STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 12, 2015

Mwana Mfalme aahidi makubwa FIFA atakapochaguliwa

http://www2.pictures.zimbio.com/gi/Ali+Bin+Al+Hussein+FIFA+Ballon+Gala+2012+NI3gHmXp6hll.jpgMGOMBEA Urais katika uchaguzi ujao wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Prince Ali bin Al Hussein amejinadi kuwa atakuwa atalifanya shirikisho hilo kuwa la uwazi na uwajibikaji kama atachaguliwa kugombea kumshinda rais wa sasa Sepp Blatter katika Uchaguzi huo.
Prince Ali mwenye umri wa miaka 39 alitangaza mipango yake ya kugombania nafasi hiyo mapema wiki hii na kuapa kusafisha jina la shirikisho hilo ambalo hivi sasa limechaguzi kwa tuhuma mbalimbali za ufisadi. Mwana mfalme huyo wa Jordan amesema kama taasisi FIFA imekuwa ikifanya mambo yake kwa siri hivyo anadhani wakati umefika wa kubadilisha suala hilo na kulileta kwa wakati tunaoishi sasa wa ukweli na uwazi. Uchaguzi wa FIFA unatarajiwa kufanyika Mei 29 mwaka huu
Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limekuwa likighubikwa na kashfa ya rushwa juu ya mchakato wa upatikanaji wa wenyeji wa fainali mbili za Kombe la Dunia za 2018 zitakazofanyika Russia na zile za 2022 zitakazochezwa Qatar.
Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Wakala wa Ronaldo atwaa tuzo kwa mara ya 5 mfululizo

http://globesoccer.wpengine.netdna-cdn.com/wp-content/uploads/2014/05/Globe-Soccer-Awards-2371.jpgWAKALA wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya wakala bora kwa mara ya tano mfululizo ijulikanayo kama Globe Soccer Awards.
Wakala huyo Jorge Mendes amepewa tuzo hiyo kwa kutambua mafanikio yake kama wakala wa wachzaji mojawapo akiwa Ronaldo.
Mendes ambaye kwa mara kwanza kunyakuwa tuzo hiyo ilikuwa mwaka 2010 amekuwa akiwasimamia wachezaji bora kabisa duniani ambapo mbali ya Ronaldo mwingine ni James Rodriguez na hata meneja wa Chelsea Jose Mourinho.
Ronaldo ndio aliyenyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka inayotolewa na Globe Soccer huku meneja wa Madrid Carlo Ancelotti akinyakuwa tuzo ya kocha bora.

Mchungaji auwawa Kanisani akiendesha ibada

Security officers examin the lifeless body of an assistant pastor George Karidhimba Muriki of the Maximum Revival Ministries Church after he was shot dead by...
maafisa wa Polisi wakimsaidia msaidizi wa mchungaji aliyeuwawa nje ya kanisa hilo (Picha:AP)
WATU wenye silaha wasiofahamika walimfyatulia risasi na kumuuwa mchungaji mmoja wakati wa ibada kanisani siku ya jumapili katika mji wa Mombasa nchini Kenya  maahala ambako polisi wanapambana na vijana wa ki-islam wenye msimamo mkali.
Mauaji hayo yalitokea ndani ya mlango mkuu wa kuingilia kwenye kanisa la Maximum Revival Centre katika mtaa wa majengo. 
Mashahidi wanasema polisi waliwazuia watu wenye silaha kuingia ndani ya kanisa na kuuwa waathirika Zaidi. Watu hao wenye silaha hawajafahamika  lakini kundi la wanamgambo wa Al-Shabab kutoka nchi jirani ya Somalia limeshambulia malengo kadhaa nchini Kenya. Kundi hilo la Al-Shabab liliapa kulipiza kisasi kwa majeshi ya Kenya kuwepo nchini Somalia kwa ajili ya kusaidia  wanajeshi wa serikali dhidi ya wanamgambo hao.
VOA

Messi, Suarez, Neymar wafunga Barca wakiua Atletico Madrid

Lionel Messi, Neymar and Luis Suarez
Nyota wa Barcelona wakishangilia ushindi wao
Lionel Messi, Neymar and Luis Suarez
Furaha tupu kwa wakali wa Nou Camp
WASHAMBULIAJI nyota wa Barcelona Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wote walifunga wakati timu yao ikiiadhibu mabingwa watetezi wa La Liga, Atletico Madrid kwa mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi hiyo ya Hispania.
Neymad alianza kufungua karamu ya mabao kwa wenyeji waliokuwa uwanja wa Nou Camp katika dakika ya 12 baada ya kumalizia kazi nzuri ya  Suarez kabla ya Suarez kufunga b ao la pili dakika ya 35 kwa kazi nzuri ya Messi.
Wenyeji walipata bao la kufutia machozi lililofungwa na Mario Mandzukic katika dakika ya 57 kwa mkwaju wa penati baada ya Messi kucheza madhambi langoni mwake dhidi ya Jesus Gamez.
Hata hivyo mshambuliaji huyo anayenyemelewa na Chelsea, alisahihisha makosa kwa kutumbukiza wavuni bao la tatu dakika tatu kabla ya pambano hilo kumalizika na kuifanya Barcelona kuwapumulia Real Madrid kwa tofauti na pointi moja, wenyewe wakiwa na 41 wakati Real wakiwa na 42.
Atletico Madrid wameendelea kusalia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 38 baada ya kucheza mechi  18 kama Barcelona, huku Real Madrid akiwa na mecho moja mkononi kwani imecheza mechi 17 tu.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Athletic Bilbao ilikubali kipigo cha 2-1 nyumbani dhidi ua Elche, Granada ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Real Sociedad inayonolewa na kocha David Moyes na leo usiku Rayo vallecano itakuwa wenyeji wa Cordoba katika mfululizo wa ligi hiyo inayozidi kushika kasi.

