Ngeleja
http://www.thecitizen.co.tz/image/view/-/2841132/medRes/1098071/-/un1399/-/Jamal+Malinzi.jpg
Malinzi
MAJUZI Wabunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, walichagua uongozi mpya wa timu yao ya Bunge Sports Club na kama zali, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja akaukwaa Uenyekiti kilaini bila kupingwa, jambo hilo limemvutia sana Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi.
Rais huyo wa TFF amepongeza uongozi wa timu hiyo uliochaguliwa mjini Dodoma, ambapo Ngeleja alitwaa kiti akimrithi Idd Azan ambaye alishindwa kurudi bungeni katika Uchaguzi Mkuu wa Taifa wa 2015.
Mbali na Ngeleja, wengine waliopewa kifyagio hicho na Malinzi ni Makamu Mwenyekiti, Esther Matiko; Meneja wa Klabu, John Kadutu pamoja Wajumbe Neema Mgaya, Faida Bakari,  Cosato Chumi, Anna Lupembe na Grace Kihwelu.Malinzi amewatakia kila la kheri Bunge Sports Club na kuwaahidi ushirikiano kutoka TFF katika kuendeleza klabu yao na michezo kwa ujumla nchini.

Kwa Buku 5 tu inaiona Stars, VIP nako bwerere Taifa

MSHINDWE wenyewe. Viingilio vya kuliona pambano la kuwania kwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mafarao wa Misri zimewekwa hadharani.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio hivyo, ambapo kile cha bei ya chini kabisa ni buku tano tu. (Sh 5,000) wakati cha juu kikiwa ni Sh. 10,000. Mnataka nini tena?!
TFF ni kama kimesikia kilio cha mashabiki wa soka, kwa kutangaza viingilio hivyo katika mchezo huo wa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mwanangu toroka uje kwa sababu tiketi zimeanza kuuzwa mitaa mbalimbali ya jiji hilo.
TFF imesema watakaolipa Buku 5 watakaa mzunguko wa viti vya rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu, wakati wanene wanaotaka kukaa kibosibosi yaani VIP B na C wenyewe watatoboka kiduchu kwa Mwekundu mmoja (Sh. 10,000).
Sasa unajua tiketi zenyewe zinapatikana wapi, wala usikonde ukienda Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam utapata, pale  Ukumbi wa Burudani Mbagala Dar Live, Vituo cha mafuta cha Oilcom - Ubungo na Buguruni (Buguruni Shell) na Ofisi za Ukumbi wa burudani Bilicanas, nako utapata.
Halafu hata kesho Jumamosi Juni 4, 2016 tiketi zitauzwa kwenye vituo hivyo na vingine vya Mwenge, Mnazi Mmoja, Makumbusho, Chang’ombe na Mgahawa wa Brake Point ulioko mkabala makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Unangoja nini mwanangu, changamka bhana!

Maskini Muhammad Ali! Alazwa tena hospitalini

https://i.ytimg.com/vi/C_fEIVwjrew/maxresdefault.jpg
Muhammad Ali katika moja ya mapambano yake akimuadhibu mpinzani wake aliyelala sakafuni.
UNAMKUMBUKA Bingwa wa Dunia wa Masumbwi uzani wa juu wa zamani Muhammad Ali? Ni hivi. Jamaa huyo aliyewatetemesha mabondia wenzake amelazwa hospitalini kufuatia maambikizi ya mapafu.
Bondia huyo nyota mwenye umri wa miaka 74 aliyekonga nyoyo za wapenzi wa ndondi kote duniani anasemekana kuwa katika hali wastani alipolazwa hospitalini.
Hata hivyo familia yake ilipendekeza alazwe hospitali kama tahadhari kwa sababu mbali na maambukizi hayo Ali anaugua kiharusi.
Bondia huyo alipatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984 baada ya kustaafu mchezo huo wa ngumi za kulipwa.
Mara ya mwisho bondia huyo mkongwe alipolazwa hospitalini ilikuwa ni Januari mwaka uliopita baada ya kupatwa maambukizi ya njia ya mkojo.
Msemaji wa familia yake hata hivyo hakuwaambia wanahabari alikolazwa wala alilazwa lini.
Chanzo: BBC Swahili

