![]() |
| Rais wa TFF, Malinzi |
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza kutoa fomu za Leseni za Klabu (Club Licensing) za Ligi ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na zile za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.
Klabu hizo zitatumiwa fomu hizo na kutakiwa kuzijaza na kuzirejesha kabla ya Juni 19, mwaka huu ikiwa ni siku 10 mara baada ya Bodi ya Ligi ya TFF (TPLB) kuwatuamia fomu hizo. Klabu itakayojaza fomu hizo kwa wakati ndiyo ambayo maombi yake ya leseni yatashughulikiwa mapema.
Tayari TFF imeteua Kamati ya Leseni ya Klabu (Club Licensing Committee) ambayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi ya leseni kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza na kutoa uamuzi wa kuzikubali au kuzikataa kwa kuzingatia Kanuni ya Leseni ya Klabu.
Wajumbe walioteuliwa kwenye Kamati hiyo inayoundwa kwa mara ya kwanza ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), David Kivembele, Hamisi Kissiwa na Prof. Mshindo Msolla.
Klabu zinatakiwa kuchukua fomu za maombi TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa kazi ambapo zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya Kanuni husika zitapatiwa leseni husika ili zishiriki michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016/2017.
Kwa klabu ambazo zitashindwa kukidhi matakwa ya leseni yanayolenga kuhakikisha mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangaji matokeo katika maeneo matano ya wachezaji (sporting), viwanja (infrastructure), utawala (administrative and personnel), umiliki wa klabu (ownership) na fedha (financial), hazitapa leseni hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki ligi.Klabu ambazo zitanyimwa leseni na kutoridhika na uamuzi huo, zitakuwa na fursa ya kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF. Kwa mujibu wa Ibara ya 5(3) ya Kanuni ya Leseni ya Klabu ya TFF, Kamati hiyo ndiyo itakayosikiliza rufani zinazopinga uamuzi wa Kamati ya Leseni ya TFF.

NA ALFRED LUCAS
MWILI wa bingwa mara wa tatu wa Dunia kwa uzito wa juu, Muhammad Ali unatarajiwa kuzikwa keshokutwa Ijumaa, lakini cha kusikitisha ni kwamba hatazikwa na Rais wa Marekani, Barack Obama.






KLABU ya Liverpool ambayo ilikaribia kutwaa taji la UEFA Europa League kama sio kuteleza kwa Sevilla ya Hispania, imedaiwa inaongoza mbio za kuwania saini ya chipukizi wa kimataifa wa Uturuki na klabu ya Nordsjaelland, Emre Mor. 

LAZIMA iwashike. England imetangaza kikosi chake cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano ya Fainali za UEFA Euro 2016, huku chipukizi wa Manchester Utd, Marcus Rashford akijumuishwa katika kikosi hicho.
SIJUI ni mikosi au basi tu. Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low amemuacha mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus katika kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.
KAKATWA. Beki wa zamani wa Arsenal, Philippe Senderos ambaye amekuwa akihaha kurejea katika kiwango chake katika misimu ya karibuni, ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uswisi kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.
WAKATI klabu nyingine zikienda likizo kwa ajili ya mapumziko ya Ligi Kuu Bara, Mbeya City haijalala kwani inatarajiwa kufanya ziara ya kisoka Malawi.