Juventus yaifyatua Napoli 3-1, yazidi kujikita kileleni

Paul Pogba akishangilia na wenzake
VINARA wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A, Juventus imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuikung'uta Napoli wakiwa ugenini kwa mabao 3-1.
Bao la Paul Pogba katika dakika ya 29 akimalizia kazi nzuri ya Llorente liliwashtua wenyeji ambao walienda mapumziko wakiwa nyuma kabla ya kuzinduka kipindi cha pili baada ya iguel Britos kusawazisha dakika ya 64.
Dakika ya 69 wageni waliongeza bao la pili kupitia Martin Cacerea aliyemaliza pande la Andrea Pirlo na katika dakika za lala salama Arturo Vidal aliifungia Juventus bao la tatu na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 43 na kuzidi kuwakimbia wapinzani wa AS Roma waliomalizishwa sare ya 2-2 nyumbani na Lazio mapema jana.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Sampdoria ilikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Empoli.

Ali Baucha, Ney wa Mitego waja na Vululu

BAADA ya kutamba na 'Chimpododo' na 'Zumzum' aliomshirikisha K-One, dansa wa zamani na mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Ali Baucha anajiandaa kuachia wimbo wake mpya uitwao 'Vululu'.
Baucha aliiambia MICHARAZO kuwa wimbo huo mpya ambao umerekodiwa katika studio za Baucha Records, ameimba akishirikiana na Ney wa Mitego.
"Katika kuukaribisha mwaka mpya wa 2015, nipo mbioni kuiachia kazi yangu mpya iitwayo 'Vululu' niliyoimba na msanii Ney wa Mitego, kila kitu kimekamilika kilichobakia ni siku ya kutoka hadharani," alisema Baucha.
Baucha alisema wimbo huo wa 'Vululu' ni miongoni mwa kazi mpya zilizotengenezwa na studio zake za Baucha Records.
Alisema kazi nyingine zitakazoachiwa ni pamoja na wimbo mpya wa K-One alioimba na Suma Lee na kazi mpya ya Fizzo aliyesumbua mwaka jana na '24 Hours' ambaye safari hii ataimba na Walter Chilambo

Rama Pentagone wa Twanga Pepeta Tajiri Penzi

MUIMBAJI mahiri wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Ramadhan Mhoza 'Pentagone' amefyatua wimbo wake binafsi uitwao 'Tajiri Penzi'.
Wimbo huo uliorekodiwa kwa mtayarishaji Amaroso ni utambulisho wa albamu binafsi ya muimbaji huyo wa zamani wa bendi ya Double M Sound, Levent Musica na Extra Bongo.
Akizungumza na MICHARAZO, Pentagone alisema wimbo huo ulio katika mahadhi ya rhumba ni kati ya nyimbo zitakazokuwa katika albamu yake aliyopanga kuitoa baadaye mwaka huu.
"Katika kutimiza ahadi yangu kwa mashabiki, nimetengeneza wimbo mpya uitwao 'Tajiri Penzi' ambao upo katika miondoko ya rhumba na ni kazi yangu binafsi nje ya Twanga Pepeta," alisema.
Pentagone alisema kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kutengeneza video ya wimbo huo kabla ya kuanza kurekodi nyimbo nyingine kukamilisha albamu yake ya kwanza itakayokuwa na jumla ya nyimbo sita au nane

Manchester United yapigwa nyumbani, yaporomoka EPL

Dusan Tadic (second right) pounces upon the rebound and converts coolly to hand Southampton the lead against Manchester United
Dusan Tadic akifunga bao pekee la Southampton
Southampton captain Jose Fonte led from the back for Southampton and kept Robin van Persie from having any impact on the game
van Persie akiwania mpira na Jose Fonte
Juan Mata (right) missed a number of good chances to level the scores shortly after Southampton went ahead against United
Juan Mata akijaribua kufunga bao
United captain Wayne Rooney cut a dejected figure as he left the pitch after the full time whistle was blown
Nahodha Wayne Rooney akiwa haamini kama wamepigwa kidude nyumbani
KLABU ya Manchester United licha ya kucheza uwanja wa nyumbani na ikiwa imefarijika kwa kurejea dimbani kwa baadhi ya nyota wake waliokuwa majeruhi imeshindwa kufurukuta baada ya kuchapwa bao 1-0 na Southampton katika mechi ya Ligi Kuu ya England.
Bao pekee la wageni ambao ni maarufu kama 'Watakatifu' lililowanyong'onyesha Mashetani Wekundu liliwekwa kimiani katika dakika ya 69 na Dusan Tadic na kuwafanya Southampton kukwea hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo wakiiengua Manchester United.
Ushindi umeifanya Southampton ambayo imelipa kisasi cha kufungwa nyumbani mwezi uliopita kwa mabao 2-1 na wapinzani wao kufikisha pointi  39, mbili zaidi ya ilizonazo vijana wa Luis Van Gaal licha ya zote kucheza mechi 21 kila moja.
Pia ni ushindi wa kwanza wa vijana wa Ronald Koeman katika uwanja wa Old Trafford tangu miaka 27 iliyopita kitu ambachop kimempa faraja kubwa koxcha huyo Mholanzi aliyewahi kuwa msaidizi wa Van Gaal.