Mkwasa aahidi raha Taifa, tunasubiri nini twendeni uwanjani

Kocha wa Stars, Boniface Mkwasa

TWENDENI Taifa kesho Jumamosi, kwani Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa 'Master' ameahidi kuifanyizia Mafarao wa Misri katika pambano lao la kuwania Afcon 2017.
Stars kesho inashuka dimbani kucheza na Misri ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 3-0 iliyopata kwenye mchezo wa awali uliochezwa mji wa Alexandria, katika ufunguzi wa mechi za Kundi G.
Stars  inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufuzu AFCON ya mwakani wakati Misri wao sare itawafanya wafikishe pointi nane ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine kwenye kundi lao.
Endapo Tanzania itashinda mchezo huo itafikisha pointi nne kwani hadi sasa ina pointi moja baada ya sare ya 0-0 na Nigeria nyumbani huku ikibakisha mchezo wa marudiano na Nigeria ugenini baadaye Septemba mwaka huu..
Kundi hili baada ya kujitoa kwa Chad limebaki na timu tatu ambazo ni Misri wenye pointi saba, Nigeria pointi nne na Tanzania yenye inashika mkia ikiwa na  pointi moja lakini Misri na Nigeria zimebakiza mchezo mmoja mmoja, wakati Tanzania ina faida ya mechi mbilim huu wa leo na mwingine ni dhidi ya Nigeria utakaochezwa Septemba.
Akizungumza na Wanahabari Kocha Mkwasa alisema mchezo wa keshoni  mgumu kwani ni sawa na fainali hivyo wanahitaji kushinda ili kujiweka pazuri kwani Misri wanakuja wakihitaji sare.
“Wachezaji wako vizuri, wako kwenye morali nzuri na tumefanya mazoezi na wachezaji wote 26 na mimi nimefanya marekebisho kwa makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo dhidi ya Kenya na kinachosubiriwa ni dakika 90 tu”, alisema Mkwasa.
Pia Mkwasa alisema anatambua Misri ni timu nzuri kwani waliifunga Tanzania mabao 3-0 kwao na anajua wanakuja kucheza mfumo wa kujilinda kuliko kushambulia kama ilivyo desturi kwa timu za kiarabu lakini wao wamejiandaa kushambulia.
“Tuna deni kubwa kwa watanzania hivyo tunajua tunatakiwa kupata matokeo mazuri ili kuwapa faraja na kufufua matumaini ya kwenda AFCON hivyo tutashambulia sana”, alisema Mkwasa
Mkwasa aliwashukia watu wanaojiita wachambuzi wa soka akisema wamekuwa wakiwavunja moyo wachezaji na kuwataka waangalie namna wanavyofanya uchambuzi kwani wanawakatisha tamaa wachezaji na kuwaasa uchambuzi mzuri ni ule ambao unafanywa baada ya mchezo.

Manji amkimbiza Alloyce Komba Kamati ya Uchaguzi ya TFF

Alloyce Komba

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi  ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Aloyce Komba, amejiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi wa klabu Yanga uliopangwa kufanyika Juni 25 , mwaka huu.
Hatua hii imekuja baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kumtuhumu kumhujumu hivyo anakaa pembeni kupisha uchunguzi
Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa, Komba alisema Manji anasema nahusika kupanga mikakati ya kupewa rushwa ili akate  jina lake na tuhuma hizi kwake ni nzito ukizingatia taaluma yake ya sheria.
“Manji ananituhumu mimi kupanga mikakati ya kupewa rushwa ili nikate jina lake, tuhuma hizi kwangu ni nzito ukizingatia taaluma yangu ya sheria, sitaki kuwa chanzo cha mgogoro Yanga”, alisema Komba
Pia Komba alisema wanasheria nguli Said El Maamry, Alex Mgongolwa,  Mapande na baadhi ya wabunge ni watu anaowaheshimu na wamemshauri juu ya suala hili hivyo kwa busara ameamua kukaa pembeni uchaguzi ufanyike.
 “Sauti zinazosemwa sizitambui, sizijui, halafu najiuliza  wanapanga kwa manufaa ya nani? Kwanini Manji katishika kuchukua fomu TFF wakati ameonyesha uwezo mkubwa wa kuongoza Yanga?”, alihoji Komba.
Komba alisema alitegemea Manji angemrahisishia kazi lakini matokeo yake anachafuka kwa vitu ambavyo si vya kweli.
Mchakato wa uchaguzi TFF unaendelea chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili Domina Mideli, ingawa uongozi wa Yanga nao unaendesha zoezi lao makao makuu kabla ya kufanya uchaguzi wao Juni 11.