Sunday, January 11, 2015

Sevilla yazidi kuchanja mbuga La Liga

http://videosdelbetis.com/wp-content/themes/Video/thumb.php?src=http://videosdelbetis.com/wp-content/uploads/2013/11/sfc.jpg&w=630&zc=1&q=80&bid=1TIMU ya Sevilla ikiwa uwanja wa ugenini ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Almeria na kujiweka katika nafasi nzuri katika mbio zao kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
Sevilla ilijikuta ikisubiri hadi kwenye kipindi cha pili kuweza kupata mabao yake hayo ambayo yalifungwa na Iborra katika dakika ya 58 kabla ya Coke kuongeza jingine dakika tano baadaye na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 36 na kushika nafasi ya nne.
Mashabiki wa soka wanatarajia kupata burudani baadaye wakati Barcelona itakayokuwa nyumbani itaikaribisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Atletico Madrid zinazofukuzana nyuma ya vinara Real Madrid ambayo jana ilizinduka katika ligi hiyo klwa kushinda mabao 3-0 dhidi ya Espanyol.

Mgambo JKT yaitoa nishai Ruvu Shooting Mkwakwani


http://tplboard.co.tz/assets/uploads/files/273f8-63.jpg
Mgambo JKT waliopata ushindi dhidi ya Ruvu Shooting
TIMU ya Mgambo JKT imeitoa nishai Ruvu Shooting katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mchezo pekee uliochezwa  leo kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga baada ya kuicharaza bao 1-0.
Ruvu Shooting inayonolewa na kocha Mkenya, Tom Oloba ilishindwa kuhimili vishindo vya maafande wenzao licha ya tambo zilizokuwa zikitolewa na uongozi wa klabu hiyo chini ya Msemaji wao, Masau Bwire.
Bao hilo la wenyeji liliwekwa kimiani na Full Maganga katika dakika ya 44, likiwa ni bao la kwanza kwa mchezaji huyo ambaye amekuwa na kismati cha kuzitungua Simba na Yanga.
Kwa ushindi huo Mgambo imefikisha pointi 12 na kuchupa kutoka nafasi ya 12 hadi nafasi ya nane wakiing'oa Ruvu Shooting ambayo imesaliwa na 11.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mchezo wa leo:
                                 P   W    D    L    F    A   GD   Pts
01. Mtibwa Sugar       08  04  04  00  11  04  07   16
02. JKT Ruvu             10  05  01  04  10  09   01  16
03. Yanga                  08  04  02  02  11  07   04  14
04.  Azam                  08  04  02  02  10  06   04  14
05.  Kagera Sugar      09  03  05  01  07  04   03  14
06.  Polisi Moro          10  03  05  02  09  08   01  14
07. Coastal Union      09  03  03   03  09  08   01  12
08.  Mgambo JKT      09  04  00  05   05    09  -4  12
09. Ruvu Shooting    10  03  02   05   05   08  -3  11
10. Stand Utd           10  02  05   03   07   12  -5  11
11. Ndanda Fc          10  03  01   06  10    14  -4  10
12. Simba                08  01  06   01   07   07  00  09
13. Mbeya City         08   02  02   04  03   06  -3   08
14. Prisons               09  01  04   04  06   08  -2   07

Wafungaji Bora:
5-
Didier Kavumbagu(Azam)
4-
Rama Salim (Coastal), Danny Mrwanda, Simon Msuva (Yanga) Ame Ally (Mtibwa), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu)

3- Ally Shomari, Emmanuel Okwi (Simba), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Jacob Massawe (Ndanda)
2- Shaaban Kisiga, (Simba), Nassor Kapama (Ndanda) Salum Kanoni (Kagera), Aggrey Morris (Azam),  Najim Magulu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Amissi Tambwe, Jerry Tegete (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Heri Mohammed, Mussa Said (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo),  Malimi Busungu (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi)
1- Joseph Owino (Simba), Coutinho, Kelvin Yondan, Haruna Niyonzima, Jaja (Yanga), Deo Julius, Steven Mazanda (Mbeya City), Bakari, Imani Mapunda, Said Bahanuzi (Polisi-Moro), Kipre Tchetche,  Aggrey Morris, SHomar Kapombe, John Bocco  (Azam), Ernest Joseph, Paul Ngalema,  (Ndanda), Jacob Mwaitalako,  Laurian Mpalile, Amir Omary, Hamis Mahingo (Prisons), Lutimba Yayo, Kennedy Masumbuko, Joseph Mahundi, Hussein Sued,Itubu Intembe (Coastal), Ramadhani Pella, Full Maganga (Mgambo), Said Mkopi, Vincent Barnabas (Mtibwa), Amos Mgina, Najim Magulu, (JKT Ruvu), Salum Kamana, Shaaban Kondo (Stand Utd), Paul Ngwai, Atupele Green(Kagera Sugar), Juma Nade, Abdulrahman Mussa, Thomas Mathayo , Hamis Kasanga ,Zubeiry Dabi (Ruvu Shooting)

Inter Milan yatamba nyumbani,

Nemanja Vidic
Vita ya Inter Milan dhidi ya Genoa leo
KLABU ya Inter Milan imefanikiwa kuifumia Genoa kwa kuicharaza mabapo 3-1 katika mechi kali ya Ligi Kuu ya Italia, Serie A, wakati AS Roma na mahasimu wao Lazio wametoshana nguvu ya maba0 2-2.
Inter ikiwa nyumbani ilipata ushindi huo kupitia mabao ya Palacio katika dakika ya 12, Mauro Icardi dakika ya 39 na Nimanja Vidic dakika mbili kabla ya mechi kumalizika, huku bao la wageni lilifungwa na Izzo dakika ya 85.
Katrika mechi nyingine za ligi hiyo,
Atlanta ikiwa nyumbani imelazimishwa sare ya 1-1 na Chievo Verona, Cagliari ikainyoa Cesena mabao 2-1 na Fiorentina ikipata ushindi mtamu nyumbani dhidi ya Palermo baada ya kuinyoa mabao 4-3.
Nayo Hellas Verona ikiitafuna Parma waliowafuata kwao kwa mabao 3-1 na Mahasimu wa jiji la Roma, AS Roma na Lazio zilishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 2-2 na Sampdoria iliilaza Empoli kwa bao 1-0 baadaye Napoli watakuwa wenyeji wa vinara Juventus.

Arsenal yaitoa nishai Stoke City Sanchez azidi kung'ara

The Arsenal players join star man Sanchez in celebration of his second goal of the afternoon
Wachezaji wa Arsenal wakipongezana
Arsenal defender Koscielny (6) heads the north London club into an early lead at the Emirates after just six minutes
Laurent Koscielny akifunga bao la kwanza la Arsenal kwa kichwa
MABAO mawili kutoka kwa Alexis Sanchez na jingine la beki Laurent Koscielny yameiwezesha Arsenal kupata ushindi mujarabu nyumbani dhidi ya 'wagumu' Stoke City katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya England.
Ushindi  huo umekuja wakati Arsenal ikitoka kupokea kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Southampton, ambapo kiungo Mesut Ozil, alirejea uwanjani katika pambano hilo la Emirates baada ya kuwa nje miezi mitatu.
Wenyeji walianza kuandika bao dakika ya 6 kupitia Koscielny kabla ya Sanchez kuongeza la pili dakika ya 33 na kuja kuongeza jingine dakika nne tangu kuanza kwa kipindi cha pili.
Katika pambano hilo Arsenal ilijikuta ikimpoteza beki wake Mathieu Debuchy aliyeumia bega mapema na nafasi yake kuchukuliwa na Bellerin dakika chache baada ya Koscielny kufunga bao la kuongoza kwa kichwa akimaliza krosi ya Sanchez ambaye kwa mabao mawili ya leo amefikisha mabao 12 katika ligi hiyo anayoicheza kwa msimu wa kwanza.

Kwa ushindi hio Arsenal imefikisha pointi 36 na kulingana na Southampton na kukamata nafasi ya tano wakati wapinzani wao wamesaliwa na pointi26 na kusalia kwenye nafasi ya 11.
Muda mchache ujao Manchester United watakuwa uwanja wa Old Trafford kupepetana na Southampton katika mechi nyingine ya ligi hiyo ambayo baadhi ya nyota wa Man Utd waliokuwa nje kwa majeraha watarejea dimbani.
Wachezaji hao ni Daley Blind na Angel di Maria  ambao wapo kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Louis Van Gaal.


Saturday, January 10, 2015

Ozil arejea Arsenal, Rojo, Blind waipa furaha Man Utd

Kipa Valdes akiwa na wachezaji wenzake wapya wa Manchester United

Daley Blind akifanya mazoezi hapa akiwa na Dogo Andreas Pereira
Rojo naye alipasha na wenzake
WAKATI Manchester United wakichelekea kurejea tena dimbani kwa nyota wake Marcos Rojo na Daley Blind, Kiungo Mesut Ozil wa Arsenal naye amepona na huenda akarejea uwanjani kesho wakati Arsenal inakipiga dhidi ya Stoke City.
Mashetani Wekundu wanatarajiwa kuwa nyumbani kuwavaa Southampton baada ya kupata sare mbili mfululizo ugenini katika Ligi Kuu ya England, lakini ikiwa na furaha kurejea kwa nyota hao sambamba na kumnasa kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes waliyemsainisha.
Kama ilivyo kwa Manchester, Arsenal wenyewe wanafurahi baada ya Ozil kurejea Ligi Kuu England baada ya kukaa nje miezi mitatu kutokana na maumivu ya goti.
Kocha Arsene Wenger amesema Ozil amekuwa akifanya mazoezi na wenzake na sasa yuko fiti, hata hivyo inaonekana ataanzia benchi.
Mjerumani huyo aliyejiunga na Arsenal akitokea Madrid aliumia katika mechi dhidi ya Chelsea, Oktoba mwaka jana.
Ozil ndiye mchezaji ghali zaidi Arsenal iliyompata kwa kitita cha pauni milioni 42.5.