UEFA Euro Cup 2016 itakuwa tamu si mchezo


http://www.uefa.com/MultimediaFiles/Photo/competitions/General/02/35/95/19/2359519_w2.jpg 
http://i4.irishmirror.ie/incoming/article7002411.ece/ALTERNATES/s1200/Screen-Shot-2015-12-12-at-185759.png 
http://e2.365dm.com/16/05/768x432/marcus-rashford-england_3476376.jpg?20160531141444
Rashford
http://talksport.com/sites/default/files/tscouk_old_image/cristiano-ronaldo_2.jpg
Ronaldo atafanya nini safari hii huko Ufaransa

MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 'UEFA Euro 2016' itaanza wiki ijayo nchini Ufaransa kwa kushuhudiwa nyota wa nchi mbalimbali barani humo wakionyeshana kazi mpaka Julai 10 atakapopatikana bingwa wake.
Hispania ndio watetezi wa taji hilo ikilishikilia kwa mihula miwili mfululizo tangu mwaka 2008 na kutetea mwaka 2012.
Michuano hiyo itafanyika huku kukiwa na rekodi kadhaa ambazo zinahitajiwa kuvunjwa ikiwamo ya mchezaji alitefunga mabao mengi katika fainali moja, iliyowekwa na aliyekuwa nyota wa Ufaransa, Michel Platini mwaka 1984.
Katika michuano hiyo Platini aliyekuwa Rais wa Uefa kabla ya kufungiwa na FIFA kwa tuhuma za kifisadi, alifunga mabao 9, huku pia akitupia hat-trick mbili ikiwa ni rekodi tena zilizofululiza, mbali na bao la mapema la michuano la dakika 18.

Unajua kuwa ni nchi mbili tu za Ujerumani na Hispania ndizo zilizotwaa mara nyingi, zikifanya hivyo mara tatu kila moja, hivyo ni wakati wao wa kuzidiana ujanja au kuzubaa na kukutwa na Ufaransa inayowafukizia ikitwaa mara mbili tangu michuano ilipoasisiwa mwaka 1960.
Pia michuano hiyo ilimpa ujiko Cristiano Ronaldo mwaka 2004 alipokuwa mchezaji mwenye umri mdogo kucheza fainali akifanya hivyo mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 19 na siku 150.
Kwa kifupi kina Marcus Rashford na makinda wenzake wanapaswa kufanya mambo ili kufikia rekodi mbalimbali ambazo zimedumu kwa miaka mingi bila kuvunjwa.

Samatta akimaliza kazi Taifa, kupewa kiwanja chake Mkuranga

Na Rahma Junior
MBWANA Samatta kesho Jumamosi ataiongoza Taifa Stars kuvaana na Misri, kwenye pambano la kuwania kwenda Gabon katika fainali za Afcon 2017, lakini Jumapili atakuwa katika sherehe moja kamambe.
Nahodha huyo wa Stars, atakuwa anakabidhiwa  kiwanja cha ekari tano kilichopo kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib 'Teacher' alisema  jijini Dar es Salaam kuwa maandalizi yamekamilika na Mbwana amewasili nchini kwa mechi ya timu ya TAifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Misri utakaochezwa Jumamosi.
Alisema sherehe hizo zitaambatana na ugawaji wa nyumba na misingi ya nyumba kwa wasanii 35 ambao wanafikisha ya wanachama 180 waliokwisha kabidhiwa nyumba zao.
Alisema SHIWATA imemzawadia Mbwana ekari tano ili ajenge kituo cha michezo kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana wa Tanzania watakaolitangaza taifa hili kwenye medani ya michezo kimataifa.
Taalib alisema mtandao  huo unaomiliki eneo la ekari 300 za kujenga makazi unawakaribisha wadau wa michezo kuwekeza kwa kujenga kumbi za burudani,shule za michezo, studio za kurekodia, viwanda vya kutengeneza vifaa vya michezo na hosteli za kufikia wachezaji.
Alisema sherehe za kugawa nyumba zinafanyika kwa mara ya tano kutoka ujenzi huo uanze katika kijiji hicho ambapo wanachama 185 wamekabidhiwa nyumba zao walizojengwewa kwa njia ya kuchangishana.
Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Mnauye ambaye atakuwa waziri wa pili kutembelea kijiji hicho baada ya Naibu wake, Anna Wambura kutembelea mapema mwaka huu.
Viongozi wengine waliowahi kutembelea kijiji hicho ni kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2014, Wakuu wa wilaya ya Mkuranga wastaafu, Mercy Silla, Clemency na Mkuu wa wilaya hiyo wa sasa, Abdallah Kihato.
Wageni wengine walioalikwa kwenye sherehe hizo ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi viongozi wa Serikali wa Wilaya ya Mkuranga na wasanii maarufu nchini.