Real Madrid yazinduka yaipiga Espanol 3-0

Gareth Bale
Bale akishangilia bao lake wakati Real ikiiadhibu Espanyol
Real Madrid v Espanyol
Nacho akishangilia bao lake
LICHA ya kucheza pungufu timu ya Real Madrid imepata ushindi wa mabao 3-0 nyumbani katika  Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Espanyol na kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Fabio Coentrao alilimwa kadi nyekundu kaytika dakika ya 53, lakini mabao ya James Rodriguez katika dakika ya 12 , Gareth Bale dakika ya 28 na  lile na Nacho la dakika ya 70 yalitosha kuwapa ushindi muhimu Real Madrid iliyoshuhudia nahodha wake, Cristiano Ronaldo akitoka uwanjani bila kufunga bao ikiwa ni mara ya kwanza baada ya muda mrefu msimu huu.
Kwa ushindi hio Madrid wamefikisha pointi 42 na kuiacha Barcelona ikiwa nafasi ya pili na pointi 38 sawa na ilizonazo nazo Atletico Madrid ambazo zinatarajiwa kushuka dimbani kesho.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, Malaga ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 na  Villarreal na hivi sasa Celta Viro ipo dimbani kuumana na Valencia nyumbani kwao na tayari wamekubali bao 1-0.

Haya ndiyo matokeo ya EPL kwa leo

Balotelli akichuana na mchezaji wa Sunderland
City ilipong'ang'aniwa na Everton ugenini leo
Chelsea wakipongezana baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle Utd
Sunderland     0 - 1     Liverpool
Burnley     2 - 1     Queens Park Rangers
Chelsea     2 - 0     Newcastle United
Everton     1 - 1     Manchester City
Leicester City     1 - 0     Aston Villa
Swansea City     1 - 1     West Ham United
West Bromwich …     1 - 0     Hull City    
Crystal Palace     2 - 1     Tottenham Hotspur

Fainali Mapinduzi ni Simba na Mtibwa

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/simba1.jpg
Simba waliowafuata Mtibwa Fainali za Kombe la Mapinduzi
Mtibwa Sugar (jezi za kijani) watakaoumana na Simba siku ya Jumanne
KLABU ya Simba imefanikiwa kutinga Fainali za michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 baada ya kuing'oa Polisi ya Zanzibar na sasa wanatarajiwa kukutana na Mtibwa Sugar siku ya Jumanne.
Mtibwa ilifanikiwa kufuzu hatua hiyo mapema leo jioni baada ya kuiondosha kwa mikwaju ya penati 4-3 'wababe' wa Yanga, JKU baada ya kumaliza dakika 90 wakiwa sare ya 0-0.
Simba iliyoonyesha mabadiliko makubwa tangu ianze kunolewa na kocha Goran Kopunovic, walipata nafasi hiyo muda mchache uliopita baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika Nusu Fainali ya pili iliyochezwa uwanja wa Amaan. Zanzibar.
Bao lililoipelekea Simba kwenye hatua hiyo na kurejesha kumbukumbu ya nusu fainali ya mwaka 2010 ambapo timu hizo zilikutana na Mtibwa kuibuka wababe kabla ya kwenda kutwaa taji kwa kuilaza Ocean View bao 1-0.
Pia fainali hizo zinarejesha pia fainali ya ABC Top 8 iliyocvhezwa mwaka juzi na Simba kuilaza Mtibwa kwa mabao 4-3.
Mechi hiyo ya faionali itachezwa usiku wa Jumanne kwenye uwanja wa Amaan huku kila timu ikiwa na matumaini makubwa ya kutwaa taji hilo lililokosa mwenyewe baada ya KCCA ya Uganda kutemeshwa hatua ya Robo Fainali baada ya kufungwa kwa penati na Polisi.

JKT Ruvu waikamata Mtibwa Sugar,, yailaza Stand Utd Ndanda

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjrGUIMxPw7cdxPgyXtAxRJHOSLFdOsz_Yetg7EBn6y-K7pPB3ToQogwImAjfSZceVrbx9aUL72b0URIua7OK30a6XbaCvr5aiWZXfZNKy95h3Kn2aQ1qmkPYpYSe6mpm7NGtNDBnXSwLZ/s640/DSC_0805.JPG
KIkosi cha JKT Ruvu kilichochupa hadi naasi ya pili ikiziengua Yanga na Azam
MAAFANDE wa JKT Ruvu jioni ya leo wamepata ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Stand United ya Shinyanga na kuikamata Mtibwa Sugar ambao wapo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015.
Samuel Kamuntu na Amos Mgina waliifungia mafaande hao mabao hayo na kuifanya timu hiyo inayonolewa na kocha Fred Felix Minziro katika mchezo uliochezwa uwanja wa Chamazi na kuifanya ifikishe pointi 16 sawa na Mtibwa waliosalia kileleni. Bao la wageni Stand lilifungwa na Mussa Said.
JKT waliotangulia michezo miwili mbele dhidi ya Mtibwa inatoautiana na vinara hao mabao ya kufunga na kufungwa, Mtibwa ikiwa na 11 na kuungwa manne ilihali JKT ikiwa na mabao 10 na kufungwa 9.
Katika mechi nyingine iliyochezwa mjini Mtwara, wenyeji Ndanda Fc ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro.
Wageni walitangulia kupata bao kupitia Said Bahanuzi kabla ya wenyeji kuchomoa kupitia Jacob Massawe na kumanya mshambuliaji huyo wa zamani wa Toto African na African Lyon kuikisha bao la tatu msimu huu.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja tu itakayowakutanishja wenyeji Mgambo JKT itakayoikaribisha Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Friday, January 9, 2015

KICHOMI NI JASHO NA DAMU-BETHA SHAIBU

MSANII na mtayarishaji chipukizi wa filamu nchini, Betha Shaibu amesema 'limemtoka' jasho na damu katika kufanikisha kuitengeneza filamu yake ya kwanza iitwayo 'Kichomi' ambayo inatarajiwa kuachiwa mwezi huu.
Akizungumza na MICHARAZO, Betha alisema filamu hiyo iliyoshirikisha mastaa kadhaa nchini ni moja ya filamu ya kimapenzi yenye mafunzo makubwa kwa jamii na hasa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Betha alisema anaomba Mungu filamu hiyo iingie sokoni ili mashabiki waone tofauti iliyopo kati ya kazi hiyo na nyingine kwa namna msuko wa filamu hiyo ulivyo.
"Kwa kweli sijapumua mpaka kazi iingie sokoni, najua mwanzo ni mgumu lakini nimekubali kupambana ili kusimama kwa kutambua nina kipaji kikubwa cha utunzi na uigizaji," alisema Betha.
Ndani ya filamu hiyo ya 'Kichomi', Betha ameshirikiana na wakali kama Hemed Suleiman, Sabrina Omari, Mzee wa Majanga na wengine na imetengenezwa kupitia kampuni ya Red Leaf Entertainment.

Safari ya Inspekta Haroun Japan sasa April

MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rashid Kahena 'Inspekta Haroun' a.k.a Babu anatarajiwa kwenda nchini Japan baadaye mwaka huu baada ya awali kushindwa kufanya hivyo mwishoni mwa mwaka jana.
Inspekta Haroun aliliambia gazeti hili kuwa, ziara yake kwenda kutengeneza kazi mpya chini ya kampuni ya Hyper Production chini ya Deejay Kay Dee Beatz ilipangwa kufanyika Desemba mwaka jana, lakini ilishindikana baada ya kukosa visa.
Alisema hivyo wamekubaliana na 'mabosi' wake safari hiyo sasa iwe mwezi April akimini kuwa kila kitu kitaenda sawa kwa ajili ya kwenda kufanya kazi chini ya lebo hiyo.
"Safari yangu ya kwenda Japan kuingia mkataba wa kufanya kazi chini ya lebo ya Hyper Production imekwama kwa kukosa visa na sasa itafanyika Aprili kwa kuamini kila kitu kitakuwa kimekamilika, ingawa tayari kampuni hiyo imetengeneza video za nyimbo zangu mbili ambazo nitaziachia hivi karibuni mashabiki wapate burudani," alisema.
Babu alisema video hizo ni za nyimbo za 'Mungu Ndiye Anayepanga alioimba na Sir Juma Nature na ule wa 'Bado Hujachelewa' alioimba pekee yake ambapo kampuni hiyo ilifanya kazi ya kuzichanganya picha na kuongeza vionjo baada ya kuvutiwa na nyimbo hizo.

K-One Suma Lee wana ngoma mpya kwa Baucha

BAADA ya kutamba na nyimbo za 'Yule' aliyoimba na Maunda Zorro na 'Jimama Zamiela', msanii K-One anajiandaa kufyatua 'ngoma' mpya aliyomshirikisha mkali wa zamani wa Parklane, Suma Lee.
Akizungumza na MICHARAZO, Mkurugenzi wa Baucha Records inayommilikia msanii K-One, Ali Baucha alisema wimbo huo upo hatua ya mwisho kabla ya kuachia rasmi mwezi ujao ukiwa umetengenezwa katika studio zake.
Baucha alisema wimbo huo ambao bado haujapewa jina ni kati ya kazi tatu mpya za studio hizo zinazotarajiwa kuachiwa karibuni, wimbo mwingine ukiwa ni wa Fizzo aliyemshirikisha Mshindi wa BSS 2013, Walter Chilambo.
"Baucha Records kwa sasa tupo katika maandalizi ya kutoa kazi mpya baada ya kuhamisha studio mahali tulipokuwapo awali pale Magomeni Mapipa, na kati ya kazi hizo moja ni wa K-One akiimba na Suma Lee na mdogo wangu anayeishi Ujerumani pamoja na ule wa Fizzo anaoimba na Walter Chilambo," alisema Baucha mmoja wa watayarishaji mahiri wa muziki wakongwe nchini.