Hivi ndivyo Copa America 2016 itakavyopigwa USA kuanzia leo

http://www.concacaf.com/wp-content/uploads/2015/10/16_CAC_GEN_GGL.jpg
#no.DateTime in ISTMatchScore
104-06-201607:00amUSA vs Colombia--
205-06-201602:30amCosta Rica vs Paraguay--
305-06-201605:00amHaiti vs Peru--
405-06-201607:30amBrazil vs Ecuador--
506-06-201602:30amJamaica vs Venezuela--
606-06-201605:30amMexico vs Uruguay--
707-06-201604:30amPanama vs Bolivia--
807-06-201607:30amArgentina vs Chile--
908-06-201605:30amUSA vs Costa Rica--
1008-06-201608:00amColombia vs Paraguay--
1109-06-201605:00amBrazil vs Haiti--
1209-06-201607:30amEcuador vs Peru--
1310-06-201605:00amUruguay vs Venezuela--
1410-06-201607:30amMexico vs Jamaica--
1511-06-201604:30amChile vs Bolivia--
1611-06-201607:00amArgentina vs Panama--
1712-06-201604:30amUSA vs Paraguay--
1812-06-201606:30amCosta Rica vs Colombia--
1913-06-201604:00amEcuador vs Haiti--
2013-06-201605:00amBrazil vs Peru--
2114-06-201605:30amMexico vs Venezuela--
2214-06-201607:30amUruguay vs Jamaica--
2315-06-201605:30amPanama vs Chile--
2415-06-201607:30amArgentina vs Bolivia--

2016 Copa America Centenario Quarter Final Match

#no.DateTime in ISTMatchScoreWinner
2517-06-201607:00amGroup A1  vs Group B2--
2618-06-201605:30amGroup B1 vs Group A2--
2719-06-201604:30amGroup D1 vs Group C2--
2819-06-201607:30amGroup C1 vs Group D2--

2016 Copa America Centenario Semi Final Match Schedule

#no.DateTime in ISTMatchScoreWinner
2922-06-201606:30amWinner M25 vs Winner M27--
3023-06-201605:30amWinner M26 vs Winner M28--

2016 Copa America Centenario Final Match Schedule

#no.DateTime in ISTMatchScoreWinner
3126-06-201605:30amLooser M29 vs Looser M30--
3227-06-201605:30amWinner M29 vs Winner M30--

Liverpool asikuambie mtu baba'ake imepania si utani!

http://static.sportskeeda.com/wp-content/uploads/2016/05/emre-mor-1463896209-800.jpgKLABU ya Liverpool ambayo ilikaribia kutwaa taji la UEFA Europa League kama sio kuteleza kwa Sevilla ya Hispania, imedaiwa inaongoza mbio za kuwania saini ya chipukizi wa kimataifa wa Uturuki na klabu ya Nordsjaelland, Emre Mor.
Mor mwenye umri wa miaka 18, anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora wanaochipukia Ulaya kwasasa baada ya kuonyesha kiwango bora katika Ligi Kuu ya Denmark na kumfanya kuitwa katika kikosi cha Uturuki kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 inayoanza Juni 10 nchini Ufaransa.
Klabu za Manchester United, Borussia Dortmund na Ajax Amsterdam nazo zinatajwa kuwa zinamwania chipukizi huyo anayemudu kiungo mshambuliaji lakini Liverpool ndio inaelezwa kuwa inaongoza mbio hizo.
Dogo huyo amefunga mabao mawili na kusaidia mengine mawili mechi 13 alizoichezea klabu yake msimu huu.