Michuano ya Taifa ya Soka kwa wanawake kuanza kesho

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcLvLEgI1HLK7c-HmKa5lTL3-7Sz3hW-nNnR1ogOhAVkhVKc6ERg0HahgcfqOkBf4_82s6MMwonfDQO7d_g2raIBEMLzyQP0shox0pazxJwKSHQDgzmt-H2s4PIlBvwSC8RTQiBheP3ss/s1600/IMG_8106.JPGMICHUANO ya soka ya Kombe la taifa kwa timu za Wanawake inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi ambapo mechi ya kwanza za raundi ya kwanza zitachezwa kesho kwenye miji 11 tofauti nchini.
Katika mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin, Geita itakuwa mwenyeji wa Kagera (Uwanja wa Geita), Tabora itacheza na Kigoma kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Simiyu na Shinyanga (Uwanja wa Simiyu), Arusha na Manyara (Sheikh Kaluta Amri Abeid), na Kilimanjaro na Tanga (Uwanja wa Ushirika).
Mechi nyingine ni Lindi itaikaribisha Mtwara kwenye Uwanja wa Ilulu, Ruvuma na Njombe (Uwanja wa Majimaji), Mbeya na Iringa (Uwanja wa Sokoine), Katavi na Rukwa (Uwanja wa Katavi), Dodoma na Singida (Uwanja wa Jamhuri) na Pwani itakuwa mwenyeji wa Morogoro katika Uwanja wa Mabatini.
Timu hizo zitarudiana Januari 13 mwaka huu, ambapo baada ya matokeo ya nyumbani na ugenini timu iliyoshinda ndiyo itakayoingia hatua inayofuata ambayo pia itashirikisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke.
Hatua hiyo, mechi zake za kwanza zitachezwa Januari 17 mwaka huu wakati zile za marudiano zitafanyika Januari 21 mwaka huu.
Baada ya hapo, hatua itakayofuata ni robo fainali, nusu fainali na fainali ambayo ndiyo itakayotoa bingwa wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini.

Wazee wa 4 waaga Mapinduzi Cup, wapigwa kidude na JKU

* Nusu fainali ni Simba v POlisi, Mtibwa v JKU

BAADA ya kutamba kwa kugawa 'dozi' nono ya mabao manne manne kwa wapinzani wao katika mechi ya makundi kabla ya kupunguzwa na Shaba kwa kuishinda bao 1-0, Yanga imeaga michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa bao 1-0 na JKU.
Yanga waliosheheni wachezaji 'ghali' na mastaa wanaotamba Afrika Mashariki walishindwa kufurukuta kwa maafande hao wa Jeshi la Kujenga Uchumi visiwani Zanzibar kunakofanyikia michuano hiyo itakayofikia tamati Jumanne.
Bao lililowazima Yanga na kuhitimisha tambo zake liliwekwa kimiani na Amour Omary 'Janja' aliyemfikia Andrey Coutinho aliye na mabao matatu katika orodha ya wafungaji.
Janja alifunga bao hilo lililokuwa la tatu kwake katika dakika ya 72 na kuwaacha vijana wa Hans van der Pluijm wakijilaumu kutokana na kukosa mabao mengi ya wazi katika muda wote wa pambano hilo lililochezwa uwanja wa Amaan.
Ushindi huo kwa JKU imeifanya timu hiyo kutinga Nusu Fainali na kupata nafasi ya kuvaana na Mtibwa Sugar waliowang'oa Azam kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza pambano lao kwa kufungana bao 1-1, Azam wakilazimika kusawazisha dakika za jioni kupitia Kipre Tchetche baada ya Shomar Ally kutangulia kufunga.
JKU imekuwa timu ya tatu kutoka kundi C ambazo zote zimepenya robo fainali na kutinga pia Nusu Fainali.
Nyingine ni Simba ambayo itaumana kesho na Polisi Zanzibar waliowavua taji la michuano hiyo KCCA ya Uganda kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka suluhu ndani ya muda wa kawaida na Mtibwa Sugar ambao ni Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Sabrina Omar, PHD 'wauza sura' katika KICHOMI

SALOME
PHD
WAIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Sabrina Omar 'Salome' na Hemed Suleiman 'PHD' wanatarajiwa kuonekana kwenye filamu mpya iitwayo 'Kichomi' ambayo imewashirikisha wakali wengine.
Mtayarishaji wa filamu hiyo, Betha Shaibu aliiambia MICHARAZO jana kuwa, filamu hiyo inayotarajiwa kuachiwa sokoni hivi karibuni, ni kazi yake ya kwanza kupitia kampuni ya Red Leaf Entertainment na kuongozwa na Joseph Jembe na Daudi.
Betha alisema filamu hiyo ya kijamii imewashirikisha nyota wakali kadhaa wenye majina nchini akiwamo Salome, Hemed Suleiman 'PHD', Raheem David 'Kibeberu' na Mzee wa Majanga.
"Ni filamu yangu ya kwanza ambayo nimeigiza kwa jina la Jameth nikishirikiana na wakali kama PHD, Sabrina Omar, Kibeberu na Mzee wa Majanga na inatarajiwa kuwa sokoni ndani ya mwezi huu," alisema Betha.
Betha alisema washiriki wa filamu hiyo wameitendea haki na kuwaomba mashabiki wasikose kuiona mara itakatoka hadharani kwani ina mafunzo makubwa kwa jamii mbali na kuburudisha.

Kitabu cha Steven Kanumba kuzinduliwa leo Landmark Hotel

Steven Kanumba enzi za uhai wake
Mwanamuziki Christian Bella na Mama yake Kanumba, Flora Mtogoha wakikinadi kitabu cha maisha ya marehemu Steven Kanumba kitakachozinduliwa leo pale Ubungo
Mtunzi wa kitabu hicho akikitambuliosha kwa wanahabari huku mratibu wa onyesho la uzinduzi, Frank akifuatilia kwa makini
MWANDISHI wa kitabu kinachohusu maisha ya nyota wa zamani wa filamu, Steven Kanumba kinachoitwa 'The Great Fallen Tree', Emmanuel Zirimwabagabo, amesema mauzo ya kitabu hicho  yataingizwa kwenye mradi wa Kanumba Foundation.
Taasisi hiyo ya inahusika na masuala ya kusaidia wajane na yatima ilianzishwa ikiwa ni njia ya kumuenzi marehemu Kanumba aliyefariki takriban miaka mitatu iliyopita.
Akizungumza na wanahabari, mtunzi huyo raia wa Canada mwenye asili ya DR Congo, alisema amefikia hatua hiyo baada ya kuongea na Mama Kanumba kuhusu ndoto za marehemu Kanumba aliyekuwa akipenda kuwasaidia yatima na alipanga kuwa na taasisi ya kusaidia wajane, lakini alifariki kabla ya kukamilisha ndoto zake.
“Mimi nilikuwa mpenzi wa kazi za Steven Kanumba baada ya kufariki niliumia sana, lakini nikafikiria ni jambo gani ambalo naweza kulifanya ili Kanumba aendelee kuishi japo hatupo naye kimwili lakini kiroho tupo naye,” alisema
“Nilifikiria kuandika kitabu kama sehemu ya heshima yangu kwake shujaa huyu kwetu sisi watu tunaopenda kazi zake, kwani Kanumba kanisaidia kujua kuongea Kiswahili kupitia filamu zake, hivyo napenda kuwe na kitu cha kumkumbuka," alisema Zirimwabagabo aliyetoa kitabu hicho kwa lugha mbili, cha Kiswahili na Kiingereza.
Naye Mama Kanumba, alitoa shukrani zake na akisema hakuwahi kufikiria kama mwanaye alikuwa na thamani kubwa kama hiyo hadi watu wa mataifa mengine kuja kuona kama ni mtu ambaye anatakiwa kuwekewa kumbukumbu kwa kuwekewa kitu au taasisi.
Kitabu hicho cha maisha ya kanumba kitazinduliwa kesho kwenye ukumbi wa Landmark Hotel, Ubungo ambako sherehe hizo zitaenda sambamba na uzinduzi wa taasisi hiyo ya Kanumba Foundation chini ya uratibu wa muigizaji Mohammed Mwikongi 'Frank' na burudani itakayosindikiza uzinduzi huo itatolewa na muimbaji Christian Bella.

2014 ni Yaya Toure tena, aweke rekodi akiifikia ile ya Samuel Eto'o

Yaya  Toure aliyenyakua tuzo ya Mwanasoka Bora akiweka rekodi ya aina yake Afrika
Samuel Eto'o aliyekuwa akishikilia rekodi ilivyofikiwa na Toure
KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya Manchester City, Yaya Toure ameibuka tena kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mara ya nne na kufikia rekodi ya Samuel Eto'o wa Cameroon.
Toure alishinda tuzo hiyo ikiwa ni rekodi ya kuwa mwanasoka wa kwanza kutwaa mara nne mfululizo katika hafila iliyofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Lagos Nigeria.
Toure, 31, aliibuka kidedea kwa kupata pointi nyingi mbele ya mshambuliaji wa Borussia Dortimund raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang na kipa wa Nigeria Vincent Enyeama.
Mchezaji huyo aliyeipa City taji la Ligi Kuu msimu uliopita na kuipeleka Tembo ya Ivory Coast kwenye Fainali za Afrika zitakazoanza wiki ijayo, alishatwaa tuzo miaka mitatu iliyopita 2011, 2012 na 2013.

Ni Eto'o pekee aliyekuwa na rekodi ya kutwaa tuzo hiyo mara nne baada ya kufanya hivyo mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010.
Katika tuzo nyingine Mwanasoka Bora anayecheza barani Afrika imeenda kwa Firmin Mubele Ndombe (DR Congo), huku Mwanasoka Bora wa Kike tuzo akiwa ni Asisat Oshoala wa Nigeria ambaye pia alinyakua tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike anayechipukia.
Mwanasoka Chipukizi kwa wanaume ilienda kwa Yacine Brahimi (Algeria) wakati tuzo ya Kocha Bora ni; Kheireddine Madoui wa ES Setif.
Timu Bora kwa 2014 ni Algeria kwa wanaume na Nigeria kwa wanawake ilihali Klabu Bora ni ES Setif (Algeria) na Kiongozi Bora ni Rais wa TT Mazembe Moise Katumbi Chapwe.
Orodha ya Mwanasoka Bora Afrika tangu 1995:
1995- George Weah (Liberia)
1996- Nwankwo Kanu(Nigeria)
 1997-    Victor Ikpeba (Nigeria)
1998-    Mustapha Hadji (Morocco)
1999-     Nwankwo Kanu (Nigeria)
2000-    Patrick Mboma (Cameroon)
2001-     El Hadji Diouf (Senegal)
2002-     El Hadji Diouf (Senegal)
2003-     Samuel Eto'o (Cameroon)
2004-    Samuel Eto'o (Cameroon)
2005-     Samuel Eto'o (Cameroon)
2006-    Didier Drogba (Ivory Coast)
2007-     Frederic Kanoute (Mali)
2008-    Emmanuel Adebayor (Togo)
2009- Didier Drogba (Ivory Coast)
2010-     Samuel Eto'o (Cameroon)
2011-     Yaya Toure     (Ivory Coast)
2012-     Yaya Toure (Ivory Coast)
2013-     Yaya Toure (Ivory Coast)
2014-     Yaya Toure (Ivory Coast)